Nehemia 3 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Nehemia 3:1-32

Wajenzi Wa Ukuta

13:1 Yer 31:38; Ezr 10:24; Neh 12:39; Za 48:12; Yn 5:2; Isa 58:2; Zek 14:10Eliashibu kuhani mkuu na makuhani wenzake walikwenda kufanya kazi na kulijenga upya Lango la Kondoo. Waliliweka wakfu na kuweka milango mahali pake, wakajenga hadi kufikia Mnara wa Mia, ambao waliuweka wakfu hadi Mnara wa Hananeli. 23:2 Ezr 2:34; Neh 7:36Watu wa Yeriko wakajenga sehemu zilizopakana nao, naye Zakuri mwana wa Imri akajenga karibu nao.

33:3 2Nya 33:14; Neh 12:39; Sef 1:10; Neh 6:1Lango la Samaki lilijengwa upya na wana wa Hasenaa. Waliweka boriti zake, na wakaweka milango yake na makomeo na nondo. 43:4 Ezr 8:33Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu iliyofuatia. Baada yake Meshulamu mwana wa Berekia, mwana wa Meshezabeli, alifanya ukarabati na aliyemfuatia ni Sadoki mwana wa Baana. 53:5 Neh 3:27; 2Sam 14:2Sehemu iliyofuatia ilikarabatiwa na watu kutoka Tekoa, lakini wakuu wao walikataa kufanya kazi chini ya wasimamizi wao.

63:6 Neh 12:36Lango la Yeshana lilikarabatiwa na Yoyada mwana wa Pasea, na Meshulamu mwana wa Besodeya. Waliweka boriti zake, na wakaweka milango, makomeo na nondo. 73:7 Yos 9:3; Neh 2:7-8Karibu nao ukarabati ulifanywa na watu kutoka Gibeoni na Mispa, yaani Melati Mgibeoni, na Yadoni Mmeronothi, sehemu hizi zikiwa chini ya mamlaka ya mtawala wa Ngʼambo ya Frati. 83:8 Neh 12:38Uzieli mwana wa Harhaya, mmoja wa masonara, alikarabati sehemu iliyofuatia, naye Hanania mmoja wa watengenezaji marashi akakarabati sehemu iliyofuatia. Walitengeneza Yerusalemu mpaka kufikia Ukuta Mpana. 9Refaya mwana wa Huri, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia. 10Kupakana na sehemu hii, Yedaya mwana wa Harumafu alikarabati sehemu iliyokuwa mkabala na nyumba yake, naye Hatushi mwana wa Hashabnea akakarabati sehemu iliyofuatia. 113:11 Neh 12:38; Ezr 2:32Malkiya mwana wa Harimu, na Hashubu mwana wa Pahath-Moabu walikarabati sehemu nyingine pamoja na Mnara wa Matanuru. 123:12 Kut 15:25; Lk 8:3; Flp 4:3Shalumu mwana wa Haloheshi, mtawala wa nusu ya wilaya ya Yerusalemu, alikarabati sehemu iliyofuatia akisaidiwa na binti zake.

133:13 Neh 2:13; 2Nya 26:9; Yos 15:34Lango la Bondeni lilikarabatiwa na Hanuni na wakazi wa Zanoa. Walilijenga upya, na kuweka milango yake na makomeo na nondo mahali pake. Pia walikarabati ukuta wenye urefu wa mita 450 hadi Lango la Samadi.

143:14 Yer 6:1; Mik 1:11Lango la Samadi lilikarabatiwa na Malkiya mwana wa Rekabu, mtawala wa wilaya ya Beth-Hakeremu. Alilijenga upya, na kuweka milango yake, na makomeo na nondo.

153:15 Yos 18:26; Amu 20:1-3; Isa 8:6; Yn 9:7Lango la Chemchemi lilikarabatiwa na Shalumu mwana wa Kolhoze, mtawala wa wilaya ya Mispa. Alilijenga upya, akaliezeka na kuweka milango yake, na makomeo na nondo mahali pake. Pia alikarabati ukuta wa Bwawa la Siloamu karibu na Bustani ya Mfalme, hadi kwenye ngazi zinazoshuka kutoka Mji wa Daudi. 163:16 Yos 15:58; Wim 3:7; Mdo 2:29Baada yake, Nehemia mwana wa Azbuki, mtawala wa nusu ya wilaya ya Beth-Suri, alikarabati kufikia mkabala na makaburi ya Daudi, mpaka kwenye bwawa lililotengenezwa, na kufikia Nyumba ya Mashujaa.

