Nehemia 10 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Nehemia 10:1-39

110:1 Neh 8:9; 1:1Wale waliotia muhuri walikuwa:

Nehemia mtawala, mwana wa Hakalia.

Sedekia, 210:2 Ezr 2:2Seraya, Azaria, Yeremia,

310:3 1Nya 9:12Pashuri, Amaria, Malkiya,

4Hatushi, Shebania, Maluki,

510:5 1Nya 24:8Harimu, Meremothi, Obadia,

6Danieli, Ginethoni, Baruku,

7Meshulamu, Abiya, Miyamini,

810:8 Neh 12:1Maazia, Bilgai na Shemaya.

Hawa ndio waliokuwa makuhani.

910:9 Neh 12:8Walawi:

Yeshua mwana wa Azania, Binui wa wana wa Henadadi, Kadmieli,

10na wenzao: Shebania,

Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani,

11Mika, Rehobu, Hashabia,

12Zakuri, Sherebia, Shebania,

13Hodia, Bani na Beninu.

14Viongozi wa watu:

Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani,

15Buni, Azgadi, Bebai,

1610:16 Ezr 8:6Adoniya, Bigwai, Adini,

17Ateri, Hezekia, Azuri,

18Hodia, Hashumu, Besai,

19Harifu, Anathothi, Nebai,

2010:20 1Nya 24:15Magpiashi, Meshulamu, Heziri,

21Meshezabeli, Sadoki, Yadua,

22Pelatia, Hanani, Anaya,

23Hoshea, Hanania, Hashubu,

24Haloheshi, Pilha, Shobeki,

25Rehumu, Hashabna, Maaseya,

26Ahiya, Hanani, Anani,

27Maluki, Harimu na Baana.

2810:28 Za 135:1; 1Nya 6:26; Neh 9:2; 13:3“Watu wengine wote, wakiwa ni makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, watumishi wa Hekalu,10:28 Yaani Wanethini. na wale wote waliojitenga na mataifa jirani kwa ajili ya Sheria ya Mungu, pamoja na wake zao na wana wao na binti zao wote waliokuwa na uwezo wa kufahamu, 2910:29 Hes 5:21; Neh 5:12; Kum 29:12basi hawa wote wanajiunga na ndugu zao na wakuu wao, na kujifunga kwa laana na kwa kiapo kufuata Sheria ya Mungu iliyotolewa kupitia kwa Mose mtumishi wa Mungu, na kutii kwa uangalifu amri zote, maagizo na sheria za Bwana, Bwana wetu.

3010:30 Kut 34:16; Kum 7:3; Mwa 6:2“Tunaahidi kutowaoza binti zetu kwa watu wanaotuzunguka, wala kuwaoza wana wetu binti zao.

3110:31 Eze 23:38; Amo 8:5; Neh 8:5; 13:15; Kut 23:11; Kum 15:1; Law 25:1-7“Wakati mataifa jirani waletapo bidhaa zao au nafaka kuuza siku ya Sabato, hatutazinunua kutoka kwao siku ya Sabato, wala siku nyingine yoyote takatifu. Kila mwaka wa saba, tutaacha kuilima ardhi na tutafuta madeni yote.

3210:32 Mwa 28:22“Tunakubali wajibu wa kutimiza amri za kutoa theluthi ya shekeli10:32 Theluthi ya shekeli hapa kama gramu 4. kila mwaka kwa ajili ya utumishi wa nyumba ya Mungu: 3310:33 Law 24:5-6; Hes 10:10; Za 81:3; 2Nya 24:5Kwa ajili ya mikate ya Wonyesho, kwa ajili ya sadaka za kawaida za nafaka na sadaka za kuteketezwa, kwa ajili ya sadaka za siku za Sabato, Sikukuu za Mwandamo wa Mwezi na sikukuu nyingine zilizoamriwa, kwa ajili ya sadaka takatifu, kwa ajili ya sadaka za dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, na kwa ajili ya kazi zote za nyumba ya Mungu wetu.

3410:34 Neh 13:31; Law 6:12; 16:8“Sisi makuhani, Walawi na watu, tumepiga kura kuamua kuwa kila mmoja wa jamaa zetu lazima alete katika nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati maalum kila mwaka mchango wa kuni za kukokea moto katika madhabahu ya Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Sheria.

3510:35 Kut 23:19; Hes 18:12; Kum 26:2“Pia tunachukua wajibu wa kuleta malimbuko ya mazao yetu na matunda ya kwanza ya kila mti wa matunda katika nyumba ya Bwana kila mwaka.

