1 Wafalme 2 – NEN & TNCV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Wafalme 2:1-46

Maagizo Ya Daudi Kwa Solomoni

12:1 2Nya 36:20; Neh 7:6; 11:3; 2Fal 24:16; 25:12; Ezr 5:8; 6:2; Es 1:1; 8:9Siku zilipokaribia za Daudi kufa, akampa mwanawe Solomoni agizo.

22:2 1Nya 3:19; 6:14; Hag 2:4; Zek 3:1-10Akasema, “Mimi ninakaribia kwenda njia ya dunia yote. Hivyo uwe hodari, jionyeshe kuwa mwanaume, 32:3 Ezr 10:25; Neh 3:25shika lile Bwana Mungu wako analokuagiza: Enenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Mose, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na popote uendako, 4ili kwamba Bwana aweze kunitimizia ahadi yake: ‘Kama wazao wako wakiangalia sana wanavyoishi, na kama wakienenda kwa uaminifu mbele zangu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, kamwe hutakosa kuwa na mtu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli.’

52:5 Neh 6:18“Sasa wewe mwenyewe unafahamu lile Yoabu mwana wa Seruya alilonitendea, lile alilofanya kwa majemadari wawili wa majeshi ya Israeli, Abneri mwana wa Neri, na Amasa mwana wa Yetheri. Aliwaua, akimwaga damu yao wakati wa amani kama vile ni kwenye vita, tena akaipaka damu ile kwenye mkanda uliokuwa kiunoni mwake na viatu alivyovaa miguuni mwake. 6Shughulika naye kwa kadiri ya hekima yako, lakini usiache kichwa chake chenye mvi kishukie kaburi kwa amani.

7“Lakini uwaonyeshe wema wana wa Barzilai wa Gileadi na uwaruhusu wawe miongoni mwa wale walao mezani pako. Walisimama nami nilipomkimbia ndugu yako Absalomu.

8“Ukumbuke, unaye Shimei mwana wa Gera, Mbenyamini kutoka Bahurimu, ambaye alinilaani kwa laana kali siku niliyokwenda Mahanaimu. Aliposhuka kunilaki huko Yordani, nilimwapia kwa Bwana: ‘Sitakuua kwa upanga!’ 9Lakini sasa, usidhani kwamba hana hatia. Wewe ni mtu wa hekima, utajua la kumtendea. Zishushe mvi zake kaburini kwa damu.”

10Kisha Daudi akapumzika pamoja na baba zake naye akazikwa katika Mji wa Daudi. 11Daudi alikuwa ametawala juu ya Israeli miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu. 12Kwa hiyo Solomoni akaketi katika kiti cha ufalme cha baba yake Daudi, nao utawala wake ukaimarika sana.

Kiti Cha Ufalme Cha Solomoni Chaimarishwa

132:13 Ezr 8:13; 7:18Basi Adoniya, mwana wa Hagithi, akaenda kwa Bathsheba, mama yake Solomoni. Bathsheba akamuuliza, “Je, umekuja kwa amani?”

Akajibu, “Ndiyo, kwa amani.” 14Kisha akaongeza, “Ninalo jambo la kukuambia.”

Akajibu, “Waweza kulisema.”

15Akasema, “Kama unavyojua, ufalme ulikuwa wangu. Israeli wote waliniangalia mimi kama mfalme wao. Lakini mambo yalibadilika, ufalme umekwenda kwa ndugu yangu, kwa maana umemjia kutoka kwa Bwana. 16Sasa ninalo ombi moja ninalokuomba. Usinikatalie.”

Bathsheba akasema, “Waweza kuliomba.”

17Kwa hiyo akaendelea kusema, “Tafadhali mwombe Mfalme Solomoni, anipatie Abishagi, Mshunami, awe mke wangu; hatakukatalia wewe.”

18Bathsheba akamjibu, “Vema sana, nitazungumza na mfalme kwa ajili yako.”

19Bathsheba alipokwenda kwa Mfalme Solomoni kuzungumza naye kwa ajili ya Adoniya, mfalme alisimama kumlaki mama yake, akamwinamia na kuketi kwenye kiti chake cha ufalme. Akaamuru kiti cha ufalme kuletwa kwa ajili ya mama yake mfalme, naye akaketi mkono wake wa kuume.

202:20 Yos 9:17Bathsheba akamwambia mfalme, “Ninalo ombi moja dogo la kukuomba; usinikatalie.”

Mfalme akajibu, “Omba, mama yangu; sitakukatalia.”

212:21 Mik 5:2; 1Nya 2:51; Rut 1:19; Mt 2:6; 2Sam 21:2; Mwa 35:19Akasema, “Mruhusu Abishagi, Mshunami, aolewe na ndugu yako Adoniya.”

