2 Wafalme 8 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 8:1-29

Ardhi Ya Mshunami Yarudishwa

18:1 2Fal 4:8-37; Kum 28:22Wakati huu, Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke ambaye mwanawe alikuwa amefufuliwa, “Ondoka wewe na jamaa yako ukaishi mahali popote unapoweza kwa kitambo kidogo, kwa sababu Bwana ameamuru njaa katika nchi hii ambayo itadumu kwa miaka saba.” 2Yule mwanamke akafanya kama vile yule mtu wa Mungu alivyosema. Yeye na jamaa yake wakaondoka na kwenda kuishi katika nchi ya Wafilisti kwa miaka saba.

3Baada ya miaka saba, yule mwanamke akarudi kutoka nchi ya Wafilisti, akaenda kwa mfalme kumsihi kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake. 4Mfalme alikuwa anazungumza na Gehazi, mtumishi wa mtu wa Mungu, naye alikuwa amesema, “Hebu niambie mambo yote makuu yaliyofanywa na Elisha.” 58:5 2Fal 4:35Wakati Gehazi alipokuwa akimweleza mfalme jinsi Elisha alivyomfufua mtu, yule mwanamke ambaye mwanawe alikuwa amefufuliwa na Elisha akaja ili amsihi mfalme kwa ajili ya nyumba yake na shamba lake.

Gehazi akasema, “Huyu ndiye huyo mwanamke, bwana wangu mfalme, na huyu ndiye mwanawe ambaye Elisha alimfufua.” 6Mfalme akamuuliza yule mwanamke kuhusu mambo hayo, naye akamweleza.

Ndipo akaamuru afisa ashughulikie shauri lake na kumwambia, “Mrudishie huyu mwanamke kila kitu kilichokuwa mali yake, pamoja na mapato yote yaliyotokana na shamba lake tangu siku alipoondoka nchini hadi sasa.”

Hazaeli Anamuua Ben-Hadadi

78:7 2Sam 8:5; 2Fal 6:27Elisha akaenda Dameski, naye Ben-Hadadi mfalme wa Aramu alikuwa mgonjwa. Mfalme alipoambiwa, “Mtu wa Mungu ametoka mbali akapanda hadi hapa,” 88:8 1Fal 19:15; 1Sam 9:7mfalme akamwambia Hazaeli. “Chukua zawadi na uende kumlaki huyo mtu wa Mungu. Muulize Bwana kupitia yeye, kwamba, ‘Je, nitapona ugonjwa huu?’ ”

9Hazaeli akaenda kumlaki Elisha, akiwa amechukua zawadi ya kila kitu kizuri kilichopatikana Dameski, mizigo iliyobebwa na ngamia arobaini. Akaingia ndani na kusimama mbele yake, akasema, “Mwanao Ben-Hadadi mfalme wa Aramu amenituma niulize, ‘Je, nitapona ugonjwa huu?’ ”

10Elisha akajibu, “Nenda ukamwambie, ‘Hakika utapona’; lakini Bwana amenifunulia kwamba kweli atakufa.” 118:11 Lk 19:41; Amu 3:25Elisha akamkazia Hazaeli macho kwa nguvu mpaka akaona aibu. Kisha mtu wa Mungu akaanza kulia.

128:12 1Fal 19:17; 2Fal 15:16Hazaeli akauliza “Kwa nini bwana wangu analia?”

Elisha akajibu, “Kwa sababu najua mabaya utakayowatendea Waisraeli. Utachoma moto ngome zao, utawaua vijana wao kwa upanga, kuwatupa chini kwa nguvu watoto wachanga, na kuwatumbua wanawake wenye mimba.”

138:13 1Sam 17:43; 1Fal 19:15Hazaeli akasema, “Itawezekanaje mtumishi wako, aliye mbwa tu, kufanya tendo la ajabu namna hiyo?”

Elisha akamjibu, “Bwana amenionyesha kuwa utakuwa mfalme wa Aramu.”

14Kisha Hazaeli akamwacha Elisha na kumrudia bwana wake. Ben-Hadadi akamuuliza, “Elisha alikuambia nini?” Hazaeli akajibu, “Aliniambia kwamba hakika utapona.” 158:15 2Fal 1:17Lakini kesho yake Hazaeli akachukua nguo nzito, akailoweka ndani ya maji, akaitandaza juu ya uso wa mfalme, hivyo akafa. Kisha Hazaeli akaingia mahali pake kuwa mfalme wa Aramu.

Yehoramu Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 21:1-20)

168:16 2Fal 1:17; 2Nya 21:1-4Katika mwaka wa tano wa Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli, wakati huo Yehoshafati akiwa mfalme wa Yuda, Yehoramu mwana wa Yehoshafati akaanza kutawala kama mfalme wa Yuda. 17Alikuwa na umri wa miaka thelathini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka minane. 18Akaenenda katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alimwoa binti wa Ahabu. Akatenda maovu machoni pa Bwana. 198:19 2Sam 21:17Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi mtumishi wake, Bwana hakutaka kuiangamiza Yuda. Alikuwa ameahidi kuidumisha taa kwa ajili ya Daudi na wazao wake milele.

208:20 1Fal 22:47Wakati wa Yehoramu, Edomu waliasi dhidi ya Yuda na kujiwekea mfalme wao wenyewe. 21Basi Yehoramu akaenda Sairi pamoja na magari yake yote ya vita. Waedomu wakamzunguka yeye na majemadari wake wa magari yake ya vita, lakini akaondoka, akapenya usiku na kuwashambulia Waedomu. Hata hivyo, jeshi lake likatorokea nyumbani mwao. 228:22 Mwa 27:40; Yos 21:13Hadi leo Edomu wameasi dhidi ya Yuda. Libna pia wakaasi wakati huo huo.

