Kutoka 20 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kutoka 20:1-26

Amri Kumi

(Kumbukumbu 5:1-21)

120:1 Kum 10:4; Neh 9:13; Za 119:9; 147:19; Mal 4:4Ndipo Mungu akasema maneno haya yote:

220:2 Mwa 17:7; Kut 16:12; Law 19:2; 20:7; Isa 43:3; Eze 20:19; Mwa 15:7; Kut 6:6; 13:3; Eze 20:6“Mimi ndimi Bwana Mungu wako, niliyekutoa Misri, kutoka nchi ya utumwa.

320:3 Kut 34:14; Kum 6:14; 13; 10; 2Fal 17:35; Za 44:20; 81:9; Yer 1:16; 7:6-9; 11:13; 19:4; 25:6Usiwe na miungu mingine ila mimi.

420:4 Kut 32:8; 34:17; Law 19:4; 26:1; Kum 4:15-23; 27:15; 2Sam 7:22; 1Fal 14:9; 2Fal 17:12; Isa 42:8; 44:9Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni, au duniani chini, au ndani ya maji. 520:5 Kut 23:13; Yos 23:7; Amu 6:10; 2Fal 17:35; Isa 44:15-19; 46:6; Kut 34:14; Kum 4:24; Yos 24:19; Mwa 9:25; Law 26:39; Kut 34:7; Hes 14:18; Yer 32:18Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 620:6 Kut 34:7; Hes 14:18; Kum 7:9; Yer 32:18; Lk 1:50; Rum 11:28lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

720:7 Kut 22:28; Law 18:21; 19:12; 22:2; 24:11, 16; Kum 6:13; 10:20; Ay 2:5-9; Za 63:11; Isa 8:21; Eze 20:39; 39:7; Mt 5:33Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa Bwana hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.

820:8 Kut 16:23; 31:13-16; 35:3; Law 19:3, 30; 26:2; Isa 56:2; Yer 17:21-27; Eze 22:8Ikumbuke siku ya Sabato, uitakase. 920:9 Kut 23:12; 31:13-17; 34:21; 35:2-3; Law 23:3; Lk 13:14Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote, 1020:10 Mwa 2:3; Kut 31:14; Law 23:38; Hes 28:9; Isa 56:2; Eze 20:12, 20lakini siku ya saba ni Sabato kwa Bwana Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wako wa kiume au wa kike, wala wanyama wako, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 1120:11 Mwa 1:3–2:1; 2:2; Kut 31:17; Eze 4:4Kwa kuwa kwa siku sita, Bwana aliumba mbingu na nchi, bahari na vyote vilivyomo, lakini akapumzika siku ya saba. Kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya Sabato na kuifanya takatifu.

1220:12 Kum 5:16; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2; Kum 6:2; Efe 6:3; Kum 11:9; 25:15; Yer 35:7Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Bwana Mungu wako.

1320:13 Mwa 4:23; Mt 5:21; 19:18; Lk 18:20; Rum 13:8-9; Yak 2:11Usiue.

1420:14 Law 18:20; 20:10; Hes 5:12, 13, 29; Mit 6:29-32; Mt 5:27; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11Usizini.

1520:15 Law 19:11-13; Eze 18:7; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9Usiibe.

1620:16 Law 19:11; Yer 9:3-5; Kut 23:1, 7; Law 19:18; Za 50:20; 101:5; 119:29; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 3:14; 18:20Usimshuhudie jirani yako uongo.

1720:17 Lk 12:15; Rum 7:7; 13:9; Efe 5:3; Ebr 13:5Usiitamani nyumba ya jirani yako. Usimtamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wa kiume au wa kike, wala ngʼombe wake au punda wake, wala chochote kile alicho nacho jirani yako.”

Watu Wanaogopa

(Kumbukumbu 5:22-33)

1820:18 Kut 19:16-19; Kum 4:36; Isa 58:1; Yer 6:17; Eze 33:3; Ebr 12:1-19; Ufu 1:10; Kut 19:18; Mwa 3:10; Kut 14:31; 19:16Watu walipoona ngurumo na radi, na kusikia mlio wa tarumbeta, na kuuona mlima katika moshi, walitetemeka kwa woga. Wakasimama mbali 1920:19 Ay 37:4-5; 40:9; Za 29:3-4; Kum 5:23-27; 18:16; Gal 3:19na wakamwambia Mose, “Sema nasi wewe mwenyewe, nasi tutakusikiliza. Lakini usimwache Mungu aseme nasi, la sivyo tutakufa.”

