2 Wafalme 5 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Wafalme 5:1-27

Naamani Aponywa Ukoma

15:1 Mwa 10:22; Lk 4:27Wakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kupitia kwake, Bwana alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari shujaa, lakini alikuwa na ukoma.5:1 Ukoma ni neno lililotumika kwa Kiebrania kueleza magonjwa mbalimbali ya ngozi ambayo si lazima yawe ni ukoma halisi.

25:2 2Fal 6:23Siku hizo vikosi kutoka Aramu vilikuwa vimekwenda na vikawa vimemteka msichana kutoka Israeli, naye akamtumikia mkewe Naamani. 35:3 Mwa 20:7Akamwambia bibi yake, “Kama bwana wangu angelimwona nabii aliyeko Samaria! Angemponya ukoma wake.”

4Naamani akaenda kwa bwana wake na kumwambia alichosema yule msichana kutoka Israeli. 55:5 Mwa 24:53; 1Sam 9:7Mfalme wa Aramu5:5 Yaani mfalme wa Shamu. akamjibu, “Hakika, nenda. Nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo Naamani akaondoka, akiwa amechukua talanta kumi5:5 Talanta 10 za fedha ni sawa na kilo 340. za fedha, shekeli 6,000 za dhahabu,5:5 Shekeli 6,000 za dhahabu ni sawa na kilo 70. na mivao kumi ya mavazi. 6Barua aliyopelekea mfalme wa Israeli iliandikwa hivi: “Pamoja na barua hii ninamtuma mtumishi wangu, Naamani, kwako ili uweze kumponya ukoma wake.”

75:7 Mwa 30:2; Kum 32:39; 1Fal 20:7Mara mfalme wa Israeli alipomaliza kuisoma ile barua, akararua mavazi yake na kusema, “Je, mimi ni Mungu? Je, mimi naweza kuua na kufufua tena? Kwa nini huyu mtu anamtuma mtu ili mimi nipate kumponya ukoma wake? Tazama jinsi anavyotafuta kuanzisha ugomvi nami!”

85:8 1Fal 22:7Elisha mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alikuwa amerarua mavazi yake, akamtumia ujumbe huu: “Kwa nini umerarua mavazi yako? Mwamuru mtu huyo aje kwangu, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli.” 9Kwa hiyo Naamani akaenda, akiwa na farasi zake na magari yake, na kusimama mlangoni mwa nyumba ya Elisha. 105:10 Yn 9:7; Law 14:7Elisha akamtuma mjumbe kumwambia, “Nenda uoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itapona, nawe utatakasika.”

115:11 Kut 7:19Lakini Naamani akaondoka akiwa amekasirika, akasema, “Hakika nilidhani kwamba angetoka nje, asimame na kuliitia jina la Bwana Mungu wake, na kuweka mkono wake juu ya mahali pagonjwa, aniponye ukoma wangu. 125:12 Mit 14:17, 29Je, Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora zaidi kuliko mito yoyote ya Israeli? Je, nisingeweza kuoga ndani ya hiyo mito na kutakasika?” Basi akageuka na kuondoka kwa hasira kuu.

135:13 2Fal 6:21Watumishi wa Naamani wakamwendea na kumwambia, “Baba yangu, kama huyo nabii angekuambia kufanya jambo lililo kubwa, je, usingelifanya? Je, si zaidi sana basi, anapokuambia, ‘Oga na utakasike!’ ” 145:14 Law 14:7; Ay 33:25Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo.

155:15 Yos 4:24; 1Sam 17:46Kisha Naamani na wahudumu wake wote wakarudi kwa yule mtu wa Mungu. Akasimama mbele yake na kusema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu katika ulimwengu wote isipokuwa katika Israeli. Tafadhali sasa upokee zawadi kutoka kwa mtumishi wako.”

165:16 Mwa 14:23; Dan 5:17Nabii akajibu, “Hakika kama Bwana aishivyo, ambaye ninamtumikia, sitapokea kitu hata kimoja.” Ingawa Naamani alimsihi sana, yeye alikataa.

