2 Samweli 5 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 5:1-25

Daudi Atawazwa Mfalme Juu Ya Israeli

(1 Nyakati 11:1-9; 14:1-7)

15:1 2Sam 19:43; Mwa 29:14; 35:26; 1Nya 11:1; 12:23Makabila yote ya Israeli yakamjia Daudi huko Hebroni na kumwambia, “Sisi tu nyama yako na damu yako hasa. 25:2 1Sam 8:5, 13, 16; 11:6; Mwa 48:15; 1Sam 16:1; 2Sam 7:7; Mt 2:6; Yn 12:16; 1Sam 12:12; 13:14; 6:21; 25:30; Za 78:71Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani. Naye Bwana alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”

35:3 2Sam 3:21; Kum 17:15; 2Sam 2:4; 1Nya 11:3; 2Fal 11:17; Amu 11:11; 1Sam 23:18Wazee wote wa Israeli wakamwendea Mfalme Daudi huko Hebroni, mfalme akafanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta kuwa mfalme wa Israeli.

45:4 Mwa 37:2; Lk 3:23; 1Fal 2:11; 1Nya 3:4; 26:31; 29:27Daudi alikuwa na miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala Israeli miaka arobaini. 55:5 2Sam 2:11; 1Fal 2:11; 1Nya 3:4Huko Hebroni alitawala Yuda kwa miaka saba na miezi sita, na katika Yerusalemu alitawala Israeli yote na Yuda kwa miaka thelathini na mitatu.

Daudi Ateka Yerusalemu

65:6 Amu 1:8; Yos 15:8; Amu 1:21; 19:11Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kuwashambulia Wayebusi walioishi humo. Wayebusi wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu, kwani hata vipofu na viwete wanaweza kukufukuza.” Walidhani, “Daudi hawezi kuingia humu.” 75:7 Za 76:2; Yer 21:13; 2Sam 6:12; 1Fal 2:10; 8:1; Isa 29:1; Yer 25:29Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.

85:8 Yos 15:8; 17:15; 18:16; 1Nya 11:6Siku ile, Daudi akasema, “Yeyote ambaye atawashinda Wayebusi, atatumia huo mfereji kuwafikia hao ‘viwete na vipofu’ ambao ni adui za Daudi.” Ndiyo sababu wanasema, “ ‘Vipofu na viwete’ hawataingia kwenye jumba la ufalme.”

95:9 2Fal 7:6; 1Fal 9:15, 24; 2Nya 32:5Ndipo Daudi akafanya makao ndani ya ngome na kuiita Mji wa Daudi. Akajenga eneo linalozunguka kuanzia Milo5:9 Milo maana yake Boma la Ngome. kuelekea ndani. 105:10 2Sam 3:1; Za 24:10; 2Fal 7:9Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye.

115:11 1Fal 15:1, 18; 2Nya 2:3; 1Fal 5:2; 1Nya 14:1Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, maseremala na waashi, nao wakajenga jumba la kifalme kwa ajili ya Daudi. 125:12 Hes 24:7; 1Fal 10:9; 2Nya 2:11; Es 4:14; Isa 45:4Naye Daudi akafahamu kuwa Bwana amemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na ameinua ufalme wake kwa ajili ya Israeli, watu wake.

135:13 Kum 17:17; 1Nya 3:9; Mwa 25:5-6Baada ya Daudi kuondoka Hebroni, akajitwalia masuria zaidi na wake huko Yerusalemu, nao wana na binti wengi walizaliwa kwake. 145:14 1Nya 3:5; Lk 3:31Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni, 15Ibihari, Elishua, Nefegi, Yafia, 16Elishama, Eliada na Elifeleti.

Daudi Awashinda Wafilisti

(1 Nyakati 14:8-17)

175:17 2Sam 23:14; 1Nya 11:16Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akateremka kwenye ngome. 185:18 Yos 15:8; 17:15; 18:16; Isa 17:5Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kusambaa kwenye Bonde la Warefai, 195:19 Amu 18:5; 1Sam 23:2; Hes 27:21; Yos 9:14kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, “Je, niende kuwashambulia Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”

Bwana akamjibu, “Nenda, kwa maana hakika nitawatia Wafilisti mikononi mwako.”

