Marko 6 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Marko 6:1-56

Nabii Hana Heshima Kwao

(Mathayo 13:53-58; Luka 4:16-30)

16:1 Mt 2:23; 13:54; Lk 4:16Yesu akaondoka huko na kwenda mji wa kwao, akiwa amefuatana na wanafunzi wake. 26:2 Mk 1:21; Mt 4:23; 7:28Ilipofika siku ya Sabato, akaanza kufundisha katika sinagogi, na wengi waliomsikia wakashangaa.

Nao wakauliza, “Mtu huyu ameyapata wapi mambo haya yote? Tazama ni hekima ya namna gani hii aliyopewa? Tazama matendo ya miujiza ayafanyayo kwa mikono yake! 36:3 Mt 12:46; 11:6; Yn 6:61Huyu si yule seremala, mwana wa Maria? Na ndugu zake si Yakobo, Yose,6:3 Yosefu kwa Kiyunani ni Joses. Yuda na Simoni? Dada zake wote si tuko nao hapa kwetu?” Nao wakachukizwa sana kwa ajili yake, wakakataa kumwamini.

46:4 Lk 4:24; Yn 4:44Yesu akawaambia, “Nabii hakosi heshima isipokuwa katika mji wake mwenyewe, na miongoni mwa jamaa na ndugu zake, na nyumbani kwake.” 56:5 Mk 5:23; Mwa 19; 22; 32:25; Mt 13:58Hakufanya miujiza yoyote huko isipokuwa kuweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya. 66:6 Mt 9:35; Lk 13:22Naye akashangazwa sana kwa jinsi wasivyokuwa na imani.

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:5-15; Luka 9:1-6)

Kisha Yesu akawa anakwenda kutoka kijiji kimoja hadi kingine akifundisha. 76:7 Mk 3:13; Kum 17:6; Lk 10:1; Mt 10:1Akawaita wale kumi na wawili, akawatuma wawili wawili, na kuwapa mamlaka kutoa pepo wachafu.

8Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari isipokuwa fimbo tu. Msichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kwenye mikanda yenu. 96:9 Mdo 12:8Vaeni viatu, lakini msivae nguo ya ziada.” 106:10 Mt 10:11; Lk 9:4; 10:7, 8Akawaambia, “Mkiingia kwenye nyumba yoyote, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 116:11 Mt 10:14Kama mahali popote hawatawakaribisha wala kuwasikiliza, mtakapoondoka huko, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.”

126:12 Lk 9:6Kwa hiyo wakatoka na kuhubiri kwamba inawapasa watu kutubu na kuacha dhambi. 136:13 Yak 5:14Wakatoa pepo wachafu wengi, wakawapaka wagonjwa wengi mafuta na kuwaponya.

Yohana Mbatizaji Akatwa Kichwa

(Mathayo 14:1-12; Luka 9:7-9)

146:14 Mt 3:1Mfalme Herode akasikia habari hizi, kwa maana jina la Yesu lilikuwa limejulikana sana. Watu wengine walikuwa wakisema, “Yohana Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu, ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.”

156:15 Mal 4:5; Mt 2:11; 16:14; Mk 8:28Wengine wakasema, “Yeye ni Eliya.”

Nao wengine wakasema, “Yeye ni nabii, kama mmojawapo wa wale manabii wa zamani.”

166:16 Mt 14:2; Lk 3:19Lakini Herode aliposikia habari hizi, akasema, “Huyo ni Yohana Mbatizaji, niliyemkata kichwa, amefufuliwa kutoka kwa wafu!”

