Kutoka 34 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 34:1-35

Vibao Vipya Vya Mawe

(Kumbukumbu 10:1-5)

134:1 Kut 24:12; Kum 10:2-4; Kut 32:19Bwana akamwambia Mose, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, nami nitaandika juu yake maneno yale yaliyokuwa kwenye vile vibao vya kwanza, ulivyovivunja. 234:2 Kut 19:11Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. 334:3 Kut 19:13Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane mtu popote juu ya mlima, wala kondoo na mbuzi au ngʼombe wasilishe karibu mbele ya huo mlima.”

434:4 Kum 10:3; Kut 32:15Kwa hiyo Mose akachonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, naye akapanda juu ya Mlima Sinai asubuhi na mapema, kama Bwana alivyokuwa amemwagiza, akachukua vile vibao viwili vya mawe mikononi mwake. 534:5 Kut 13:21; 19:9; 6:3; 33:19Kisha Bwana akashuka katika wingu akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, Bwana. 634:6 Kut 22:27; Hes 14:20; Za 86:15; 78:18; Rum 2:4; Yer 15:15; Mwa 19:16; Za 61:7; Yoe 2:13; Mao 3:23; Yak 5:11; Hes 14:18Bwana akapita mbele ya Mose, akitangaza, “Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, 734:7 Kut 20:5-6; Kum 5:10; 1Fal 8:30; Za 86:5; 103:3; 130:4-8; Isa 43:25; Dan 9:9; 1Yn 1:9; Kut 23:7; Yos 24:19; Ay 7:20-21; 10:14; Mik 6:1-16; Nah 1:3akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.”

8Mara Mose akasujudu na kuabudu. 934:9 Kut 33:13-15; Hes 11:15; Kut 32:9; Hes 14:19; 1Fal 8:30; 2Nya 6:21; Za 19:12; 25:11; Yer 33:8; Hos 14:2; Kut 6:7; 19:5; Kum 4:20; 7:6; 9:26-29; 14:2; 26:18; 32:9; 1Sam 10:1; 2Sam 14:16; 1Fal 8:51, 53; Za 28:9; 33:12; 74:2; 79:1; 94:14; 106:5, 40; Isa 19:25; 63:17; Yer 10:16; 51:19; Mik 7:18; Zek 2:12Mose akasema, “Ee Bwana, kama nimepata kibali mbele zako, basi Bwana uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.”

Kufanya Agano Upya

(Kutoka 23:14-19; Kumbukumbu 7:1-5; 16:1-17)

1034:10 Mwa 6:18; 9:15; 15:15, 18; Kum 5:2-3; Kut 3:20; 33:16Kisha Bwana akasema: “Tazama ninafanya Agano mbele ya watu wako wote. Mbele ya watu wako wote nitafanya maajabu ambayo hayajafanyika katika taifa lolote katika ulimwengu wote. Watu wale mnaoishi miongoni mwao wataona jinsi ilivyo ya kushangaza ile kazi nitakayowafanyia mimi Bwana wenu. 1134:11 Kum 6:25; Yos 11:15; Kut 23:28; 32:2Tii yale ninayokuamuru leo. Tazama nawafukuza mbele yako Waamori, Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi. 1234:12 Amu 2:2; Kut 10:7; 23:32-33Uwe mwangalifu, usifanye agano na wale wanaokaa katika nchi ile unayoiendea, la sivyo watakuwa mtego katikati yako. 1334:13 Kut 23:24; Hes 33:52; Kum 7:5; 12:3; Amu 6:26; 1Fal 15:13; 2Nya 15:16; 17:6; 34:3-4; Mik 5:4Bomoa madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia na ukatekate nguzo zao za Ashera. 1434:14 Kut 20:3-4; Isa 9:6; Kum 4:24Usiabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu.

1534:15 Law 17:7; Hes 25:2; Kum 32:17; Za 106:37; Law 27:29; Kum 13:5; 17:2-5; 18:20; 2Nya 15:1334:15 Kum 23:6; Ezr 9:12; Kut 22:20; 32:8; Kum 31:16; Amu 2:17; 2Nya 17:8; 1Nya 17:8; 5:25; 2Nya 11:15; Amo 2:4; Kut 32:6; 1Kor 8:4“Uwe mwangalifu usifanye agano na wale watu wanaoishi katika nchi, kwa maana wakati wanapojifanyia ukahaba kwa miungu yao na kuwatolea kafara, watakualika wewe nawe utakula sadaka za matambiko yao. 1634:16 Kum 7:3; 17:17; Yos 23:12; Amu 3:6; 14:2-3; 1Fal 11:1-2; 16:31; Ezr 9:2; 10:3; Neh 10:30; 13:25-26; Kum 7:4; 12:31; 20:18; 1Fal 11:4; 2Fal 21:3-15; Za 106:34-41; Mal 2:11Unapowachagua baadhi ya binti zao kuwa wake wa wana wenu na binti hao wakajifanyia ukahaba kwa miungu yao, watawaongoza wana wenu kufanya vivyo hivyo.