23Kwa matukio mengine ya utawala wa Yehoramu na yote aliyoyafanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? 24Yehoramu akalala pamoja na baba zake, na akazikwa pamoja nao katika Mji wa Daudi. Naye Ahazia mwanawe akawa mfalme baada yake.

Ahazia Mfalme Wa Yuda

(2 Nyakati 22:1-6)

258:25 2Fal 9:29Katika mwaka wa kumi na mbili wa utawala wa Yoramu mwana wa Ahabu mfalme wa Israeli, Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda alianza kutawala. 268:26 2Fal 8:18; 1Fal 16:23Ahazia alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala, naye akatawala katika Yerusalemu kwa mwaka mmoja. Mama yake aliitwa Athalia, mjukuu wa Omri mfalme wa Israeli. 278:27 1Fal 16:30; 15:26Akaenenda katika njia za nyumba ya Ahabu, na kutenda maovu machoni pa Bwana, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa imefanya, kwa kuwa alikuwa ameoa kutoka nyumba ya Ahabu.

288:28 Kum 4:43; 2Fal 9:1, 14Ahazia akaenda vitani na Yoramu mwana wa Ahabu kupigana na Hazaeli mfalme wa Aramu huko Ramoth-Gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu. 298:29 1Fal 21:29; 2Fal 10:13Hivyo Mfalme Yoramu akarudi Yezreeli ili apate kuuguza majeraha aliyojeruhiwa na Waaramu huko Ramothi8:29 Yaani Rama kwa Kiebrania. alipopigana na Hazaeli mfalme wa Aramu.

Ndipo Ahazia mwana wa Yehoramu mfalme wa Yuda akashuka kwenda Yezreeli kumtazama Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu alikuwa amejeruhiwa.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

列王紀下 8:1-29

書念婦人得回產業

1以利沙曾經救活了一位書念婦人的兒子。他對那婦人說:「你和家人要離開這裡去別處寄居,因為耶和華已決定使這裡遭受七年饑荒。」 2那婦人遵照上帝僕人的話,舉家遷往非利士,在那裡寄居了七年。 3七年後,她從非利士返回,去向王請求收回自己的房屋和田地。 4那時,王正與上帝僕人的侍者基哈西談話,讓基哈西以利沙所做的一切大事講給他聽。 5基哈西正在向王講述以利沙如何使死人復活的時候,那位書念婦人剛好進宮求見王,基哈西便說:「我主我王,這就是那婦人,這是她那個被以利沙救活的兒子。」 6王問那婦人,她便原原本本地將那件事稟告王。王委派一位臣僕處理她的事情,並吩咐說:「凡屬於這婦人的東西,包括從她離開本地直到今天她田地的所有出產,要全部還給她。」

以利沙對哈薛的預言

7一天,以利沙到了大馬士革。當時亞蘭便·哈達正在生病,他得知上帝的僕人來了, 8便對哈薛說:「你帶著禮物去見上帝的僕人,請他求問耶和華,看看我這病能否痊癒。」 9哈薛用四十頭駱駝馱著大馬士革的各種美物前去拜見以利沙。到了那裡,他站在以利沙面前說:「你兒子亞蘭便·哈達派我來問你,他的病能否痊癒?」

10以利沙哈薛說:「你去告訴他,他一定會痊癒。不過,耶和華告訴我他會死。」 11他目不轉睛地盯著哈薛,盯得他很不安。然後,上帝的僕人哭了。 12哈薛問:「我主為什麼哭呢?」以利沙說:「因為我知道你會加害以色列人。你會放火燒他們的堡壘,用刀殺戮他們的壯丁,摔死他們的孩童,剖開他們的孕婦。」 13哈薛說:「你僕人算什麼,不過是一條狗,怎能做這樣的大事呢?」以利沙說:「耶和華告訴我,你要做亞蘭王。」 14哈薛辭別以利沙回去了。王問他:「以利沙對你說什麼?」他答道:「以利沙告訴我,你一定會痊癒。」 15第二天,哈薛拿了一床浸透水的被子,蒙在王的臉上,王窒息而死。於是哈薛篡位。

約蘭做猶大王

16以色列亞哈的兒子約蘭執政第五年,猶大約沙法讓位給兒子約蘭17約蘭三十二歲登基,在耶路撒冷執政八年。 18他與亞哈家一樣步以色列諸王的後塵,因為他娶了亞哈的女兒為妻,做耶和華視為惡的事。 19但耶和華因祂僕人大衛的緣故而不願毀滅猶大,因為祂曾應許讓大衛的子孫永遠做王。 20約蘭執政期間,以東人反叛猶大,自己立王。 21約蘭率領所有戰車前往撒益,他和戰車長們被以東人包圍。他們乘夜出擊,突出重圍,各自逃回家去。 22以東人至今仍脫離猶大的統治。立拿人也在那個時候叛變了。

23約蘭其他的事及其一切所作所為都記在猶大列王史上。 24約蘭與祖先同眠後,葬在大衛城他的祖墳裡。他兒子亞哈謝繼位。

亞哈謝做猶大王

25以色列亞哈的兒子約蘭執政第十二年,猶大約蘭的兒子亞哈謝登基。 26他二十二歲登基,在耶路撒冷執政一年。他母親叫亞她利雅,是以色列暗利的孫女。 27亞哈謝亞哈家的女婿,他步亞哈家的後塵,做耶和華視為惡的事。

28他聯合亞哈的兒子約蘭基列拉末亞蘭哈薛交戰。約蘭受了傷, 29便回到耶斯列療傷。猶大亞哈謝前去探望。