Ayubu 4 – NEN & NIRV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 4:1-21

Elifazi Anazungumza: Ayubu Ametenda Dhambi

14:1 Mwa 36:11; Ay 15:1; 22:1Ndipo Elifazi Mtemani akajibu:

24:2 Yer 4:19; 20:9; Ay 32:20“Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe,

kutakukasirisha?

Lakini ni nani awezaye

kujizuia asiseme?

34:3 Sef 3:16; Hos 6:3; Ebr 12:12; Kum 32:2; Ay 29:23; 26:2; Za 71:9; Isa 13:7; 35:3Fikiri jinsi ambavyo umewafundisha watu wengi,

jinsi ambavyo umeitia nguvu

mikono iliyokuwa dhaifu.

44:4 Yer 31:8; Ay 16:5; 29:16, 25; Isa 1:17; 35:3; Ebr 12:12Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa;

umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu.

54:5 Rut 1:13; Za 38:2; Ay 6:14; Mit 24:10; Lk 4:23Lakini sasa hii taabu imekujia wewe,

nawe unashuka moyo;

imekupiga wewe,

nawe unafadhaika.

64:6 Mwa 6:9; Za 71:5; Mit 3:26; Ay 1:1; 1Fal 18:19Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa

ndiyo matumaini yako

na njia zako kutokuwa na lawama

ndilo taraja lako?

74:7 Za 41:12; 91:9-10; 37:25; 2Pet 2:9; Mit 12:21; Ay 5:11; 36:7; Mt 19:23“Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia?

Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa?

84:8 Amu 14:18; Gal 6:7-8; Hos 8:7; Za 7:14; Yos 1:9; Ay 5:3; 15:17; 5:6; 15:35; Mt 11:18Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza,

wale walimao ubaya

na wale hupanda uovu,

huvuna hayo hayo hayo.

94:9 Kut 15:10; 2The 2:8; Law 26:38; Isa 25:7; Ay 41:21; 40:13Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa;

kwa mshindo wa hasira zake huangamia.

104:10 Ay 38:15; 29:17; Za 22:13; 17:12; 22:21; Mt 28:15Simba anaweza kunguruma na kukoroma,

lakini bado meno ya simba mkubwa huvunjika.

114:11 Kum 28:41; Mit 30:14; Ay 5:4; Za 34:10; 58:6; Ay 27:14; 29:17Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo,

nao wana wa simba jike hutawanyika.

124:12 Ay 26:14; 33:14; 32:13; 12:23; Yer 9:23; Za 78:59“Neno lililetwa kwangu kwa siri,

masikio yangu yakasikia mnongʼono wake.

134:13 Ay 33:15Katikati ya ndoto za kutia wasiwasi wakati wa usiku,

hapo usingizi mzito uwapatapo wanadamu,

144:14 Dan 10:8; Hab 3:16; Ay 21:6; Za 48:6; 55:5; 119:120, 161; Yer 5:22; 2Kor 7:15hofu na kutetemeka kulinishika

na kufanya mifupa yangu yote itetemeke.

154:15 Za 104:4; Mt 14:26; Ebr 1:14; Dan 5:6; 7:15, 28; 10:8Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu,

nazo nywele za mwili wangu zikasimama.

164:16 1Fal 19:12Yule roho akasimama,

lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani.

Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu,

kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti:

174:17 Za 143:2; Mdo 17:24; Mal 2:10; Mit 20:9; Ay 9:2; 8:3; 10:3; 14:4; 15:14; 13:18; Mhu 7:20; Isa 51:13‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu?

Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake?

184:18 Ay 25:5; 21:22; 5:4; 1Pet 2:4; Ebr 1:14Kama Mungu hawaamini watumishi wake,

kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea,

194:19 Isa 64:8; 2Kor 4:7; 2Pet 2:4; Mwa 2:7ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba

za udongo wa mfinyanzi,

ambazo misingi yake ipo mavumbini,

ambao wamepondwa kama nondo!

204:20 Za 89:47; 90:5-6; Yak 4:14; Ay 14:2, 20; 15:33; 20:7Kati ya mawio na machweo

huvunjwa vipande vipande;

bila yeyote kutambua,

huangamia milele.

214:21 Ay 8:22; Isa 38:12; Mit 5:23; Yn 8:24; Yer 9:3Je, kamba za hema yao hazikungʼolewa,

hivyo hufa bila hekima?’

New International Reader’s Version

Job 4:1-21

The First Speech of Eliphaz

1Then Eliphaz the Temanite replied,

2“Job, suppose someone tries to talk to you.

Will that make you uneasy?

I can’t keep from speaking up.

3Look, you taught many people.

You made weak hands strong.

4Your words helped those who had fallen down.

You made shaky knees strong.

5Now trouble comes to you. And you are unhappy about it.

It strikes you down. And you are afraid.

6Shouldn’t you worship God and trust in him?

Shouldn’t your honest life give you hope?

7“Here’s something to think about.

Have people who aren’t guilty ever been wiped out?

Have honest people ever been completely destroyed?

8Here’s what I’ve observed.

People gather a crop from what they plant.

If they plant evil and trouble, that’s what they will harvest.

9The breath of God destroys them.

The blast of his anger wipes them out.

10Powerful lions might roar and growl.

But their teeth are broken.

11Lions die because they don’t have any food.

Then their cubs are scattered.

12“A message came to me in secret.

It was as quiet as a whisper.

13I had a scary dream one night.

I was sound asleep.

14Fear and trembling seized me.

That made every bone in my body shake.

15A spirit glided past my face.

The hair on my body stood on end.

16Then the spirit stopped.

But I couldn’t tell what it was.

Something stood there in front of me.

I heard a soft voice.

17It said, ‘Can a human being be more right than God?

Can even a strong man be more pure than the God who made him?

18God doesn’t trust those who serve him.

He even brings charges against his angels.

19So he’ll certainly find fault with human beings.

After all, they are made out of dust.

They can be crushed more easily than a moth.

20Between sunrise and sunset they are broken to pieces.

Nobody even notices. They disappear forever.

21Like a tent that falls down, they get weak.

They die because they didn’t follow God’s wisdom.’ ”