2 Nyakati 34 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 34:1-33

Yosia Afanya Matengenezo

(2 Wafalme 22:1-2)

134:1 1Nya 3:14; Sef 1:1; 1Fal 3:7-9; 13:2; 2Nya 35:25Yosia alikuwa na miaka minane alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka thelathini na mmoja. 234:2 2Nya 29:2Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana na kuenenda katika njia za Daudi baba yake, hakugeuka upande wa kuume wala wa kushoto.

334:3 1Fal 13:2; 1Sam 1:24; 1Nya 16:11; Mit 8:17; Za 119:9; 2Tim 3:15; 2Nya 15:2; 1Fal 13:2Katika mwaka wa nane wa utawala wake, alipokuwa angali bado mdogo, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi baba yake. Katika mwaka wake wa kumi na mbili alianza kusafisha mahali pa juu pa kuabudia miungu pa Yuda na Yerusalemu, akiondoa nguzo za Ashera, sanamu za kuchonga na vinyago vya kusubu. 434:4 Kut 34:13; 2Fal 23:11; Mik 1:5; Kut 32:30; Law 26:30Mbele ya macho yake, wakazibomoa madhabahu za Mabaali, wakazivunja madhabahu za kufukizia uvumba zilizokuwa zimesimama juu yake, wakazivunja nguzo za Ashera, sanamu na vinyago. Hivi alivivunja vipande vipande na kuvisambaza juu ya makaburi ya waliokuwa wamevitolea kafara. 534:5 1Fal 13:2Akachoma mifupa ya makuhani wao juu ya madhabahu zao na kwa njia hiyo akaitakasa Yuda na Yerusalemu. 6Katika miji ya Manase, Efraimu na Simeoni, hadi Naftali na kwenye magofu yanayoizunguka, 734:7 Kut 32:20; Kum 9:21; 2Nya 31:1akavunja madhabahu na nguzo za Ashera na kuzipondaponda hizo sanamu hadi zikawa unga na kukata vipande vipande madhabahu zote za kufukizia uvumba katika Israeli yote. Kisha akarudi Yerusalemu.

834:8 2Fal 22:3Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yosia, ili kutakasa nchi na Hekalu, akawatuma Shafani, mwana wa Azalia na Maaseya mtawala wa mji, pamoja na Yoa mwana wa Yoahazi, mwandishi ili kukarabati Hekalu la Bwana Mungu wake.

934:9 1Nya 6:13; 2Nya 35:8; 2Fal 12:4Wakamwendea Hilkia kuhani mkuu na kumpa fedha ambazo zilikuwa zimeletwa ndani ya Hekalu la Bwana ambazo Walawi waliokuwa mabawabu walikuwa wamezikusanya kutoka kwa watu wa Manase, Efraimu na mabaki wote wa Israeli kutoka kwa watu wote wa Yuda na Benyamini na wakazi wa Yerusalemu. 10Kisha wakazikabidhi hizo fedha kwa watu waliowekwa ili kusimamia kazi ya Hekalu la Bwana. Hawa watu waliwalipa wafanyakazi waliokarabati na kutengeneza Hekalu lipate kurudi katika hali yake. 1134:11 2Nya 24:12; 33:4-7Wakawapa pia mafundi seremala na waashi fedha ili kununua mawe yaliyochongwa, mbao kwa ajili ya kufungia na boriti kwa ajili ya majengo ambayo wafalme wa Yuda walikuwa wameyaacha yakawa magofu.

1234:12 2Nya 12:15; 1Nya 25:1; Neh 7:2; 1Kor 4:2; 2Fal 12:15; 22:7; Mt 28:20Watu wakafanya kazi kwa uaminifu. Waliokuwa wamewekwa juu yao ili kuwaelekeza ni Yahathi na Obadia, Walawi wa uzao wa Merari, Zekaria na Meshulamu, waliotoka kwenye uzao wa Kohathi. Walawi wote waliokuwa na ufundi wa kupiga ala za uimbaji, 1334:13 1Nya 23:4; Ezr 7:6; Yer 8:8; Mt 26:3wakawa wasimamizi wa vibarua na kuwaongoza wale waliofanya kila aina ya kazi. Baadhi ya Walawi walikuwa waandishi, maafisa na mabawabu.

Kitabu Cha Sheria Chapatikana

(2 Wafalme 22:3-20)

1434:14 Kum 31:24-26; 2Fal 22:8Wakati walikuwa wakizitoa nje fedha zilizokuwa zimetolewa kwenye Hekalu la Bwana, kuhani Hilkia akakipata kile Kitabu cha Sheria ya Bwana kilichokua kimetolewa kwa mkono wa Mose. 1534:15 2Fal 22:8; Neh 8:1Hilkia akamwambia Shafani mwandishi, “Nimekipata Kitabu cha Sheria ndani ya Hekalu la Bwana.” Akampa Shafani kile Kitabu.

