1 Wafalme 8 – NEN & NSP

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 8:1-66

Sanduku La Agano Laletwa Hekaluni

(2 Nyakati 5)

18:1 Ezr 7:7Kisha Mfalme Solomoni akawaita mbele zake huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi. 28:2 1Nya 3:22Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa Mfalme Solomoni wakati wa sikukuu ya mwezi wa Ethanimu, ndio mwezi wa saba.

38:3 1Nya 3:22; Ezr 2:3Wazee wote wa Israeli walipofika, makuhani wakajitwika Sanduku la Agano, 48:4 Ezr 2:6nao wakalipandisha Sanduku la Bwana, na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani na Walawi wakavibeba, 5naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli waliokusanyika kumzunguka walikuwa mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu nyingi za kondoo na ngʼombe ambao idadi yao haikuwezekana kuandikwa au kuhesabiwa.

68:6 Ezr 2:15; Neh 7:20Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la Bwana hadi mahali pake ndani ya sehemu takatifu ndani ya Hekalu, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi. 7Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kutia kivuli Sanduku pamoja na mipiko yake ya kubebea. 8Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilionekana kutoka Mahali Patakatifu mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo. 9Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili za mawe ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo Bwana alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.

10Makuhani walipoondoka katika Mahali Patakatifu, wingu likajaza Hekalu la Bwana. 11Nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu lake.

12Ndipo Solomoni akasema, “Bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene; 138:13 Ezr 2:13naam, hakika nimekujengea Hekalu zuri sana, mahali pako pa kuishi milele.”

Hotuba Ya Solomoni

(2 Nyakati 6:3-11)

14Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki. 158:15 Ezr 2:40; 7:7; Mdo 16:13; 20:28; Za 137:1; Mit 27:23; Ebr 13:17; Ezr 7:7; Hes 8:1Kisha akasema:

“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mkono wake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema, 16‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo ili Jina langu lipate kuwamo humo, bali nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’

178:17 Ezr 2:43“Ilikuwa moyoni mwa Daudi baba yangu kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 188:18 Ezr 5:5; 7:28; Neh 8:7; Rum 8:28; Mit 3:6; Law 10:10-11; 2Nya 30:22Lakini Bwana akamwambia Daudi baba yangu, ‘Kwa sababu ilikuwa moyoni mwako kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu, ulifanya vyema kuwa na jambo hili moyoni mwako. 19Hata hivyo, sio wewe utakayenijengea hekalu, bali mwanao, ambaye ni nyama yako na damu yako mwenyewe, yeye ndiye atakayejenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’

208:20 1Nya 9:2; Ezr 2:43Bwana ametimiza ahadi aliyoiweka: Nimeingia mahali pa Daudi baba yangu na sasa ninakikalia kiti cha ufalme cha Israeli, kama vile Bwana alivyoahidi, nami nimejenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 218:21 2Nya 9:2; Ezr 2:438:21 2Nya 20:3; Za 27:11; Law 16:29; Za 5:8; 2Nya 20:3; Law 16:29; Isa 58:3-5Nimetenga nafasi humo kwa ajili ya Sanduku la Agano, ambamo ndani yake kuna lile Agano la Bwana alilofanya na baba zetu wakati alipowatoa Misri.”

Maombi Ya Solomoni Ya Kuweka Hekalu Wakfu

(2 Nyakati 6:12-42)

228:22 Neh 2:9; Yer 41:16; 2Nya 15:2; 1Kor 9:15; 1Nya 28:9; Ezr 7:6-9; Za 33:18-19; Isa 3:10; Rum 8:28; 1Pet 3:12; Za 34:16; 2Nya 15:2Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana machoni pa kusanyiko lote la Israeli, akakunjua mikono yake kuelekea mbinguni 238:23 2Nya 33:13; Kum 4:29; Mdo 14:23; 1Nya 5:20; Isa 19:22; Yer 29:12-13na kusema:

“Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni wala chini duniani, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote. 24Umetimiza ahadi yako kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, kwa kinywa chako uliahidi na kwa mkono wako umetimiza, kama ilivyo leo.

258:25 Ezr 7:15-16“Sasa Bwana, Mungu wa Israeli, mtimizie mtumishi wako Daudi baba yangu ahadi zako ulizomwahidi uliposema, ‘Kamwe hutakosa kuwa na mtu atakayeketi mbele zangu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli, kama wanao wakiangalia yote wayafanyayo kuenenda mbele zangu kama vile ulivyofanya.’ 26Sasa, Ee Mungu wa Israeli, acha neno lako lile ulilomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu litimie.

