Hesabu 2 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Hesabu 2:1-34

Mpangilio Wa Kambi Za Makabila

1Bwana aliwaambia Mose na Aroni: 22:2 Za 74:4; Isa 31:9; Yer 4:21“Waisraeli watapiga kambi zao kuzunguka Hema la Kukutania kwa umbali fulani kutoka kwenye hema, kila mwanaume chini ya alama yake pamoja na bendera ya jamaa yake.”

32:3 Hes 6:23; Rut 4:20; 1Nya 2:10; Lk 3:32-33; Hes 10:14Kwa upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua, kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu. 4Kundi lake lina watu 74,600.

52:5 Hes 1:8; 10:15Kabila la Isakari watapiga kambi karibu na Yuda. Kiongozi wa watu wa Isakari ni Nethaneli mwana wa Suari. 62:6 Hes 26:25Kundi lake lina watu 54,400.

72:7 Hes 1:9; 10:16; Mwa 49:13; Kum 33:18Kabila la Zabuloni litafuata. Kiongozi wa watu wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni. 8Kundi lake lina watu 57,400.

92:9 Hes 10:14; Amu 1:1; 1Nya 5:2; Za 78:52Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni 186,400. Wao watatangulia kuondoka.

102:10 Hes 1:5, 53; Kum 33:6Kwa upande wa kusini kutakuwa kambi ya makundi ya Reubeni chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Reubeni ni Elisuri mwana wa Shedeuri. 11Kundi lake lina watu 46,500.

122:12 Hes 10:19; 1:6Kabila la Simeoni watapiga kambi karibu na Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Surishadai. 13Kundi lake lina watu 59,300.

142:14 Hes 10:20; 1:14Kabila la Gadi litafuata. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli. 15Kundi lake lina watu 45,650.

162:16 Hes 10:18; Mwa 49:3Wanaume wote walio katika kambi ya Reubeni, kufuatana na makundi yao, ni 151,450. Nao watakuwa nafasi ya pili kuondoka.

172:17 Hes 1:50; 10:21; Mdo 4:4; Ebr 8:2; 1Kor 14:40Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake.

182:18 Hes 1:10, 53; Mwa 48:20; Yer 31:18-20; Za 80:1; Hos 11:3Upande wa magharibi kutakuwepo na kambi ya makundi ya Efraimu chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi. 19Kundi lake lina watu 40,500.

202:20 Mwa 48:20; Hes 1:10Kabila la Manase litafuata baada ya Efraimu. Kiongozi wa watu wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri. 21Kundi lake lina watu 32,200.

222:22 Hes 10:24; 1:11; Za 68:27Kabila la Benyamini litafuata baada ya Manase. Kiongozi wa watu wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni. 23Kundi lake lina watu 35,400.

242:24 Hes 10:22; Za 80:2Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni 108,100. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka.

252:25 Hes 1:22, 53; 10:25; Kum 32:22Upande wa kaskazini kutakuwa na makundi ya kambi ya Dani, chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai. 26Kundi lake lina watu 62,700.

272:27 Hes 1:13; 10:26Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani. 28Kundi lake lina watu 41,500.

292:29 Hes 1:15; 10:27; Mwa 30:8; 49:21; 2Fal 15:29Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani. 30Kundi lake lina watu 53,400.

312:31 Hes 10:25; Yos 6:9Wanaume wote walio katika kambi ya Dani ni 157,600. Wao watakuwa wa mwisho kuondoka chini ya alama yao.

322:32 Hes 1:45; Kut 12:35-37; 38:26Hawa ndio Waisraeli, wakiwa wamehesabiwa kufuatana na jamaa zao. Wote walio kambini kwa makundi yao ni watu 603,550. 332:33 Hes 1:47; 26:57-62Hata hivyo, Walawi hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine, kama Bwana alivyomwagiza Mose.

342:34 Kut 12:37; Hes 24:2, 9; Isa 45:12Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kitu Bwana alichomwamuru Mose. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya alama zao, pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

民數記 2:1-34

營地的安排

1耶和華對摩西亞倫說: 2以色列人要各歸本旗,按本族的旗號,在會幕四圍稍遠的地方安營。」 3東邊,即日出的方向,是猶大營區及其旗號。猶大人的首領是亞米拿達的兒子拿順4率領七萬四千六百人。 5猶大支派旁邊安營的是以薩迦支派,首領是蘇押的兒子拿坦業6率領五萬四千四百人。 7然後是西布倫支派,首領是希倫的兒子以利押8率領五萬七千四百人。 9猶大營區的人共十八萬六千四百人,他們是開路先鋒。

10南邊是呂便營區及其旗號。呂便人的首領是示丟珥的兒子以利蘇11率領四萬六千五百人。 12呂便支派旁邊安營的是西緬支派,首領是蘇利沙代的兒子示路蔑13率領五萬九千三百人。 14然後是迦得支派,首領是丟珥的兒子以利雅薩15率領四萬五千六百五十人。 16呂便營區共十五萬一千四百五十人,他們是第二隊。 17隨後是會幕和利未人的營區,在其他各營中間。他們各就各位,各歸本旗,照安營時的次序出發。

18西邊是以法蓮營區及其旗號。以法蓮人的首領是亞米忽的兒子以利沙瑪19率領四萬零五百人。 20以法蓮支派旁邊是瑪拿西支派,首領是比大蘇的兒子迦瑪列21率領三萬二千二百人。 22然後是便雅憫支派,首領是基多尼的兒子亞比但23率領三萬五千四百人。 24以法蓮營區共十萬八千一百人,他們是第三隊。

25北邊是營區及其旗號。人的首領是亞米沙代的兒子亞希以謝26率領六萬二千七百人。 27支派旁邊安營的是亞設支派,首領是俄蘭的兒子帕結28率領四萬一千五百人。 29然後是拿弗他利支派,首領是以南的兒子亞希拉30率領五萬三千四百人。 31營區共有十五萬七千六百人,他們是後隊。

32以上照宗族和隊伍統計的以色列人共六十萬三千五百五十名。 33照耶和華對摩西的吩咐,利未人沒被統計在其中。

34於是,以色列人照耶和華對摩西的吩咐,各按自己的旗號安營,各按自己的宗族啟行。