Amosi 2 – NEN & HOF

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Amosi 2:1-16

12:1 Eze 25:8; Sef 2:8; 2Fal 3:27; Isa 16:6; 33:2Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Moabu,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu alichoma mifupa ya mfalme wa Edomu,

ikawa kama chokaa.

22:2 Yer 48:7, 24; Ay 39:25; Yos 6:20Nitatuma moto juu ya Moabu

ambao utateketeza ngome za Keriothi.

Moabu ataanguka kwa ghasia kubwa

katikati ya vilio vya vita na mlio wa tarumbeta.

32:3 Hes 24:17; Za 2:10; Isa 40:23; Eze 25:8-11; Sef 2:8-9Nitamwangamiza mtawala wake

na kuwaua maafisa wake wote pamoja naye,”

asema Bwana.

42:4 Law 26:14; 2Sam 12:9, 10; 2Nya 36:14-17; Neh 1:7; Hos 12:2; Eze 9:11; Dan 9:11; 2Fal 17:19; Yer 6:19; 16:12; Isa 5:24; 9:16; 28:15; Kut 34:15Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Yuda,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Kwa sababu wameikataa sheria ya Bwana

na hawakuzishika amri zake,

kwa sababu wamepotoshwa na miungu ya uongo,

miungu ambayo babu zao waliifuata.

52:5 Yer 17:27; Hos 8:14; 2Fal 25:9; Amo 3:11; 2Nya 36:19Nitatuma moto juu ya Yuda

ambao utateketeza ngome za Yerusalemu.”

Hukumu Juu Ya Israeli

62:6 Isa 29:21; Yoe 3:3; Amo 5:11, 12; 8:6Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kwa dhambi tatu za Israeli,

hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.

Wanawauza wenye haki kwa fedha,

na maskini kwa jozi ya viatu.

72:7 Eze 36:20; 22:11; Law 18:21; 20:3; Amo 8:4; 5:11-12; Rum 2:24; Isa 10:2Wanakanyaga juu ya vichwa vya maskini,

kama vile juu ya mavumbi ya nchi,

na kukataa haki kwa walioonewa.

Baba na mwanawe hushiriki msichana mmoja,

kwa hivyo hulinajisi Jina langu takatifu.

82:8 Kut 22:26; Hos 7:14; 1Kor 10:21; Hab 2:6; Amo 6:6; Kum 24:12-14Watu hulala kando ya kila madhabahu

juu ya nguo zilizowekwa rehani.

Katika nyumba ya mungu wao hunywa mvinyo

ulionunuliwa kwa fedha walizotozwa watu.

92:9 Hes 13:32; 21:23-26; Yos 10:12; Ay 18:16; Mal 4:1; Isa 10:33; Za 29:9“Nilimwangamiza Mwamori mbele yao,

ingawa alikuwa mrefu kama mierezi,

na mwenye nguvu kama mialoni.

Niliyaangamiza matunda yake juu

na mizizi yake chini.

102:10 Kut 6:6; 20:2; Hes 21:23; Yos 13:4; Amo 9:7; Kum 8:2; 2:7“Niliwapandisha toka Misri,

na nikawaongoza miaka arobaini jangwani

niwape nchi ya Waamori.

112:11 Kut 18:18; Yer 7:25; Hes 6:2-3; Amu 13:5Pia niliinua manabii kutoka miongoni mwa wana wenu

na Wanadhiri kutoka miongoni mwa vijana wenu.

Je, hii si kweli, enyi watu wa Israeli?”

asema Bwana.

122:12 Mdo 4:18; Isa 30:10; Yer 11:21; Amo 7:12-13; Mik 2:6“Lakini mliwafanya Wanadhiri kunywa mvinyo

na kuwaamuru manabii wasitoe unabii.

13“Sasa basi, nitawaponda

kama gari lipondavyo wakati limejazwa nafaka.

142:14 1Fal 20:11; Yer 9:23; Za 33:16; Ay 11:20; Isa 30:16-17Mkimbiaji hodari hatanusurika,

wenye nguvu wataishiwa nguvu zao,

na shujaa hataweza kuokoa maisha yake.

