Nahumu 3 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Nahumu 3:1-19

Ole Wa Ninawi

13:1 Eze 22:2; Mik 3:10; Za 12:2Ole wa mji umwagao damu,

uliojaa uongo,

umejaa nyara,

usiokosa kuwa na vitu vya kuteka nyara.

23:2 Isa 34:3; Yer 47:3Kelele za mijeledi,

vishindo vya magurudumu,

farasi waendao mbio

na mshtuo wa magari ya vita!

3Wapanda farasi wanaenda mbio,

panga zinameremeta,

na mikuki inangʼaa!

Majeruhi wengi,

malundo ya maiti,

idadi kubwa ya miili isiyohesabika,

watu wanajikwaa juu ya mizoga:

43:4 Isa 47:9; 23:17; 2The 2:9, 10; Dan 2:2; Ufu 9:20, 21; Eze 16:25-29yote haya kwa sababu ya wingi wa tamaa za kahaba,

anayeshawishi, bibi wa mambo ya uchawi,

anayewatia utumwani mataifa kwa ukahaba wake

na pia jamaa za watu kwa ulozi wake.

53:5 Nah 2:13; Isa 47:2-3; 20:4; Yer 13:22Bwana Mwenye Nguvu Zote anasema,

“Mimi ni kinyume na ninyi.

Nitafunika uso wako kwa gauni lako.

Nitaonyesha mataifa uchi wako

na falme aibu yako.

63:6 Kut 29:14; Ay 9:31; 1Sam 2:30; Yer 51:37; Isa 14:16Nitakutupia uchafu,

nitakufanyia dharau

na kukufanya kioja.

73:7 Isa 13:14; 31:9; Nah 1:1; Ay 3:14; Yer 51:37Wote wanaokuona watakukimbia na kusema,

‘Ninawi ipo katika kuangamia:

ni nani atakayeomboleza kwa ajili yake?’

Nitampata wapi yeyote wa kukufariji?”

83:8 Amo 6:2; Yer 46:25; Isa 19:6-9Je, wewe ni bora kuliko No-Amoni,

uliopo katika Mto Naili,

uliozungukwa na maji?

Mto ulikuwa kinga yake,

nayo maji yalikuwa ukuta wake.

93:9 Mwa 10:6; 2Nya 12:3; Eze 27:10; 30:5Kushi3:9 Kushi ni Ethiopia. na Misri walikuwa nguvu zake zisizo na mpaka;

Putu na Libia walikuwa miongoni mwa wale walioungana naye.

103:10 Isa 20:4; 2Fal 8:12; Isa 13:16; Hos 13:16; Ay 6:26-27; Eze 24:6; Yer 40:1; Yoe 3:3; Oba 1:11Hata hivyo alichukuliwa mateka

na kwenda uhamishoni.

Watoto wake wachanga walivunjwa vunjwa vipande

kwenye mwanzo wa kila barabara.

Kura zilipigwa kwa watu wake wenye heshima,

na watu wake wote wakuu walifungwa kwa minyororo.

113:11 Isa 49:26; 2:10Wewe pia utalewa;

utakwenda mafichoni

na kutafuta kimbilio kutoka kwa adui.

123:12 Wim 2:13; Ufu 6:13; Isa 28:4Ngome zako zote ni kama mitini

yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva;

wakati inapotikiswa,

tini huanguka kwenye kinywa chake alaye.

133:13 Isa 19:16; 45:2; Yer 50:37; Nah 2:6Tazama vikosi vyako:

wote ni wanawake!

Malango ya nchi yako

yamekuwa wazi kwa adui zako;

moto umeteketeza mapingo yake.

143:14 2Nya 32:4; Nah 2:1Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako,

imarisha ulinzi wako,

Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi,

yakanyage matope,

karabati tanuru la kuchomea matofali!

153:15 Isa 27:1; 2Sam 2:26; Yer 51:14; Yoe 1:4Huko moto utakuteketeza,

huko upanga utakuangusha chini

na kama vile panzi, watakumaliza.