176:17 Mt 11:12; Lk 3:19-20Kwa kuwa Herode alikuwa ameagiza kwamba Yohana Mbatizaji akamatwe, afungwe na kutiwa gerezani. Alifanya hivi kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, ambaye Herode alikuwa amemwoa. 186:18 Law 18:16; 20:21Yohana alikuwa amemwambia Herode, “Si halali kwako kuwa na mke wa ndugu yako.” 19Kwa hiyo Herodia alikuwa amemwekea Yohana kinyongo akataka kumuua. Lakini hakuweza, 206:20 Mt 11:9; 21:26kwa sababu Herode alimwogopa Yohana akijua kwamba ni mtu mwenye haki na mtakatifu, hivyo akamlinda. Herode alifadhaika sana alipomsikia Yohana, lakini bado alipenda kumsikiliza.

216:21 Es 1:3; 2:18; Lk 3:1Mfalme Herode alifanya karamu kubwa wakati wa sikukuu ya kuzaliwa kwake. Akawaalika maafisa wake wakuu, majemadari wa jeshi na watu mashuhuri wa Galilaya. Hatimaye Herodia alipata wasaa aliokuwa akiutafuta. 22Binti yake Herodia alipoingia na kucheza, akamfurahisha Herode pamoja na wageni wake walioalikwa chakulani.

Mfalme Herode akamwambia yule binti, “Niombe kitu chochote utakacho, nami nitakupa.” 236:23 Es 5:3-6; 7:2Tena akamwahidi kwa kiapo, akamwambia, “Chochote utakachoomba nitakupa, hata kama ni nusu ya ufalme wangu.”

24Yule binti akatoka nje, akaenda kumuuliza mama yake, “Niombe nini?”

Mama yake akamjibu, “Omba kichwa cha Yohana Mbatizaji.”

25Yule binti akarudi haraka kwa mfalme, akamwambia, “Nataka unipe sasa hivi kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sinia.”

266:26 Mt 14:9Mfalme akasikitika sana, lakini kwa sababu alikuwa ameapa viapo mbele ya wageni wake, hakutaka kumkatalia. 27Mara mfalme akatuma askari mmojawapo wa walinzi wake kukileta kichwa cha Yohana. Akaenda na kumkata Yohana kichwa humo gerezani, 28akakileta kichwa chake kwenye sinia na kumpa yule msichana, naye yule msichana akampa mama yake. 29Wanafunzi wa Yohana walipopata habari hizi, wakaja na kuuchukua mwili wake, wakauzika kaburini.

Yesu Awalisha Wanaume 5,000

(Mathayo 14:13-21; Luka 9:10-17; Yohana 6:1-14)

306:30 Lk 24:10; Mdo 1:2, 26; Lk 9:10Wale mitume wakakusanyika kwa Yesu na kumpa taarifa ya mambo yote waliyokuwa wamefanya na kufundisha. 316:31 Mk 3:20Basi kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakawa hawana nafasi ya kula, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.”

326:32 Mk 6:45; 4:36Hivyo wakaondoka kwa mashua peke yao, wakaenda mahali pasipo na watu. 33Lakini watu wengi waliowaona wakiondoka, wakawatambua, nao wakaenda haraka kwa miguu kutoka miji yote, nao wakatangulia kufika. 346:34 Mt 9:36Yesu alipofika kando ya bahari, aliona makutano makubwa ya watu, akawahurumia kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.

356:35 Mk 8:1-9; Mt 14:15; Lk 9:11Mchana ulipokuwa umeendelea sana, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, nazo saa zimekwenda sana. 36Waage watu ili waende mashambani na vijijini jirani, wakajinunulie chakula.”

376:37 2Fal 4:42-44Lakini Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.”

Wakamwambia, “Je, twende tukanunue mikate ya dinari 2006:37 Dinari moja ilikuwa kama mshahara wa kibarua wa siku moja; hivyo dinari 200 ni sawa na mshahara wa siku 200. ili tuwape watu hawa wale?”

386:38 Mt 15:34; Mk 8:5Akawauliza, “Kuna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.”

Walipokwisha kujua wakarudi, wakamwambia, “Kuna mikate mitano na samaki wawili.”

39Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye majani, 40nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na wengine hamsini hamsini. 416:41 Mt 14:19Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. 42Watu wote wakala, wakashiba. 436:43 Kum 28:5Nao wanafunzi wake wakakusanya vipande vilivyosalia vya mikate na samaki, wakajaza vikapu kumi na viwili. 44Idadi ya wanaume waliokula walikuwa 5,000.

Yesu Atembea Juu Ya Maji

(Mathayo 14:22-33; Yohana 6:15-21)

456:45 Mt 11:21Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda Bethsaida, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 466:46 Lk 3:21Baada ya kuwaaga wale watu, akaenda mlimani kuomba.

476:47 Mt 14:23; Yn 6:16, 17Ilipofika jioni, ile mashua ilikuwa imefika katikati ya bahari, na Yesu alikuwa peke yake katika nchi kavu. 486:48 Lk 24:28Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Yesu akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, 496:49 Lk 24:27lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, 506:50 Lk 14:27kwa sababu wote walipomwona waliogopa.

Mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!” 516:51 Mk 6:32; 4:39Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa, 526:52 Mk 8:17-21kwa kuwa walikuwa hawajaelewa kuhusu ile mikate. Mioyo yao ilikuwa migumu.

536:53 Yn 6:24-25Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti, wakatia nanga. 54Mara waliposhuka kutoka mashua yao, watu wakamtambua Yesu. 55Wakaenda katika vijiji vyote upesi, wakawabeba wagonjwa kwenye mikeka ili kuwapeleka mahali popote waliposikia kuwa Yesu yupo. 566:56 Mt 9:20; Mk 5:27, 28; Mdo 19:12Kila mahali Yesu alipokwenda, iwe vijijini, mijini au mashambani, watu waliwaweka wagonjwa wao masokoni. Wakamwomba awaruhusu hao wagonjwa waguse japo upindo wa vazi lake. Nao wote waliomgusa waliponywa.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬可福音 6:1-56

拿撒勒人厭棄耶穌

1耶穌帶著門徒離開那地方,回到自己的家鄉。 2到了安息日,祂開始在會堂裡教導人,眾人聽了都很驚奇,說:「這個人從哪裡學來這些本領?祂怎麼會有這種智慧?祂怎麼能行這樣的神蹟? 3這不是那個木匠嗎?祂不是瑪麗亞的兒子嗎?祂不是雅各約西猶大西門的大哥嗎?祂的妹妹們不也住在我們這裡嗎?」他們就對祂很反感。

4耶穌對他們說:「先知到處受人尊敬,只有在本鄉、本族、本家例外。」 5耶穌不能在那裡行任何神蹟,只把手按在幾個病人身上,醫治了他們。 6他們的不信令耶穌詫異,於是祂就去周圍的村莊教導人。

差遣十二使徒

7耶穌召集了十二個使徒,差遣他們兩個兩個地出去,賜給他們制伏污鬼的權柄, 8又吩咐他們除了手杖之外,不用帶食物和背囊,腰包裡也不要帶錢, 9只穿一雙鞋子和一套衣服就夠了。 10祂說:「你們無論到哪裡,就住在那些接待你們的人家裡,一直住到離開。 11如果某地方的人不接待你們,不聽你們傳的道,你們在離開之前要跺掉腳上的塵土,作為對他們的警告!」

12使徒便出去傳道,勸人悔改, 13趕出許多鬼,為許多病人抹油,治好他們。

施洗者約翰遇害

14耶穌聲名遠播,希律王也聽說了祂的事。有人說:「施洗者約翰從死裡復活了,所以能夠行這些神蹟。」

15也有人說:「祂是先知以利亞。」

還有人說:「祂是個先知,跟古代的一位先知相似。」

16希律聽到這些議論,就說:「祂一定是被我斬了頭的約翰從死裡復活了。」 17原來希律娶了他兄弟腓力的妻子希羅底,並為她的緣故而派人逮捕了約翰,把他關押在監牢裡。 18因為約翰屢次對希律說:「你娶弟弟的妻子不合法。」

