Ayubu 16 – NEN & NAV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ayubu 16:1-22

Hotuba Ya Tano Ya Ayubu

Ayubu Anathibitisha Tena Hali Yake Ya Kutokuwa Na Hatia

1Kisha Ayubu akajibu:

216:2 Ay 6:15; 13:4; Za 69:20“Nimepata kusikia mambo mengi kama haya,

nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha!

316:3 Ay 6:26; 11:2; 18:2Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho?

Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno?

416:4 Mt 27:29; Yer 18:16; Mao 2:15Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi,

kama mngekuwa katika hali yangu;

ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu,

na kuwatikisia ninyi kichwa changu.

516:5 Ay 29:25; Mwa 37:35Lakini kinywa changu kingewatia moyo;

faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu.

616:6 Ay 6:3; 7:21“Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi;

nami kama nikijizuia, wala hayaondoki.

716:7 Amu 8:5; Ay 7:3; 1:19Ee Mungu, hakika umenichakaza;

umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote.

816:8 Mao 5:17; Ay 10:17; 17:7; 19:20; Za 22:17; 88:9; 6:7Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi;

nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu.

916:9 Ay 12:14; 13:24; Mao 2:16; Mdo 7:54; Hos 6:1; Ay 30:21; 9:5; 18:4; 19:11Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake,

na kunisagia meno yake;

adui yangu hunikazia macho yake makali.

1016:10 Za 22:13; Mao 3:30; Mdo 7:57; 23:2; Za 27:3; Mik 5:1Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki;

hunipiga shavuni mwangu kwa dharau,

na kuungana pamoja dhidi yangu.

1116:11 Ay 9:24Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya,

na kunitupa katika makucha ya waovu.

1216:12 Ay 9:17; 6:4; Mao 3:12Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja;

amenikamata shingo na kuniponda.

Amenifanya mimi kuwa shabaha yake;

1316:13 Mit 7:23; Mao 3:13wapiga upinde wake wananizunguka.

Bila huruma, huchoma figo zangu,

na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi.

1416:14 Ay 9:17; 10:3; Yoe 2:7Huniponda tena na tena;

hunishambulia kama shujaa wa vita.

1516:15 Mwa 37:34; Ay 2:8“Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu

nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi.

1616:16 Ay 16:20; 2:7; 17:7; 30:17, 30; Isa 52:14; Za 6:6Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia,

macho yangu yamepigwa na giza kuu.

1716:17 Yer 18:11; Yon 3:8Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri,

na maombi yangu ni safi.

1816:18 Mwa 4:10; Ay 27:9; Isa 26:21; Za 66:18-19; Ebr 11:4“Ee nchi, usiifunike damu yangu,

nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe.

1916:19 Mwa 31:50; Rum 1:9; 1The 2:5; Ay 22:12; 19:27; Za 113:5; Isa 33:5Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni;

wakili wangu yuko juu.

2016:20 Mao 2:19; Rum 8:34; Yn 15:15; Ay 16:16Mwombezi wangu ni rafiki yangu

macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu;

2116:21 1Fal 8:45; Za 140:12kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu

kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake.

2216:22 Ay 10:21; Mhu 12:5“Ni miaka michache tu itapita

kabla sijaenda safari ambayo sitarudi.

Ketab El Hayat

أيوب 16:1-22

أيوب

1فَقَالَ أَيُّوبُ: 2«قَدْ سَمِعْتُ كَثِيراً مِثْلَ هَذَا الْكَلامِ وَأَنْتُمْ كُلُّكُمْ مُعَزُّونَ مُتْعِبُونَ. 3أَمَا لِهَذَا اللَّغْوِ مِنْ نِهَايَةٍ؟ وَمَا الَّذِي يُثِيرُكَ حَتَّى تَرُدَّ عَلَيَّ؟ 4فِي وُسْعِي أَنْ أَتَكَلَّمَ مِثْلَكُمْ لَوْ كُنْتُمْ مَكَانِي، وَأُلْقِيَ عَلَيْكُمْ أَقْوَالَ مَلامَةٍ، وَأَهُزَّ رَأْسِي فِي وُجُوهِكُمْ، 5بَلْ كُنْتُ أُشَجِّعُكُمْ بِنَصَائِحِي، وَأُشَدِّدُكُمْ بِتَعْزِيَاتِي.

6إِنْ تَكَلَّمْتُ لَا تُمْحَى كَآبَتِي، وَإِنْ صَمَتُّ، فَمَاذَا يُخَفِّفُ الصَّمْتُ عَنِّي؟ 7إِنَّ اللهَ قَدْ مَزَّقَنِي حَقّاً وَأَهْلَكَ كُلَّ قَوْمِي. 8لَقَدْ كَبَّلْتَنِي فَصَارَ ذَلِكَ شَاهِداً عَلَيَّ، وَقَامَ هُزَالِي لِيَشْهَدَ ضِدِّي. 9مَزَّقَنِي غَضَبُهُ، وَاضْطَهَدَنِي. حَرَّقَ عَلَيَّ أَسْنَانَهُ. طَعَنَنِي عَدُوِّي بِنَظْرَاتِهِ الْحَادَّةِ. 10فَغَرَ النَّاسُ أَفْوَاهَهُمْ عَلَيَّ، لَطَمُونِي تَعْيِيراً عَلَى خَدِّي، وَتَضَافَرُوا عَلَيَّ جَمِيعاً. 11أَسْلَمَنِي اللهُ إِلَى الظَّالِمِ، وَطَرَحَنِي فِي يَدِ الأَشْرَارِ. 12كُنْتُ مُطْمَئِنّاً مُسْتَقِرّاً، فَزَعْزَعَنِي الرَّبُّ وَقَبَضَ عَلَيَّ مِنْ عُنُقِي، وَحَطَّمَنِي وَنَصَبَنِي لَهُ هَدَفاً. 13حَاصَرَنِي رُمَاتُهُ وَشَقَّ كُلْيَتَيَّ مِنْ غَيْرِ رَحْمَةٍ، أَهْرَقَ مَرَارَتِي عَلَى الأَرْضِ. 14اقْتَحَمَنِي مَرَّةً تِلْوَ مَرَّةٍ، وَهَاجَمَنِي كَجَبَّارٍ. 15خِطْتُ مِسْحاً عَلَى جِلْدِي، وَمَرَّغْتُ عِزِّي فِي التُّرَابِ. 16احْمَرَّ وَجْهِي مِنَ الْبُكَاءِ، وَغَشِيَتْ ظِلالُ الْمَوْتِ أَهْدَابِي، 17مَعَ أَنَّنِي لَمْ أَقْتَرِفْ ظُلْماً، وَصَلاتِي مُخْلِصَةٌ.

18يَا أَرْضُ لَا تَسْتُرِي دَمِي، وَلا يَكُنْ لِصُرَاخِي قَرَارٌ. 19هُوَذَا الآنَ شَاهِدِي فِي السَّمَاءِ، وَكَفِيلِي فِي الأَعَالِي 20أَمَّا أَصْحَابِي فَهُمُ السَّاخِرُونَ بِي، لِذَلِكَ تَفِيضُ دُمُوعِي أَمَامَ اللهِ، 21لَكَمْ أَحْتَاجُ لِمَنْ يُدَافِعُ عَنِّي أَمَامَ اللهِ، كَمَا يُدَافِعُ إِنْسَانٌ عَنْ صَدِيقِهِ. 22إِذْ مَا إِنْ تَنْقَضِي سَنَوَاتُ عُمْرِي الْقَلِيلَةُ حَتَّى أَمْضِيَ فِي طَرِيقٍ لَا أَعُودُ مِنْهَا.