27“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga! 288:28 Kum 33:8; Law 21:6; 22:2-3; 2Nya 24:14; Hes 4:4; Isa 52:11; 1Nya 23:28Hata hivyo sikiliza dua ya mtumishi wako na maombi yake kwa huruma, Ee Bwana Mungu wangu. Sikia kilio na dua ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako siku hii ya leo. 298:29 1Nya 26:20-26; Lk 12:38-39Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa. 30Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia kutoka mbinguni, mahali pa makao yako na usikiapo, samehe.

318:31 Ay 5:19-24; Isa 41:10-14; Ezr 7:6-7, 28“Mtu anapomkosea jirani yake na akatakiwa kuapa, akija na kuapa mbele ya madhabahu yako ndani ya Hekalu hili, 328:32 Mwa 40:13; Neh 2:11; Isa 56:6; 14:1basi, sikia kutoka mbinguni na ukatende. Hukumu kati ya watumishi wako, ukimhukumu yule mwenye hatia na kuleta juu ya kichwa chake yale aliyoyatenda. Umtangazie mwenye haki kwamba hana hatia, hivyo ukathibitishe kuwa haki kwake.

338:33 Neh 3:3, 21-24“Wakati watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, watakapokugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili, 34basi usikie kutoka mbinguni, ukasamehe dhambi ya watu wako Israeli na kuwarudisha katika nchi uliyowapa baba zao.

358:35 Ezr 6:17“Wakati mbingu zitakapokuwa zimefungwa kusiwe na mvua kwa sababu watu wako wametenda dhambi dhidi yako, watakapoomba kuelekea mahali hapa na kulikiri jina lako nao wakageuka kutoka dhambi zao kwa sababu umewaadhibu, 368:36 Ezr 7:21-24; Zek 8:1-23; Es 9:3basi usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi.

37“Wakati njaa au tauni vikija juu ya nchi, au koga au kawa, nzige au panzi, au wakati adui atakapowazingira katika mji wao wowote, maafa ya namna yoyote au ugonjwa wowote unaoweza kuwajia, 38wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akitambua taabu za moyo wake mwenyewe, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili: 39basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote), 40ili wakuogope kwa wakati wote watakaoishi katika nchi uliyowapa baba zetu.

41“Kwa habari ya mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako, 42kwa maana watu watasikia juu ya Jina lako kuu na juu ya mkono wako wenye nguvu na mkono wako ulionyooshwa, atakapokuja na kuomba kuelekea Hekalu hili, 43basi na usikie kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, ukafanye lolote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli nao wapate pia kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako.

44“Wakati watu wako watakapokwenda vitani dhidi ya adui zao, popote utakapowapeleka, wakati watakapoomba kwa Bwana kuelekea mji ambao umeuchagua, na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, 45basi usikie dua na maombi yao kutoka mbinguni, ukawatetee haki yao.

46“Watakapotenda dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna mtu yeyote ambaye hatendi dhambi, nawe ukachukizwa nao na kuwakabidhi kwa adui, ambaye atawachukua utumwani katika nchi yake mwenyewe, mbali au karibu; 47na kama watabadilika mioyo yao katika nchi wanakoshikiliwa mateka, nao wakatubu na kukulilia katika nchi ya wale waliowashinda na kusema, ‘Tumetenda dhambi, tumefanya makosa, tumetenda uovu’; 48kama wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako; 49basi kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, usikie dua yao na maombi yao na kuitetea haki yao. 50Uwasamehe watu wako, waliotenda dhambi dhidi yako; uwasamehe makosa yote waliyoyatenda dhidi yako, ukawafanye wale waliowashinda kuwaonea huruma; 51kwa maana ni watu wako na urithi wako, uliowatoa Misri, kutoka kwenye lile tanuru la kuyeyushia chuma.

52“Macho yako na yafumbuke juu ya ombi la mtumishi wako na ombi la watu wako Israeli, nawe uwasikilize wakati wowote wanapokulilia. 53Kwa maana uliwachagua wao kutoka mataifa yote ya ulimwengu kuwa urithi wako mwenyewe, kama ulivyotangaza kupitia mtumishi wako Mose wakati wewe, Ee Bwana Mwenyezi, ulipowatoa baba zetu kutoka Misri.”

