Hosea 1 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hosea 1:1-11

11:1 Mik 1:1; Isa 1:1; 2Fal 13:13; 14:12; 1Nya 3:12-13; Yer 1:2; 2Fal 14:21Neno la Bwana lililomjia Hosea mwana wa Beeri wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, na wakati wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi, mfalme wa Israeli.

Mke Wa Hosea Na Watoto

21:2 Amu 2:17; Yer 3:14; Hos 2:5; 3:1; Yer 3:1; Kum 31:16Wakati Bwana alipoanza kuzungumza kupitia Hosea, Bwana alimwambia, “Nenda ukajitwalie mwanamke wa uzinzi na watoto wa uzinzi, kwa sababu nchi ina hatia ya uzinzi wa kupindukia kwa kumwacha Bwana.” 31:3 Hos 1:6Kwa hiyo alimwoa Gomeri binti Diblaimu, naye akachukua mimba na kumzalia Hosea mwana.

41:4 1Sam 29:1; 1Fal 18:45; 2Fal 10:1-14; Hos 2:22Kisha Bwana akamwambia Hosea, “Mwite Yezreeli,1:4 Yezreeli maana yake Mungu hupanda. kwa kuwa kitambo kidogo nitaiadhibu nyumba ya Yehu kwa ajili ya mauaji ya kule Yezreeli, nami nitaukomesha ufalme wa Israeli. 51:5 Yos 15:56; 1Sam 29:1; 2Fal 15:29Katika siku ile nitavunja upinde wa Israeli katika Bonde la Yezreeli.”

61:6 Hos 2:4, 23; 1:6Gomeri akachukua tena mimba akamzaa binti. Kisha Bwana akamwambia Hosea, “Mwite Lo-Ruhama,1:6 Lo-Ruhama maana yake Sio mpenzi wangu. kwa maana sitaonyesha tena upendo kwa nyumba ya Israeli, kwamba nisije kabisa nikawasamehe. 71:7 Za 44:6; Zek 2:6Hata hivyo nitaonyesha upendo kwa nyumba ya Yuda, nami nitawaokoa si kwa upinde, upanga au vita, wala kwa farasi na wapanda farasi, bali kwa njia ya Bwana Mungu wao.”

8Baada ya Gomeri kumwachisha Lo-Ruhama kunyonya, Gomeri alipata mwana mwingine. 91:9 Eze 11:19-20; 1Pet 2:10Kisha Bwana akasema, “Mwite Lo-Ami1:9 Lo-Ami maana yake Sio watu wangu. kwa maana ninyi si watu wangu, nami si Mungu wenu.

101:10 Mwa 22:17; Yer 33:22; Rum 9:26; Hos 2:23; Hes 23:10; Yos 3:10“Hata hivyo Waisraeli watakuwa kama mchanga kando ya bahari, ambao hauwezi kupimika wala kuhesabiwa. Mahali pale walipoambiwa, ‘Ninyi si watu wangu,’ wao wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.’ 111:11 Isa 11:12-13; Yer 23:5-8; 30:9; Eze 37:15-28Watu wa Yuda na watu wa Israeli wataunganishwa tena, nao watamchagua kiongozi mmoja nao watakwea watoke katika nchi, kwa kuwa siku ya Yezreeli itakuwa kuu sana.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

何西阿书 1:1-11

1乌西雅约坦亚哈斯希西迦犹大王,约阿施的儿子耶罗波安以色列王期间,耶和华将祂的话传给备利的儿子何西阿

何西阿娶妓女为妻

2耶和华首次向何西阿说话时,对他说:“你去娶一个妓女为妻,和她生养儿女,因为这片土地上的人极其淫乱,背弃了耶和华。” 3于是,何西阿娶了滴拉音的女儿歌蜜为妻,她怀孕为他生了一个儿子。 4耶和华对何西阿说:“给他取名叫耶斯列1:4 耶斯列”意思是“上帝撒种”。此处指上帝要像撒种一样驱散以色列人,但在1:11指上帝要赐福他们,就像撒种后获得了大丰收。,因为再过不久,我就要因耶户家在耶斯列的屠杀而惩罚他们,消灭以色列国。 5那时,我要在耶斯列平原折断以色列的弓。” 6后来,歌蜜又怀孕生了一个女儿。耶和华对何西阿说:“给她取名叫罗·路哈玛1:6 罗·路哈玛”意思是“不蒙怜悯”。,因为我将不再怜悯以色列家,也不再赦免他们的罪。 7但我要怜悯犹大家,使他们依靠他们的上帝耶和华得到拯救,而不是依靠战弓、刀剑、马匹、骑兵和战争。” 8罗·路哈玛断奶后,歌蜜又怀孕生了一个儿子。 9耶和华说:“给他取名叫罗·阿米1:9 罗·阿米”意思是“不是我的子民”。,因为以色列人不再是我的子民,我也不再是他们的上帝。

以色列的复兴

10“然而,以色列的人数必像海沙一样量不尽、数不完。从前我在什么地方对他们说‘你们不是我的子民’,将来也要在那里对他们说‘你们是永活上帝的儿女’。 11那时,犹大人和以色列人将被聚集起来,为自己选立一位首领,从流亡之地返回故乡,安居乐业。耶斯列的日子将是伟大的日子。