Kutoka 4 – Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu) NEN

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 4:1-31

Ishara Za Mose

14:1 Kut 3:18Mose akamjibu, “Itakuwaje kama hawataniamini au kunisikiliza, waseme, ‘Bwana hakukutokea’?”

24:2 Mwa 38:18; Kut 7:19; 8:5; 14:16, 21; 17:5-9; Hes 17:2; 20:8; Yos 8:18; Amu 6:21; 1Sam 14:27; 2Fal 4:29Ndipo Bwana akamwambia, “Ni nini hicho kilicho mkononi mwako?”

Akajibu, “Fimbo.”

34:3 Kut 7:8-15Bwana akasema, “Itupe chini.”

Mose akaitupa chini hiyo fimbo nayo ikawa nyoka, naye akaikimbia. 4Kisha Bwana akamwambia, “Nyoosha mkono wako umkamate mkiani.” Basi Mose akanyoosha mkono akamkamata yule nyoka, naye akabadilika tena kuwa fimbo mkononi mwake. 54:5 Kut 3:6; 14:31; 19:9Bwana akasema, “Hivi ndivyo Waisraeli watakavyoamini kuwa Bwana, Mungu wa baba zao, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo, amekutokea wewe.”

64:6 Law 13:2, 11; Hes 12:10; Kum 24:9; 2Fal 5:1; 2Nya 26:21Kisha Bwana akamwambia, “Weka mkono wako ndani ya joho lako.” Basi Mose akaweka mkono wake ndani ya joho lake, naye alipoutoa, ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.

74:7 2Fal 5:14; Mt 8:3; Lk 17:12-14Mungu akamwambia, “Sasa urudishe tena huo mkono ndani ya joho lako.” Basi Mose akaurudisha mkono wake ndani ya joho lake na alipoutoa, ulikuwa mzima, kama sehemu zingine za mwili wake.

84:8 Kut 3:8; Amu 6:17; 1Fal 3:3; Isa 7:14; Yer 44:28-29Ndipo Bwana akamwambia, “Kama hawatakuamini wewe, au kutojali ishara ya kwanza, wataamini ishara ya pili. 94:9 Kut 7:17-21Lakini kama hawataamini ishara hizi mbili au hawatawasikiliza ninyi, chukua kiasi cha maji kutoka Mto Naili uyamimine juu ya ardhi kavu. Maji mtakayotoa mtoni yatakuwa damu juu ya ardhi.”

104:10 Kut 3:11Mose akamwambia Bwana, “Ee Bwana, kamwe sijapata kuwa msemaji kwa ufasaha wakati uliopita wala tangu ulipoanza kuzungumza na mtumishi wako. Ulimi wangu ni mzito kuzungumza.”

114:11 Kut 3:11; Lk 1:20, 64; Za 94:9; Mt 11:5; Yn 10:21Bwana akamwambia, “Ni nani aliyempa mwanadamu kinywa? Ni nani aliyemfanya mtu kuwa kiziwi au bubu? Ni nani anayempa mtu kuona au upofu? Je, si mimi, Bwana? 124:12 Kut 3:10; Hes 23:5; Kum 18:15-18; Isa 50:4; 51:16; Mt 10:19-20; Mk 13:11; Lk 12:12Sasa nenda, nitakusaidia kusema, nami nitakufundisha jambo la kusema.”

134:13 Yon 1:1-3Lakini Mose akasema, “Ee Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine kufanya kazi hiyo.”

144:14 Hes 11:1; 12:9; 16:15; 22:22; 24:10; 32:13; Kum 7:25; Ay 17:8; Yos 7:1; 1Sam 10:2-5Ndipo hasira ya Bwana ikawaka dhidi ya Mose, akamwambia, “Vipi kuhusu ndugu yako, Aroni Mlawi? Ninajua yeye anaweza kuzungumza vizuri. Naye yuko tayari njiani kukulaki, na moyo wake utafurahi wakati atakapokuona. 154:15 Hes 23:5, 12-16; Kum 18:18; Isa 51:16; 59:21; Yer 1:9; 31:33Utazungumza naye na kuweka maneno kinywani mwake. Nitawasaidia ninyi wawili kusema, nami nitawafundisha jambo la kufanya. 164:16 Kut 7:1-2; Yer 15:19; 36:6; Hes 33:1; Za 77:20; 105:26; Mik 6:4Aroni ataongea na watu badala yako na itakuwa kwamba yeye amekuwa kinywa chako nawe utakuwa kama Mungu kwake. 174:17 Kut 7:9-21; 8:5; 9:22; 10:12-15, 21-23; 14:15-26; 17:6; Hes 14:11; Kum 4:34; Za 74:9; 78:43; 105:27Lakini chukua fimbo hii mkononi mwako ili uweze kuitumia kufanya ishara hizo za ajabu.”

