Mika 7 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mika 7:1-20

Taabu Ya Israeli

17:1 Yer 2:3; Hos 9:10; Wim 2:13Taabu gani hii niliyo nayo!

Nimefanana na yule akusanyaye

matunda ya kiangazi,

aokotaye masazo baada ya kuvunwa

shamba la mizabibu;

hakuna kishada chenye matunda ya kula,

hakuna hata ile tini ya mwanzoni ninayoitamani.

27:2 Za 10:8; 12:1; 57:6; Yer 2:29; 8:6; 5:26; Mit 6:17; 1Sam 24:11; Hab 1:15; Mik 3:10; Isa 3:5Wanaomcha Mungu wameondolewa kutoka nchi;

hakuna mtu mnyofu hata mmoja aliyebaki.

Watu wote wanavizia kumwaga damu,

kila mmoja anamwinda ndugu yake kwa wavu.

37:3 Mit 4:16; Kut 23:8; Hos 4:18; Isa 1:23; Eze 22:12Mikono yote miwili ni hodari katika kufanya ubaya,

mtawala anadai zawadi,

hakimu anapokea rushwa,

wenye nguvu wanaamuru wanachotaka:

wote wanafanya shauri baya pamoja.

47:4 Hes 33:55; Eze 2:6; Ay 31:14; 2Sam 23:6; Isa 22:5; Hos 9:7Aliye mwema kupita wote kati yao

ni kama mchongoma,

anayeonekana mnyofu zaidi miongoni mwao

ni mbaya kuliko uzio wa miiba.

Siku ya walinzi wako imewadia,

siku atakayokutembelea Mungu.

Sasa ni wakati wao

wa kuchanganyikiwa.

5Usimtumaini jirani;

usiweke matumaini kwa rafiki.

Hata kwa yule alalaye kifuani mwako

uwe mwangalifu kwa maneno yako.

67:6 Eze 22:7; Mwa 9:22-24; Mt 10:21, 35-36; Mk 13:12Kwa kuwa mwana humdharau baba yake,

naye binti huinuka dhidi ya mama yake,

mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake:

adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa.

77:7 Isa 21:8; 25:9; Za 4:3; 130:5Lakini mimi, namtazama Bwana kwa matumaini,

namngoja Mungu Mwokozi wangu;

Mungu wangu atanisikia mimi.

Israeli Atainuka

87:8 Za 20:8; 22:17; 37:24; 37:5, 6; Mit 24:17; Mik 4:11; Mao 4:21; 2Sam 22:29; Isa 9:2Usifurahie msiba wangu, ee adui yangu!

Ingawa nimeanguka, nitainuka.

Japo ninaketi gizani,

Bwana atakuwa nuru yangu.

97:9 Mao 3:39-40; Za 107:10; 119:154; Isa 46:13Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi yake,

nitabeba ghadhabu ya Bwana,

mpaka atakaponitetea shauri langu

na kuithibitisha haki yangu.

Atanileta nje kwenye mwanga,

nami nitaiona haki yake.

107:10 Za 35:26; 42:3; Isa 5:5; 51:23; Ay 40:12; Zek 10:5; 2Sam 22:43Kisha adui yangu ataliona

naye atafunikwa na aibu,

yule aliyeniambia,

“Yu wapi Bwana Mungu wako?”

Macho yangu yataona kuanguka kwake,

hata sasa atakanyagwa chini ya mguu

kama tope barabarani.

117:11 Amo 9:11; Isa 54:11Siku ya kujenga kuta zako itawadia,

siku ya kupanua mipaka yako.

127:12 Isa 19:23-25; 11:11; 60:4Siku hiyo watu watakuja kwako

kutoka Ashuru na miji ya Misri,

hata kutoka Misri hadi Frati

na kutoka bahari hadi bahari

na kutoka mlima hadi mlima.

137:13 Isa 3:10-11; Eze 12:19; 33:28-29Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake,

kwa sababu ya matunda ya matendo yao.

Sala Na Sifa

147:14 Za 23:4; 28:9; 95:7; Mik 5:4; 7:14; Hes 23:9; Kum 33:28; Wim 4:1; Isa 33:9; Yer 50:19; Eze 36:11Wachunge watu wako kwa fimbo yako,

kundi la urithi wako,

ambalo linaishi peke yake msituni,

katika nchi ya malisho yenye rutuba.

Waache walishe katika Bashani na Gileadi

kama ilivyokuwa siku za kale.

157:15 Kut 3:20; Za 78:12“Kama siku zile mlipotoka Misri,

nitawaonyesha maajabu yangu.”

167:16 Isa 26:11; Amu 18:19Mataifa yataona na kuaibika,

waliondolewa nguvu zao zote.

Wataweka mikono yao kwenye vinywa vyao

na masikio yao yatakuwa na uziwi.

177:17 Mwa 3:14; 2Sam 22:46; Isa 25:3; 59:19Wataramba mavumbi kama nyoka,

kama viumbe vitambaavyo juu ya ardhi.

Watatoka nje ya mapango yao wakitetemeka;

watamgeukia Bwana Mungu wetu kwa hofu

nao watakuogopa.

187:18 Kut 10:8; 1Sam 2:2; Isa 43:25; 54:9; 57:16; Zek 3:4; Yer 31:20; 50:20; Kut 15:11; 34:6, 7, 9; Za 89:6-8; 103:9; 2Nya 6:21; 30:9; Za 103:8-13; Yoe 2:32; Amo 5:15; Mik 2:12Ni nani Mungu kama wewe,

ambaye anaachilia dhambi

na kusamehe makosa

ya mabaki ya urithi wake?

Wewe huwi na hasira milele,

bali unafurahia kuonyesha rehema.

197:19 Isa 43:25; Rum 6:6; Yer 31:34Utatuhurumia tena,

utazikanyaga dhambi zetu

chini ya nyayo zako,

na kutupa maovu yetu yote

katika vilindi vya bahari.

207:20 Gal 3:16; Kum 11:29; 7:8; Lk 1:72; Za 108:4Utakuwa wa kweli kwa Yakobo,

nawe utamwonyesha Abrahamu rehema,

kama ulivyowaahidi kwa kiapo baba zetu

siku za kale.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

弥迦书 7:1-20

以色列的败坏

1我真悲惨!

就像夏天的果子已被收尽,

葡萄已被摘净,

找不到一串可吃的,

寻不见我心中渴望的初熟无花果。

2虔敬人已从大地上灭绝,

世间再没有正直人。

人人伺机杀人流血,

用网罗猎取自己的弟兄。

3他们善于作恶。

领袖和审判官索要贿赂,

显贵袒露心中的恶欲,朋比为奸。

4他们当中最好的不过是蒺藜,

最正直的也不过是荆棘篱笆。

你们的守望者所说的日子,

就是你们受惩罚的日子已经来到。

你们必惊慌失措。

5不要相信邻居,

不要信赖朋友,

即使对你怀中的妻子也要守口如瓶。

6因为儿子藐视父亲,

女儿与母亲作对,

媳妇与婆婆作对;

家人之间反目成仇。

7至于我,

我要仰望耶和华,

等候拯救我的上帝;

我的上帝必垂听我的祈求。

8我的仇敌啊,

你们不要对我幸灾乐祸!

我虽跌倒,但必再爬起来;

我虽坐在黑暗里,

但耶和华必做我的光。

9我得罪了耶和华,

所以要忍受祂的惩罚,

直到祂为我辩护,替我申冤。

祂必领我进入光明,

我必亲睹祂的公义。

10从前嘲笑我说“你的上帝耶和华在哪里”的仇敌看见这事,

都必满面羞愧。

我必亲眼看见他们遭到报应,

他们要像街上的泥土一样被人践踏。

11以色列啊,

终有一日你会重建自己的城墙。

到那日,你必扩张自己的疆域。

12那日,从亚述埃及的各城,

埃及幼发拉底河,

从天涯到海角7:12 从天涯到海角”希伯来文是“从海到海,从山到山”。

人们都要到你这里来。

13然而,大地要因地上居民的罪恶而荒凉。

14耶和华啊,

求你用你的杖牧放属于你的羊群,

就是你的子民。

他们独自居住在丛林中,

住在肥沃的田园间。

愿他们像从前一样在巴珊基列吃草。

15耶和华说:

“我要向他们显出神迹奇事,

就像他们离开埃及时一样。”

16列国看见这一切,

都必因自己势力衰微而羞愧,

都必用手捂口,耳朵变聋。

17他们要像蛇一样舔土,

又如地上的爬虫,

战战兢兢地走出营寨;

他们必畏惧我们的上帝耶和华,

他们必对你充满恐惧。

18有何神明像你一样赦免罪恶,

饶恕你幸存子民的过犯?

你不会永远发怒,

因为你乐于施恩。

19你必再怜悯我们,

将我们的罪恶践踏在脚下,

把我们的一切过犯抛进深海。

20你必按古时给我们列祖的誓言,

以信实待雅各

以慈爱待亚伯拉罕