Isaya 20 – NEN & NIVUK

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 20:1-6

Unabii Dhidi Ya Misri Na Kushi

120:1 2Fal 18:17; Yos 11:22; 13:3Katika mwaka ule ambao jemadari mkuu alitumwa na Mfalme Sargoni wa Ashuru, naye akaja mpaka Ashdodi, akaushambulia na kuuteka, 220:2 Zek 13:4; Mt 3:4; Isa 3:24; Eze 4:1-12; 24:17, 23; 1Sam 19:24; Isa 13:1; 1Fal 1:8; Mik 1:8wakati ule Bwana alisema kwa kinywa cha Isaya mwana wa Amozi. Akamwambia, “Vua nguo ya gunia kutoka mwilini mwako na viatu kutoka miguuni mwako.” Naye akafanya hivyo, akatembea huku na huko uchi, bila viatu.

320:3 Kut 3:12; Yer 7:25; Isa 8:18; 22:20; 41:8-9; Mwa 10:6; Mdo 21:11Kisha Bwana akasema, “Kama vile mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na bila viatu kwa miaka mitatu, kama ishara na dalili mbaya dhidi ya nchi ya Misri na Kushi, 420:4 Yer 13:22-26; Isa 19:4; 47:3; Nah 3:5; Yer 46:19; 2Sam 10:4; Ay 12:17vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawaongoza mateka wa Wamisri, na watu wa uhamisho wa Kushi, uchi na bila viatu, vijana hata wazee, wakiwa matako wazi, kwa aibu ya Wamisri. 520:5 2Fal 18:21; Isa 31:1-3; 8:12; 30:5; Eze 29:16Wale waliotegemea Kushi na kujivunia Misri wataogopa na kuaibika. 620:6 Isa 10:3; 2:11Katika siku ile watu wanaoishi katika pwani hii watasema, ‘Tazama lililowapata wale tuliowategemea, wale tuliowakimbilia kwa msaada na wokovu kutoka mikononi mwa mfalme wa Ashuru! Tutawezaje basi kupona?’ ”

New International Version – UK

Isaiah 20:1-6

A prophecy against Egypt and Cush

1In the year that the supreme commander, sent by Sargon king of Assyria, came to Ashdod and attacked and captured it – 2at that time the Lord spoke through Isaiah son of Amoz. He said to him, ‘Take off the sackcloth from your body and the sandals from your feet.’ And he did so, going around stripped and barefoot.

3Then the Lord said, ‘Just as my servant Isaiah has gone stripped and barefoot for three years, as a sign and portent against Egypt and Cush,20:3 That is, the upper Nile region; also in verse 5 4so the king of Assyria will lead away stripped and barefoot the Egyptian captives and Cushite exiles, young and old, with buttocks bared – to Egypt’s shame. 5Those who trusted in Cush and boasted in Egypt will be dismayed and put to shame. 6In that day the people who live on this coast will say, “See what has happened to those we relied on, those we fled to for help and deliverance from the king of Assyria! How then can we escape?” ’