Kumbukumbu 11 – NEN & JCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Kumbukumbu 11:1-32

Mpende Na Umtii Bwana

111:1 Kum 6:5; Law 8:35; Zek 3:7Mpende Bwana Mungu wako na kushika masharti yake, amri zake, sheria zake na maagizo yake siku zote. 211:2 Kum 31:13; Za 78:6; 136:12; Kum 3:24; 5:24; 8:5; Za 11:3; Kut 7:8-21Kumbuka hivi leo kwamba sio watoto wako walioona na kujua adhabu ya Bwana Mungu wako: utukufu wake, mkono wake wenye nguvu, mkono wake ulionyooshwa; 3ishara alizozifanya na mambo aliyoyafanya katikati ya Misri, kwa Farao mfalme wa Misri na kwa nchi yake yote; 411:4 Kut 15:1; 14:27; Hes 21:4lile alilolifanyia jeshi la Wamisri, farasi na magari yake, jinsi alivyowafurikisha na maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwafuatilia ninyi, na jinsi Bwana alivyowaletea angamizo la kudumu juu yao. 5Sio watoto wenu walioyaona yale Mungu aliyowafanyia huko jangwani mpaka mkafika mahali hapa, 611:6 Hes 16:1-35; Za 106:16-18; Isa 24:19wala lile Mungu alilowafanyia Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu wa kabila la Reubeni, wakati ardhi ilipofungua kinywa chake katikati ya Israeli yote, ikawameza pamoja na walio nyumbani mwao, hema zao na kila kitu kilichokuwa hai ambacho kilikuwa mali yao. 711:7 Kum 5:3Bali ilikuwa ni macho yenu wenyewe ambayo yaliyaona mambo haya yote makuu Bwana aliyoyatenda.

811:8 Ezr 9:10; Kum 31:6-7, 23; Yos 1:7Kwa hiyo fuateni maagizo yote ninayowapa leo, ili mpate kuwa na nguvu za kuingia na kuiteka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki, 911:9 Kum 5:16; 9:5; Kut 3:8; Mit 10:27; Kum 4:40; Mit 3:1, 26ili mpate kuishi siku nyingi katika nchi ile ambayo Bwana aliapa kuwapa baba zenu na wazao wao, nchi itiririkayo maziwa na asali. 1011:10 Isa 11:15; 37:25; Zek 8:7Nchi mnayoiingia kuimiliki haifanani na nchi ya Misri mlikotoka ambako mlipanda mbegu yenu na kuinywesha, kama bustani ya mboga. 1111:11 Eze 36:4; Kum 8:7; Neh 9:25Lakini nchi mnayovuka Yordani kuimiliki ni nchi ya milima na mabonde inywayo mvua kutoka mbinguni. 1211:12 1Fal 8:29; 9:3Ni nchi ambayo Bwana Mungu wenu anaitunza; macho ya Bwana Mungu wenu yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.

1311:13 Kum 6:17; 10:12; 4:29; Yer 17:24; 2The 3:5Hivyo kama mkiyatii maagizo yangu ninayowapa leo kwa uaminifu, yaani kwa kumpenda Bwana Mungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wako wote na kwa roho yenu yote, 1411:14 Law 26:4; Mdo 14:17; Za 147:8; Yer 3:3; Yoe 2:23; Yak 5:7; Yer 5:24ndipo atawanyweshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta. 1511:15 Za 104:14; Law 26:5; Kum 6:11; Za 104:14; Yoe 2:19Nitawapa majani kwa ajili ya ngʼombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

