Kumbukumbu 8 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kumbukumbu 8:1-20

Usimsahau Bwana

18:1 Kum 4:1; Kut 19:5; Ay 36:11; Za 16; 11; Eze 20:19Uwe mwangalifu kufuata kila agizo ninalokupa wewe leo, ili mweze kuishi, kuongezeka na mweze kuingia mkamiliki nchi ambayo Bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zenu. 28:2 Kum 29:5; Za 136:16; Amo 2:10; Mwa 22:1; Yos 6:17; 11:11; Kut 23:32; Amu 1:24; 2:2Kumbuka jinsi Bwana Mungu wenu alivyowaongoza katika njia yote katika jangwa kwa miaka hii arobaini, kukunyenyekeza na kukujaribu ili ajue lililoko moyoni mwako, kwamba utayashika maagizo yake au la. 38:3 Isa 2:11; Yer 44:10; Kut 16:14; 1Fal 8:36; Za 25:5; 94:12; 119:171; Mwa 3:19; Ay 23:12; Za 104:15; Mit 28:21; Isa 51:14; Yer 42:14; Ay 22:22; Za 119:13; 138:4; Kut 16:2-3; Mt 4:4; Lk 4:4Alikudhili na kukufanya uone njaa kisha akulishe kwa mana, ambayo wewe wala baba zako hamkuijua, awafundishe kuwa mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Bwana. 48:4 Kum 29:5; Neh 9:21Nguo zenu hazikuchakaa wala miguu yenu haikuvimba kwa miaka hii arobaini. 58:5 Kum 4:36; 2Sam 7:14; Ay 5:17; 33:19; Mit 3:11-12; Ebr 12:5-11; Ufu 3:19Mjue basi ndani ya mioyo yenu kama mtu anavyomwadibisha mwanawe, ndivyo Bwana Mungu wako atawaadibisha ninyi.

68:6 Kut 33:13; 1Fal 3:14; Za 81:13; 95:10; Kum 5:33Shikeni maagizo ya Bwana Mungu wenu mtembee katika njia zake na kumheshimu. 78:7 Za 106:24; Yer 3:19; Eze 20:6; Kum 11:9-12; Yer 2:7Kwa kuwa Bwana Mungu wenu anawaleta katika nchi nzuri, nchi yenye vijito na mabwawa ya maji, yenye chemchemi zinazotiririka mabondeni na katika vilima; 88:8 Kut 9:31; Mwa 49:11; Hes 13:23; 1Fal 4:25; Kum 32:13; Za 81:16nchi yenye ngano na shayiri, mizabibu na mitini, mikomamanga, mafuta ya zeituni na asali; 98:9 Amu 18:10; Ay 28:2nchi ambayo chakula hakitapungua na hamtakosa chochote; nchi ambayo miamba yake ni chuma na mnaweza kuchimba shaba kutoka kwenye vilima.

108:10 Kum 6:10-12Wakati mtakapokwisha kula na kushiba, msifuni Bwana Mungu wenu kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa. 118:11 Kum 4:9Jihadharini msimsahau Bwana Mungu wenu, mkashindwa kushika maagizo yake, sheria na amri zake ambazo ninawapa leo. 128:12 Mit 30:9; Hos 13:6Angalia wakati mtakapokuwa mmekula na kushiba, mkajenga nyumba nzuri na kukaa humo, 13na wakati makundi yenu ya ngʼombe na mbuzi na kondoo yatakapoongezeka na fedha na dhahabu yenu itakapoongezeka na vyote mlivyo navyo vitakapozidishwa, 148:14 Za 78:7; 106:21basi mioyo yenu isiwe na kiburi mkamsahau Bwana Mungu wenu aliyewatoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. 158:15 Kum 1:19; 32:13; 32:10; Hes 21:6; Isa 14:29; 30:6; Kut 17:6; Ay 28:9; Za 78:15; 114:8Aliwaongoza kupitia jangwa lile kubwa na la kutisha, nchi ile ya kiu isiyo na maji, yenye nyoka wa sumu na nge. Aliwatolea maji kutoka kwenye mwamba mgumu. 168:16 Kut 16:14; 16:15; Mwa 22:1; Rum 8:28; 2Kor 4:17; Ebr 12:11; Yak 1:12; 1Pet 1:7Aliwapa mana ya kula jangwani, kitu ambacho baba zenu hawakukijua, ili kuwanyenyekesha na kuwajaribu ninyi ili mwishoni apate kuwatendea mema. 178:17 Kum 9:4, 24; 31:27; Amu 7:2; Za 44:3; Isa 10:13Mnaweza kusema, “Uwezo wangu na nguvu za mikono yangu ndizo zilizonipatia utajiri huu.” 188:18 Mwa 26:13; Kum 26:10; 28:4; 1Sam 2:7; Za 25:13; 112:3; Mit 8:18; 10:22; Mhu 9:11; Hos 2:8Lakini kumbukeni Bwana Mungu wenu, ndiye ambaye huwapa uwezo wa kupata utajiri, na hivyo kulithibitisha Agano lake, ambalo aliwaapia baba zenu, kama ilivyo leo.

198:19 Kum 6:14; 4:26; 30:18; Za 16:4; Yer 7:6; 13:10; 25:6Ikiwa mtamsahau Bwana Mungu wenu, mkaifuata miungu mingine, mkaiabudu na kuisujudia, ninashuhudia dhidi yenu leo kwamba hakika mtaangamizwa. 208:20 2Fal 21:2; Za 10:16; Eze 5:5-17; Mao 1:1-22; 2:17; Dan 9:12; Zek 1:6Kama mataifa Bwana aliyoyaangamiza mbele yenu, ndivyo ninyi mtakavyoangamizwa kwa kutokumtii Bwana Mungu wenu.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

申命记 8:1-20

不可忘记耶和华

1“你们要谨遵我今日吩咐你们的一切诫命,以便能够存活,生养众多,并且得到耶和华起誓要赐给你们祖先的土地。 2要记住这四十年来你们的上帝耶和华怎样在旷野引领你们,祂磨炼你们、考验你们,好知道你们的心意如何、肯不肯遵守祂的诫命。 3祂让你们忍饥挨饿,然后赐给你们祖祖辈辈从未见过的吗哪吃,为了使你们明白人活着不是单靠食物,乃是靠祂口中的每一句话。 4这四十年来,你们的衣服没有穿破,双脚也没有走肿。 5你们心里要明白,你们的上帝耶和华管教你们,如同父亲管教儿子。

6“所以,你们要遵守你们的上帝耶和华的诫命,行祂的道,敬畏祂, 7因为祂要带你们到一个佳美之地。那里的谷中和山间流淌着条条溪流、股股清泉; 8那里盛产大麦、小麦、葡萄、无花果、石榴、橄榄油和蜂蜜; 9那里食物充足,一无所缺;那里矿产资源丰富,石头就是铁,山中可以采铜。 10你们吃饱喝足后,要赞美你们的上帝耶和华,因为祂赐给你们那佳美之地。

11“你们要谨慎,免得忘记你们的上帝耶和华,不遵守我今天吩咐你们的诫命、典章和律例。 12当你们丰衣足食、居室华美、 13牛羊众多、金银日增的时候, 14切勿心骄气傲,忘记你们的上帝耶和华。祂把你们从受奴役之地——埃及救出来, 15带领你们走过干旱、可怕、毒蛇和蝎子出没的大旷野。祂使坚硬的磐石流出水来给你们喝, 16在旷野中把你们祖先从未见过的吗哪赐给你们吃,为要磨炼你们、考验你们,使你们最终得到益处。 17你们切勿以为是凭自己的双手和能力致富的。 18要记住,是你们的上帝耶和华赐给你们致富的能力,为要坚立祂给你们祖先的誓约,正如今日的情形。

19“我今天警告你们,如果你们忘记你们的上帝耶和华,去追随、供奉、祭拜其他神明,你们必灭亡。 20如果你们不听从你们的上帝耶和华,你们必灭亡,正如祂使列国在你们面前灭亡一样。