Ezekieli 11 – NEN & NVI

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ezekieli 11:1-25

Hukumu Juu Ya Viongozi Wa Israeli

111:1 Eze 8:16; 43:4-5; 3:12-14; Yer 5:5Ndipo Roho akaniinua na kunileta mpaka kwenye lango la nyumba ya Bwana linalotazama upande wa mashariki. Pale kwenye ingilio la lango kulikuwepo wanaume ishirini na watano, nami nikaona miongoni mwao Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu. 211:2 Isa 29:20; Nah 1:11Bwana akaniambia, “Mwanadamu, hawa ndio wafanyao hila na kutoa mashauri potovu katika mji huu. 311:3 Yer 1:13; Eze 24:3; 12:22, 27; Mik 3:3Wao husema, ‘Je, hivi karibuni hautakuwa wakati wa kujenga nyumba? Mji huu ni chungu cha kupikia, nasi ndio nyama.’ 411:4 Eze 3:4, 17Kwa hiyo toa unabii dhidi yao, tabiri, Ewe mwanadamu.”

511:5 Ebr 4:11; Za 26:2; Yer 17:10Kisha Roho wa Bwana akaja juu yangu, naye akaniambia niseme: “Hili ndilo Bwana asemalo: Hili ndilo ninyi mnalosema, ee nyumba ya Israeli, lakini ninajua mnalowaza mioyoni mwenu. 611:6 Eze 7:23; 22:6Mmewaua watu wengi katika mji huu na kujaza barabara zake maiti.

711:7 Mik 3:2-3; Eze 24:3-13; Yer 1:13“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: maiti ulizozitupa huko ni nyama na mji huu ni chungu, lakini nitawaondoa mtoke huko. 811:8 Mit 10:24; Isa 66:4; Law 26:25; Yer 42:16Mnaogopa upanga, nao upanga huo ndio nitakaouleta juu yenu, asema Bwana Mwenyezi. 911:9 Za 106:41; Eze 5:8; Kum 28:36Nitawaondoa mtoke katika mji na kuwatia mikononi mwa wageni nami nitawaadhibu. 1011:10 Yer 39:6; 2Fal 14:25Mtaanguka kwa upanga, nami nitatimiza hukumu dhidi yenu katika mipaka ya Israeli. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana. 1111:11 Eze 24:6Mji huu hautakuwa chungu kwa ajili yenu, wala hamtakuwa nyama ndani yake. Nitatoa hukumu dhidi yenu katika mipaka ya Israeli. 1211:12 Law 18:4; Eze 18:9; 8:10; 6:7Nanyi mtajua ya kuwa Mimi ndimi Bwana, kwa kuwa hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu, bali mmefuata mwenendo wa mataifa yanayowazunguka.”

1311:13 Eze 9:8; Amo 7:2Basi nilipokuwa ninatoa unabii, Pelatia mwana wa Benaya akafa. Ndipo nikaanguka kifudifudi, nikalia kwa sauti kuu nikasema, “Ee Bwana Mwenyezi! Je utaangamiza kabisa mabaki ya Israeli?”

14Neno la Bwana likanijia kusema: 1511:15 Eze 33:24“Mwanadamu, ndugu zako, ndugu zako ambao ni wa uhusiano wa damu na nyumba yote ya Israeli, ndio wale ambao watu wa Yerusalemu wamesema, ‘Wako mbali na Bwana; nchi hii tulipewa sisi kuwa milki yetu.’

Ahadi Ya Kurudi Kwa Israeli

1611:16 Za 31:20; Isa 8:14; Za 91:9; Isa 4:6“Kwa hiyo sema, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ingawa niliwapeleka mbali miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbalimbali, lakini kwa kitambo kidogo mimi nimekuwa mahali patakatifu kwao katika nchi walizokwenda.’

1711:17 Neh 1:9; Yer 24:5-6; 3:18; 31:16; Eze 20:41; 28:25; 34:13“Kwa hiyo sema: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitawakusanyeni kutoka mataifa na kuwarudisha kutoka nchi ambazo mmetawanywa, nami nitawarudishia nchi ya Israeli.’

1811:18 Eze 5:11; 37:2311:18 Eze 5:11; 37:23“Watairudia nchi na kuondoa vinyago vyote vya upotovu na sanamu zote za machukizo. 1911:19 Za 86:11; Yer 32:36; Zek 7:12; Yer 24:7; Rum 2:5; 2Kor 3:3; Eze 36:26; 18:31; 2Nya 30:12Nitawapa moyo mmoja na kuweka roho mpya ndani yao, nitaondoa kutoka ndani yao moyo wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama. 2011:20 Za 105:45; Kut 6:7; Ebr 8:10; Yer 11:4; 32:38; Eze 36:26-28Kisha watafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii sheria zangu. Watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao. 2111:21 Yer 16:11; Eze 16:43; Ebr 3:12; Eze 9:10Lakini kwa wale ambao mioyo yao imeambatana na vinyago vyao vya upotovu na sanamu zao za machukizo, nitaleta juu ya vichwa vyao yale waliyotenda asema Bwana Mwenyezi.”