19希羅底約翰懷恨在心,想要殺掉他,只是不能得逞。 20因為希律知道約翰是個公義聖潔的人,所以敬畏他,並對他加以保護。儘管約翰所講的道理令他困惑不安,他仍然喜歡聽。

21機會終於來了。希律在自己的生日那天設宴招待文武百官和加利利的顯要。 22希羅底的女兒進來跳舞,甚得希律和客人的歡心。王對她說:「你想要什麼,只管說。」 23王還對她起誓說:「無論你要什麼,哪怕是我的半壁江山,我都會給你。」

24她便出去問她母親:「我應該要什麼呢?」

她母親說:「要施洗者約翰的頭!」

25她馬上回去對王說:「願王立刻把施洗者約翰的頭放在盤子裡送給我。」

26王聽了這個請求,感到十分為難,但因為在賓客面前起了誓言,就不好拒絕。 27他立刻命令衛兵進監牢砍了約翰的頭, 28放在盤子裡送給這女子,她又轉送給她母親。 29約翰的門徒聽到這個消息,就來把約翰的屍體領回去,安葬在墳墓裡。

耶穌使五千人吃飽

30使徒們聚集在耶穌身邊,向祂報告事工和傳道的經過。 31耶穌對他們說:「你們私下跟我到僻靜的地方去歇一會兒吧。」因為當時來來往往找他們的人實在太多,他們連吃飯的時間都沒有。

32他們乘船悄悄地到了一處僻靜的地方。 33可是有許多人看見他們離開,認出了他們,便從各城鎮步行趕往那裡,比他們先到達。 34耶穌一下船,看見這一大群人好像沒有牧人的羊,心裡憐憫他們,於是教導了他們許多道理。

35天色晚了,門徒過來對耶穌說:「時候已經不早了,這裡又是荒郊野外, 36請遣散眾人,好讓他們到周圍的村莊去自己買些吃的。」

37耶穌說:「你們給他們吃的吧。」

門徒說:「我們哪來這麼多錢買東西給他們吃啊?」

38耶穌說:「看看你們有多少餅。」

他們察看後,說:「有五個餅和兩條魚。」

39耶穌吩咐門徒叫大家分組坐在草地上。 40於是眾人坐下,有的五十人一組,有的一百人一組。 41耶穌拿起那五個餅、兩條魚,舉目望著天祝謝後,掰開遞給門徒,讓他們分給眾人。祂又照樣把那兩條魚分給眾人。 42大家都吃了,並且吃飽了。 43門徒把剩下的碎餅、碎魚收拾起來,裝滿了十二個籃子。 44當時吃餅的男人有五千。

耶穌在湖面上行走

45隨後,耶穌催門徒上船,叫他們先渡到湖對岸的伯賽大,祂則遣散眾人。 46祂辭別了眾人後,就上山去禱告。 47到了晚上,門徒的船在湖中心,耶穌獨自留在岸上。 48大約凌晨三點鐘,祂看見門徒在逆風中搖櫓,非常吃力,就從水面上朝門徒走去,想要從他們旁邊經過。 49門徒看見有人在湖面上走,以為是幽靈,嚇得驚叫起來。 50全船的人看見祂,都嚇壞了,耶穌立刻對他們說:「放心吧,是我,不要怕!」

51耶穌上了船,來到他們那裡,風便停了。門徒心裡十分驚奇, 52因為他們仍然不明白耶穌分餅那件事的意義,心裡還是愚頑。 53他們渡到湖對岸,來到革尼撒勒,在那裡靠岸, 54剛一下船,眾人立刻認出了耶穌。 55他們跑遍那一帶地方,用墊子把生病的人抬來,聽到耶穌在哪裡,就把病人抬到哪裡。 56耶穌不論到哪一個城市、鄉鎮和村莊,人們總是把病人抬到街市上,求耶穌讓他們摸一摸祂衣裳的穗邊,所有摸過的病人都好了。