152:15 Eze 39:3; Kut 15:21; Zek 10:5; Mhu 9:11Mpiga upinde atakimbia,

askari wapiga mbio hawataweza kutoroka,

na mpanda farasi hataokoa maisha yake.

162:16 Yer 48:41Hata askari walio mashujaa sana

siku hiyo watakimbia uchi,”

asema Bwana.

Hoffnung für Alle

Amos 2:1-16

1So spricht der Herr: Die Leute von Moab begehen ein abscheuliches Verbrechen nach dem anderen. Sie haben die Gebeine des Königs von Edom zu feiner Asche2,1 Oder: zu Kalk. – Dieser wurde als weißer Farbstoff verwendet, um Wände zu tünchen. verbrannt. Das werde ich nicht ungestraft lassen! 2Das ganze Land und auch die Paläste von Kerijot werden ein Raub der Flammen. Die Feinde blasen zum Angriff, sie stimmen das Kriegsgeschrei an, und die Moabiter fallen im lauten Getöse der Schlacht. 3Den Herrscher von Moab bringe ich um, mitsamt den führenden Männern. Darauf gebe ich, der Herr, mein Wort!«

Auch Juda und Israel kommen nicht davon

4»So spricht der Herr: Die Leute von Juda begehen ein abscheuliches Verbrechen nach dem anderen. Sie treten mein Gesetz mit Füßen und leben nicht nach den Geboten, die ich, der Herr, ihnen gegeben habe. Sie ließen sich von den falschen Göttern verführen, denen schon ihre Vorfahren nachgelaufen sind. Das werde ich nicht ungestraft lassen! 5Ich brenne das ganze Land nieder, und Jerusalems Paläste werden ein Raub der Flammen.

6So spricht der Herr: Die Leute von Israel begehen ein abscheuliches Verbrechen nach dem anderen. Das werde ich nicht ungestraft lassen! Ehrbare Menschen, die ihnen Geld schulden, verkaufen sie in die Sklaverei, ja, sie verkaufen einen Armen schon, wenn er ein Paar Schuhe nicht bezahlen kann! 7Den Wehrlosen treten sie in den Staub, und dem Schwachen verweigern sie sein Recht. Vater und Sohn gehen mit ein und demselben Mädchen ins Bett und ziehen damit meinen heiligen Namen in den Schmutz. 8Neben jedem Altar machen sie sich weiche Polster aus den Kleidern, die sie den Armen als Pfand wegnehmen. Im Tempel ihres Gottes2,8 Oder: ihrer Götter. saufen sie Wein, den sie für nicht bezahlte Schulden gefordert haben!

9Dabei war ich es doch, der die Amoriter vernichtet hat, um ihr Land den Israeliten zu geben! Sie waren so groß wie Zedern und so stark wie Eichen, aber ich habe sie mit Stumpf und Stiel ausgerottet. 10Ja, ich habe euch aus Ägypten befreit und vierzig Jahre lang durch die Wüste geleitet, bis ihr das Land der Amoriter in Besitz nehmen konntet. 11Einige von euch habe ich als Propheten erwählt und junge Männer berufen, sich mir zum Dienst zu weihen. Ich, der Herr, frage euch Israeliten: Habe ich nicht dies alles für euch getan? 12Ihr aber habt diejenigen, die sich mir geweiht hatten, gezwungen, ihr Gelübde zu brechen und Wein zu trinken. Den Propheten habt ihr verboten, euch meine Botschaft weiterzusagen.

13Darum werde ich euch eine Last aufbürden, unter der ihr hin- und herschwankt wie ein zu voller Erntewagen!2,13 Der hebräische Text ist nicht sicher zu deuten. 14Sogar der Schnellste unter euch kann dann nicht mehr entfliehen, dem Stärksten hilft seine Kraft nicht mehr, und der beste Soldat verliert sein Leben. 15Die Bogenschützen werden überrannt, die besten Läufer und schnellsten Reiter auf der Flucht getötet. 16Selbst der mutigste Soldat lässt an jenem Tag die Waffen fallen und rennt um sein Leben. Darauf gebe ich, der Herr, mein Wort!