175:17 Kut 20:24Naamani akasema, “Ikiwa hutapokea, tafadhali mtumishi wako na apewe udongo kiasi cha mzigo wa kuweza kubebwa na punda wawili, kwa sababu mtumishi wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa na dhabihu kwa mungu mwingine isipokuwa Bwana. 185:18 2Fal 7:2Lakini Bwana na amsamehe mtumishi wake kwa kitu hiki kimoja: Wakati bwana wangu atakapoingia kwenye hekalu la Rimoni ili kusujudu, naye akiwa anauegemea mkono wangu, nami nikasujudu huko pia, wakati nitakaposujudu ndani ya hekalu la Rimoni, Bwana na amsamehe mtumishi wako kwa ajili ya jambo hili.”

195:19 1Sam 1:17; Mdo 15:33Elisha akamwambia, “Nenda kwa amani.”

Baada ya Naamani kusafiri umbali fulani, 205:20 Kut 20:7Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akajiambia mwenyewe, “Bwana wangu amemwachia kirahisi sana Naamani, huyu Mwaramu, kwa kutokupokea kutoka kwake vile alivyovileta. Hakika kama Bwana aishivyo, nitamkimbilia na kupata kitu kutoka kwake.”

21Hivyo Gehazi akaharakisha kumfuatilia Naamani. Naamani alipomwona akikimbia kumwelekea, akashuka chini kutoka kwenye gari lake na kwenda kumlaki. Akauliza, “Je, mambo yote ni sawa?”

225:22 2Fal 5:5; Mwa 45:22Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa. Bwana wangu amenituma nikuambie, ‘Vijana wawili kutoka kwa wana wa manabii wamenijia kutoka nchi ya vilima ya Efraimu. Tafadhali wape talanta ya fedha5:22 Talanta ya fedha ni sawa na kilo 34. na mivao miwili ya mavazi.’ ”

23Naamani akasema, “Hakika, chukua talanta mbili za fedha.” Akamsihi Gehazi azipokee, kisha akafunga talanta mbili za fedha katika mifuko miwili pamoja na mivao miwili ya mavazi. Akawapa watumishi wake wawili mizigo hiyo, nao wakaibeba wakitangulia mbele ya Gehazi. 24Gehazi alipofika kwenye kilima, akavichukua vile vitu kutoka kwa wale watumishi na kuvificha ndani ya nyumba. Akawaaga wale watu, nao wakaondoka. 25Kisha akaingia ndani na kusimama mbele ya Elisha bwana wake.

Elisha akamuuliza, “Gehazi, ulikuwa wapi?”

Gehazi akajibu, “Mtumishi wako hakwenda popote.”

265:26 2Fal 5:16; Yer 45:5Lakini Elisha akamwambia, “Je, roho yangu haikuwa pamoja nawe wakati yule mtu aliposhuka kutoka kwenye gari lake ili kukulaki? Je, huu ni wakati wa kupokea fedha au kupokea nguo, mashamba ya mizeituni, mashamba ya mizabibu, makundi ya kondoo na mbuzi, makundi ya ngʼombe, au watumishi wa kiume na wa kike? 275:27 Hes 12:10; Kut 4:6Ukoma wa Naamani utakushika wewe na wazao wako milele.” Kisha Gehazi akaondoka mbele ya Elisha, mwenye ukoma, mweupe kama theluji.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