54Wakati Solomoni alipomaliza dua hizi zote na maombi kwa Bwana, akainuka kutoka mbele ya madhabahu ya Bwana, mahali alipokuwa amepiga magoti, mikono yake ikawa imekunjuliwa kuelekea juu mbinguni. 55Akasimama na kubariki kusanyiko lote la Israeli kwa sauti kubwa akisema:

56“Ahimidiwe Bwana, aliyewapa pumziko watu wake Israeli kama vile alivyokuwa ameahidi. Hakuna hata neno moja lililopunguka kati ya ahadi zote nzuri alizozitoa kupitia mtumishi wake Mose. 57Bwana Mungu wetu na awe pamoja nasi kama alivyokuwa na baba zetu, kamwe asituache wala kutukataa. 58Yeye na aielekeze mioyo yetu kwake, ili tutembee katika njia zake zote na kuzishika amri na maagizo na masharti aliyowapa baba zetu. 59Nami maneno yangu haya, ambayo nimeyaomba mbele za Bwana, yawe karibu na Bwana Mungu wetu usiku na mchana, ili kwamba atetee shauri la mtumishi wake na la watu wake Israeli kulingana na hitaji lao la kila siku, 60ili kwamba mataifa yote ya dunia wajue kwamba Bwana ndiye Mungu na kwamba hakuna mwingine. 61Lakini ni lazima mwiweke mioyo yenu kikamilifu kwa Bwana Mungu wetu, kuishi kwa maagizo yake na kutii amri zake, kama ilivyo wakati huu.”

Kuwekwa Wakfu Hekalu

(2 Nyakati 7:4-10)

62Kisha mfalme na Israeli wote pamoja naye wakatoa dhabihu mbele za Bwana. 63Solomoni akatoa dhabihu sadaka za amani kwa Bwana: ngʼombe 22,000, pamoja na kondoo na mbuzi 120,000. Hivyo ndivyo mfalme na Waisraeli wote walivyoweka wakfu Hekalu la Bwana.

64Siku iyo hiyo mfalme akaweka wakfu sehemu ya katikati ya ua uliokuwa mbele ya Hekalu la Bwana na hapo akatoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele za Bwana ilikuwa ndogo sana kuweza kubeba sadaka hizo za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta ya sadaka ya amani.

65Hivyo Solomoni akaiadhimisha sikukuu kwa wakati ule, na Israeli wote pamoja naye. Walikuwa kusanyiko kubwa sana, watu kutoka Lebo-Hamathi hadi Kijito cha Misri. Wakaiadhimisha mbele za Bwana Mungu wetu kwa siku saba na siku saba zaidi, yaani, jumla siku kumi na nne. 66Siku iliyofuata, aliwaruhusu watu waondoke. Wakambariki mfalme, kisha wakaenda nyumbani, wakiwa na mashangilio na furaha rohoni kwa ajili ya mambo yote mema ambayo Bwana ametenda kwa ajili ya Daudi mtumishi wake na watu wake Israeli.

New Serbian Translation

1. Књига о царевима 8:1-66

Освећење Дома

1Тада је Соломон окупио у Јерусалиму израиљске старешине, све племенске кнезове и вође израиљских породица, да пренесу Ковчег савеза Господњег из Давидовог града, са Сиона. 2Сви Израиљци су се окупили код цара Соломона на празник у месецу Етаниму, што је седми месец.

3Кад су дошле све израиљске старешине, свештеници су понели Ковчег. 4Понели су и Ковчег Господњи и Шатор од састанка и све свето посуђе, које је било у Шатору; носили су их свештеници и Левити. 5А цар Соломон и сва заједница Израиљаца, који су се окупили код њега пред Ковчегом, приносили су на жртву толико ситне и крупне стоке да их се није могло избројити ни прорачунати.

6Затим су свештеници донели Ковчег савеза Господњег на његово место, у унутрашње Светилиште Дома, у Светињу над светињама, под крила херувима. 7Наиме, херувими су имали раширена крила над Ковчегом, тако да су од горе заклањали Ковчег и његове дршке. 8Дршке су биле толико дугачке да су се њихови крајеви видели из Светилишта испред Светиње над светињама. Ипак, нису се виделе споља. Тамо су до дана данашњег. 9У Ковчегу није било ничег осим две камене плоче, које је тамо положио Мојсије на Хориву, кад је Господ склопио савез са Израиљцима, након што су изашли из Египта.

