Mika 5 – NEN & CST

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mika 5:1-15

Mtawala Aliyeahidiwa Kutoka Bethlehemu

15:1 Ay 16:10; Mt 27:30; Mao 3:30Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi,

kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu.

Watampiga mtawala wa Israeli

shavuni kwa fimbo.

25:2 Yn 7:42; Mwa 35:19; 48:7; 1Sam 13:14; Hes 24:19; 2Sam 6:21; 2Nya 7:18; Za 90:2; 132:6; 102:25; Isa 9:6; Mit 8:22; Yn 1:1; Mt 2:6“Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi,

ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda,

kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu

yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli,

ambaye asili yake ni kutoka zamani,

kutoka milele.”

35:3 Yer 7:29Kwa hiyo Israeli utaachwa mpaka wakati

mwanamke aliye na utungu atakapozaa

na ndugu zake wengine warudi

kujiunga na Waisraeli.

45:4 Isa 40:11; 49:9; 52:13; Za 72:8; Zek 9:10; Mik 7:14; Eze 34:11-15; Lk 1:32Atasimama na kulichunga kundi lake

katika nguvu ya Bwana,

katika utukufu wa jina la Bwana Mungu wake.

Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo

ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.

55:5 Isa 8:7; 9:6; 10:24-27; Lk 2:14; Efe 2:14; Kol 1:19-20Naye atakuwa amani yao.

Ukombozi Na Uharibifu

Wakati Mwashuru atakapovamia nchi yetu

na kupita katika ngome zetu,

tutawainua wachungaji saba dhidi yake,

hata viongozi wanane wa watu.

65:6 Mwa 10:8; Sef 2:13; Lk 1:71; Nah 2:11-13Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga,

nchi ya Nimrodi kwa upanga.

Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru

atakapoivamia nchi yetu

na kuingia katika mipaka yetu.

75:7 Amo 5:15; Mik 2:12; Isa 44:4; Za 110:3; 133:3Mabaki ya Yakobo yatakuwa

katikati ya mataifa mengi

kama umande kutoka kwa Bwana,

kama manyunyu juu ya majani,

ambayo hayamngoji mtu

wala kukawia kwa mwanadamu.

85:8 Mwa 49:9; Mik 4:13; Zek 10:5; Isa 5:29; Za 50:22; Hos 5:14Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa,

katikati ya mataifa mengi,

kama simba miongoni mwa wanyama wa msituni,

kama mwana simba miongoni

mwa makundi ya kondoo,

ambaye anaumiza vibaya na kuwararua

kila anapopita katikati yao,

wala hakuna awezaye kuokoa.

95:9 Za 10:12Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako,

nao adui zako wote wataangamizwa.

105:10 Kut 15:4, 19; Hos 14:3; Hag 2:22; Zek 9:10“Katika siku ile,” asema Bwana,

“nitaangamiza farasi zenu katikati yenu

na kubomoa magari yenu ya vita.

115:11 Kum 29:23; Isa 6:11; Mao 2:2; Hos 10:14; Amo 5:9Nitaiangamiza miji ya nchi yenu

na kuziangusha chini ngome zenu zote.

125:12 Kum 18:10-12; Isa 8:19; 2:9Nitaangamiza uchawi wenu

na hamtapiga tena ramli.

135:13 Nah 1:14; Hos 2:10; Isa 2:8; 2:18; Eze 6:9; Zek 13:2Nitaangamiza vinyago vyenu vya kuchonga

na mawe yenu ya ibada yatoke katikati yenu;

hamtasujudia tena

kazi ya mikono yenu.

145:14 Kut 34:13; Amu 3:7; 2Fal 17:10Nitangʼoa nguzo za Ashera katikati yenu

na kubomoa miji yenu.

155:15 Isa 65:12Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu

juu ya mataifa ambayo hayajanitii.”

Nueva Versión Internacional (Castilian)

Miqueas 5:1-15

Humillación y exaltación de la dinastía davídica

1Reagrupa tus tropas, ciudad guerrera,

porque nos asedian.

Con vara golpearán en la mejilla

al gobernante de Israel.

2Pero de ti, Belén Efrata,

pequeña entre los clanes de Judá,

saldrá el que gobernará a Israel;

sus orígenes se remontan hasta la antigüedad,

hasta tiempos inmemoriales.

3Por eso Dios los entregará al enemigo

hasta que tenga su hijo la que va a ser madre,

y vuelva junto al pueblo de Israel

el resto de sus hermanos.

4Pero surgirá uno para pastorearlos

con el poder del Señor,

con la majestad del nombre del Señor su Dios.

Vivirán seguros, porque él dominará

hasta los confines de la tierra.

5¡Él traerá la paz!

Si Asiria llega a invadir nuestro país

para pisotear nuestras fortalezas,

le haremos frente con siete pastores,

y aun con ocho líderes del pueblo;

6ellos pastorearán a Asiria con la espada;

con la daga, a la tierra de Nimrod.

Si Asiria llega a invadir nuestro país,

si llega a profanar nuestras fronteras,

¡él nos rescatará!

El remanente

7Será el remanente de Jacob,

en medio de muchos pueblos,

como rocío que viene del Señor,

como abundante lluvia sobre la hierba,

que no depende de los hombres,

ni espera nada de ellos.

8Será el remanente de Jacob entre las naciones,

en medio de muchos pueblos,

como un león entre los animales del bosque,

como un cachorro entre las ovejas del rebaño,

que al pasar las pisotea y las desgarra,

sin que nadie pueda rescatarlas.

9Levantarás la mano contra tus enemigos,

y acabarás con todos tus agresores.

Purificación de un pueblo idólatra y belicoso

10Esto afirma el Señor:

«En aquel día exterminaré tu caballería,

y destruiré tus carros de guerra.

11Exterminaré las ciudades de tu país

y derribaré todas tus fortalezas.

12Pondré fin a tus hechicerías

y no tendrás más adivinos.

13Acabaré con tus ídolos

y con tus monumentos sagrados;

nunca más volverás a postrarte

ante las obras de tus manos.

14Arrancaré tus imágenes de Aserá,

y reduciré a escombros tus ciudades;

15con ira y con furor me vengaré

de las naciones que no me obedecieron».