Esta 7 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Esta 7:1-10

Hamani Aangikwa

17:1 Mwa 40:20-21; Mt 22:1-14Basi mfalme na Hamani wakaenda kula chakula pamoja na Malkia Esta. 27:2 Es 5:3Walipokuwa wakinywa mvinyo katika siku ya pili, mfalme akauliza tena, “Malkia Esta, ni nini haja yako? Utapewa. Ombi lako ni nini? Hata nusu ya ufalme, utapewa.”

3Kisha Malkia Esta akajibu, “Kama nimepata kibali kwako, ee mfalme, tena kama inapendeza utukufu wako, nijalie maisha yangu, hii ndiyo haja yangu. Pia uokoe watu wangu, hili ndilo ombi langu. 47:4 Es 3:9Kwa kuwa mimi na watu wangu tumeuzwa kwa kuangamizwa, kuchinjwa na kuharibiwa. Kama tungalikuwa tumeuzwa tu kuwa watumwa wa kiume na wa kike, ningalinyamaza kimya, kwa sababu shida kama hii isingalitosha kumsumbua mfalme.”

5Mfalme Ahasuero akamuuliza Malkia Esta, “Ni nani huyu? Yuko wapi mtu huyu aliyethubutu kufanya jambo kama hili?”

6Esta akasema, “Mtesi na adui ni huyu mwovu Hamani.”

Hamani alifadhaika mbele ya mfalme na malkia. 77:7 Mwa 34:7; 2Fal 21:18Mfalme akainuka kwa ghadhabu, akaacha mvinyo wake, akaenda kwenye bustani ya jumba la kifalme. Lakini Hamani, akitambua kwamba mfalme ameshaamua hatima yake, alibaki nyuma kumsihi Malkia Esta aokoe maisha yake.

8Mara mfalme aliporudi kutoka bustani ya jumba la kifalme na kuja kwenye ukumbi wa karamu, Hamani alikuwa akijitupa juu ya kiti mahali ambapo Esta alikuwa akiegemea.

Mfalme akasema kwa nguvu, “Je, atamdhalilisha malkia hata huku nyumbani akiwa pamoja nami!”

Mara neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, walifunika uso wa Hamani. 97:9 Za 7:14-16; Mit 11:5-6Kisha Harbona, mmoja wa matowashi wanaomtumikia mfalme, akasema, “Mahali pa kuangika watu penye urefu wa mita ishirini na mbili pako nyumbani mwa Hamani. Alikuwa amepatengeneza kwa ajili ya Mordekai, ambaye alizungumza ili kumsaidia mfalme.”

Mfalme akasema, “Mwangikeni juu yake!” 107:10 Mwa 40:22; Mit 10:28Kwa hiyo wakamtundika Hamani mahali alipokuwa ameandaa kwa ajili ya Mordekai. Ndipo ghadhabu ya mfalme ikatulia.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

以斯帖记 7:1-10

哈曼被处死

1王带着哈曼去赴以斯帖王后的宴席。 2在这第二次宴会中,王在席间又问以斯帖:“以斯帖王后啊,你要什么?我必赐给你。你有何要求?就是半壁江山,也必为你成就。” 3以斯帖回答说:“我若得到王的恩宠,王若愿意,就请王把我的性命和我本族人的性命赐给我——这是我所求的。 4因为我和我本族的人都被卖了,我们将被铲除、杀光、灭尽。如果只是卖我们为奴为婢,我会闭口不语,因为那样的痛苦不值得来打扰王7:4 因为那样的痛苦不值得来打扰王”或译“但王的损失,敌人无法补偿”。。” 5亚哈随鲁王问以斯帖王后:“谁敢这样做?他在哪里?” 6以斯帖回答说:“敌人和仇家就是这恶人哈曼!”哈曼在王和王后面前十分惊恐。

7王大怒,离席去了御花园。哈曼见王定意要惩罚他,便留下来求以斯帖王后饶命。 8王从御花园回到席上,见哈曼伏在以斯帖所靠的榻上,便说:“他竟敢在宫中当着我的面侮辱王后吗?”王这话一出口,便有人蒙了哈曼的脸。 9服侍王的太监哈波拿说:“哈曼为那救驾有功的末底改做了一个二十三米高的木架,如今正立在哈曼家里。”王说:“把哈曼吊在上面!” 10于是,哈曼被吊在他为末底改预备的木架上,王的怒气这才平息。