Ongezeka kama panzi,

ongezeka kama nzige!

163:16 Kut 10:13Umeongeza idadi ya wafanyabiashara wako

mpaka wamekuwa wengi kuliko nyota za angani,

lakini kama nzige wanaacha nchi tupu

kisha huruka na kwenda zake.

173:17 Ufu 9:7; Yer 51:17Walinzi wako ni kama nzige,

maafisa wako ni kama makundi ya nzige

watuao kwenye kuta wakati wa siku ya baridi:

lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao,

na hakuna ajuaye waendako.

183:18 Za 76:5-6; Yer 25:27; 50:18; Eze 31:3; Isa 56:10; 1Fal 22:17Ee mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wanasinzia;

wakuu wako wanalala chini mavumbini kupumzika.

Watu wako wametawanyika juu ya milima

bila kuwa na mtu yeyote wa kuwakusanya.

193:19 Yer 30:13; Mik 1:9; Ay 27:23; Mao 2:15; Sef 2:15; Isa 14:8; 37:18Hakuna kitu kinachoweza kuponya jeraha lako;

jeraha lako ni la kukuua.

Kila anayesikia habari zako,

hupiga makofi kwa kuanguka kwako,

kwa kuwa ni nani ambaye hajaguswa

na ukatili wako usio na mwisho?

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

那鸿书 3:1-19

尼尼微的灾祸

1充满血腥的尼尼微有祸了!

城中充满诡诈和暴力,

害人的事从未止息。

2鞭声啪啪,车轮隆隆,

战马奔腾,战车疾驰,

3骑士冲锋,刀光闪闪,矛枪生辉;

被杀者众多,尸骨成堆,

人们被遍地的尸体绊倒。

4这全是因为尼尼微像妖媚的妓女大肆淫乱,

惯行邪术,

以淫行诱惑列国,

靠邪术欺骗各族。

5万军之耶和华说:

“我要与你为敌。

我要把你的衣裙掀到你脸上,

使列国看见你的裸体,

使列邦看见你的羞耻。

6我要把可憎之物抛在你身上,

侮辱你,

让众人观看。

7凡看见你的都要逃避,说,

尼尼微毁灭了!

谁会为她悲伤呢?’

我到哪里去寻找安慰你的人呢?”

8你能强过底比斯3:8 底比斯”希伯来文是“挪亚们”。吗?

底比斯位于尼罗河上,

四面环水,

水是她的屏障,

又是她的城墙。

9古实埃及是她无穷的力量,

人和利比亚人是她的帮手。

10可是,她却被掳到远方,

她的婴孩被摔死在各个街头。

她的官长被抽签瓜分,

她所有的首领都被锁链锁着。

11尼尼微啊,

你也必像醉汉一样,

你必寻找藏身之处躲避敌人。

12你所有的堡垒都像无花果树上的初熟果子,

一摇树,果子就掉进吃的人口中。

13看啊,

你的军队就像柔弱的女人,

你境内的关口向敌人敞开,

你的门闩被火烧毁。

14你要蓄水以防围困,

要加强防御!

要走进土坑踩泥,

拿起砖模造砖!

15但在那里,火要吞噬你,

刀剑要杀戮你,

要像蝗虫吞没你。

你只管像蝗虫一样繁殖,

如蚱蜢一般增多吧!

16你的商贾多过天上的繁星,

但他们像吃光后飞去的蝗虫。

17你的臣仆像蝗虫,

你的将领像成群的蚱蜢。

它们寒日聚集在墙上,

太阳一出来就飞走了,

无人知道它们的行踪。

18亚述王啊!

你的牧人沉睡,贵族酣眠,

你的百姓分散在群山上,

无人招聚他们。

19你的创伤无法救治,

你的伤势极其严重。

听见这消息的人必鼓掌欢呼,

因为谁没受过你无休止的暴虐呢?