3610:36 Kut 13:2-12; Hes 18:14-16; Law 27:26-27“Kama pia ilivyoandikwa katika Sheria, tutawaleta wazaliwa wetu wa kwanza wa kiume, na wa mifugo yetu, yaani wa ngʼombe wetu na wa makundi yetu ya kondoo na mbuzi, katika nyumba ya Mungu wetu, kwa ajili ya makuhani wanaohudumu huko.

3710:37 Law 23:17; Hes 15:19; Law 27:30; Hes 18:21; Kum 14:22-29“Zaidi ya hayo, tutaleta katika ghala za nyumba ya Mungu wetu, kwa makuhani, vyakula vya kwanza vya mashamba yetu, sadaka zetu za nafaka, matunda ya miti yetu yote, divai yetu mpya na mafuta. Nasi tutaleta zaka za mazao yetu kwa Walawi, kwa kuwa Walawi ndio ambao hukusanya zaka katika miji yote tunakofanya kazi. 3810:38 Hes 18:26; 2Nya 31:11Kuhani atokanaye na uzao wa Aroni atashirikiana na Walawi wakati wanapopokea zaka, nao Walawi itawapasa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu katika ghala za hazina. 3910:39 Neh 13:10-12; Kum 12:6; Mt 18:20Watu wa Israeli pamoja na Walawi itawapasa kuleta michango yao ya nafaka, divai mpya na mafuta katika vyumba vya ghala, mahali vifaa vya mahali patakatifu vinapohifadhiwa, na wanapokaa makuhani wanaohudumu, na mabawabu na waimbaji.

“Hatutaacha kuijali nyumba ya Mungu wetu.”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

尼希米記 10:1-39

在約上蓋印的人

1在上面蓋印的有哈迦利亞的兒子尼希米省長,以及西底迦

2祭司有西萊雅亞撒利雅耶利米3巴施戶珥亞瑪利雅瑪基雅4哈突示巴尼瑪鹿5哈琳米利末俄巴底亞6但以理近頓巴錄7米書蘭亞比雅米雅民8瑪西亞璧該示瑪雅

9利未人有亞散尼的兒子耶書亞希拿達的子孫賓內甲篾10以及他們的弟兄示巴尼荷第雅基利他毗萊雅哈難11米迦利合哈沙比雅12撒刻示利比示巴尼13荷第雅巴尼比尼努

14民眾首領有巴錄巴哈·摩押以攔薩土巴尼15布尼押甲比拜16亞多尼雅比革瓦伊亞丁17亞特希西迦押朔18荷第雅哈順比賽19哈拉亞拿突尼拜20抹比押米書蘭希悉21米示薩別撒督押杜亞22毗拉提哈難亞奈雅23何細亞哈拿尼雅哈述24哈羅黑毗利哈朔百25利宏哈沙拿瑪西雅26亞希雅哈難亞南27瑪鹿哈琳巴拿

約的內容

28其餘的民眾、祭司、利未人、殿門守衛、歌樂手、殿役和所有與外族人隔離以便遵從上帝律法的人,以及他們的妻子和兒女等所有能夠明白的人, 29都跟隨他們的貴族同胞起誓要謹遵上帝藉祂僕人摩西頒佈的律法,遵守我們的主耶和華的一切誡命、典章和律例。 30我們不將女兒嫁給當地的人,也不為兒子娶當地的女子。 31如果這地方的居民在安息日或其他聖日帶來貨物和五穀要賣給我們,我們必不購買。我們每逢第七年必不耕種,也必不追討債務。

32我們為自己定下律例,每人每年捐獻四克銀子,供我們上帝的殿使用, 33以支付供餅、日常獻的素祭和燔祭,安息日、朔日10·33 朔日」即每月初一。和其他節期所獻的聖物,為以色列人獻上的贖罪祭,以及我們上帝殿中的各項費用。 34我們的祭司、利未人和民眾抽籤,決定每年哪一族要在指定的時間把獻祭時所需用的木材帶到我們上帝的殿裡,按照律法的規定燒在我們的上帝耶和華的壇上。 35我們把每年地裡初熟的物產和各種樹上初熟的果子獻到耶和華的殿裡。 36我們按照律法的規定獻上我們的長子和頭胎的牛羊,把他們帶到我們上帝的殿中,交給在那裡供職的祭司。 37我們把上好的麵團、舉祭、各樣果子、新酒和新油交給祭司,收進我們上帝殿的庫房裡,並把我們地裡收成的十分之一交給利未人,這是他們在我們所有城邑的出產中當收取的份。 38利未人收取十分之一的時候,要有亞倫子孫中的一位祭司陪同,利未人要從這十分之一中抽出十分之一帶到我們上帝的殿中,收進庫房裡。 39以色列人和利未人要將這些五穀、新酒和新油作為舉祭帶到收藏聖所器皿的地方,即供職的祭司、殿門守衛和歌樂手所住的房子。這樣,我們便不會忽略我們上帝的殿。