2211:22 Eze 9:3; 10:19; Kut 24:16Ndipo wale makerubi, wenye magurudumu pembeni mwao, wakakunjua mabawa yao, nao utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao. 2311:23 Eze 1:28; 8:4; Zek 14:4; Eze 10:4Basi utukufu wa Bwana ukapaa juu kutoka mji, ukatua juu ya mlima ulio upande wa mashariki ya mji. 2411:24 2Kor 12:2; Eze 8:3Roho akaniinua na kunileta mpaka kwa watu wa uhamisho huko Ukaldayo nikiwa katika yale maono niliyopewa na Roho wa Mungu.

Ndipo maono niliyokuwa nimeyaona yakanitoka, 2511:25 Eze 3:4, 11; Mdo 20:20nami nikawaeleza wale watu wa uhamisho kila kitu Bwana alichokuwa amenionyesha.

Nueva Versión Internacional

Ezequiel 11:1-25

Juicio contra los líderes de Israel

1El Espíritu me levantó y me llevó hasta la entrada oriental del Templo del Señor. A la entrada vi a veinticinco hombres, entre los cuales estaban Jazanías, hijo de Azur, y Pelatías, hijo de Benaías, que eran líderes del pueblo. 2El Señor me dijo: «Hijo de hombre, estos son los que están tramando maldades y dando malos consejos en esta ciudad. 3Dicen: “Todavía no es el momento de reconstruir las casas. La ciudad es la olla y nosotros somos la carne”. 4Por eso, hijo de hombre, profetiza contra ellos; ¡sí, profetiza!».

5El Espíritu del Señor vino sobre mí y me ordenó proclamar: «Así dice el Señor: “Ustedes, pueblo de Israel, han dicho esto y yo conozco sus pensamientos. 6Han matado a mucha gente en esta ciudad y han llenado las calles de cadáveres.

7»”Por eso yo, el Señor y Dios, les digo: Los cadáveres que ustedes han arrojado son la carne y la ciudad es la olla, pero yo los sacaré de ahí. 8¿Temen a la espada? Pues bien, yo, el Señor y Dios, declaro que con espadas iré contra ustedes. 9Los sacaré de la ciudad, los entregaré en manos de extranjeros y los juzgaré con justicia. 10Morirán a filo de espada; yo los juzgaré en las mismas fronteras de Israel y así sabrán que yo soy el Señor. 11La ciudad no les servirá de olla ni serán ustedes la carne dentro de ella. Yo los juzgaré en la frontera misma de Israel. 12Entonces sabrán que yo soy el Señor. No han seguido mis estatutos ni han cumplido con mis leyes, sino que han adoptado las costumbres de las naciones que los rodean”».

13Mientras yo profetizaba, Pelatías, hijo de Benaías, cayó muerto. Entonces caí rostro en tierra y clamé a gritos: «¡Ay, mi Señor y Dios! ¿Vas a exterminar al remanente de Israel?».

14La palabra del Señor vino a mí y me dijo: 15«Hijo de hombre, esto es lo que dicen los habitantes de Jerusalén en cuanto a tus hermanos, tus parientes y todo el pueblo de Israel: “Ellos se han alejado del Señor, y por eso se nos ha dado esta tierra en posesión”.

16»Por tanto, adviérteles que así dice el Señor y Dios: “Aunque los desterré a naciones lejanas y los dispersé por países extraños, por un tiempo les he servido de santuario en las tierras adonde han ido”.

17»Adviérteles también que así dice el Señor y Dios: “Yo los reuniré de entre las naciones; los juntaré de los países donde han estado dispersos y les daré la tierra de Israel.

18»”Ellos volverán a su tierra y echarán de allí a los ídolos detestables y pondrán fin a todas las abominaciones. 19Yo les daré un corazón sincero y pondré en ellos un espíritu renovado. Les arrancaré el corazón de piedra que ahora tienen y pondré en ellos un corazón de carne, 20para que cumplan mis estatutos y pongan en práctica mis leyes. Entonces ellos serán mi pueblo, y yo seré su Dios. 21Pero a los que van tras esos ídolos detestables y siguen prácticas abominables, yo les pediré cuentas de su conducta”», afirma el Señor y Dios.

La gloria del Señor abandona Jerusalén

22Los querubines desplegaron sus alas. Las ruedas estaban junto a ellos y la gloria del Dios de Israel estaba por encima de ellos. 23La gloria del Señor se elevó de en medio de la ciudad y se detuvo sobre la montaña que está al oriente de Jerusalén. 24En una visión, el Espíritu me levantó y me trasladó hasta donde estaban los exiliados en Babilonia;11:24 Lit. Caldea. y la visión terminó. 25Entonces comuniqué a los exiliados todo lo que el Señor me había revelado.