Isaya 66 – NEN & HTB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 66:1-24

Hukumu Na Matumaini

166:1 2Nya 6:18; Mt 23:22; Mdo 17:24; 1Fal 8:27; Mt 5:34-35; Za 2:4; 2Sam 7:7Hili ndilo asemalo Bwana,

“Mbingu ni kiti changu cha enzi,

nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.

Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu?

Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?

266:2 Isa 40:26; Mdo 17:24; Ezr 9:4; Mit 28:14; Mdo 7:50; Isa 57:15; Mt 5:3-4; Lk 18:13-14Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,

hivyo vikapata kuwepo?”

asema Bwana.

“Mtu huyu ndiye ninayemthamini:

yeye ambaye ni mnyenyekevu

na mwenye roho yenye toba,

atetemekaye asikiapo neno langu.

366:3 Isa 1:11; Law 2:2; Isa 57:17; Kum 27:15; Eze 8:9-13Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali

ni kama yeye auaye mtu,

na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo,

ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa.

Yeyote atoaye sadaka ya nafaka,

ni kama yule aletaye damu ya nguruwe,

na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu,

ni kama yule aabuduye sanamu.

Wamejichagulia njia zao wenyewe,

nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao.

466:4 Mit 10:24; 1Sam 8:19; Mit 1:24; 2Fal 21:2-6; Isa 10:12; 41:28; 65:12Hivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali,

nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa.

Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu,

niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza.

Walifanya maovu machoni pangu

na kuchagua lile linalonichukiza.”

566:5 Za 38:20; Yn 15:18-21; Lk 13:17; Tit 2:13; Ezr 9:4; Isa 60:15; 44:9Sikieni neno la Bwana,

ninyi mtetemekao kwa neno lake:

“Ndugu zenu wanaowachukia ninyi

na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema,

Bwana na atukuzwe,

ili tupate kuona furaha yenu!’

Hata sasa wataaibika.

666:6 1Sam 2:10; Za 68:33; Law 26:28; Isa 65:6; Yoe 3:7Sikieni hizo ghasia kutoka mjini,

sikieni hizo kelele kutoka hekaluni!

Ni sauti ya Bwana ikiwalipa adui zake

yote wanayostahili.

766:7 Isa 54:1; Ufu 12:5“Kabla hajasikia utungu, alizaa;

kabla hajapata maumivu,

alizaa mtoto mwanaume.

866:8 Isa 64:4; Yer 18:13; Isa 49:20, 21Ni nani amepata kusikia jambo kama hili?

Ni nani amepata kuona mambo kama haya?

Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja,

au taifa laweza kutokea mara?

Mara Sayuni alipoona utungu,

alizaa watoto wake.

966:9 Isa 37:3Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa

na nisizalishe?” asema Bwana.

“Je, nifunge tumbo la uzazi

wakati mimi ndiye nizalishaye?”

asema Mungu wako.

1066:10 Kum 32:43; Rum 15:10; Za 26:8; Isa 25:9; 57:19; 61:2“Shangilieni pamoja na Yerusalemu na mfurahi kwa ajili yake,

ninyi nyote mnaompenda,

shangilieni kwa nguvu pamoja naye,

ninyi nyote mnaoomboleza juu yake.

1166:11 Hes 11:12; Isa 60:16; Mwa 49:25; Isa 25:6; Hes 25:1Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka

katika faraja ya matiti yake;

mtakunywa sana,

na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”

1266:12 Isa 33:21; 48:18; Hes 11:12; Isa 60:4-5; Za 72:3; 119:165; Isa 9:6Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:

“Nitamwongezea amani kama mto,

nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho;

utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake

na kubembelezwa magotini pake.

1366:13 Isa 40:1; 2Kor 1:4; 1The 2:7; Isa 49:15Kama mama anavyomfariji mtoto wake,

ndivyo nitakavyokufariji wewe,

nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”

1466:14 Eze 37:1; Isa 10:5; 30:27; 25:9; Za 72:16; Isa 54:17; 41:20Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia,

nanyi mtastawi kama majani;

mkono wa Bwana utajulikana kwa watumishi wake,

bali ghadhabu yake kali

itaonyeshwa kwa adui zake.