列王紀下 5:1-27

以利沙醫治乃縵

1乃縵亞蘭王的元帥,甚得亞蘭王器重,因為耶和華藉他使亞蘭人打了許多勝仗。他是英勇的戰士,只是患了痲瘋病。 2亞蘭人襲擊以色列時,曾擄回一個以色列少女,這少女做了乃縵妻子的婢女。 3有一天,她對主母說:「要是我主人去見撒瑪利亞的那位先知就好了!他一定能治好我主人的痲瘋病。」 4乃縵把這以色列少女的話告訴亞蘭王。 5亞蘭王說:「你去吧。我會寫信給以色列王的。」於是,乃縵帶了三百四十公斤銀子、七十公斤金子和十套衣服,啟程前往以色列6他帶給以色列王的信上寫著:「謹以此信介紹我的臣僕乃縵到你那裡,你要醫好他的痲瘋病。」 7以色列王讀完信後,就撕裂衣服說:「難道我是上帝嗎?我能操縱人的生死嗎?這人竟叫我醫好一個人的痲瘋病!他只是想找藉口攻打我。」

8上帝的僕人以利沙聽說以色列王撕裂了衣服,便派人去對王說:「你為什麼撕裂衣服呢?讓那人到我這裡來,我要讓他知道以色列有先知。」 9乃縵帶領車輛和馬匹到了以利沙的家,站在門口。 10以利沙派使者出去對乃縵說:「你到約旦河裡洗七次,你的皮膚就會復原,並得到潔淨。」 11乃縵卻怒沖沖地走了。他說:「我以為他一定會出來見我,為我站著求告他的上帝耶和華,用手在我的患處晃一晃,醫好我的痲瘋病。 12大馬士革亞波納河和法爾法河不比以色列所有的河都好嗎?難道我在那裡洗就不能得到潔淨嗎?」於是,他怒沖沖地轉身走了。 13他的僕人上前對他說:「我父啊,先知若吩咐你做一件大事,難道你會不去做嗎?何況他只是說你去洗洗就可以潔淨!」 14乃縵就去約旦河,照上帝僕人的話在河裡洗了七次,便潔淨了,皮膚變得像小孩子的一樣。

15乃縵率領全體隨從回到上帝的僕人那裡,站在他面前說:「如今我才知道,除了以色列,普天下沒有上帝。請你收下僕人的禮物。」 16以利沙說:「我憑我事奉的永活上帝起誓,我決不接受。」乃縵再三請求,他仍不肯接受。 17乃縵說:「如果你不肯接受禮物,請你容許僕人用兩頭騾子馱些泥土回去。從此以後,我不再獻燔祭或平安祭給其他神明,只獻給耶和華。 18但有一件事,願耶和華饒恕僕人。我主人進入臨門廟祭拜時,他會扶著我的手,這樣我也得隨著他彎腰。若我在臨門廟裡彎腰,願耶和華饒恕我。」 19以利沙對他說:「你安心地走吧。」

20乃縵剛走不遠,上帝僕人以利沙的僕人基哈西心想:「我主人沒有收亞蘭乃縵帶來的禮物就讓他走了。我憑永活的耶和華起誓,我一定要追上去,向他要點東西。」 21他便去追趕乃縵乃縵見後面有人趕來,就下車迎接他,問他:「一切都好嗎?」 22基哈西答道:「一切都好。我主人派我來告訴你,剛才有兩位年輕的先知從以法蓮山區來見他,請你賜給他們三十四公斤銀子和兩套衣服。」 23乃縵說:「請你拿走六十八公斤銀子吧!」並再三請他接受,然後把六十八公斤銀子裝進兩個袋子,連同兩套衣服,交給他的兩個僕人抬走,基哈西跟在他們後面。 24到了山岡,基哈西接過銀子和衣服,放進屋裡,便讓他們回去了。 25基哈西進去侍立在以利沙面前,以利沙問他:「基哈西,你剛才去哪裡了?」基哈西答道:「僕人哪裡也沒有去。」 26以利沙對他說:「那人下車回頭迎接你的時候,我的心不也在那裡嗎?現在豈是接受人家銀子、衣服、橄欖園、葡萄園、牛羊和僕婢的時候? 27因此,你和你的後代會永遠沾染乃縵的痲瘋病。」基哈西離開以利沙時,患了痲瘋病,皮膚像雪一樣白。