2020:20 Mwa 15:1; 22:1; Kum 4:10; 6:2; 10:12; Za 111:10; 128:1; Mit 1:7; Mhu 12:13; Isa 8:13; Ay 1:8; 2:3; 28:28; Mit 3:7; 8:13; 14:16; 16:6Mose akawaambia watu, “Msiogope! Mungu amekuja kuwajaribu, ili kwamba hofu ya Mungu iwakalie, msitende dhambi.”

2120:21 Kut 19:9; Kum 5:22; Za 81:8; 68:4; 97:2; Isa 19:1Watu wakabaki mbali, wakati Mose alipolisogelea lile giza nene mahali pale Mungu alipokuwa.

Sanamu Na Madhabahu

2220:22 Kum 5:24-26; Neh 9:13Kisha Bwana akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli hivi: ‘Mmejionea wenyewe kwamba nimesema nanyi kutoka mbinguni: 2320:23 Kut 22:20; 32:4, 8; 34:17; Kum 29:17-18; Neh 9:18Msijifanyizie miungu yoyote na kuilinganisha nami, msijitengenezee miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu.

2420:24 Kut 27:1; 40:29; Hes 16:38; Kum 27:5; Yos 8:30; 2Fal 16:14; 2Nya 4:1; Eze 43:13; Mwa 8:20; Kut 18:12; Kum 12:5; 16:6, 11; 26:2; 1Fal 9:3; 2Fal 21:4-7; 2Nya 6:6; 12:13; Ezr 6:12; Mwa 12:2; 22:17“ ‘Utanitengenezea madhabahu ya udongo, na juu yake utoe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani, kondoo zako, mbuzi na ngʼombe zako. Popote nitakapofanya Jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki. 2520:25 Yos 8:31; 1Fal 6:7Ikiwa unanitengenezea madhabahu ya mawe, usiijenge kwa mawe ya kuchonga, maana mkitumia chombo cha kuchongea mtaitia unajisi. 2620:26 Eze 43:17Msitumie ngazi kupandia kwenye madhabahu yangu, uchi wako usije ukadhihirika kwa chini.’

New International Version

Exodus 20:1-26

The Ten Commandments

1And God spoke all these words:

2“I am the Lord your God, who brought you out of Egypt, out of the land of slavery.

3“You shall have no other gods before20:3 Or besides me.

4“You shall not make for yourself an image in the form of anything in heaven above or on the earth beneath or in the waters below. 5You shall not bow down to them or worship them; for I, the Lord your God, am a jealous God, punishing the children for the sin of the parents to the third and fourth generation of those who hate me, 6but showing love to a thousand generations of those who love me and keep my commandments.

7“You shall not misuse the name of the Lord your God, for the Lord will not hold anyone guiltless who misuses his name.

8“Remember the Sabbath day by keeping it holy. 9Six days you shall labor and do all your work, 10but the seventh day is a sabbath to the Lord your God. On it you shall not do any work, neither you, nor your son or daughter, nor your male or female servant, nor your animals, nor any foreigner residing in your towns. 11For in six days the Lord made the heavens and the earth, the sea, and all that is in them, but he rested on the seventh day. Therefore the Lord blessed the Sabbath day and made it holy.

12“Honor your father and your mother, so that you may live long in the land the Lord your God is giving you.

13“You shall not murder.

14“You shall not commit adultery.

15“You shall not steal.

16“You shall not give false testimony against your neighbor.

17“You shall not covet your neighbor’s house. You shall not covet your neighbor’s wife, or his male or female servant, his ox or donkey, or anything that belongs to your neighbor.”

18When the people saw the thunder and lightning and heard the trumpet and saw the mountain in smoke, they trembled with fear. They stayed at a distance 19and said to Moses, “Speak to us yourself and we will listen. But do not have God speak to us or we will die.”

20Moses said to the people, “Do not be afraid. God has come to test you, so that the fear of God will be with you to keep you from sinning.”

21The people remained at a distance, while Moses approached the thick darkness where God was.

Idols and Altars

22Then the Lord said to Moses, “Tell the Israelites this: ‘You have seen for yourselves that I have spoken to you from heaven: 23Do not make any gods to be alongside me; do not make for yourselves gods of silver or gods of gold.

24“ ‘Make an altar of earth for me and sacrifice on it your burnt offerings and fellowship offerings, your sheep and goats and your cattle. Wherever I cause my name to be honored, I will come to you and bless you. 25If you make an altar of stones for me, do not build it with dressed stones, for you will defile it if you use a tool on it. 26And do not go up to my altar on steps, or your private parts may be exposed.’