Unabii Dhidi Ya Mfalme Wa Tiro
1Neno la Bwana likanijia kusema: 228:2 Isa 14:13; Mwa 3:4-5; 2The 2:4; Kum 8:14; Mit 16:18; Sef 2:15; Za 9:20“Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna
na umesema, “Mimi ni mungu;
nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungu
katika moyo wa bahari.”
Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu,
ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu.
328:3 Dan 1:20; 2:20-23, 28; Zek 9:2; Eze 14:14Je, wewe una hekima kuliko Danieli?
Je, hakuna siri iliyofichika kwako?
428:4 Zek 9:3; Isa 10:13Kwa hekima yako na ufahamu wako,
umejipatia utajiri,
nawe umejikusanyia dhahabu
na fedha katika hazina zako.
528:5 Ay 31:25; Hos 13:6; Kum 8:12-14; Isa 23:8; Yer 9:23; 9:23; Eze 27:33Kwa werevu wako mwingi katika biashara,
umeongeza utajiri wako
na kwa sababu ya utajiri wako
moyo wako umekuwa na kiburi.
6“ ‘Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Kwa sababu unafikiri una hekima,
mwenye hekima kama mungu,
728:7 Eze 32:12; 30:11; 31:12; Yer 9:23; Eze 7:24mimi nitawaleta wageni dhidi yako,
taifa katili kuliko yote;
watafuta panga zao dhidi ya uzuri wa hekima yako,
na kuchafua fahari yako inayongʼaa.
828:8 Za 55:23; Eze 32:30; 27:27; 26:12; Ufu 18:7Watakushusha chini shimoni,
nawe utakufa kifo cha kikatili
katika moyo wa bahari.
928:9 Isa 31:3; Eze 16:49Je, wakati huo utasema, “Mimi ni mungu,”
mbele ya wale wanaokuua?
Utakuwa mwanadamu tu, wala si mungu,
mikononi mwa hao wanaokuua.
1028:10 1Sam 14:6; Yer 9:26; Eze 32:18-19Utakufa kifo cha wasiotahiriwa
kwa mkono wa wageni.
Kwa kuwa mimi nimenena, asema Bwana Mwenyezi.’ ”
11Neno la Bwana likanijia kusema: 1228:12 Eze 19:1; 27:2-4“Mwanadamu, mfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, nawe umwambie: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Ulikuwa kipeo cha ukamilifu,
ukiwa umejaa hekima
na mkamilifu katika uzuri.
1328:13 Mwa 2:8; Eze 31:8-9; 27:16; Ufu 17:4; Isa 14:11; Ufu 21:20Ulikuwa ndani ya Edeni,
bustani ya Mungu;
kila kito cha thamani kilikupamba:
akiki nyekundu, yakuti manjano na zumaridi,
krisolitho, shohamu na yaspi,
yakuti samawi, almasi na zabarajadi.
Kuwekwa kwa hayo mapambo na kushikizwa kwake
kulifanywa kwa dhahabu;
siku ile ulipoumbwa yaliandaliwa tayari.
1428:14 Kut 30:26; 40:9; 25:17-20Ulitiwa mafuta kuwa kerubi mlinzi,
kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu.
Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu;
ulitembea katikati ya vito vya moto.
15Ulikuwa mnyofu katika njia zako
tangu siku ile ya kuumbwa kwako,
hadi uovu ulipoonekana ndani yako.
1628:16 Mwa 6:11; Hab 2:17; Mwa 3:24Kutokana na biashara yako iliyoenea,
ulijazwa na dhuluma,
nawe ukatenda dhambi.
Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka mlima wa Mungu,
nami nikakufukuza, ee kerubi mlinzi,
kutoka katikati ya vito vya moto.
1728:17 Isa 10:12; Eze 16:49; 31:10; 19:12Moyo wako ukawa na kiburi
kwa ajili ya uzuri wako,
nawe ukaiharibu hekima yako
kwa sababu ya fahari yako.
Kwa hiyo nikakutupa chini;
nimekufanya kioja mbele ya wafalme.
1828:18 Oba 1:18; Mal 4:3; Zek 9:2-4Kwa dhambi zako nyingi na biashara yako ya dhuluma,
umenajisi mahali pako patakatifu.
Kwa hiyo nilifanya moto utoke ndani yako,
nao ukakuteketeza,
nami nikakufanya majivu juu ya nchi,
machoni pa wote waliokuwa wakitazama.
1928:19 Yer 51:64; Eze 26:21; Law 26:21Mataifa yote yaliyokujua
yanakustajabia;
umefikia mwisho wa kutisha
na hutakuwepo tena milele.’ ”
Unabii Dhidi Ya Sidoni
20Neno la Bwana likanijia kusema: 2128:21 Eze 6:2; 13:17; Yer 25:2; Mwa 10:15“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake, 2228:22 Kut 14:4; Za 9:16; Eze 30:19; 39:13; Law 10:3nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:
“ ‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni,
nami nitapata utukufu ndani yako.
Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana,
nitakapotekeleza hukumu zangu
na kuonyesha utakatifu wangu ndani yake.
2328:23 Eze 5:17; 38:22Nitapeleka tauni ndani yake
na kufanya damu itiririke katika barabara zake.
Waliochinjwa wataanguka ndani yake,
kwa upanga dhidi yake kila upande.
Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.
2428:24 Hes 33:55; Yos 23:13; Isa 5:6; Eze 2:6“ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana Mwenyezi.
2528:25 Za 106:47; Yer 32:37; Isa 11:12; Eze 20:41; Yer 12:15; 12:15; 23:8; Eze 11:17“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo. 2628:26 Law 25:18; Yer 23:6; Hos 2:15; Amo 9:14-15; 1Fal 4:25; Yer 17:25; Kum 20:6; Eze 38:8; 39:26-27; Isa 65:21Wataishi humo kwa salama na watajenga nyumba na kupanda mashamba ya mizabibu, wataishi kwa salama nitakapowaadhibu majirani zao wote ambao waliwafanyia uovu. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana, Mungu wao.’ ”
Profeti imod fyrsten over Tyrus
1Herren sagde til mig: 2„Du menneske, sig til fyrsten over Tyrus:
Du er så stolt og hovmodig,
at du tror, du selv er en gud.
Du sidder på din høje trone,
hersker over havet og praler.
Men du er kun et menneske,
der bilder sig ind at være en gud.
3Du tror, du er klogere end Daniel
og kender alle hemmeligheder.
4Du brugte din visdom og forstand
til at samle mængder af guld og sølv.
5Dit handelstalent gjorde dig rig,
men din rigdom gjorde dig hovmodig.
6Derfor siger Gud Herren:
Fordi du tror, at du selv er en gud,
7sender jeg en grusom fjendehær,
der gør ende på din rigdom og pragt.
8Til dødsriget sender de dig ned,
du bliver dræbt og kastet i havet.
9Vil du mon fortsat hævde, du er en gud,
når fjenderne er ved at slå dig ihjel?
I hænderne på dem er du ingen gud,
men kun et almindeligt menneske.
10Du skal dø som en hund for de fremmedes hånd.
Jeg, Herren har talt.”
11Endvidere sagde Herren til mig: 12„Du menneske, istem en klagesang over Tyrus’ fyrste og sig til ham:
Engang var du fuldkommen,
smuk og fuld af visdom.
13Du levede som i Paradis,
smykket med utallige juveler:
rubin, topas og diamant,
krysolit, onyks og jaspis,
safir, granat og smaragd.
Alle juveler var indsat i guld,
de lå klar til dig ved din fødsel.
14Jeg satte dig som en kerub,
der skulle vogte og beskytte
det hellige bjerg, jeg havde skabt,
Du vandrede blandt funklende ædelsten.
15Der var intet at udsætte på dig
fra den dag, du blev født,
indtil din ondskab blev afsløret.
16Din store rigdom gjorde dig korrupt,
så vold og synd fyldte dit hjerte.
Da jog jeg dig bort fra mit hellige bjerg
og de funklende ædelsten, du skulle beskytte.
Jeg slog dig ned, du vældige kerub.
17Din skønhed gjorde dig stolt,
din rigdom spændte ben for din visdom.
Derfor kastede jeg dig til jorden
som en advarsel for andre fyrster.
18Din uhæderlige handel
afsporede din gudsdyrkelse.
Derfor lod jeg ild bryde frem og fortære dig,
så du blev til aske på jorden for alles øjne.
19Alle var skrækslagne over din skæbne.
Du blev et skræmmende eksempel
ved din totale og endelige udslettelse.”
Profeti imod Sidon
20Herren sagde til mig:
21„Du menneske, vend dig mod Sidon og profetér over byen. 22Sig til den:
Sidon, jeg er din fjende,
og jeg vil demonstrere min magt på dig.
Alle skal få at se, at jeg er Herren,
når jeg åbenbarer min hellighed på dig
ved at straffe dig for dine synder.
23Jeg sender epidemier og krig,
så blodet flyder i gaderne.
Fjenden angriber fra alle sider
og slår folk ned til højre og venstre.
Da vil du indse, at jeg er Herren.
Et løfte til Guds folk
24Israels nabofolk skal ikke længere stikke mit folk som tidsler og torne. Alle I, som nu håner mit folk, skal få at se, at jeg er Herren.
25Hør, hvad Herren siger: Når jeg samler Israels folk fra de folkeslag, de er spredt iblandt, og fører dem tilbage til deres eget land, det land, jeg gav min tjener Jakob, da vil alle folk indse, at jeg er en hellig og mægtig Gud. 26Derefter skal mit folk bo trygt i deres land, bygge huse og plante vingårde, mens jeg straffer alle dem, som behandlede dem med foragt. Da vil de indse, at jeg er Herren, deres Gud.”