1611:16 Kum 4:19; 8:19; 29:18; Ay 31:9; 27Jihadharini, la sivyo mtashawishika kugeuka na kuabudu miungu mingine na kuisujudia. 1711:17 Kum 6:15; 9:19; 1Fal 17:1; 2Nya 6:26; 7:13; Law 26:20; Kum 4:26; 28:12, 24Ndipo hasira ya Bwana itawaka dhidi yenu, naye atafunga mbingu ili mvua isinyeshe nayo ardhi haitatoa mazao, nanyi mtaangamia mara katika nchi nzuri ambayo Bwana anawapa. 1811:18 Kut 13:9; Kum 6:6-8Yawekeni haya maneno yangu katika mioyo yenu na akili zenu, yafungeni kama alama juu ya mikono yenu na kwenye paji za nyuso zenu. 1911:19 Kut 12:26; Kum 6:7; Za 145:4; Isa 38:19; Yer 32:39; Kum 4:9-10Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni wakati mketipo nyumbani na wakati mtembeapo njiani, wakati mlalapo na wakati mwamkapo. 2011:20 Kum 6:9; Hab 2:2Yaandikeni juu ya miimo ya nyumba zenu na juu ya malango yenu, 2111:21 Ay 5:26; Mit 3:2; 4:10; 9:11; Za 72:5ili kwamba siku zenu na siku za watoto wenu zipate kuwa nyingi katika nchi ile Bwana aliyoapa kuwapa baba zenu, kama zilivyo nyingi siku za mbingu juu ya nchi.

2211:22 Kum 6:17; 6:5; 10:20Kama mkishika kwa makini maagizo haya yote ninayowapa kuyafuata, ya kumpenda Bwana Mungu wenu, kuenenda katika njia zake zote na kushikamana naye kwa uthabiti, 2311:23 Kum 9:5; 4:38; Kut 23:28; Kum 9:1ndipo Bwana atawafukuza mataifa haya yote mbele yako, nawe utawafukuza mataifa yaliyo makubwa na yenye nguvu kukuliko wewe. 2411:24 Mwa 15:18; Kum 1:36; 12:20; 19:8; Yos 1:3; 14:9; Mwa 2:14Kila mahali mtakapoweka mguu wenu patakuwa penu: Nchi yenu itaenea kutoka jangwa la Lebanoni, na kutoka mto wa Frati hadi bahari ya magharibi11:24 Yaani Bahari ya Mediterania. 2511:25 Kum 2:25; Kut 23:27; Kum 7:24Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama dhidi yenu. Bwana Mungu wenu, kama alivyoahidi, ataweka juu ya nchi yote utisho na hofu kwa ajili yenu popote mwendako.

2611:26 Za 24:5; Law 26:14-17; Kum 27:13-26; 30:1, 15, 19; Mao 2:17; Dan 9:11; Mal 3:9; 4:6Tazama, leo ninaweka mbele yenu baraka na laana: 2711:27 Kum 28:1-14; Za 24:5baraka kama mtatii maagizo ya Bwana Mungu wenu, ambayo ninawapa leo; 2811:28 2Nya 24:20; Yer 42:13; 44:16; Kum 4:28; 13:6-13; 29:26; 1Sam 26:19laana kama hamtatii maagizo ya Bwana Mungu wenu na kuacha njia ambayo ninawaamuru leo kwa kufuata miungu mingine, ambayo hamkuijua. 2911:29 Mwa 9:7; Kum 27:4; Yos 8:30; Kum 27:12-13; Yos 8:33; Yn 4:20Wakati Bwana Mungu wenu atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali. 3011:30 Mwa 12:6; Yos 4:19; 5:9; 9:6; 10:6; 14:6; 15:7; Amu 2:1; 2Fal 2:1; Mik 6:5; Hes 33:53; Kum 12:10; Yos 1:11; 11:23Kama mnavyofahamu, milima hii ipo ngʼambo ya Yordani, magharibi ya barabara, kuelekea machweo ya jua, karibu na miti mikubwa ya More, katika nchi ya wale Wakanaani wanaoishi Araba, jirani na Gilgali. 3111:31 Kum 28:1-14; Za 24:5Karibu mvuke ngʼambo ya Yordani kuingia na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa. Wakati mtakapokuwa mmeichukua na mnaishi humo, 32hakikisheni kwamba mnatii amri na sheria zote ninazoziweka mbele yenu leo.

