Ezekieli 12 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 12:1-28

Kutekwa Kwa Yuda Kwaelezewa

1Neno la Bwana likanijia kusema: 212:2 Isa 6:10; Mk 8:18; Yer 5:21; Mt 13:15; Za 78:40; Yer 42:21; Mk 4:12“Mwanadamu, unaishi miongoni mwa watu waasi. Wana macho ya kuona, lakini hawaoni na masikio ya kusikia lakini hawasikii, kwa kuwa ni watu waasi.

312:3 Yer 36:3; 26:3; Eze 3:27; 2Tim 2:25-26“Kwa hiyo, mwanadamu, funga mizigo yako kwa kwenda uhamishoni tena wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toka nje na uende mahali pengine kutoka hapo ulipo. Labda wataelewa, ingawa wao ni nyumba ya kuasi. 412:4 2Fal 25:4; Yer 39:4Wakati wa mchana, wakiwa wanakutazama, toa nje mizigo yako iliyofungwa kwa ajili ya kwenda uhamishoni. Kisha wakati wa jioni, wakiwa wanakutazama toka nje kama wale waendao uhamishoni. 512:5 Yer 52:7; Amo 4:3Wakiwa wanakutazama, toboa ukuta utolee mizigo yako hapo. 612:6 Isa 8:18; 20:3Beba mizigo hiyo begani mwako wakikuangalia uichukue nje wakati wa giza la jioni. Funika uso wako ili usione nchi, kwa maana nimekufanya ishara kwa nyumba ya Israeli.”

712:7 Eze 24:18; 37:10Basi nikafanya kama nilivyoamriwa. Wakati wa mchana nilitoa vitu vyangu nje vilivyofungwa tayari kwa uhamishoni. Kisha wakati wa jioni nikatoboa ukuta kwa mikono yangu. Nikachukua mizigo yangu nje wakati wa giza la jioni, nikiwa nimeibeba mabegani mwangu huku wakinitazama.

8Asubuhi neno la Bwana likanijia kusema: 912:9 Eze 20:49; 24:19; 7:12“Mwanadamu, je, nyumba ile ya kuasi ya Israeli haikukuuliza, ‘Unafanya nini?’

1012:10 Mal 1:1“Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Neno hili linamhusu mkuu aliye katika Yerusalemu na nyumba yote ya Israeli ambao wako huko.’ 1112:11 2Fal 25:7; Yer 15:2; Isa 8:18; Zek 3:8; Yer 52:15Waambie, ‘Mimi ndiye ishara kwenu.’

“Kama vile nilivyotenda, basi litatendeka vivyo hivyo kwao. Watakwenda uhamishoni kama mateka.

1212:12 Yer 39:4; 52:7“Naye mkuu aliye miongoni mwao atabeba mizigo yake begani mwake kwenye giza la jioni na kuondoka na tundu litatobolewa ukutani kwa ajili yake ili kupitia hapo. Atafunika uso wake ili kwamba asiweze kuiona nchi. 1312:13 Ay 19:6; Eze 32:3; Hos 7:12; Isa 24:17-18; Mao 4:20; Yer 39:7; 24:8; Eze 17:20; 19:8; 17:16Nitatandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa kwenye mtego wangu, nitamleta mpaka Babeli, nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona, naye atafia huko. 1412:14 Eze 5:10; 2Fal 25:5; Yer 21:7; Eze 17:21Wote wanaomzunguka nitawatawanya pande zote, watumishi wake na majeshi yake yote, nami nitawafuatilia kwa upanga uliofutwa.

1512:15 Za 9:16; Eze 6:7, 14; 11:10“Wao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana, nitakapowatawanya miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi zote. 1612:16 Yer 4:27; 22:8-9; Eze 36:20; 6:8-10; 14:22Lakini nitawaacha wachache wao waokoke na upanga, njaa na tauni, ili kwamba katika mataifa watakakokwenda waweze kutambua matendo ya machukizo waliotenda. Ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.”

17Neno la Bwana likanijia kusema: 1812:18 Mao 5:9; Eze 4:16“Mwanadamu, tetemeka wakati ulapo chakula chako, tetemeka kwa hofu wakati unywapo maji yako. 1912:19 Yer 10:22; Zek 7:14; Eze 4:16; 6:6-14; Mik 7:13Waambie watu wa nchi: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo kuhusu hao wanaoishi Yerusalemu na katika nchi ya Israeli: Watakula chakula chao kwa wasiwasi na kunywa maji yao kwa kufadhaika, kwa kuwa nchi yao itanyangʼanywa kila kitu chake kwa sababu ya udhalimu wa wote wanaoishi humo. 2012:20 Isa 7:23-24; Yer 4:7; 25:9Miji inayokaliwa na watu itaharibiwa na nchi itakuwa ukiwa. Ndipo mtakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.’ ”

