Marko 4 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Marko 4:1-41

Mfano Wa Mpanzi

(Mathayo 13:1-9; Luka 8:4-8)

14:1 Mk 2:13; 3:7Yesu akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umekusanyika kumzunguka ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba ilimbidi Yesu aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari. 24:2 Mk 2:11; 3:23Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema: 34:3 Mk 4:26“Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. 4Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. 5Nyingine zilianguka kwenye ardhi yenye mwamba isiyo na udongo wa kutosha. Zikaota haraka, kwa kuwa udongo ulikuwa haba. 6Lakini jua lilipozidi, mimea ikanyauka na kukauka kwa kuwa mizizi yake haikuwa na kina. 7Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba hiyo ikakua, ikaisonga hiyo mimea, hivyo haikutoa mazao. 84:8 Yn 15:5; Kol 1:16Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikaota vizuri na kukua, zikatoa mazao, moja mara thelathini, nyingine mara sitini, na nyingine mara mia moja.”

94:9 Mk 4:23; Mt 11:15Kisha Yesu akasema, “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”

Sababu Za Mifano

(Mathayo 13:10-17; Luka 8:9-10)

104:10 Mt 13:10; Lk 8:9Alipokuwa peke yake, watu waliokuwepo naye pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili wakamuuliza kuhusu mifano yake. 114:11 Mt 3:2; 1The 4:12; 1Tim 3:7Naye akawaambia, “Ninyi mmepewa kujua siri ya Ufalme wa Mungu. Lakini kwa wale walioko nje, kila kitu husemwa kwao kwa mifano, 124:12 Isa 6:9-10; Mk 13:13-15ili,

“ ‘daima waone lakini wasitambue,

daima wasikie lakini wasielewe;

wasije wakageuka, wakatubu na kusamehewa!’ ”

Yesu Afafanua Maana Ya Mfano Wa Mbegu

(Mathayo 13:18-23; Luka 8:11-15)

13Kisha Yesu akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Basi mtaelewaje mifano mingine? 144:14 Mdo 16:6; Flp 1:14Yule mpanzi hupanda neno. 154:15 Mt 4:10Hawa ndio wale walio kando ya njia ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulinyakua lile neno lililopandwa ndani yao. 16Nazo zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, ni wale wanaolisikia neno, na mara hulipokea kwa furaha. 17Lakini kwa kuwa hawana mizizi, wao hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, mara wao huiacha imani. 18Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno; 194:19 1Tim 6:9-17; 1Yn 2:15-17lakini masumbufu ya maisha haya, na udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae. 20Wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri, hulisikia lile neno, wakalipokea na kuzaa mazao. Wao huzaa mara thelathini, au mara sitini, au mara mia ya mbegu iliyopandwa.”

Mfano Wa Taa

(Luka 8:16-18)

214:21 Mt 5:15Akawaambia, “Je, taa huwashwa na kufunikwa chini ya kikapu au mvunguni mwa kitanda? Je, haiwashwi na kuwekwa juu ya kinara chake? 224:22 Yer 16:17; Lk 12:2Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni. 234:23 Mk 4:9; Mt 11:15Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”

244:24 Mt 7:2; Lk 6:38Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi. 254:25 Mt 13:12; 25:29Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa.”

Mfano Wa Mbegu Inayoota

264:26 Mt 13:24Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. 274:27 Yak 5:7Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. 28Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke. 294:29 Ufu 14:15; Yoe 3:13Lakini nafaka inapokuwa imekomaa, mara mkulima huingia shambani na mundu wa kuvunia, maana mavuno yamekuwa tayari.”

Mfano Wa Mbegu Ya Haradali

(Mathayo 13:31-32, 34; Luka 13:18-19)

304:30 Mt 13:24Akawaambia tena, “Tuufananishe Ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuueleza? 31Ni kama punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini. 324:32 Dan 4:12, 21; Eze 17:23; 31; 6Lakini ikishaota, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote ya bustanini, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wanaweza kujenga viota kwenye matawi yake.”

334:33 Yn 16:25; Mt 13:34Kwa mifano mingine mingi kama hii Yesu alinena nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulielewa. 344:34 Yn 16:25Hakusema nao neno lolote pasipo mfano. Lakini alipokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu.