1734:17 Kut 20:4; 32:8“Usijifanyie sanamu za kusubu.

1834:18 Kut 12:17; Mt 26:17; Lk 22:1; Mdo 12; Kut 12:15; 12:2“Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, kama nilivyokuamuru. Fanya hivi kwa wakati ulioamriwa, katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa kuwa katika mwezi huo ndipo wewe ulipotoka Misri.

1934:19 Kut 13:2“Mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo ni mali yangu, pamoja na wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa mifugo yako, ikiwa ni wa ngʼombe au wa kondoo au mbuzi. 2034:20 Kut 13:13; 13:2; 22:29; Kum 16:16; Eze 46:9Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume.

“Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu.

2134:21 Mwa 2:2-3; Neh 13:15; Isa 56:2; 58; 13; Lk 13:14“Kwa siku sita utafanya kazi, lakini siku ya saba utapumzika, hata ikiwa ni majira ya kulima au ya kuvuna lazima upumzike.

2234:22 Kut 23:19; Law 2:12-14; 7:13; 23:10, 17; Hes 28:26; Kut 23:14-16; 34:23“Utaadhimisha Sikukuu ya Majuma kwa malimbuko ya mavuno ya ngano, na Sikukuu ya Mavuno mwishoni mwa mwaka. 2334:23 Kut 23:14Mara tatu kwa mwaka wanaume wako wote watakuja mbele za Bwana Mwenyezi, Mungu wa Israeli. 2434:24 Kut 23:28; Kum 12:20; 19:8; Ay 12:23; Za 78:55Nitawafukuza mataifa mbele yako na kupanua mipaka ya nchi yako, wala hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yako wakati unapokwenda mara tatu kila mwaka kuonana na Bwana Mungu wako.

2534:25 Kut 23:18; 12:8-10“Usinitolee damu ya dhabihu pamoja na kitu chochote chenye chachu, wala usibakize dhabihu yoyote ya Sikukuu ya Pasaka mpaka asubuhi.

2634:26 Kut 22:29; Hes 18:12; Kut 23:19“Leta matunda ya kwanza yaliyo bora zaidi ya ardhi yako katika nyumba ya Bwana Mungu wako.

“Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.”

2734:27 Kut 17:14; Mwa 6:18; 15:18; Kut 24:4; Kum 31:9; Isa 30:8Kisha Bwana akamwambia Mose, “Andika maneno haya, kwa maana kulingana na maneno haya, nimefanya Agano na wewe pamoja na Israeli.” 2834:28 Mwa 7:4; Mt 4:2; Lk 4:2; Kum 9:9, 18; Kut 24:18; Ezr 10:6; Kut 31:18; Kum 4:13; 10:4Mose alikuwa huko pamoja na Bwana kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya Agano, yaani zile Amri Kumi.

Mngʼao Wa Uso Wa Mose

2934:29 Kut 19:11; 32:15; Za 34:5; Isa 60:5; Mt 17:2; 2Kor 3:7, 13Mose alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa ukingʼaa, kwa sababu alikuwa amezungumza na Bwana. 30Aroni na Waisraeli wote walipomwona Mose, kuwa uso wake unangʼaa, waliogopa kumkaribia. 3134:31 Kut 16:22Lakini Mose akawaita, kwa hiyo Aroni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao. 3234:32 Kut 21:1; 35:1-4Baadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote Bwana alizompa katika Mlima wa Sinai.

3334:33 2Kor 3:13Mose alipomaliza kuzungumza nao, akaweka utaji kwenye uso wake. 34Lakini kila wakati Mose alipoingia mbele za Bwana kuzungumza naye, aliondoa ule utaji mpaka alipotoka nje. Naye alipotoka nje na kuwaambia Waisraeli lile ambalo ameagizwa, 35waliona kuwa uso wake unangʼaa. Kisha Mose angeliweka tena utaji juu ya uso wake mpaka alipokwenda kuzungumza na Bwana.

King James Version

Exodus 34:1-35

1And the LORD said unto Moses, Hew thee two tables of stone like unto the first: and I will write upon these tables the words that were in the first tables, which thou brakest. 2And be ready in the morning, and come up in the morning unto mount Sinai, and present thyself there to me in the top of the mount. 3And no man shall come up with thee, neither let any man be seen throughout all the mount; neither let the flocks nor herds feed before that mount.