21Neno la Bwana likanijia kusema: 2212:22 Isa 5:19; 2Pet 3:4; Za 37:13; 49:4; Eze 3:11; Amo 6:3“Mwanadamu, ni nini hii mithali mlio nayo katika nchi ya Israeli: ‘Siku zinapita na hakuna maono yoyote yanayotimia?’ 2312:23 Yoe 2:1; Sef 1:14; Eze 7:7; 18:3; Za 37:13Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaikomesha mithali hii, nao hawataitumia tena katika Israeli.’ Waambie, ‘Siku zimekaribia wakati kila maono yatakapotimizwa. 2412:24 Mik 3:6; Zek 13:2-4; Mao 2:14; Yer 14:14; Eze 13:23Kwa maana hapatakuwepo tena na maono ya uongo wala ubashiri wa udanganyifu miongoni mwa watu wa Israeli. 2512:25 Hes 14:28-32; Dan 9:12; Hab 1:5; Hes 11:23; Eze 13:6; Isa 14:24; Yer 15:9Lakini Mimi Bwana nitasema neno nitakalo, nalo litatimizwa bila kuchelewa. Kwa maana katika siku zako, wewe nyumba ya kuasi, nitatimiza kila nisemalo, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

26Neno la Bwana likanijia kusema: 2712:27 Dan 10:14; Mt 24:48-50; Isa 5:19; Eze 11:3“Mwanadamu, nyumba ya Israeli inasema, ‘Maono yale anayoyaona ni kwa ajili ya miaka mingi ijayo, naye hutabiri kuhusu siku zijazo zilizo mbali.’

28“Kwa hiyo, waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakuna maneno yangu yatakayocheleweshwa tena zaidi, lolote nisemalo litatimizwa, asema Bwana Mwenyezi.’ ”

King James Version

Ezekiel 12:1-28

1The word of the LORD also came unto me, saying, 2Son of man, thou dwellest in the midst of a rebellious house, which have eyes to see, and see not; they have ears to hear, and hear not: for they are a rebellious house. 3Therefore, thou son of man, prepare thee stuff for removing, and remove by day in their sight; and thou shalt remove from thy place to another place in their sight: it may be they will consider, though they be a rebellious house.12.3 stuff: or, instruments 4Then shalt thou bring forth thy stuff by day in their sight, as stuff for removing: and thou shalt go forth at even in their sight, as they that go forth into captivity.12.4 as they…: Heb. as the goings forth of captivity 5Dig thou through the wall in their sight, and carry out thereby.12.5 Dig…: Heb. Dig for thee 6In their sight shalt thou bear it upon thy shoulders, and carry it forth in the twilight: thou shalt cover thy face, that thou see not the ground: for I have set thee for a sign unto the house of Israel. 7And I did so as I was commanded: I brought forth my stuff by day, as stuff for captivity, and in the even I digged through the wall with mine hand; I brought it forth in the twilight, and I bare it upon my shoulder in their sight.12.7 digged: Heb. digged for me

8¶ And in the morning came the word of the LORD unto me, saying, 9Son of man, hath not the house of Israel, the rebellious house, said unto thee, What doest thou? 10Say thou unto them, Thus saith the Lord GOD; This burden concerneth the prince in Jerusalem, and all the house of Israel that are among them. 11Say, I am your sign: like as I have done, so shall it be done unto them: they shall remove and go into captivity.12.11 they…: Heb. by removing go into captivity 12And the prince that is among them shall bear upon his shoulder in the twilight, and shall go forth: they shall dig through the wall to carry out thereby: he shall cover his face, that he see not the ground with his eyes. 13My net also will I spread upon him, and he shall be taken in my snare: and I will bring him to Babylon to the land of the Chaldeans; yet shall he not see it, though he shall die there. 14And I will scatter toward every wind all that are about him to help him, and all his bands; and I will draw out the sword after them. 15And they shall know that I am the LORD, when I shall scatter them among the nations, and disperse them in the countries. 16But I will leave a few men of them from the sword, from the famine, and from the pestilence; that they may declare all their abominations among the heathen whither they come; and they shall know that I am the LORD.12.16 a few…: Heb. men of number

17¶ Moreover the word of the LORD came to me, saying, 18Son of man, eat thy bread with quaking, and drink thy water with trembling and with carefulness; 19And say unto the people of the land, Thus saith the Lord GOD of the inhabitants of Jerusalem, and of the land of Israel; They shall eat their bread with carefulness, and drink their water with astonishment, that her land may be desolate from all that is therein, because of the violence of all them that dwell therein.12.19 all that…: Heb. the fulness thereof 20And the cities that are inhabited shall be laid waste, and the land shall be desolate; and ye shall know that I am the LORD.

21¶ And the word of the LORD came unto me, saying, 22Son of man, what is that proverb that ye have in the land of Israel, saying, The days are prolonged, and every vision faileth? 23Tell them therefore, Thus saith the Lord GOD; I will make this proverb to cease, and they shall no more use it as a proverb in Israel; but say unto them, The days are at hand, and the effect of every vision. 24For there shall be no more any vain vision nor flattering divination within the house of Israel. 25For I am the LORD: I will speak, and the word that I shall speak shall come to pass; it shall be no more prolonged: for in your days, O rebellious house, will I say the word, and will perform it, saith the Lord GOD.

26¶ Again the word of the LORD came to me, saying, 27Son of man, behold, they of the house of Israel say, The vision that he seeth is for many days to come, and he prophesieth of the times that are far off. 28Therefore say unto them, Thus saith the Lord GOD; There shall none of my words be prolonged any more, but the word which I have spoken shall be done, saith the Lord GOD.