2 Nyakati 10 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 10:1-19

Israeli Wanamwasi Rehoboamu

(1 Wafalme 12:1-20)

110:1 1Fal 12:11Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Waisraeli wote walikuwa wamekwenda huko kumfanya yeye kuwa mfalme. 210:2 1Fal 11:40; 2Nya 9:29Yeroboamu mwana wa Nebati aliposikia hili (alikuwa bado yuko Misri alikokuwa amekimbilia awe mbali na Mfalme Solomoni), akarudi kutoka Misri. 3Kwa hiyo wakatuma watu kumwita Yeroboamu, yeye na kusanyiko lote la Israeli wakamwendea Rehoboamu na kumwambia, 410:4 2Nya 2:2; 1Sam 8:11-18; Mt 23:4; 1Fal 4:7; 5:15; 9:15; Mt 11:29-30; 1Yn 5:3“Baba yako aliweka nira nzito, lakini sasa tupunguzie kazi za kikatili na nira nzito aliyoweka juu yetu, nasi tutakutumikia.”

5Rehoboamu akajibu, “Nendeni kwa muda wa siku tatu na kisha mnirudie.” Basi watu wakaenda zao.

610:6 Ay 12:12; 32:7; 8:8-9Kisha Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee ambao walimtumikia Solomoni baba yake wakati wa uhai wake akawauliza, “Mnanishauri nini katika kuwajibu watu hawa?”

710:7 Mit 15:1; Neh 5:19; 1Fal 12:7; Za 112:5Wakajibu, “Kama leo utakuwa mtumishi wa watu hawa na kuwahudumia na kuwapa jibu linaloridhisha, watakuwa watumishi wako daima.”

810:8 2Sam 17:14; Mit 13:20; 2Nya 25:16; Mit 1:25; Mhu 10:2Lakini Rehoboamu akakataa shauri alilopewa na wazee na akataka ushauri kwa vijana wanaume rika lake waliokuwa wakimtumikia. 9Akawauliza, “Ninyi ushauri wenu ni nini? Tutawajibuje watu hawa wanaoniambia, ‘Ifanye nyepesi nira baba yako aliyoweka juu yetu?’ ”

10Wale vijana wa rika lake wakamjibu, “Waambie watu hawa waliokuambia, ‘Baba yako aliweka nira nzito juu yetu, lakini ifanye nira yetu nyepesi,’ kuwa, ‘Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. 11Baba yangu aliweka nira nzito juu yenu, mimi nitaifanya hata iwe nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi; mimi nitawachapa kwa nge.’ ”

12Siku tatu baadaye, Yeroboamu na watu wote wakamrudia Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amesema, “Rudini kwangu baada ya siku tatu.” 1310:13 Mit 12:13; 14:16Mfalme akawajibu watu kwa ukatili. Akikataa shauri alilopewa na wazee, 14akafuata shauri la vijana wa rika lake na kusema, “Baba yangu alifanya nira yenu kuwa nzito, mimi nitaifanya kuwa nzito zaidi. Baba yangu aliwachapa kwa mijeledi, mimi nitawachapa kwa nge.” 1510:15 Mwa 50:20; 2Nya 25:16-20; 11:4; 1Fal 11:29; Amo 3:6; 1Sam 2:25; 1Fal 12:15, 24Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa jambo hili lilitoka kwa Mungu ili kutimiza neno ambalo Bwana alikuwa amenena kwa Yeroboamu mwana wa Nebati kupitia Ahiya Mshiloni.

1610:16 1Nya 9:1; 2Sam 20:1Israeli wote walipoona kuwa mfalme amekataa kuwasikiliza, wakamjibu mfalme:

“Tuna fungu gani kwa Daudi?

Sisi hatuna urithi kwa mwana wa Yese.

Nendeni kwenye mahema yenu, ee Israeli,

angalia nyumba yako mwenyewe, ee Daudi!”

Hivyo Waisraeli wakaenda kwenye mahema yao. 17Lakini kwa habari ya Waisraeli waliokuwa wakiishi katika miji ya Yuda, Rehoboamu akaendelea kuwatawala bado.

1810:18 2Sam 20:24; 1Fal 5:14Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoniramu10:18 Kiebrania ni Hadoramu. aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu, akafanikiwa kuingia kwenye gari lake na kutorokea Yerusalemu. 1910:19 1Fal 12:19; 2Fal 17:21-23; 2Nya 13:5-7; Mhu 2:9Hivyo Israeli wakaasi dhidi ya nyumba ya Daudi hadi leo.

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志下 10:1-19

北方支派背叛羅波安

1羅波安前往示劍,因為以色列人都去了那裡要立他為王。 2尼八的兒子耶羅波安曾為了躲避所羅門王而逃往埃及,並一直住在那裡。他聽到消息便返回以色列3以色列人派人去請他,他就和以色列眾人去見羅波安,說: 4「你父親使我們負擔沉重,求你減輕我們的負擔吧,我們一定效忠你。」 5羅波安對他們說:「你們三天之後再來見我。」眾人就離開了。

6羅波安王去徵詢曾服侍他父親所羅門的老臣的意見,說:「你們認為我該怎樣回覆這些百姓?」 7他們回稟說:「王若善待這些百姓,使他們喜悅,對他們好言相待,他們會永遠做王的僕人。」

8羅波安卻沒有採納老臣的意見。他又去徵詢那些和他一起長大的青年臣僚的意見, 9說:「百姓求我減輕我父親加給他們的重擔。你們認為我該怎樣回覆他們?」 10他們說:「百姓說你父親使他們負擔沉重,請求你減輕他們的負擔。你可以這樣回覆他們,『我的小指頭比我父親的腰還粗。 11我父親使你們負重擔,我要使你們負更重的擔子;我父親用鞭子打你們,我要用刺鞭打你們。』」

12過了三天,耶羅波安和百姓遵照羅波安王的話來見他。 13-14羅波安王沒有採納老臣的建議,而是照青年臣僚的建議,疾言厲色地對他們說:「我父親使你們負重擔,我要使你們負更重的擔子!我父親用鞭子打你們,我要用刺鞭打你們!」 15王不聽百姓的請求。這事出於耶和華上帝,為要應驗祂藉示羅亞希雅先知對尼八的兒子耶羅波安說的話。

16以色列人見王不聽他們的請求,就說:

「我們與大衛有何相干?

我們與耶西的兒子沒有關係!

以色列人啊,各自回家吧!

大衛家啊,自己照顧自己吧!」

於是,以色列人都各自回家了。 17但住在猶大城邑的以色列人仍受羅波安統治。 18羅波安王派勞役總管哈多蘭以色列人那裡,以色列人卻用石頭打死了他,羅波安王連忙上車逃回耶路撒冷19從此,以色列人反叛大衛家,直到今天。