Kumbukumbu 18 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kumbukumbu 18:1-22

Sadaka Kwa Makuhani Na Walawi

118:1 Yer 33:21; Hes 18:8, 20; 1Kor 9:13Makuhani ambao ni Walawi, yaani kabila lote la Lawi, hawatakuwa na mgawo wala urithi pamoja na Israeli. Wataishi kwa sadaka zitolewazo kwa ajili ya Bwana za kuteketezwa kwa moto, kwa maana huo ndio urithi wao. 218:2 Hes 18:20; Yos 13:14Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao; Bwana ndiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

318:3 Kut 29:27; Law 1:5; 7:28-34; Hes 18:12Hili ndilo fungu la makuhani kutoka kwa watu watakaotoa dhabihu ya fahali au kondoo: mguu wa mbele, mataya na matumbo. 418:4 Kut 22:29; Hes 18:12Mtawapa malimbuko ya nafaka zenu, divai mpya, mafuta na sufu ya kwanza kutoka manyoya ya kondoo zenu, 518:5 Kut 28:1; 29:9; Kum 10:8; Kut 29:9kwa kuwa Bwana Mungu wenu amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila yenu kusimama na kuhudumu katika jina la Bwana siku zote.

618:6 Hes 35:2-3; Kum 12:5Ikiwa Mlawi atahama kutoka mmojawapo ya miji yenu popote katika Israeli ambapo anaishi, akaja kwa moyo wote mahali ambapo Bwana atapachagua, 718:7 1Fal 18:32; 22:16; Za 118:26anaweza akahudumu katika jina la Bwana Mungu wake kama Walawi wenzake wote wanaohudumu hapo mbele za Bwana. 818:8 Hes 18:24; 2Nya 31:4; Neh 12:44, 47; 13:12Atashiriki sawa katika mafao yao, hata kama amepokea fedha kutoka mauzo ya mali ya jamaa yake.

Matendo Ya Machukizo

918:9 Kum 9:5; 12:29-31; Law 18:3; 2Fal 21:2; 2Nya 28:3; 33:2; 34:33; Ezr 6:21; 9:11; Yer 44:4Wakati mtakapoingia katika nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko. 1018:10 Law 18:21; 1Sam 15:23; Kut 7:11; Law 19:31; Kum 12:31Asionekane mtu yeyote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi, 1118:11 Isa 47:9; Kut 22:18; 1Sam 28:13wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu. 1218:12 Law 18:24; Kum 9:4Mtu yeyote afanyaye mambo haya ni chukizo kwa Bwana, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maana Bwana Mungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu. 1318:13 Mwa 6:9; 17:1; Za 119:1; Mt 5:48Kamwe msilaumiwe mbele za Bwana Mungu wenu.

Nabii

1418:14 2Fal 21:6Mataifa mtakayowafukuza husikiliza wale wafanyao ulozi na uaguzi. Lakini kwenu ninyi, Bwana Mungu wenu hajawaruhusu kufanya hivyo. 1518:15 Mt 21:11; Lk 2:25-35; Yn 1:21; Mdo 3:22; 7:37; Hes 24:17; Isa 11:1; 61:1; Mt 11:3; 21:11; Lk 2:25-34; 4:16-22; 7:16; 24:19; Yn 4:19-26; 6:14; 7:40Bwana Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msikilizeni yeye. 1618:16 Kut 20:19; Kum 5:23-27Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwomba Bwana Mungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti ya Bwana Mungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”

17Bwana akaniambia: “Wanachosema ni vyema. 1818:18 Mwa 20:7; Isa 2:3; 26:8; 51:4; Mik 4:2; Kut 4:12; Yn 4:25-26; 14:24; Mdo 3:22; Yn 17:8; 4:25; 8:28; 12:49, 50Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru. 1918:19 Kut 23:21; Law 19:12; 2Fal 2:24; Yos 22:23; Mdo 3:23; Ebr 12:25Kama mtu yeyote hatasikiliza maneno yangu ambayo huyo nabii atayasema kwa Jina langu, mimi mwenyewe nitamwajibisha. 2018:20 Kut 23:13; Kum 13:1-5; 17:12; Yer 14:14; 2:8; Zek 13:3Lakini nabii ambaye atathubutu kusema kwa Jina langu kitu chochote ambacho sikumwamuru akiseme, au nabii ambaye husema kwa jina la miungu mingine ni lazima auawe.”

21Mnaweza kuulizana wenyewe, “Tutawezaje kujua wakati ujumbe haukusemwa na Bwana?” 2218:22 Kum 13:2; 1Sam 3:20; 1Fal 22:28; Yer 28:9Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la Bwana hakikutokea au kutimia, huo ni ujumbe ambao Bwana hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

申命记 18:1-22

利未人的产业

1利未祭司及其他利未支派的人在以色列不可拥有土地。他们吃的是献给耶和华的火祭,那是他们的产业。 2他们在众支派中没有自己的产业,因为耶和华是他们的产业,这是祂的应许。 3众人所献的牛羊的前腿、腮颊和胃应归祭司。 4你们要给祭司初收的五谷、新酒、新油和初剪的羊毛。 5因为你们的上帝耶和华从各支派中拣选了利未人,让他们世代奉祂的名事奉。

6以色列境内任何地方的利未人若愿意离开自己所住的城,去耶和华选定的地方, 7他可以像在耶和华面前事奉的其他利未人一样,在那里事奉他的上帝耶和华。 8除了变卖产业所得之外,他还可以分到与其他祭司同等分量的祭物。

不可随从外族风俗

9“你们进入你们的上帝耶和华将要赐给你们的土地后,不可仿效当地民族的可憎行径。 10你们当中不可有人焚烧自己的子女作祭物,不可有人占卜、算命、作法、行邪术、 11念咒、做灵媒、行巫术或求问亡灵。 12凡做这些事的人都是耶和华所憎恶的。正是因为当地的民族做这些可憎之事,你们的上帝耶和华才要当着你们的面把他们赶走。 13你们要在你们的上帝耶和华面前纯全无过。

耶和华使一位先知兴起

14“你们将要赶走的那些民族听信术士和巫师,但你们的上帝耶和华不准你们仿效他们。 15你们的上帝耶和华要在你们中间选立一位像我一样的先知,你们要听从他。 16这正是你们在何烈山聚会时向你们的上帝耶和华所求的,当时你们说,‘不要让我们再听见我们上帝耶和华的声音,也不要让我们再看见这烈火,免得我们死亡。’ 17于是,耶和华对我说,‘他们说的对。 18我要在他们当中选立一位像你一样的先知,我会告诉他该说的话,他要把我的一切吩咐告诉他们。 19如果有人不听从他奉我的名所说的话,我必亲自惩罚那人。 20若有先知冒我的名说我未曾吩咐他的话,或以其他神明的名义说话,必须处死他。’ 21你们也许心里会问,‘我们如何知道是否是耶和华说的话呢?’ 22如果先知奉耶和华的名说的话没有应验,他的话就不是耶和华说的。他是妄自说预言,你们不用怕他。