16Kisha Shafani akakipeleka kile Kitabu kwa mfalme na kumwambia, “Maafisa wako wanafanya kila kitu kama walivyokabidhiwa kufanya. 17Wamelipa fedha zilizokuwa katika Hekalu la Bwana na wamewakabidhi wasimamizi na wafanyakazi.” 1834:18 Kum 17:19; Yos 1:8Kisha Shafani mwandishi akamwarifu mfalme kuwa, “Kuhani Hilkia amenipa Kitabu.” Naye Shafani akakisoma mbele ya mfalme.

1934:19 Kum 28:3-68; Yos 7:6; Gal 2:19; 3:10-11; Rum 7:7-14; Hab 3:16; Rum 3:20; 2Fal 19:1; Neh 8:9; Za 94:12-13; 119:120; Yer 23:9; Yoe 2:13Mfalme aliposikia yale maneno ya Sheria, akayararua mavazi yake. 2034:20 2Fal 22:3-12Akatoa maagizo haya kwa Hilkia, Ahikamu mwana wa Shafani, Abdoni mwana wa Mika, Shafani mwandishi na Asaya mtumishi wa mfalme, 2134:21 Mao 2:4; 4:11; Eze 36:18; 2Fal 17:6“Nendeni mkamuulize Bwana kwa ajili yangu na kwa ajili ya mabaki walioko Israeli na Yuda kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya Bwana ni kubwa mno ambayo imemwagwa juu yetu kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la Bwana wala hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa katika Kitabu hiki.”

2234:22 Kut 15:20; Lk 2:36; Mdo 21:9; Neh 6:14; Amu 4:4; 2Fal 22:14Hilkia pamoja na wale wote mfalme aliokuwa amewatuma pamoja naye wakaenda kuzungumza na nabii mke aitwaye Hulda, aliyekuwa mke wa Shalumu mwana wa Tokhathi, mwana wa Hasra mtunzaji wa chumba cha mavazi. Hulda aliishi Yerusalemu, katika Mtaa wa Pili.

23Akawaambia, “Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli: Mwambieni yule mtu aliyewatuma ninyi kwangu, 2434:24 Mit 16:4; 2Nya 36:14-20; Kum 28:15-68; Dan 9:11-16; Yos 23:16; 2Fal 21:12; 23:26-27; Isa 5:5; Yer 25:9; Amo 3:6; Zek 1:6‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana: Nitaleta maafa juu ya mahali hapa na watu wake, laana zote zilizoandikwa ndani ya hicho kitabu ambazo zimesomwa mbele ya mfalme wa Yuda. 2534:25 2Nya 33:3-6; Yer 22:9Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kunighadhibisha kwa kazi yote ya mikono yao, hivyo hasira yangu itamwagwa juu ya mahali hapa, wala haitatulizwa.’ 26Mwambieni mfalme wa Yuda, ambaye amewatuma kumuuliza Bwana, ‘Hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli kuhusu maneno uliyoyasikia: 2734:27 2Nya 12:7; 32:26; Za 86:5Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za Mungu uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake na kwa sababu ulijinyenyekeza mbele zangu na uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema Bwana. 2834:28 2Nya 35:20-25; 32:26Basi nitakukusanya kwa baba zako, nawe utazikwa kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote nitakayoleta juu ya mahali hapa na juu ya wote wanaoishi hapa.’ ”

Kwa hiyo wakampelekea mfalme jibu lake.

Yosia Afanya Agano La Kutii

(2 Wafalme 23:1-20)

2934:29 2Fal 23:1Kisha mfalme akawaita pamoja wazee wote wa Yuda na Yerusalemu. 30Akapanda kwenda hekaluni mwa Bwana pamoja na watu wa Yuda, watu wa Yerusalemu, makuhani na Walawi, watu wote, wakubwa kwa wadogo. Akasoma wakiwa wanasikia maneno yote ya Kitabu cha Agano, ambacho kilikuwa kimepatikana katika Hekalu la Bwana. 3134:31 1Fal 7:15; 2Fal 11:14-17; 2Nya 29:10; Kum 13:4Mfalme akasimama karibu na nguzo yake na kufanya upya Agano mbele za Bwana ili kumfuata Bwana na kuzishika amri zake, maagizo na sheria kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote na ili kuyatii maneno ya Agano yaliyoandikwa katika kitabu hiki.

3234:32 Yer 3:10; 2Nya 14:2Ndipo akamtaka kila mmoja katika Yerusalemu na Benyamini kuweka ahadi zao wenyewe kwa hilo Agano, watu wa Yerusalemu wakafanya hivyo kwa kufuata Agano la Bwana, Mungu wa baba zao.