10Кад су свештеници изашли из Светилишта, облак је испунио Дом Господњи. 11Свештеници нису могли да стоје и обављају службу због облака, јер је слава Господња испунила Дом Господњи.

12Тада Соломон рече: „Господ је рекао да ће пребивати у густој тами. 13Ја сам ти саградио величанствени Дом, стан где ћеш пребивати довека.“

Соломонов говор

14Затим се цар окренуо и благословио сав збор Израиљев, док је сав збор Израиљев стајао.

15Тада рече:

„Нека је благословен Господ, Бог Израиљев, који је својом руком извршио оно што је својим устима обећао моме оцу Давиду, рекавши: 16’Од дана кад сам извео свој народ Израиљ из Египта, нисам изабрао град међу свим племенима Израиљевим да се сагради Дом где би пребивало моје име; али сам изабрао Давида да влада над мојим народом Израиљем.’

17Мој отац Давид је наумио да сазида Дом имену Господа, Бога Израиљевог. 18Но, Господ рече моме оцу Давиду: ’Добро си учинио што си у свом срцу наумио да сазидаш Дом моме имену. 19Ипак, нећеш ти саградити Дом, него ће твој син, који је потекао из твојих бедара, саградити Дом моме имену.’

20Господ је одржао обећање, те сам ја наследио свога оца Давида на Израиљевом престолу, како је Господ обећао, и изградио Дом имену Господа, Бога Израиљевог. 21Поставио сам и место за Ковчег, где је савез Господњи, који је он склопио са нашим прецима кад их је извео из Египта.“

Соломонова молитва

22Соломон је стао пред жртвеник Господњи, испред свег збора Израиљевог, испружио руке према небу 23и рекао:

„О, Господе, Боже Израиљев, нема Бога као што си ти, горе на небесима, ни доле на земљи, који чуваш савез и милост својим слугама који ходају пред тобом свим својим срцем. 24Ти си испунио што си рекао своме слузи, моме оцу Давиду; што си рекао својим устима, то си извршио својом руком, као што је то данас.

25А сад, Господе, Боже Израиљев, одржи што си обећао своме слузи, моме оцу Давиду, кад си рекао: ’Неће ти нестати потомка преда мном који ће седети на Израиљевом престолу, само ако твоји синови буду пазили на свој пут и ходили преда мном, као што си ти ходио преда мном.’ 26А сад, Боже Израиљев, нека се обистини твоја реч, коју си рекао своме слузи, моме оцу Давиду.

27Али зар ће Бог заиста боравити на земљи? Ни највиша те небеса не могу обухватити, а камоли овај Дом што сам саградио. 28Обазри се на молитву слуге свога и на његову молбу, Господе Боже; послушај вапај и молитву, коју слуга твој упућује данас пред тобом. 29Нека твоје очи мотре на овај Дом и ноћу и дању, према месту за које си рекао: ’Моје ће име бити тамо’, како би чуо молитву коју ти слуга твој упућује на овом месту. 30Почуј преклињање свога слуге и свога народа Израиља којим се моле на овом месту. Послушај на небу, на месту где пребиваш – послушај и опрости.

31Кад неко згреши против свог ближњега, те се од њега тражи да се закуне, и он дође и закуне се пред твојим жртвеником у овом Дому, 32ти чуј с небеса и делуј, те осуди онога који је учинио безакоње сваљујући на његову главу према ономе што је учинио. А праведника награди према његовој праведности.

33Ако твој народ Израиљ буде поражен од непријатеља зато што су згрешили против тебе, али се покају пред тобом и дају славу твоме имену, па се помоле и преклињу за милост у овом Дому, 34ти чуј на небесима и опрости грех свога народа Израиља, и врати их у земљу коју си дао њиховим прецима.

35Ако се небо затвори и не даје кишу, јер су згрешили против тебе, па се помоле на овом месту, те одају славу твоме имену и покају се за своје грехе, пошто их понизиш, 36ти чуј на небесима и опрости грех својих слугу, свога народа Израиља. И кад их научиш добром путу да по њему ходе, пошаљи кишу својој земљи, коју си дао своме народу у наследство.

37Ако земљу задеси глад, или помор, суша, кукољ, скакавци, гусенице, или кад их непријатељ опколи у којем од њихових градова; каква год да је пошаст или болест, 38па било ко од свег твог народа Израиља осети тегобу у свом срцу и упути молитву или молбу ширећи руке према овом Дому, 39услиши на небесима, на твом Пребивалишту. Опрости и делуј: дај свакоме по свим његовим делима, јер ти знаш његово срце – само ти знаш срце свих људи – 40да би те се бојали у све дане док живе у земљи коју си дао њиховим оцима.