1566:15 2Fal 2:11; Za 68:17; Kum 28:20; Za 39:11; Isa 1:31; 42:25Tazama, Bwana anakuja na moto,

magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli,

atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali,

na karipio lake pamoja na miali ya moto.

1666:16 Amo 7:4; Eze 24:21; Isa 1:20; 30:30; 13:9-11; Yer 2:35; Eze 36:5; Isa 10:4Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake

Bwana atatekeleza hukumu juu ya watu wote,

nao wengi watakuwa ni wale

waliouawa na Bwana.

1766:17 Isa 65:3; Za 37:20; Isa 1:28-29; Law 11:7, 29“Watu wote wanaojiweka wakfu na kujitakasa wenyewe ili kwenda bustanini, wakimfuata aliye katikati ya wale ambao hula nyama za nguruwe na panya pamoja na vitu vingine vilivyo machukizo, watafikia mwisho wao pamoja,” asema Bwana.

1866:18 Mit 24:2; Isa 65:2; 2:3; Zek 12:3; Kut 16:17; Isa 59:19“Nami, kwa sababu ya matendo yao na mawazo yao, niko karibu kuja na kukusanya mataifa yote na lugha zote, nao watakuja na kuuona utukufu wangu.

1966:19 Lk 2:34; Isa 11:10-11; Mt 24:30; Eze 27:10; 1Nya 16:24; Isa 24:15; Yer 46:9“Nitaweka ishara katikati yao, nami nitapeleka baadhi ya hao walionusurika kwa mataifa, hadi Tarshishi, kwa Puli66:19 Puli hapa inamaanisha Libya. na Waludi (wanaojulikana kama wapiga upinde), kwa Tubali na Uyunani, hadi visiwa vya mbali ambavyo havijasikia juu ya sifa zangu au kuuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa. 2066:20 Isa 52:11; Rum 15:16; Yer 31:23; Eze 34:13; Kum 33:19; Yer 25:22Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka mataifa yote, mpaka kwenye mlima wangu mtakatifu katika Yerusalemu kama sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asema Bwana. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu la Bwana, katika vyombo safi kwa kufuata desturi za ibada. 2166:21 Kut 19:6; 1Pet 2:5-9Nami nitachagua baadhi yao pia wawe makuhani na Walawi,” asema Bwana.

2266:22 2Pet 3:13; Isa 65:17; 1Pet 1:4-5; Isa 48:19; Ebr 12:26-27; Yn 10:27-29“Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ninazozifanya zitakavyodumu mbele zangu,” asema Bwana, “ndivyo jina lenu na wazao wenu watakavyodumu. 2366:23 Eze 46:1-3; Ufu 15:4; Za 22:29; Zek 14:16; Isa 19:21; 44:5Kutoka Mwezi Mpya hata mwingine, na kutoka Sabato hadi nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asema Bwana. 2466:24 Isa 14:11; 1:31; Mt 25:41; Mk 9:48; Za 110:6; Isa 1:2“Nao watatoka nje na kuona maiti za wale walioniasi mimi. Funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa kitu cha kuchukiza sana kwa wanadamu wote.”

Het Boek

Jesaja 66:1-24

Gods zorgt voor zijn volk

1De hemel is mijn troon, zegt de Here, en de aarde mijn voetenbank, welke tempel kunt u voor Mij bouwen die Mij tot een huis zou kunnen zijn om daarin te wonen? 2Mijn hand heeft dat alles toch gemaakt, zij zijn mijn eigendom. Toch rust mijn oog op de man met een nederig en verslagen hart die beeft voor mijn woord. 3Maar zij die hun eigen wegen kiezen en behagen scheppen in hun zonden, zijn vervloekt. God zal hun offers niet aanvaarden. Als zulke mensen een os offeren op het altaar van God, is het net zo min aanvaardbaar voor Hem als een mensenoffer. Als zij een lam offeren of een graanoffer brengen, is dat voor God hetzelfde als wanneer zij een hond of het bloed van een zwijn op zijn altaar leggen! Als zij reukwerk voor Hem verbranden, rekent Hij hun dat aan alsof zij een afgod zegenen. 4Ik zal hun grootste angsten laten uitkomen, want toen Ik hen riep, weigerden zij te antwoorden en toen Ik tegen hen sprak, wilden zij niet luisteren. Integendeel, zij deden kwaad voor mijn ogen en kozen dát waarvan zij wisten dat Ik het verafschuwde.

