Hesabu 29 – NEN & BPH

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 29:1-40

Sikukuu Ya Tarumbeta

(Walawi 23:23-25)

129:1 Hes 28:18“ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta. 229:2 Hes 28:2; Law 1:9; Hes 28:11; Law 1:3; Hes 28:3Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayo Bwana ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 329:3 Hes 28:12Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume, andaa unga sehemu ya kumi mbili za efa; 429:4 Hes 28:13na pamoja na wana-kondoo saba kila mmoja aandaliwe na sehemu ya kumi ya efa ya unga. 529:5 Hes 28:15Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi kufanya upatanisho kwa ajili yenu. 629:6 Hes 28:11; 28:3; 28:5; 28:7; Law 1:9; Hes 28:2; Dan 12:11; Law 6:9; Hes 15:11, 12Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku pamoja na sadaka zake za nafaka na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwa Bwana kwa moto, harufu inayopendeza.

Siku Ya Upatanisho

(Walawi 23:26-32)

729:7 Mdo 27:9; Kut 31:15; Law 16:29; Ezr 8:21; Za 35:13; Isa 58:5; Lk 13:3-4; 1Kor 9:27; Yak 4:9“ ‘Kwenye siku ya kumi ya mwezi huu wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu. Mtajikana wenyewe na msifanye kazi. 829:8 Law 22:20; Hes 28:19; 29:8; Kum 15:21; 17:1Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza Bwana. 929:9 Hes 28:12Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini; 1029:10 Hes 28:13na kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba andaa sehemu ya kumi ya unga laini kwa kila mmoja. 1129:11 Hes 28:12; Law 16:3Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.

Sikukuu Ya Vibanda

(Walawi 23:33-44)

1229:12 1Fal 8:2; 12:32; Law 23:24“ ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Adhimisheni sikukuu kwa Bwana kwa siku saba. 1329:13 Hes 28:2; 28:3; Ebr 10:1-18; Ezr 3:8; Dan 9:24Toeni sadaka ya kuteketezwa mafahali wachanga kumi na watatu, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendeza Bwana. 1429:14 Hes 15:6Pamoja na hao mafahali kumi na watatu, kila mmoja aandaliwe na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume wawili, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini; 1529:15 Hes 28:13na kwa wana-kondoo kumi na wanne, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi ya efa ya unga laini. 1629:16 Hes 28:15Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka ya vinywaji.

1729:17 Law 23:36; Hes 28:3“ ‘Katika siku ya pili andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 1829:18 Hes 28:7, 14; 15:4-12; Law 2:1Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 1929:19 Hes 28:15; 28:3Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

20“ ‘Katika siku ya tatu andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 21Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 22Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

23“ ‘Katika siku ya nne andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 24Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 25Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

2629:26 Yn 1:29; Ebr 7:26; Ufu 5:6-14“ ‘Katika siku ya tano andaeni mafahali tisa, kondoo dume wawili na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 27Pamoja na mafahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za kinywaji kulingana na idadi iliyoainishwa. 28Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji.

29“ ‘Katika siku ya sita andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 30Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 31Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

32“ ‘Katika siku ya saba andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 33Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 34Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

3529:35 Law 23:36; Za 47:5-6; Isa 11:10; Ufu 7:9-17; 11:15“ ‘Katika siku ya nane mtakuwa na kusanyiko, na msifanye kazi ya kawaida. 36Toeni sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri inayompendeza Bwana, sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari. 37Pamoja na fahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka, na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa. 38Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji.

3929:39 Hes 36:2; 7:16; 23:2; 1:3; 1Nya 23:31; 2Nya 31:3; Law 3:1“ ‘Zaidi ya kile unachoweka nadhiri na sadaka zenu za hiari, andaeni hizi kwa ajili ya Bwana kwenye sikukuu zenu zilizoamriwa: sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za vinywaji, pamoja na sadaka zenu za amani.’ ”

4029:40 Kut 24:3; Kum 5:27-31; Yn 7:19; Mdo 7:37-38; 7:38Mose akawaambia Waisraeli yale yote Bwana alimwagiza.