41Ако и странац, који није од твог народа Израиља, дође из далеке земље ради твог имена, 42јер ће се чути за твоје велико име и за твоју моћну руку и испружену мишицу – ако дође и помоли се у овом Дому – 43услиши га на небесима, на твом Пребивалишту, и учини све за шта ти овај странац завапи, да би народи на земљи упознали твоје име и да би те се бојали, као твој народ Израиљ, и да би знали да се твоје име призива над овим Домом који сам саградио.

44Ако твој народ изађе у бој против свога непријатеља путем којим га ти пошаљеш, и они се помоле Господу према граду који си изабрао, и према Дому који сам саградио твоме имену, 45чуј на небесима њихову молитву и њихову молбу, те им додели правду.

46Ако згреше против тебе – јер нема човека који не чини грех – и ти се разгневиш на њих и изручиш их њиховим непријатељима, који их одведу као заробљенике у непријатељску земљу, било далеко или близу, 47ако тада дођу к себи у земљи у којој су заробљени и покају се, те се почну молити теби у земљи својих поробљивача, говорећи: ’Згрешили смо, учинили смо неправду, скривили смо’, 48па се врате к теби свим срцем и свом душом у земљи својих непријатеља који су их поробили, и помоле се теби према својој земљи коју си дао њиховим оцима и према граду који си изабрао и према Дому који сам саградио за твоје име, 49ти чуј на небесима, на твом Пребивалишту, њихову молитву и молбу, и учини им по правди. 50Тада опрости своме народу, који је згрешио против тебе и за све преступе који су учинили против тебе, и смилуј им се пред њиховим поробљивачима да би се они смиловали на њих. 51Јер они су твој народ и твоје наследство, кога си извео из Египта, из топионице гвожђа.

52Нека твоје очи бдију над молбом твога слуге и над молбом твога народа Израиља, и услиши их кад год те призову. 53Јер ти си их, Господе Боже, издвојио себи за наследство од свих народа на земљи, као што си рекао преко свога слуге Мојсија, кад си извео наше очеве из Египта.“

Соломон благосиља народ

54Кад је Соломон завршио сву ову молитву и молбу коју је упутио Господу, устао је испред жртвеника Господњег где је клечао на својим коленима с раширеним рукама према небу. 55Затим се усправио, па је громким гласом благословио сав збор Израиљев, рекавши:

56„Нека је благословен Господ који је дао починак своме народу Израиљу, као што је обећао; ниједна реч није остала неиспуњена од свих добрих обећања које је дао преко свога слуге Мојсија. 57Нека Господ, Бог наш, буде с нама као што је био с нашим оцима; нека нас не напусти и не остави. 58Нека приклони наша срца к себи, да следимо све његове путеве, и да држимо његове заповеди, прописе и одредбе, које је заповедио нашим оцима. 59Нека ове речи што сам измолио пред Господом, буду близу Господа, Бога нашега, дању и ноћу, да би дан за даном чинио правду своме слузи и своме народу Израиљу, 60те да би сви народи на земљи знали да Господ јесте Бог и да нема другог. 61Стога, нека ваше срце буде потпуно предано Господу, Богу нашем, следећи његове прописе и држећи његове заповеди, као овога дана.“

Посвећење Дома

62Затим су цар и сав израиљски народ с њим принели жртве пред Господом. 63Соломон је принео Господу као жртву мира двадесет две хиљаде говеда и стотину двадесет хиљада оваца. Тако су цар и сви Израиљци посветили Дом Господњи.

64Тог дана је цар посветио средиште дворишта, које је испред Дома Господњег. Наиме, тамо је принео жртву свеспалницу, житну жртву, и сало жртава мира, пошто је бронзани жртвеник који је био пред Господом био премален да би на њега стале жртве свеспалнице, житне жртве и сало жртава мира.

65У то време је Соломон, са свим Израиљем, приредио свечаност – велики сабор пред Господом, Богом нашим, с народом од Лево-Амата до Египатског потока, седам дана и још седам дана, укупно четрнаест дана. 66Осмог дана је отпремио народ, а они су благословили цара и отишли својим кућама, веселећи се и радујући се у срцу због свег добра што је Господ учинио своме слузи Давиду и своме народу Израиљу.