173:17 Yos 15:44Baada yake, ukarabati ulifanywa na Walawi chini ya uongozi wa Rehumu mwana wa Bani. Aliyefuatia ni Hashabia, mtawala wa nusu ya wilaya ya Keila, aliyekarabati sehemu ya wilaya yake. 183:18 Yos 15:44; 1Sam 23:1Baada yake, ukarabati ulifanywa na ndugu zao chini ya usimamizi wa Binui mwana wa Henadadi, mtawala wa nusu hiyo ingine ya wilaya ya Keila. 193:19 2Nya 26:9Baada yao, Ezeri mwana wa Yeshua, mtawala wa Mispa, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia ile sehemu inayotazamana na mwinuko wa kuelekea kwenye ghala la kuhifadhia silaha, mpaka kwenye pembe ya ukuta. 203:20 Mhu 9:10; Rum 12:11Baada yake, Baruku mwana wa Zakai alikarabati kwa bidii sehemu nyingine kuanzia ile pembe, mpaka kwenye lango la nyumba ya Eliashibu kuhani mkuu. 213:21 Ezr 8:33Kupakana naye, Meremothi mwana wa Uria, mwana wa Hakosi, alikarabati sehemu nyingine, kuanzia penye lango la nyumba ya Eliashibu mpaka mwisho wake.

22Baada yake, ukarabati ulifanywa na makuhani waliotoka eneo lililouzunguka mji. 23Baada yao Benyamini na Hashubu walikarabati mbele ya nyumba zao, na baada yao Azaria mwana wa Maaseya, mwana wa Anania alifanya ukarabati kando ya nyumba yake. 243:24 Yer 3:19; Ezr 8:33Baada yake, Binui mwana wa Henadadi alikarabati sehemu nyingine, kuanzia kwenye nyumba ya Azaria mpaka kwenye pembe ya ukuta. 253:25 Yer 32:2; 37:21; Ezr 2:3Naye Palali, mwana wa Uzai alijenga sehemu iliyokuwa mkabala na pembe ya ukuta, mpaka kwenye mnara wa juu ambao unajitokeza kuanzia kwenye jumba la kifalme, kando ya ua wa walinzi. Baada yake, Pedaya mwana wa Paroshi, 263:26 Ezr 2:43; Neh 7:46; 2Nya 33:14; Neh 12:37; 8:1-3na watumishi wa Hekalu walioishi juu ya kilima cha Ofeli walikarabati hadi kufikia mkabala na Lango la Maji, kuelekea mashariki na ule mnara uliojitokeza. 273:27 Za 48:12; Neh 3:5Baada yao, watu wa Tekoa walikarabati sehemu nyingine, kuanzia mnara mkubwa utokezao hadi ukuta wa Ofeli.

283:28 2Nya 23:15; Yer 31:40; 2Fal 11:16Makuhani walifanya ukarabati juu ya Lango la Farasi, kila mmoja mbele ya nyumba yake. 293:29 Yer 19:2Baada yao, Sadoki mwana wa Imeri alifanya ukarabati mkabala na nyumba yake. Baada yake, Shemaya mwana wa Shekania, mlinzi wa Lango la Mashariki, alifanya ukarabati. 30Baada yake, Hanania mwana wa Shelemia, na Hanuni mwana wa sita wa Salafu walikarabati sehemu nyingine. Baada yao, Meshulamu mwana wa Berekia alikarabati sehemu iliyokuwa mkabala na nyumba zake za kuishi. 31Baada yake Malkiya, mmoja wa masonara, alifanya ukarabati mpaka kwenye nyumba za watumishi wa Hekalu3:31 Yaani Wanethini. na wafanyabiashara, mkabala na Lango la Ukaguzi, hadi kufikia chumba kilicho juu ya pembe. 323:32 Neh 12:39; Yn 5:2Masonara na wafanyabiashara walifanya ukarabati kutoka chumba kilichoko juu ya pembe hadi Lango la Kondoo.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