5Luister naar de woorden van de Here, allen die Hem vrezen en beef voor zijn woorden: uw broers haten en verstoten u, omdat u trouw bent aan mijn naam. ‘Glorie aan God,’ spotten zij, ‘laat ons uw geluk in de Here maar eens zien!’ Zij zullen te schande worden gemaakt. 6Wat is dat voor een opschudding in de stad? Wat komt daar voor een vreselijk lawaai uit de tempel? Het is de stem van de Here, die vergelding over zijn vijanden brengt. 7-8 Wie heeft ooit zoiets vreemds gezien of gehoord? Want in één dag zal plotseling een volk, Israël, worden geboren, zelfs nog voordat de weeën zijn begonnen. Nauwelijks begon de pijn of de baby was er al. Het volk is ontstaan. 9Zou Ik de geboorte op gang brengen zonder dat een kind gebaard wordt? vraagt de Here, uw God. Nee! Nooit! 10Wees blij met Jeruzalem en verheug u met haar, allen die van haar houden en die om haar rouwden. 11Wees blij om Jeruzalem, drink met volle teugen van haar glorie zoals een kind drinkt en verzadigd wordt aan zijn moeders borst. 12Voorspoed zal Jeruzalem als een rivier overspoelen, zegt de Here, want Ik zal het sturen, de rijkdommen van andere volken zullen naar haar toestromen. Haar kinderen zullen aan haar borst worden gevoed, op haar heup worden gedragen en op haar schoot worden geknuffeld. 13Ik zal u daar troosten, zoals een kind wordt getroost door zijn moeder. 14Als u Jeruzalem ziet, zal uw hart blij zijn. U zult een stralende gezondheid krijgen. De hele wereld zal Gods goede hand op zijn volk zien rusten, evenals zijn toorn over zijn vijanden.

15Want kijk, de Here zal komen met vuur en snelle wagens van vervloeking en Hij zal zijn toorn als een vuur alles laten verbranden. 16Want de Here zal de wereld met vuur en met zijn zwaard straffen en het aantal slachtoffers zal groot zijn! 17Zij die afgoden aanbidden, verscholen achter een boom in de tuin en daar feestvieren met varkensvlees, muizen en ander verboden voedsel, zullen ellendig aan hun einde komen, zegt de Here. 18Ik zie heel goed wat zij doen, Ik weet wat zij denken, daarom is het tijd geworden alle volken rond Jeruzalem te verzamelen, waar zij mijn glorie zullen zien. 19Ik zal een machtig wonder onder hen doen en zij die aan het oordeel ontkomen, zal Ik als zendelingen uitzenden naar de volken: naar Tarsis, Pul, Tubal, Lud, Jawan en naar de landen overzee die niet hebben gehoord van mijn faam, noch mijn glorie hebben gezien. Daar zullen zij mijn glorie bekendmaken onder volken die Mij niet kennen. 20En zij zullen al uw broeders uit alle volken mee terugbrengen als een geschenk voor de Here, op paarden, in rijtuigen, op draagstoelen, muildieren en snelle kamelen, naar mijn heilige berg, naar Jeruzalem, zegt de Here. Het zal lijken op de offers die in de oogsttijd de tempel binnenstromen, gedragen in vaten, die aan de Here zijn gewijd. 21En Ik zal enkelen van hen die terugkeren, aanwijzen als mijn priesters en Levieten, zegt de Here. 22Zo zeker als mijn nieuwe hemel en aarde zullen bestaan, zo zeker zult u voor altijd mijn volk zijn, met een naam die nooit zal verdwijnen.

23De hele mensheid zal Mij week in, week uit, maand in, maand uit komen aanbidden. 24Zij zullen uitgaan en de dode lichamen zien van hen die tegen Mij opstonden, want de worm die aan hen knaagt zal nooit sterven, hun vuur zal niet doven en zij zullen een vreselijke aanblik vormen voor de hele mensheid.