205:20 Mwa 38:29; Isa 28:21Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu.5:20 Maana yake Bwana Afurikae. 215:21 Kum 7:5; Isa 46:2Wafilisti wakaiacha miungu yao huko, naye Daudi na watu wake wakaichukua.

22Wafilisti walikwea kwa mara nyingine na kusambaa katika Bonde la Warefai. 23Kwa hiyo Daudi akamuuliza Bwana, naye akamjibu, “Usipande moja kwa moja, bali wazungukie kwa nyuma na uwashambulie mbele ya miti ya miforosadi. 245:24 Kut 14:24; Amu 4:14; 2Fal 7:6Mara utakaposikia sauti ya kutembea kutoka kwenye vilele vya miti ya miforosadi, nenda haraka, kwa sababu hiyo itamaanisha kuwa Bwana ametangulia mbele yako kupiga jeshi la Wafilisti.” 255:25 2Sam 8:12; 21:15; Isa 28:21; Yos 10:33; 1Nya 14:16Basi Daudi akafanya kama Bwana alivyomwagiza, naye akawaangusha Wafilisti njia yote kuanzia Geba5:25 Kwa Kiebrania mji huu uliitwa Gibeoni (ona 1Nya 14:16). hadi Gezeri.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

撒母耳記下 5:1-25

大衛統治全以色列

1以色列各支派都來希伯崙大衛,對他說:「我們是你的骨肉同胞。 2從前掃羅做王的時候,率領以色列人出征打仗的是你,耶和華也曾應許讓你做祂以色列子民的牧者和首領。」 3以色列的長老都到希伯崙大衛王,大衛與他們在耶和華面前立約,他們膏立大衛以色列的王。 4大衛三十歲登基,執政共四十年。 5他在希伯崙統治猶大七年半,在耶路撒冷統治以色列猶大三十三年。

6大衛率領軍隊來到耶路撒冷,要攻打那裡的耶布斯人。耶布斯人對大衛說:「你攻不進來,就連我們這裡的瞎子、瘸子都可以把你趕走。」他們以為大衛攻不進去。 7結果大衛的軍隊攻取了錫安的堡壘,即後來的大衛城。 8那天,大衛下令軍隊從地下水道爬進城去,攻打那些「瞎子、瘸子」,他憎惡這些耶布斯人。後來便有一句俗語:「瞎子、瘸子不得進殿!」 9大衛住在錫安的堡壘裡,並稱之為大衛城,他又從米羅興建環城圍牆。 10大衛日漸強盛,因為萬軍之上帝耶和華與他同在。

11泰爾希蘭差遣使者帶著香柏木、木匠和石匠去為大衛建造宮殿。 12那時,大衛知道耶和華已立他做以色列王,並因祂以色列子民的緣故而使他國家興旺。

13大衛希伯崙遷到耶路撒冷以後,又選立妃嬪,生了更多的兒女。 14以下是他在耶路撒冷生的兒子:沙姆亞朔罷拿單所羅門15益轄以利書亞尼斐雅非亞16以利沙瑪以利雅大以利法列

大衛戰勝非利士人

17非利士人聽說大衛已被膏立為以色列王,就全軍出動,要搜尋大衛大衛得到消息便退到堅城裡。 18非利士人大軍壓境,散佈在利乏音谷。 19大衛求問耶和華:「我可以去迎戰非利士人嗎?你會把他們交在我手裡嗎?」耶和華說:「去吧,我必把他們交在你手裡。」 20大衛前往巴力·毗拉心,在那裡打敗了敵人。他說:「耶和華像洪水決堤一樣為我沖垮了仇敵。」於是他稱那地方為巴力·毗拉心5·20 巴力·毗拉心」意思是「沖垮之主」。21大衛和他的軍隊帶走了非利士人所丟棄的神像。

22後來非利士人又捲土重來,散佈在利乏音谷。 23大衛又求問耶和華,耶和華說:「你不要正面出擊,要繞到他們後面,從桑林對面攻打他們。 24當你聽見桑樹梢上響起腳步聲時,就要快速進攻,因為那表示耶和華已在你前頭去攻擊非利士的軍隊了。」 25大衛遵命而行,打敗非利士人,由迦巴一直殺到基色