3334:33 1Fal 11:5; Yer 3:10; 2Nya 24:2Yosia akaondoa machukizo yote ya sanamu kutoka nchi yote iliyokuwa mali ya Waisraeli na akawataka wale wote waliokuwako katika Israeli wamtumikie Bwana Mungu wao. Kwa muda wote alioishi, hawakushindwa kumfuata Bwana, Mungu wa baba zao.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志下 34:1-33

猶大王約西亞

1約西亞八歲登基,在耶路撒冷執政三十一年。 2他做耶和華視為正的事,效法他祖先大衛,不偏不離。

約西亞清除偶像

3他執政第八年,雖然還年幼,卻開始尋求他祖先大衛的上帝。他執政第十二年,開始清除猶大耶路撒冷的邱壇、亞舍拉神像、雕刻和鑄造的偶像。 4眾人在他面前拆毀巴力的祭壇,他砍掉高高的香壇,又把亞舍拉神像及雕刻和鑄造的偶像磨成粉末,撒在祭拜它們之人的墳墓上, 5把它們祭司的骸骨放在它們的壇上焚燒。這樣,他潔淨了猶大耶路撒冷6約西亞還在瑪拿西以法蓮西緬,遠至拿弗他利的各城邑及其周圍的荒廢之地做了同樣的事情。 7他拆毀祭壇和亞舍拉神像,把偶像磨成粉末,砍掉以色列境內所有的香壇,然後回到耶路撒冷

發現律法書

8約西亞執政第十八年,潔淨國土和聖殿以後,就差遣亞薩利雅的兒子沙番耶路撒冷的總督瑪西雅約哈斯的兒子約亞史官負責整修他的上帝耶和華的殿。 9他們到希勒迦大祭司那裡,把獻給上帝殿的銀子交給他。這銀子是守殿門的利未人從瑪拿西人和以法蓮人,所有剩下的以色列人,所有的猶大人和便雅憫人,以及耶路撒冷的居民那裡收來的。 10他們把銀子交給負責管理耶和華殿的督工,由他們轉交給整修耶和華殿的工人, 11也就是木匠和石匠,讓他們用來購買鑿好的石頭、木架和棟樑,整修猶大諸王毀壞的殿。 12工人都忠誠地工作。他們的督工是利未米拉利的子孫雅哈俄巴底哥轄的子孫撒迦利亞米書蘭。其他精通樂器的利未13負責監督搬運工人,還有一些做書記、官員和殿門守衛。

14他們把奉獻到耶和華殿裡的銀子拿出來的時候,希勒迦祭司發現了摩西所傳的耶和華的律法書。 15希勒迦就對沙番書記說:「我在耶和華的殿裡發現了律法書。」希勒迦就把書卷交給沙番16沙番把書卷帶到王那裡,向王稟告說:「凡交給僕人們辦的事,都已辦妥。 17耶和華殿裡的銀子已被取出來交給督工和工人。」 18沙番書記又對王說:「希勒迦祭司交給我一卷書。」沙番就在王面前誦讀這書。 19王聽了律法書上的話,就撕裂衣服, 20吩咐希勒迦沙番的兒子亞希甘米迦的兒子亞比頓沙番書記和王的臣僕亞撒雅21「你們去為我、為以色列猶大的餘民求問耶和華有關這書卷上的話。耶和華的烈怒已經臨到我們身上,因為我們的祖先沒有遵守耶和華的話,沒有遵行這書卷上的話。」

22於是,王派去的人跟著希勒迦去求問女先知戶勒妲,她是負責管理禮服的沙龍之妻。沙龍哈斯拉的孫子、特瓦的兒子。戶勒妲住在耶路撒冷第二區。他們向她說明來意, 23她對他們說:「以色列的上帝耶和華要你們回去告訴差你們來見我的人, 24耶和華說,『我要照在猶大王面前所讀的那書上的一切咒詛,降災難給這地方及這裡的居民。 25因為他們背棄我,給別的神明燒香,製造偶像惹我發怒,所以我的怒火要在這地方燃燒,絕不止息。』 26你們告訴差你們來求問耶和華的猶大王,『至於你所聽見的那些話,以色列的上帝耶和華說, 27因為你聽到我對這地方及這裡居民的警告,便悔改,在我面前謙卑、撕裂衣服,向我哭泣,我垂聽了你的禱告。這是我耶和華說的。 28我會讓你平安入土,你不會看到我要降給這地方及這裡居民的一切災難。』」他們便回去稟告王。

約西亞立約順服上帝

29於是,王召集猶大耶路撒冷的所有長老, 30猶大人和耶路撒冷的居民、祭司和利未人等全體民眾,不論貴賤,一同上到耶和華的殿。王把在耶和華殿中發現的約書念給他們聽。 31王站在自己的位置上,在耶和華面前立約,要全心全意地跟隨耶和華,遵從祂的一切誡命、法度和律例,履行約書上的規定。 32他使耶路撒冷便雅憫的人都遵行這約。於是,耶路撒冷的居民都遵行他們祖先的上帝的約。 33約西亞除去以色列境內所有的可憎之物,又吩咐所有住在以色列的人都事奉他們的上帝耶和華。約西亞在世時,他們都沒有偏離他們祖先的上帝耶和華。