2 Samweli 4 – NEN & OL

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Samweli 4:1-12

Ish-Boshethi Auawa

14:1 2Sam 3:27; Ezr 4:4Ish-Boshethi mwana wa Sauli aliposikia kwamba Abneri amekufa huko Hebroni, akakosa ujasiri, nayo Israeli yote wakatiwa hofu kuu. 24:2 Yos 9:17; 18:25Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa viongozi wa vikundi vya uvamizi. Mmoja aliitwa Baana na mwingine Rekabu, waliokuwa wana wa Rimoni, Mbeerothi, kutoka kabila la Benyamini. Beerothi alihesabiwa kuwa sehemu ya Benyamini, 34:3 Neh 11:33kwa sababu watu wa Beerothi walikimbilia huko Gitaimu na wameishi huko kama wageni mpaka siku hii ya leo.

44:4 1Sam 18:1; 31:9; Law 21:18; 2Sam 9:8-12; 16:1-4; 19:24; 21:7-8; 1Nya 8:34; 9:40(Yonathani mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa mlemavu miguu yote miwili. Alikuwa na miaka mitano wakati habari kuhusu Sauli na Yonathani zilipofika kutoka Yezreeli. Yaya wake akambeba ili kukimbia, lakini yaya alipokuwa anaharakisha kuondoka, mtoto alianguka akawa kiwete. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.)

54:5 2Sam 2:8; Rut 2:7Basi Rekabu na Baana, wana wa Rimoni Mbeerothi wakaenda nyumbani kwa Ish-Boshethi, nao walifika huko wakati alipokuwa kwenye mapumziko yake ya mchana. 64:6 2Sam 2:23; Amu 5:25; Za 147:14Wakaingia kwenye chumba cha ndani kana kwamba wanachukua ngano, wakamchoma Ish-Boshethi mkuki wa tumboni. Ndipo Rekabu na Baana nduguye wakatoroka.

74:7 Kum 3:17; 1Sam 17:54; 31:9; Mt 14:11Walikuwa wameingia ndani ya nyumba wakati alipokuwa amelala kitandani chumbani kwake. Baada ya kumchoma mkuki na kumuua, walikata kichwa chake. Wakiwa wamekichukua, walitembea usiku kucha kwa njia ya Araba. 84:8 2Sam 20:21; 2Fal 10:7; 1Sam 24:4; 25:29; Hes 31:3; 1Sam 23:15Wakamletea Daudi kichwa cha Ish-Boshethi huko Hebroni, wakamwambia mfalme, “Hiki hapa kichwa cha Ish-Boshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyejaribu kuondoa uhai wako. Siku hii ya leo Bwana amemlipia kisasi mfalme bwana wangu dhidi ya Sauli na mzao wake.”

94:9 Mwa 48:16; 1Fal 1:29; Za 31:7; 103:4; 106:10Daudi akawajibu Rekabu na Baana nduguye, wana wa Rimoni, Mbeerothi, akasema, “Hakika kama Bwana aishivyo, ambaye ameniokoa kutoka taabu zote, 104:10 2Sam 1:2-16yule mtu aliponiambia, ‘Sauli amekufa,’ akadhani ananiletea habari njema, nilimkamata, nikamuua huko Siklagi. Hiyo ndiyo zawadi niliyompa kwa ajili ya taarifa yake! 114:11 Mwa 4:10; 9:5; Za 9:12; 72:14Je, ni mara ngapi zaidi wakati watu waovu wamemuua mtu asiye na hatia akiwa ndani ya nyumba yake mwenyewe na kwenye kitanda chake mwenyewe? Je, sasa nisidai damu yake mikononi mwenu na kuwaondoa duniani?”

124:12 2Sam 1:15; 3:32Kwa hiyo Daudi akawaamuru watu wake, wakawaua. Wakakata mikono yao na miguu, na kutundika viwiliwili vyao kando ya dimbwi huko Hebroni. Lakini wakakichukua kichwa cha Ish-Boshethi na kukizika katika kaburi la Abneri huko Hebroni.

O Livro

2 Samuel 4:1-12

Isbosete é assassinado

1Quando Isbosete soube da morte de Abner em Hebrom ficou cheio de medo e todo o povo de Israel ficou alarmado. 2O comando das tropas israelitas recaiu agora sobre os dois irmãos Baaná e Recabe, que eram capitães do príncipe Isbosete, liderando as suas ações de guerrilha. Eram filhos de Rimom, originários de Beerote, povoação sob a jurisdição de Benjamim. 3A população de Beerote é considerada benjamita, apesar de ter fugido para Gitaim, onde agora vive.

4Havia um neto do rei Saul de nome Mefibosete, filho de Jónatas, que era aleijado dos pés. Tinha 5 anos na altura em que o pai e o avô morreram na batalha de Jezreel. Quando a notícia dessa derrota chegou à capital, a ama pegou na criança e fugiu, mas tropeçou e deixou-o cair, ficando assim aleijado.

5Recabe e Baaná chegaram a casa de Isbosete certo dia. O Sol estava a pique e ele passava pelo sono. 6Dirigiram-se à cozinha, como se fossem buscar um saco de trigo, mas entraram no quarto e assassinaram-no. 7Cortaram-lhe a cabeça e fugiram com ela pelo caminho de Arabá4.7 Arabá geralmente define uma região desértica. Neste contexto, implica toda a região seca ao longo do rio Jordão., durante essa noite toda. 8Foram apresentá-la a David em Hebrom: “Aqui tens a cabeça de Isbosete, o filho do teu inimigo Saul, que tentou matar-te. Hoje o Senhor vingou-te de Saul e de toda a sua família!”

9David respondeu: “Tão certo como vive o Senhor que sempre me salvou dos meus inimigos! 10Quando alguém me disse ‘Saul morreu’, pensando dar-me boas notícias, eu matei-o em Ziclague! Foi desta forma que recompensei as supostas boas notícias que me trazia. 11Desta vez, com muito mais razão, farei o mesmo a esta gente malvada que matou um homem inocente, na sua própria casa, na sua cama! Não exigiria eu as vossas vidas?”

12Então ordenou aos rapazes da sua guarda que os matassem. Eles obedeceram; cortaram-lhes os pés e penduraram os corpos junto ao poço em Hebrom. A cabeça de Isbosete enterraram-na no túmulo de Abner também em Hebrom.