尼希米记 3:1-32

重建耶路撒冷的城墙

1于是,大祭司以利亚实及其他祭司一起重建羊门,将它献给上帝,又安上门。他们重建城墙,一直建到哈米亚楼和哈楠业楼,并将它献给上帝。

2下一段由耶利哥人修建。

再下一段由音利的儿子撒刻修建。

3哈西拿的子孙修建鱼门,架上横梁,安上门,装上门闩和门锁。

4再下一段由哈哥斯的孙子、乌利亚的儿子米利末修筑。

再下一段由米示萨别的孙子、比利迦的儿子米书兰修筑。

再下一段由巴拿的儿子撒督修筑。

5再下一段由提哥亚人修筑,但他们的贵族不肯做督工所分派的工作。

6巴西亚的儿子耶何耶大比所玳的儿子米书兰修筑古门,架上横梁,安上门,装上门闩和门锁。

7再下一段由基遍米拉提米伦雅顿和其他基遍人,以及河西省省长管辖的米斯巴人修筑。

8再下一段由哈海雅的儿子金匠乌薛修筑。

再下一段由制造香料的哈拿尼雅修筑,他们修筑耶路撒冷的城墙,直到宽墙。

9再下一段由管理半个耶路撒冷户珥的儿子利法雅修筑。

10接下来,哈路抹的儿子耶大雅修筑他房子对面的那一段。

再下一段由哈沙尼的儿子哈突修筑。

11哈琳的儿子玛基雅巴哈·摩押的儿子哈述修筑另一段城墙,包括炉楼。

12再下一段由哈罗黑的儿子、管理另一半耶路撒冷沙龙和他的女儿们修筑。

13哈嫩撒挪亚的居民修筑谷门,安上门,装上门闩和门锁,之后又修建城墙四百四十五米,直到粪厂门。

14利甲的儿子、管理伯·哈基琳玛基雅修筑粪厂门,修好后安上门,装上门闩和门锁。

15各荷西的儿子、管理米斯巴沙仑修筑泉门,修好后盖上门顶,安上门,装上门闩和门锁。他还从靠近御花园的西罗亚池的城墙,一直修到大卫城下来的台阶处。

16再下一段由押卜的儿子、管理半个伯·夙尼希米修筑,他一直修到大卫墓地对面,远至人工池和勇士堂。

修筑城墙的利未人

17再下一段由巴尼的儿子利宏带领的利未人修筑。

接下来,管理半个基伊拉哈沙比雅修筑了自己的辖区。

18再下一段由他的同族兄弟、管理另一半基伊拉希拿达的儿子巴瓦伊修筑。

19再下一段由耶书亚的儿子、管理米斯巴以谢修筑,他从斜坡对面修到城墙转角的兵器库。

20再下一段由萨拜的儿子巴录修筑,他从城墙转角修到以利亚实大祭司的家门口。

21再下一段由哈哥斯的孙子、乌利亚的儿子米利末修筑,他从以利亚实家门口修到以利亚实家的尽头。

修筑城墙的祭司

22再下一段由住在周围郊区的祭司修筑。

23接下来,便雅悯哈述修筑自家对面的那一段。

再接下来,亚南尼的孙子、玛西雅的儿子亚撒利雅修筑自家旁边的那一段。

24再下一段由希拿达的儿子宾内修筑,他从亚撒利雅的房子修到城墙的转角。

25-26再接下来,乌赛的儿子巴拉修筑了城墙转角的对面和护卫院附近上宫凸出的城楼。

再下一段由巴录的儿子毗大雅与住在俄斐勒的殿役修筑,他们修到东面的水门对面和凸出的城楼那里。

其他修筑的人

27再下一段由提哥亚人修筑,他们从凸出来的大城楼对面修到俄斐勒的城墙。

28接下来,祭司修筑了马门以北的城墙,他们各自修筑自家对面的部分。

29再接下来,音麦的儿子撒督修筑自家对面的那一段。

再下一段由看守东门的、示迦尼的儿子示玛雅修筑。

30再下一段由示利米雅的儿子哈拿尼雅萨拉的第六个儿子哈嫩修筑。

接下来,比利迦的儿子米书兰修筑自家对面的那一段。

31再下一段由金匠玛基雅修筑,他修到哈米弗甲门对面的殿役和商人的房子,直到城的角楼。

32金匠和商人修筑从城的角楼到羊门的那一段。