Mose Anarudi Misri

18Kisha Mose akarudi kwa Yethro mkwewe akamwambia, “Niruhusu nirudi kwa watu wangu Misri kuona kama yuko hata mmoja wao ambaye bado anaishi.”

Yethro akamwambia, “Nenda, nami nakutakia mema.”

194:19 Kut 2:15, 23; Mt 2:20Basi Bwana alikuwa amemwambia Mose huko Midiani, “Rudi Misri kwa maana watu wote waliotaka kukuua wamekufa.” 204:20 Kut 2:22; 18:3; Mdo 7:29Basi Mose akamchukua mkewe na wanawe, akawapandisha juu ya punda na kuanza safari kurudi Misri. Naye akaichukua ile fimbo ya Mungu mkononi mwake.

214:21 Kut 3:19, 20; 7:3, 13; 8:15, 32; 9:12, 17, 35; 10:20-27; 11:10; 14:4, 8; Kum 2:30; Yos 11:20; Za 105:25; Isa 6:10; 63:17; Yn 12:40; Rum 9:18Bwana akamwambia Mose, “Utakaporudi Misri, hakikisha kwamba utafanya mbele ya Farao maajabu yote niliyokupa uwezo wa kuyafanya. Lakini nitafanya moyo wake kuwa mgumu ili kwamba asiwaruhusu watu waende. 224:22 Mwa 10:15; Kum 32:6; Isa 9:6; 63:16; 64:8; Yer 3:19; 31:9; Hos 11:1; Mal 2:10; Rum 9:4; 2Kor 6:18Kisha mwambie Farao, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Israeli ni mwanangu mzaliwa wa kwanza, 234:23 Kut 3:18; 5:1; 7:16; 11:5; 12:12, 29; Mwa 49:3; Hes 8:17; 33:4; Za 78:51; 105:36; 135:8; 136:10nami nilikuambia, “Ruhusu mwanangu aondoke, ili aweze kuniabudu mimi.” Lakini ukakataa kumruhusu kwenda, basi nitaua mwana wako mzaliwa wa kwanza.’ ”

244:24 Hes 22:22Mose alipokuwa mahali pa kulala wageni akiwa njiani kurudi Misri, Bwana akakutana naye, akataka kumuua. 254:25 Kut 2:21; Mwa 17:14; Yos 5:2-3Lakini Sipora akachukua jiwe gumu, akakata govi la mwanawe na kugusa nalo miguu ya Mose. Sipora akasema, “Hakika wewe ni bwana arusi wa damu kwangu.” 26Sipora alipomwita Mose, “Bwana arusi wa damu,” alikuwa anamaanisha ile tohara. Baada ya hayo Bwana akamwacha.

274:27 Kut 3:1; Mwa 27:27; 29:13Bwana akamwambia Aroni, “Nenda jangwani ukamlaki Mose.” Basi akakutana na Mose kwenye mlima wa Mungu, akambusu. 28Kisha Mose akamwambia Aroni kila kitu Bwana alichomtuma kusema, vilevile habari za ishara na maajabu alizokuwa amemwamuru kufanya.

294:29 Kut 3:16Mose na Aroni wakawakusanya wazee wote wa Waisraeli, 30naye Aroni akawaambia kila kitu Bwana alichokuwa amemwambia Mose. Pia akafanya ishara mbele ya watu, 314:31 Kut 2:25; 3:18; Mwa 16:11; 24:26nao wakaamini. Nao waliposikia kuwa Bwana anajishughulisha nao, na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu.