Kumbukumbu 26 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kumbukumbu 26:1-19

Malimbuko Na Zaka

1Mtakapokuwa mmeingia nchi ile ambayo Bwana Mungu wenu anawapa kama urithi na mtakapokuwa mmeimiliki na kukaa ndani yake, 226:2 Kut 22:29; 20:24; Kum 12:5; Hes 18:12; Mit 3:9; Rum 6:23; Yak 1:18chukueni baadhi ya mavuno ya kwanza ya yale yote mtakayozalisha kutoka udongo wa nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa na mweke kwenye kapu. Kisha uende mahali ambapo Bwana Mungu wako atapachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina lake 3na umwambie kuhani atakayekuwepo kwa wakati huo, “Ninatangaza leo kwa Bwana Mungu wako kwamba nimekuja katika nchi ambayo Bwana aliwaapia baba zetu kwamba atatupa.” 4Kuhani atapokea lile kapu mikononi mwako na kuliweka chini mbele ya madhabahu ya Bwana Mungu wako. 526:5 Mwa 26:13; 25:20; 34:30; 43:14; 12:2; Hes 12:12; Kum 10:22Kisha utatangaza mbele za Bwana Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi. 626:6 Hes 20:15; Kut 1:13Lakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu. 726:7 Mwa 21:17; Kut 3:9; 2Fal 13:4; 14:26; Mwa 16:11; Za 42:9; 44:24; 72:14Kisha tulimlilia Bwana, Mungu wa baba zetu, naye Bwana akasikia sauti yetu na akaona huzuni yetu, taabu yetu na mateso yetu. 826:8 Hes 20:16; Kut 3:20; Kum 4:34; 34:11-12Kwa hiyo Bwana akatutoa nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, pamoja na utisho mkuu, ishara za miujiza na maajabu. 926:9 Kut 3:8Akatuleta mahali hapa akatupa nchi hii, nchi inayotiririka maziwa na asali; 1026:10 Kum 8:18nami sasa ninaleta malimbuko ya ardhi ambayo wewe, Ee Bwana, umenipa.” Weka kapu mbele za Bwana Mungu wako na usujudu mbele zake. 1126:11 Mit 10:2226:11 Kum 12:7, 12, 18; Mhu 5:18-20; Isa 65:14; Mdo 2:46, 47; Flp 4:4; 1Tim 6:17; Za 63:3, 5Kisha wewe pamoja na Walawi na wageni wote walioko miongoni mwenu mtafurahi katika vitu vyote vizuri ambavyo Bwana Mungu wenu amewapa pamoja na wa nyumbani mwenu.

1226:12 Mwa 14:20; Hes 18:24; Kum 14:28-29; Ebr 7:5-9; Law 27:30Wakati utakapokuwa umeshatoa zaka zote za mazao yako katika mwaka wa tatu, ambao ni mwaka wa zaka, utampa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, ili waweze kula katika miji yenu na kushiba. 1326:13 Za 119:141, 153, 176Kisha umwambie Bwana Mungu wako: “Nimeondoa katika nyumba yangu ile sehemu iliyowekwa wakfu na nimempa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, kulingana na yote uliyoamuru. Sijazihalifu amri zako wala kusahau hata mojawapo. 1426:14 Law 7:20; 21:1, 11; Hos 9:4Sijala sehemu iliyowekwa wakfu wakati nilipokuwa nikiomboleza, wala sijaondoa mojawapo wakati nilipokuwa najisi, wala sijatoa sehemu yake yoyote kwa wafu. Nimemtii Bwana Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoniamuru. 1526:15 Za 68:5; 80:14; 102:19; Isa 63:12; Zek 2:13; Kut 39:43; 2Nya 6:26-27; Mdo 7:49Angalia chini kutoka mbinguni, maskani yako matakatifu, uwabariki watu wako Israeli pamoja na nchi uliyotupa kama ulivyoahidi kwa kiapo kwa baba zetu, nchi inayotiririka maziwa na asali.”

Fuata Maagizo Ya Bwana

1626:16 Kum 4:29Bwana Mungu wako anakuagiza leo kufuata amri hizi na sheria; zishike kwa bidii kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. 1726:17 Kut 19:8; Za 48:14Umetangaza leo kwamba Bwana ndiye Mungu wako na kwamba utafuata njia zake, kwamba utayashika maagizo yake, amri zake na sheria zake nawe utamtii. 1826:18 Kut 6:7; Kum 7:6Naye Bwana ametangaza leo kwamba ninyi ni taifa lake, hazina yake ya thamani kama alivyoahidi, ili kwamba mpate kuyashika maagizo yake yote. 1926:19 Isa 62:7; Sef 3:20; Kum 4:7-8; 28:1, 13, 44; 1Nya 14:2; Za 148:14; Isa 40:11; Kum 7:4; Kut 19:6; 1Pet 2:9Ametangaza kwamba atawaweka juu kuliko mataifa mengine aliyoyafanya katika sifa, kuwa fahari na heshima, na kwamba mtakuwa taifa takatifu kwa Bwana Mungu wenu, kama alivyoahidi.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

申命记 26:1-19

奉献初熟的物产

1“你们进入你们的上帝耶和华将要赐给你们作产业的土地,征服那里,安居下来以后, 2要把在那里收获的各种初熟的物产放在篮子里,带到你们的上帝耶和华选定的敬拜场所。 3你们要对当值的祭司说,‘今天我们要向我们的上帝耶和华宣告,我们已经进入祂向我们祖先起誓要赐给我们的土地。’ 4祭司要从你们手中接过篮子,放在你们的上帝耶和华的祭坛前。 5你们要在你们的上帝耶和华面前宣告,‘我们的祖先原是到处流浪的亚兰人。他到埃及寄居时,家中人丁稀少,后来成为人口众多的强大民族。 6埃及人苦待我们,压迫我们,强迫我们做奴隶。 7于是,我们呼求我们祖先的上帝耶和华。祂听见我们的呼求,看见我们的艰难、困苦和所受的压迫, 8就伸出臂膀,用大能的手行神迹奇事,以伟大而可畏的作为带领我们离开埃及9祂带领我们来到这个地方,把这奶蜜之乡赐给我们。 10耶和华啊,现在我们从你赐给我们的土地上带来初熟的物产。’你们要把篮子放在你们的上帝耶和华面前,敬拜祂。 11你们和利未人以及住在你们中间的外族人,都要因你们的上帝耶和华赐给你们和你们家人的美物而欢喜快乐。

十一奉献年

12“每逢第三年是十一奉献年。你们应当把自己的十一奉献拿出来分给利未人、寄居者和孤儿寡妇,使他们在你们居住的城邑吃饱喝足。 13然后,你们要在你们的上帝耶和华面前宣告,‘我们已经按照你的诫命,从我们家里拿出圣物分给利未人、寄居者和孤儿寡妇。我们没有触犯也没有忘记你的任何诫命。 14这些圣物,我们守丧期间没有吃过,不洁净时没有拿过,也没有献给死人。我们听从你——我们的上帝耶和华,遵行你的一切吩咐。 15求你从天上圣洁的居所垂看,赐福给你的以色列子民和你赐给我们的土地——你向我们祖先起誓应许的奶蜜之乡。’

16“你们的上帝耶和华今天吩咐你们遵守这些律例和典章,你们要全心全意地谨慎遵守。 17你们今天已经宣称耶和华是你们的上帝,答应要听从祂,行祂的道,遵守祂的一切律例、诫命和典章。 18耶和华今天已经照祂的应许宣称你们是祂的子民,是祂宝贵的产业。因此,你们要遵守祂的一切诫命, 19这样祂必使你们备受赞誉和尊崇,超越祂所造的万国,并照着祂的应许使你们做属于祂的圣洁子民。”