Bibelen på hverdagsdansk

4. Mosebog 29:1-39

Nytårsofferet

1Den første dag i den syvende29,1 Svarende til september-oktober. måned skal I indvarsle det nye år ved hornblæsning og fest.29,1 Ifølge jødisk tradition (Mishnah) er det et vædderhorn (shofar), der bruges her. Muligvis blev der også blæst i sølvtrompeten. Teksten taler blot om at blæse et signal. På den dag skal I hvile fra det daglige arbejde og samles for Herrens ansigt. 2I skal ofre liflige brændofre bestående af en ung tyr, en vædder og syv etårs vædderlam, alle uden skavanker. 3De tilhørende afgrødeofre skal bestå af seks liter fint mel blandet med olivenolie for hver tyr, fire liter fint mel blandet med olivenolie for hver vædder 4og to liter fint mel blandet med olivenolie for hvert lam. 5Derudover skal I ofre en gedebuk som soning for jeres synder 6samt det månedlige og det daglige offer med tilhørende afgrødeofre og drikofre efter de forskrifter, som allerede er givet. Disse ofre vil frembringe en liflig duft for Herren.

Ofre på forsoningsdagen

7På den tiende dag i den syvende måned skal I atter samles for Herrens ansigt. På den dag skal I faste og lade det daglige arbejde hvile. 8I skal ofre brændofre til Herren bestående af en ung tyr, en vædder og syv etårs vædderlam, alle uden skavanker. Disse ofre vil frembringe en liflig duft for Herren. 9Det tilhørende afgrødeofre skal bestå af seks liter fint mel blandet med olivenolie for hver tyr, fire liter fint mel blandet med olivenolie for hver vædder 10og to liter fint mel blandet med olivenolie for hvert lam. 11Desuden skal der ofres en gedebuk som syndoffer. Dette er ud over det særlige forsoningsoffer på den dag og de daglige brændofre med tilhørende afgrødeofre og drikofre.

Ofre under løvhyttefesten

12På den 15. dag i den syvende måned skal I atter hvile fra det daglige arbejde og samles for Herrens ansigt, for da begynder løvhyttefesten til Herrens ære, og den varer i syv dage. 13Det særlige brændoffer der skal bringes på den dag, og som vil frembringe en liflig duft for Herren, består af 13 unge tyre, to væddere og 14 etårs vædderlam, alle uden skavanker. 14De tilhørende afgrødeofre skal bestå af seks liter fint mel blandet med olivenolie for hver tyr, fire liter fint mel blandet med olivenolie for hver vædder 15og to liter fint mel blandet med olivenolie for hvert lam. 16Ud over de daglige brændofre, afgrødeofre og drikofre skal der også ofres en gedebuk som syndoffer.

17På festugens anden dag skal der ofres 12 unge tyre, to væddere og 14 etårs vædderlam, alle uden skavanker, 18med de tilhørende afgrødeofre og drikofre for hvert dyr. 19Ud over de daglige ofre skal der også ofres en gedebuk som syndoffer med tilhørende afgrøde- og drikofre.

20På festugens tredje dag skal der ofres 11 unge tyre, to væddere og 14 etårs vædderlam, alle uden skavanker, 21med tilhørende afgrøde- og drikofre. 22Ud over de daglige ofre skal der igen med tilhørende afgrøde- og drikofre ofres en gedebuk som syndoffer.

23-34Sådan skal I fortsætte ugen ud. Hver dag skal der ud over de daglige ofre ofres en gedebuk som syndoffer med tilhørende afgrøde- og drikofre samt de særlige brændofre, afgrødeofre og drikofre. For hver dag der går, skal der dog ofres en tyr mindre end dagen før, således at der den sidste dag—på festens syvende dag—ofres syv unge tyre. Men de øvrige ofre er de samme hver dag.

35På den ottende dag skal I hvile fra det daglige arbejde og samles for Herrens ansigt. 36-37Den dag skal brændofferet bestå af en ung tyr, en vædder og syv etårs vædderlam, alle uden skavanker, samt de tilhørende afgrøde- og drikofre. Disse ofre vil frembringe en liflig duft for Herren. 38Desuden skal I ofre de daglige ofre og en gedebuk med tilhørende afgrøde- og drikofre som syndoffer.

39Det er de ofre, I skal bringe i forbindelse med de årlige højtider. Hertil kommer de frivillige ofre og ofre i forbindelse med løfter, som I har aflagt over for Herren, hvad enten det drejer sig om brændofre, afgrødeofre, drikofre eller takofre.”