4¶ And he hewed two tables of stone like unto the first; and Moses rose up early in the morning, and went up unto mount Sinai, as the LORD had commanded him, and took in his hand the two tables of stone.

5And the LORD descended in the cloud, and stood with him there, and proclaimed the name of the LORD. 6And the LORD passed by before him, and proclaimed, The LORD, The LORD God, merciful and gracious, longsuffering, and abundant in goodness and truth, 7Keeping mercy for thousands, forgiving iniquity and transgression and sin, and that will by no means clear the guilty; visiting the iniquity of the fathers upon the children, and upon the children’s children, unto the third and to the fourth generation. 8And Moses made haste, and bowed his head toward the earth, and worshipped. 9And he said, If now I have found grace in thy sight, O Lord, let my Lord, I pray thee, go among us; for it is a stiffnecked people; and pardon our iniquity and our sin, and take us for thine inheritance.

10¶ And he said, Behold, I make a covenant: before all thy people I will do marvels, such as have not been done in all the earth, nor in any nation: and all the people among which thou art shall see the work of the LORD: for it is a terrible thing that I will do with thee. 11Observe thou that which I command thee this day: behold, I drive out before thee the Amorite, and the Canaanite, and the Hittite, and the Perizzite, and the Hivite, and the Jebusite. 12Take heed to thyself, lest thou make a covenant with the inhabitants of the land whither thou goest, lest it be for a snare in the midst of thee: 13But ye shall destroy their altars, break their images, and cut down their groves:34.13 images: Heb. statues 14For thou shalt worship no other god: for the LORD, whose name is Jealous, is a jealous God: 15Lest thou make a covenant with the inhabitants of the land, and they go a whoring after their gods, and do sacrifice unto their gods, and one call thee, and thou eat of his sacrifice; 16And thou take of their daughters unto thy sons, and their daughters go a whoring after their gods, and make thy sons go a whoring after their gods. 17Thou shalt make thee no molten gods.

18¶ The feast of unleavened bread shalt thou keep. Seven days thou shalt eat unleavened bread, as I commanded thee, in the time of the month Abib: for in the month Abib thou camest out from Egypt. 19All that openeth the matrix is mine; and every firstling among thy cattle, whether ox or sheep, that is male.34.19 sheep: or, kid 20But the firstling of an ass thou shalt redeem with a lamb: and if thou redeem him not, then shalt thou break his neck. All the firstborn of thy sons thou shalt redeem. And none shall appear before me empty.34.20 lamb: or, kid

21¶ Six days thou shalt work, but on the seventh day thou shalt rest: in earing time and in harvest thou shalt rest.

22¶ And thou shalt observe the feast of weeks, of the firstfruits of wheat harvest, and the feast of ingathering at the year’s end.34.22 year’s end: Heb. revolution of the year

23¶ Thrice in the year shall all your men children appear before the Lord GOD, the God of Israel. 24For I will cast out the nations before thee, and enlarge thy borders: neither shall any man desire thy land, when thou shalt go up to appear before the LORD thy God thrice in the year. 25Thou shalt not offer the blood of my sacrifice with leaven; neither shall the sacrifice of the feast of the passover be left unto the morning. 26The first of the firstfruits of thy land thou shalt bring unto the house of the LORD thy God. Thou shalt not seethe a kid in his mother’s milk. 27And the LORD said unto Moses, Write thou these words: for after the tenor of these words I have made a covenant with thee and with Israel.

28And he was there with the LORD forty days and forty nights; he did neither eat bread, nor drink water. And he wrote upon the tables the words of the covenant, the ten commandments.34.28 commandments: Heb. words

29¶ And it came to pass, when Moses came down from mount Sinai with the two tables of testimony in Moses’ hand, when he came down from the mount, that Moses wist not that the skin of his face shone while he talked with him. 30And when Aaron and all the children of Israel saw Moses, behold, the skin of his face shone; and they were afraid to come nigh him. 31And Moses called unto them; and Aaron and all the rulers of the congregation returned unto him: and Moses talked with them. 32And afterward all the children of Israel came nigh: and he gave them in commandment all that the LORD had spoken with him in mount Sinai. 33And till Moses had done speaking with them, he put a vail on his face. 34But when Moses went in before the LORD to speak with him, he took the vail off, until he came out. And he came out, and spake unto the children of Israel that which he was commanded. 35And the children of Israel saw the face of Moses, that the skin of Moses’ face shone: and Moses put the vail upon his face again, until he went in to speak with him.