Japanese Contemporary Bible

申命記 11:1-32

11

主を愛し、従え

1あなたの神、主を愛し、すべての命令に従いなさい。 2いいですか、私はあなたがたの子どもたちにではなく、あなたがた自身に話しているのです。子どもたちはまだ、主に罰せられたこともなく、その偉大さや恐ろしいまでの御力を見たこともありません。 3もちろん、主がエジプトの国や王に行った数々の奇跡も見ていません。 4エジプト軍がイスラエル人を追って来た時、主が彼らを馬や戦車もろとも紅海の底に沈め、それ以来エジプト人があなたがたに手出しできないようにされたことも見ていません。 5その後も、ここに来るまでの長い道中、荒野をさまようあなたがたを主が守り続けてこられたことも知りません。 6また、エリアブの子で、ルベンの孫に当たるダタンとアビラムが反逆したこと、そのためにイスラエル人全員の目の前で、彼らも家族も一人残らず、天幕(テント)もろとも地にのみ込まれてしまったことも、子どもたちは見ていません。

7しかし、あなたがたは違います。あの目をみはるような奇跡を確かに見たのです。 8だから、今日私が与える戒めをどんなに注意深く守らなければならないか、よくわかるはずです。そうして初めて、今、目前にしている地を占領できるのです。 9それを守れば、先祖以来約束されてきた地で、いつまでも幸せに暮らせます。そこは、乳とみつの流れる地なのです。 10エジプトのように灌漑する必要もありません。 11雨に恵まれ、丘や渓谷もある地だからです。 12あなたの神、主はあなたがたのことをいつも心にかけ、絶えずその地を見守ってくださいます。

13今日私が与えるすべての戒めを注意深く守り、心を尽くし、たましいを尽くして主を愛するなら、 14主は春と秋に必ず雨を降らせ、穀物も、ぶどう酒用のぶどうも、油を採るオリーブも豊かに実らせてくださいます。 15家畜には青々とした牧草地を、あなたがたには十分な食糧を与えてくださるのです。

16しかし、気持ちがゆるんで神様から離れ、外国の神々を拝んだりしないようにくれぐれも気をつけなさい。 17万一そんなことをしたら、主は激しくお怒りになり、雨を一滴も降らせないでしょう。収穫がなくなり、主が下さった良い地にいながら、みすみす飢え死にすることになります。 18そうなりたくなかったら、主のことばと戒めをしっかり心に刻みつけなさい。それをしるしとして手に結び、額に張りつけて絶えず覚えなさい。 19子どもたちにも教えなさい。家に座っているときも、外を歩いているときも、寝るときも、朝食の前にも話して聞かせなさい。 20家の門と戸に書き記しなさい。 21そうすれば、天地の続く限り、約束の地で子々孫々まで幸せに暮らせます。

22私が与える戒めをみな注意深く守り、主を愛し、主に頼って歩めば、 23どんなに強大な民であっても、主が必ず追い払ってくださいます。 24行く所はどこもあなたがたの土地になるのです。南はネゲブから北はレバノンまで、東と西はそれぞれユーフラテス川と地中海までも。 25だれ一人、あなたがたに太刀打ちできる者はいません。主はお約束どおり、行く先々で敵に恐れと不安を抱かせるからです。

26主の祝福を選ぶかのろいを選ぶか、今はっきり決めなさい。 27私が与える主の戒めに従うなら祝福されます。 28しかし、それを拒否し、外国の神々を拝んだりするならのろわれます。

29あなたの神、主が約束の地に導き入れてくださったら、ゲリジム山から祝福を、エバル山からのろいを宣言しなさい。 30どちらもカナン人が住むヨルダン川の西側の地域にある山で、ギルガルに近く、モレの樫の木のある荒野にそびえています。 31あなたがたは、これからヨルダン川を渡り、主が与えてくださる地に入るのです。 32だから、今日、私が与えるすべての律法を守りなさい。