2 Nyakati 24 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 24:1-27

Yoashi Akarabati Hekalu

(2 Wafalme 12:1-16)

124:1 2Fal 11:21; 12:1Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka arobaini. Mama yake aliitwa Sibia aliyekuwa ametoka Beer-Sheba. 224:2 2Nya 25:2; 26:5Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana miaka yote ya Yehoyada kuhani. 3Yehoyada akamwoza wake wawili, akazaa watoto wa kiume na wa kike.

4Baada ya muda, Yoashi akaamua kukarabati Hekalu la Bwana. 524:5 Kut 30:16; Mt 17:24; 1Nya 26:20; 11:1; 2Fal 12:4; 2Nya 29:3; 34:8Akawaita pamoja makuhani na Walawi akawaambia, “Nendeni katika miji ya Yuda mkakusanye fedha wanazopaswa kulipa kila mwaka kutoka kwa Israeli wote, ili kukarabati Hekalu la Mungu wenu. Fanyeni hivyo sasa.” Lakini Walawi hawakufanya upesi.

624:6 Kut 35:21; Hes 1:50; Mdo 7:44; Hes 17:7-8; Kut 30:12-16; 2Fal 12:7Kwa hiyo mfalme akamwita Yehoyada kuhani mkuu na kumwambia, “Kwa nini hukuwaambia Walawi walete kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyowekwa na Mose mtumishi wa Bwana pamoja na kusanyiko la Israeli kwa ajili ya Hema ya Ushuhuda?”

724:7 2Nya 21:17; 22:3-4; Za 12:8Kwa kuwa wana wa yule mwanamke mwovu Athalia, walikuwa wamevunja na kuingia katika Hekalu la Mungu, nao wakawa wamevitumia hata vile vitu vilivyowekwa wakfu kwa Bwana kwa mabaali.

824:8 2Fal 12:9Kwa amri ya mfalme, likatengenezwa kasha, nalo likawekwa nje kwenye lango la Hekalu la Bwana. 924:9 Kut 36:6Tangazo likatolewa katika Yuda na Yerusalemu kwamba inapasa wamletee Bwana kodi ile ambayo Mose, mtumishi wa Bwana alikuwa amewaagiza Israeli huko jangwani. 1024:10 Kut 25:2; 1Nya 29:3-9Maafisa wote na watu wote wakaleta michango yao kwa furaha, wakaweka kwenye kasha mpaka likajaa. 1124:11 2Fal 12:10Ikawa kila wakati kasha lilipoletwa ndani na Walawi kwa maafisa wa mfalme na kuona kwamba kuna kiasi kikubwa cha fedha, mwandishi wa mfalme na afisa wa kuhani mkuu walikuwa wanakuja na kumimina, kisha kulirudisha mahali pake. Walifanya hivi mara kwa mara, nao wakakusanya fedha nyingi sana. 1224:12 2Nya 34:11Mfalme na Yehoyada wakawapa wale watu waliofanya kazi iliyotakiwa katika Hekalu la Bwana. Wakawaajiri waashi na maseremala ili kutengeneza Hekalu la Bwana, pia wafanyakazi za chuma na shaba ili kukarabati Hekalu la Bwana.

1324:13 Neh 4:7Watu walioshughulika na kazi walikuwa wenye bidii, nayo kazi ya kukarabati ikaendelea vizuri mikononi mwao. Wakalitengeneza upya Hekalu la Bwana likarudi katika hali yake ya awali na kuliimarisha. 1424:14 1Fal 7:50; 2Fal 12:13; Kut 29:38; Ebr 7:27; 1Pet 1:18-19; Ufu 5:9Walipokamilisha kazi hiyo ya kukarabati, wakaleta fedha zilizobaki wakampa mfalme na Yehoyada, nao kwa hizo wakatengeneza vyombo kwa ajili ya Hekalu la Bwana: Vyombo kwa ajili ya huduma na kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, pia mabakuli na vitu vingine vya dhahabu na fedha. Wakati wote Yehoyada alipokuwa hai, sadaka za kuteketezwa zilitolewa wakati wote katika Hekalu la Bwana.

