Ezekieli 26 – NEN & JCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 26:1-21

Unabii Dhidi Ya Tiro

126:1 Eze 24:1; 29:1; 30:20Mwaka wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana likanijia kusema: 226:2 Yos 19:29; 2Sam 5:11; Eze 25:3; Yoe 3:4-6“Mwanadamu, kwa sababu Tiro amesema kuhusu Yerusalemu, ‘Aha! Lango la kwenda kwa mataifa limevunjika, nayo milango yake iko wazi mbele yangu, sasa kwa kuwa amekuwa magofu nitastawi.’ 326:3 Isa 5:30; Yer 50:42; 51:42Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na wewe, ee Tiro, nami nitaleta mataifa mengi dhidi yako, kama bahari inayovurumisha mawimbi yake. 426:4 Isa 23:1, 11; Amo 1:10Watavunja kuta za Tiro na kuibomoa minara yake, nitakwangua udongo wake na kuufanya mwamba mtupu. 526:5 Eze 27:32; Hes 14:3; Eze 29:19; Mt 4:19-21; Eze 47:10; Zek 9:2-4Itakuwa huko katikati ya bahari patakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki, kwa maana nimenena, asema Bwana Mwenyezi. Atakuwa nyara kwa mataifa, 626:6 Eze 25:5nayo makao yake huko bara yataangamizwa kwa upanga. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.

726:7 Yer 27:6; Ezr 7:12; Dan 2:37; Nah 2:3-4; Eze 23:24“Kwa maana hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kutoka kaskazini nitamleta dhidi ya Tiro Mfalme Nebukadneza wa Babeli, mfalme wa wafalme, akiwa na farasi na magari ya vita, wapanda farasi na jeshi kubwa. 826:8 Yer 6:6; 33:4; Eze 21:22; 2Sam 20:15Atayaharibu makao yako huko bara kwa upanga, ataweka jeshi kukuzingira, atakuzingira mpaka kwenye kuta za ngome zako na kuinua ngao zake dhidi yako. 926:9 Eze 21:22Ataelekeza mapigo ya vyombo vyake vya kubomolea dhidi ya kuta zako na kubomoa minara yako kwa silaha zake. 1026:10 Yer 4:13; 46:9; Eze 23:24Farasi zake zitakuwa nyingi sana kiasi kwamba utafunikwa na mavumbi watakayotimua. Kuta zako zitatikisika kwa mshindo wa farasi wa vita, magari makubwa na magari ya vita wakati aingiapo malango yako kama watu waingiao mji ambao kuta zake zimebomolewa kote.

1126:11 Isa 5:28; Yer 43:13; Isa 26:5“Kwato za farasi zake zitakanyaga barabara zako zote, atawaua watu wako kwa upanga na nguzo zako zilizo imara zitaanguka chini. 1226:12 Yer 4:7; Hab 1:8; Isa 23:8; Eze 27:3-27Watateka utajiri wako na kuchukua nyara bidhaa zako, watazivunja kuta zako na kuzibomoa nyumba zako nzuri, watatupa baharini mawe yako, mbao zako na kifusi chako. 1326:13 Yer 7:34; Za 137:2; Isa 14:11; Ay 30:31; Ufu 18:22; Hos 2:11Nitakomesha kelele za nyimbo zako, na uimbaji wako wa kinubi kamwe hautasikika tena. 1426:14 Ay 12:14; Mal 1:4Nitakufanya mwamba mtupu, nawe utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za kuvulia samaki. Kamwe hutajengwa tena, kwa maana Mimi Bwana nimenena, asema Bwana Mwenyezi.

1526:15 Isa 41:5; Eze 27:35; Yer 49:21; Ay 24:12“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kwa Tiro: ‘Je, nchi za pwani hazitatetemeka kwa kishindo cha anguko lako, wakati majeruhi wanapolia kwa maumivu makali na wakati mauaji yanaendelea ndani yako? 1626:16 Ay 8:22; Hos 11:10; Isa 3:26; Eze 32:10; Kut 26:36; Ay 2:8-13; Law 26:32Ndipo wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuweka kando majoho yao na kuvua nguo zao zilizotariziwa. Wakiwa wamevikwa hofu kuu, wataketi chini ardhini, wakiwa wanatetemeka kila dakika na wakikustajabia. 1726:17 Eze 19:1; Isa 14:12Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia:

“ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa,

ee mji uliokuwa na sifa,

wewe uliyekaliwa na mabaharia!

Ulikuwa na nguvu kwenye bahari,

wewe na watu wako;

wote walioishi huko,

uliwatia hofu kuu.