Yesu Atuliza Dhoruba

(Mathayo 8:23-27; Luka 8:22-25)

354:35 Mt 8:18, 23-27; Lk 8:22-25Siku hiyo ilipokaribia jioni, aliwaambia wanafunzi wake, “Tuvukeni twende mpaka ngʼambo.” 364:36 Mk 5:2, 21; 6:32, 45Wakauacha ule umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua nyingine nyingi pamoja naye. 37Kukawa na dhoruba kali, nayo mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikawa karibu kujaa maji. 38Yesu alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kama tunazama?”

39Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, “Uwe kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa.

404:40 Mt 14:31Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?”

41Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?”

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬可福音 4:1-41

撒種的比喻

1耶穌又到湖邊講道,周圍聚集了許多人,耶穌只好上到湖邊的船上坐下,眾人都站在岸上。 2耶穌用比喻教導他們許多事,在教導中祂說: 3「聽著!有一個農夫出去撒種。 4撒種的時候,有些種子落在路旁,被飛鳥吃掉了; 5有些落在石頭地上,因為泥土不深,種子很快就發芽了, 6然而因為沒有根,被太陽一曬就枯萎了; 7有些落在荊棘叢中,荊棘長起來便把嫩苗擠住了,以致不能結實; 8有些落在沃土裡,就發芽生長,結出果實,收成多達三十倍、六十倍、一百倍!」 9然後祂說:「有耳可聽的,都應當聽。」

10當耶穌獨自一人的時候,十二使徒和追隨祂的人來請教比喻的意思。 11耶穌說:「上帝國的奧祕只讓你們知道,對於外人,我只用比喻, 12使他們『看了又看,卻不領悟;聽了又聽,卻不明白,免得他們回心轉意,得到赦免。』」

13耶穌又對他們說:「你們不明白這個比喻,又怎能明白其他比喻呢? 14農夫撒的是上帝的道。 15種子落在路旁,是指人聽了道,撒旦立刻過來奪去了撒在他們心裡的道。 16種子落在石頭地上,是指人聽了道後,立刻歡喜地接受了, 17但他們心裡沒有根基,不過是暫時接受,一旦為道遭受患難和迫害,就立刻放棄了。 18種子落在荊棘叢中,是指人雖然聽過道, 19但生活的憂慮、錢財的迷惑和其他慾望把道擠住了,以致不能結出果實。 20種子落在沃土裡,是指人聽了道,領受了,又結出果實,收成多達三十倍、六十倍、甚至一百倍。」

燈的比喻

21耶穌繼續說:「人會把燈拿來放在籃子底下或床底下嗎?當然不會,他一定會把它放在燈臺上。 22隱藏的事是不能掩蓋的,終會顯露出來。 23有耳可聽的,就應當聽。」 24耶穌又說:「要好好思想你們所聽到的,你們用什麼量器量給人,就用什麼量器量給你們,甚至要多給你們。 25因為凡有的,還要給他更多;凡沒有的,連他僅有的也要奪去!」

種子生長的比喻

26祂又說:「上帝的國就像一個人在地上撒種。 27他天天日出而作,日落而息。種子就在他不知不覺中漸漸發芽長大。 28大地會使種子生長,先發苗後吐穗,最終結出飽滿的籽粒。 29莊稼成熟後,他就拿起鐮刀來收割,因為收成的時候到了。」

芥菜種的比喻

30耶穌說:「我們拿什麼比作上帝的國呢?用什麼比喻來解釋呢? 31上帝的國就像一粒芥菜種。它是種子中最小的, 32但種在地裡,卻能長得比各樣蔬菜都大,有粗大的枝條,可以讓飛鳥在它的樹蔭中築巢。」

33耶穌用了許多類似的比喻,按照眾人所能領悟的,把上帝的道講給他們聽。 34祂總是用比喻對他們講論,只有單獨和門徒在一起的時候,才把一切解釋清楚。

平息風浪

35那天晚上,耶穌對門徒說:「我們渡到對面去吧。」 36他們就離開眾人,上了耶穌乘坐的船,一起渡到湖的對岸,還有其他船隻跟著去。 37忽然,湖面上狂風大作,波浪撞擊船身,船內幾乎灌滿了水。 38耶穌卻還在船尾枕著枕頭睡覺。門徒叫醒了祂,說:「老師,我們快淹死了,你怎麼不管呢?」

39耶穌起來斥責狂風,對著湖面說:「靜下來!停下來!」於是就風平浪靜了。 40祂對門徒說:「你們為什麼這樣害怕呢?你們還是沒有信心嗎?」

41他們極其害怕,彼此議論說:「祂到底是誰?連風浪都聽祂的!」