1524:15 Ay 5:26Basi Yehoyada alikuwa mzee aliyeshiba siku wakati alipofariki. Alikufa akiwa na umri wa miaka 130. 1624:16 1Fal 2:10Wakamzika pamoja na wafalme katika Mji wa Daudi, kwa sababu ya mema aliyokuwa ametenda katika Israeli kwa ajili ya Mungu na Hekalu lake.

Uovu Wa Yoashi

1724:17 Mdo 20:29Baada ya kifo cha Yehoyada, wakuu wa Yuda walikuja kumpa mfalme heshima, naye akawasikiliza. 1824:18 Yos 24:20; 1Fal 14:23; Yer 17:2; Yos 22:20; 2Nya 19:2; Amu 5:8; 2Sam 24:1; 2Nya 28:13; Hos 5:10Wakaacha Hekalu la Bwana, Mungu wa baba zao, wakaabudu nguzo za maashera na sanamu. Kwa sababu ya hatia yao, hasira ya Mungu ikawajia Yuda na Yerusalemu. 1924:19 Hes 11:29; Zek 1:4; 2Nya 36:15; Neh 9:26; Yer 7:25-26; 25:4; Lk 11:47-51Ingawa Bwana aliwatuma manabii wawarudishe watu kwake na ingawa waliwaonya, hawakuwasikiliza.

2024:20 Amu 3:10; Mt 23:35; 1Nya 12:18; Hes 14:41; 2Nya 15:2; Kum 31:17; 2Nya 15:1-2; Amu 6:34; 1Sam 13:13-14; Kum 29:25-26; Yer 2:19Ndipo Roho wa Bwana akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada kuhani. Akasimama mbele ya watu akasema, “Hili ndilo asemalo Mungu, ‘Kwa nini mnakataa kuzitii amri za Bwana? Hamtafanikiwa kwa kuwa mmemwacha Bwana, yeye naye amewaacha ninyi.’ ”

2124:21 Yos 7:25; Mdo 7:58-59; Neh 9:26; Yer 26:21; 20:2; Mt 23:35Lakini wakafanya shauri baya juu yake na kwa amri ya mfalme wakampiga kwa mawe mpaka akafa katika ukumbi wa Hekalu la Bwana. 2224:22 Mwa 9:5Mfalme Yoashi hakukumbuka wema aliotendewa na Yehoyada baba yake Zekaria ila alimuua mwanawe, ambaye alisema wakati akiwa amelala akingojea kufa, “Bwana na alione hili na alipize kisasi.”

2324:23 2Fal 12:17-18Mwishoni mwa ule mwaka, jeshi la Waaramu likaja dhidi ya Yoashi, likavamia Yuda na Yerusalemu na kuwaua viongozi wote wa watu. Wakapeleka nyara zao zote kwa mfalme wao huko Dameski. 2424:24 2Nya 14:9; Law 26:23-25; Kum 28:25; 32:30; Isa 10:5; 30:17Ingawa jeshi la Waaramu lilikuwa limekuja na watu wachache tu, Bwana akatia mikononi mwao jeshi kubwa kuliko lao. Kwa sababu Yuda walikuwa wamemwacha Bwana, Mungu wa baba zao, hukumu ilitekelezwa juu ya Yoashi. 2524:25 2Nya 21:20; 2Fal 12:18-20; Za 10:14Waaramu walipoondoka, walimwacha Yoashi akiwa mgonjwa sana. Maafisa wake wakafanya hila dhidi yake kwa sababu alikuwa amemuua mwana wa Kuhani Yehoyada, nao wakamuulia kitandani mwake. Hivyo akafa na wakamzika katika Mji wa Daudi, lakini si katika makaburi ya wafalme.

2624:26 2Fal 12:21; Rut 1:4Wale waliofanya hila mbaya dhidi yake walikuwa Zabadi, mwana wa Shimeathi mwanamke Mwamoni, Yehozabadi, mwana wa Shimrithi mwanamke Mmoabu. 27Kwa habari za wanawe, unabii mwingi kumhusu na kumbukumbu za kutengenezwa upya kwa Hekalu la Mungu, zimeandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme. Amazia mwanawe akawa mfalme baada yake.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志下 24:1-27

猶大王約阿施

1約阿施七歲登基,在耶路撒冷執政四十年。他母親叫西比亞,是別示巴人。 2耶何耶大祭司在世之日,約阿施做耶和華視為正的事。 3耶何耶大為他娶了兩個妻子,她們都為他生兒育女。

4之後,約阿施有意整修耶和華的殿, 5便召集祭司和利未人,對他們說:「你們到猶大各城去向所有以色列人徵收銀子,用來作每年整修你們上帝殿的費用。你們要立刻辦理這事。」可是,利未人沒有立刻辦理。 6王就召來耶何耶大大祭司,問他:「你為什麼不吩咐利未人到耶路撒冷猶大去收稅呢?這稅是耶和華的僕人摩西以色列的會眾定的,以備聖幕之用。」 7因為惡婦亞她利雅的爪牙曾闖入耶和華上帝的殿,拿殿裡的聖物去供奉巴力

8於是,王下令造一個箱子,放在耶和華殿的門外, 9通告猶大耶路撒冷的人民要將上帝的僕人摩西在曠野為以色列人定的稅帶來獻給耶和華。 10全體首領和民眾都高高興興地把銀子帶來投進箱子裡,直到箱子滿了。 11利未人見箱子滿了,就抬到王的官員那裡。王的書記和大祭司的屬下會把箱子倒空,然後把箱子放回原處。日復一日,他們收了很多銀子。 12王與耶何耶大把銀子交給耶和華殿裡的辦事人員,他們就雇用石匠、木匠、鐵匠和銅匠來整修耶和華的殿。 13工人辛勤整修,工程進展順利,上帝的殿恢復了原貌,而且非常堅固。 14完工後,他們把剩餘的銀子交給王與耶何耶大,這些銀子被用來製造耶和華殿裡的器具:供奉和獻祭用的器皿、碟子和其他金銀器皿。耶何耶大在世之日,民眾常在耶和華的殿裡獻燔祭。

耶何耶大的政策被廢棄

15耶何耶大壽終正寢,享年一百三十歲。 16民眾把他葬在大衛城的王陵裡,因為他在以色列為上帝和上帝的殿做了美善的事。

17耶何耶大死後,猶大眾首領來朝拜王,王對他們言聽計從。 18他們離棄他們祖先的上帝耶和華的殿,去供奉亞舍拉神像及其他偶像。因他們所犯的罪,上帝的烈怒臨到猶大耶路撒冷19但耶和華仍然派先知到他們中間,引導他們歸向祂。先知警告他們,他們卻不聽。

20上帝的靈感動了耶何耶大祭司的兒子撒迦利亞,他便站在高處對民眾說:「耶和華上帝這樣說,『你們為什麼違反耶和華的誡命,以致不得亨通呢?既然你們背棄我,我也必離棄你們。』」 21他們想謀害撒迦利亞,就照著王的命令,在耶和華殿的院子裡用石頭打死了他。 22約阿施王不但不顧念撒迦利亞的父親耶何耶大對他的恩惠,還殺死了耶何耶大的兒子。撒迦利亞臨死的時候說:「願耶和華鑒察,為我伸冤!」

約阿施被殺

23當年年底,亞蘭的軍兵前來攻擊約阿施,入侵猶大耶路撒冷,殺了民眾的所有首領,把戰利品全都送到大馬士革王那裡。 24雖然亞蘭軍只來了一小隊,但耶和華把大隊的猶大軍兵交在他們手中,以懲罰約阿施,因為猶大人背棄了他們祖先的上帝耶和華。

25亞蘭人退兵的時候,約阿施受了重傷,他的臣僕叛變,把他殺死在床上,為耶何耶大祭司的兒子報了血仇。約阿施死後葬在大衛城,但沒有葬在王陵裡。 26殺他的是亞捫婦人示米押的兒子撒拔摩押婦人示米利的兒子約薩拔27至於約阿施的眾子、他所受的警告以及他整修上帝殿的事都記在列王史上。他兒子亞瑪謝繼位。