1826:18 Isa 23:5; 41:5; Za 46:6; Yer 49:21; Eze 27:35Sasa nchi za pwani zinatetemeka

katika siku ya anguko lako;

visiwa vilivyomo baharini

vinaogopa kwa kuporomoka kwako.’

1926:19 Isa 8:7-8; Mwa 7:11“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitakapokufanya uwe mji wa ukiwa, kama miji isiyokaliwa tena na watu, nitakapoleta vilindi vya bahari juu yako na maji yake makuu yatakapokufunika, 2026:20 Amo 9:2; Yon 2:2-6; Ay 28:13; Isa 14:9-10; Eze 32:18; Ay 28:13; Hes 16:30ndipo nitakapokushusha chini pamoja na wale washukao shimoni, kwa watu wa kale, nami nitakufanya uishi katika pande za chini za nchi kama katika magofu ya kale, pamoja na wale washukao shimoni, nawe hutarudi au kurejea kwenye makao yako katika nchi ya walio hai. 2126:21 Yer 20:4; Ufu 18:21; Za 37:36; Yer 51:64; Dan 11:19Nitakufikisha mwisho wa kutisha wala hutakuwepo tena. Watu watakutafuta, lakini kamwe hutaonekana tena, asema Bwana Mwenyezi.”

Japanese Contemporary Bible

エゼキエル書 26:1-21

26

ツロについての預言

1エホヤキン王が捕囚となって十一年目のその月の第一日、主から新しいことばが示されました。

2「人の子よ。

ツロはエルサレムの滅亡を喜んで、

『それ見たことか。エルサレムは地中海沿岸と、

ヨルダン川沿いの南北に通じる通商路を支配し、

利益を得ていたが、ついに打ち破られた。

あとは私のものだ。

エルサレムが廃墟になったので、

私は金持ちになれる』と言った。」

3それゆえ、神である主はこう語ります。

「ツロよ。わたしはおまえを攻める。

波が打ち寄せるように、

たくさんの国が次から次へと攻め寄せる。

4彼らはツロの城壁を破壊し、やぐらを倒す。

わたしは、その土を削り取って、

そこを裸の岩にしよう。

5島には、住む人もなく、

ただ漁師が網をしかける場所となる。」

これを語ったのはわたしであると、

神である主が言います。

「ツロは多くの国のえじきとなる。

6本土にあるツロの町も剣によって滅びる。

その時、彼らはわたしが主であることを知る。」

7神である主はこう語ります。

「北から、王の王であるバビロンの王

ネブカデネザルを連れて来よう。

彼は騎兵と戦車の大軍を率いて、ツロに攻め寄せる。

8まず、周辺の村々を攻略し、

それから本土の町を包囲してとりでを築き、

盾を屋根のように掲げて攻撃する。

9破城槌で城壁を突きくずし、

大づちをふるってとりでを粉砕する。

10騎兵隊の巻き上げる土煙で、

町は息もつけないありさまとなるだろう。

打ち破られた城内から、

戦車を引いて疾駆する馬の地響きに、

城壁は震え上がるだろう。

11騎兵たちが町にひしめき、

住民を片っぱしから殺して回る。

あの名高い、大きな柱も倒される。

12財宝も商品も残らず略奪され、城壁も打ち壊される。

快適な家は取り壊され、石も木も、そしてちりまでも、

海に投げ捨てられる。

13わたしは、おまえが歌うのをやめさせる。

もう竪琴の音も聞こえなくなる。

14おまえを裸岩とし、

漁師たちが網をしかける所とする。

おまえは二度と建て直されることはない。

主であるわたしが言うのだ。

15おまえがくずれ落ちる響きで国中が震え、虐殺が続けられる中で、傷ついた者たちが悲鳴を上げる。

16その時、海辺の諸国の指導者たちは、王座から降り、王衣も美しい衣服も脱ぎ捨て、あまりに恐ろしい光景に、身を震わせながら地に座り込む。 17彼らはおまえのために嘆き悲しみ、こんな哀歌を口にする。

『ああ、難攻不落を誇った港の町。

その強大な海軍力が本土を恐れさせたのに、

どうして海に消えてしまったのか。

18島々はおまえの滅亡に恐怖に駆られ、

おびえたまなざしで見つめている。』」

19神である主は語ります。「わたしはツロを完全に滅ぼす。ツロは大洪水のような敵の猛攻撃で、その下に沈められる。大海がおまえをのみ込んでしまうのだ。 20わたしはおまえを地獄の穴に送り込み、昔の民といっしょに横たえさせる。町は荒れはて、死の町となる。再び人が住むことはなく、その美しさを取り戻すこともない。 21わたしはおまえに恐ろしい最期を遂げさせる。いくら捜しても、おまえを見つけることはできない。」このように主が語るのです。