22Mfalme Solomoni akamjibu mama yake, “Kwa nini uombe Abishagi, Mshunami, kwa ajili ya Adoniya? Ungeweza pia kuomba ufalme kwa ajili yake, kwani yeye ni ndugu yangu mkubwa: naam, kwa ajili yake, na kwa kuhani Abiathari na Yoabu mwana wa Seruya!”

23Mfalme Solomoni akaapa kwa Bwana, akasema: “Mungu na aniulie mbali, tena bila huruma, ikiwa Adoniya hatalipa kwa uhai wake kwa ajili ya ombi hili! 24Basi sasa, hakika kama Bwana aishivyo, yeye ambaye ameniimarisha salama kwenye kiti cha ufalme cha Daudi baba yangu, naye amenipa ufalme wa kudumu kama alivyoahidi, Adoniya atauawa leo!” 25Hivyo Mfalme Solomoni akatoa amri kwa Benaya mwana wa Yehoyada, naye akampiga Adoniya akafa.

262:26 Yos 21:18; 1Sam 22:20; 2Sam 15:14Mfalme akamwambia kuhani Abiathari, “Nenda huko Anathothi katika mashamba yako. Wewe unastahili kufa, lakini sitakuua sasa, kwa sababu ulilichukua Sanduku la Bwana Mwenyezi mbele ya Daudi baba yangu na ulishiriki taabu zote za baba yangu.” 27Hivyo Solomoni akamwondoa Abiathari kwenye ukuhani wa Bwana, akilitimiza neno la Bwana alilokuwa amenena huko Shilo kuhusu nyumba ya Eli.

282:28 Mwa 12:8Habari zilipomfikia Yoabu, ambaye alikuwa amefanya shauri baya na Adoniya, lakini sio na Absalomu, alikimbilia kwenye hema la Bwana na kushika pembe za madhabahu. 29Mfalme Solomoni akaambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema la Bwana naye alikuwa kando ya madhabahu. Basi Solomoni akamwagiza Benaya mwana wa Yehoyada: “Nenda ukamuue!”

30Ndipo Benaya akaingia kwenye hema la Bwana na kumwambia Yoabu, “Mfalme anasema, ‘Toka nje!’ ”

Lakini akajibu, “La! Nitafia hapa hapa.”

Benaya akamwarifu mfalme, “Hivi ndivyo Yoabu alivyonijibu.”

312:31 Ezr 2:7Kisha mfalme akamwamuru Benaya, “Fanya kama asemavyo. Muue na kumzika, ili uniondolee mimi na nyumba ya baba yangu dhambi ya damu isiyokuwa na hatia ile Yoabu aliyoimwaga. 32Bwana atamlipiza kwa ajili ya damu aliyoimwaga, kwa sababu pasipo Daudi baba yangu kujua, aliwashambulia watu wawili na kuwaua kwa upanga. Wote wawili, Abneri mwana wa Neri, jemadari wa jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Yetheri, jemadari wa jeshi la Yuda, walikuwa watu wazuri na wanyofu kuliko yeye. 33Hatia ya damu yao na iwe juu ya kichwa cha Yoabu na wazao wake milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, nyumba yake na kiti chake cha ufalme, iwepo amani ya Bwana milele.”

342:34 Kum 34:3; 2Nya 28:15; 1Fal 16:34Basi Benaya mwana wa Yehoyada akakwea, akampiga na kumuua Yoabu, naye akazikwa katika nchi yake mwenyewe katika jangwa. 35Mfalme akamweka Benaya mwana wa Yehoyada juu ya jeshi kwenye nafasi ya Yoabu na kumweka kuhani Sadoki badala ya Abiathari.

362:36 1Nya 9:10; 24:7Kisha mfalme akatuma ujumbe kwa Shimei na kumwambia, “Ujijengee nyumba huko Yerusalemu uishi huko, lakini usiende mahali pengine popote. 372:37 1Nya 24:14; Ezr 10:20Siku utakayoondoka kuvuka Bonde la Kidroni, uwe na hakika utakufa; damu yako itakuwa juu ya kichwa chako mwenyewe.”

382:38 1Nya 9:12; Ezr 10:22Shimei akamjibu mfalme, “Ulilolisema ni jema. Mtumishi wako atatenda kama bwana wangu mfalme alivyosema.” Naye Shimei akakaa Yerusalemu kwa muda mrefu.

392:39 1Nya 24:8Lakini baada ya miaka mitatu, watumwa wawili wa Shimei wakatoroka kwenda kwa Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi, naye Shimei akaambiwa, “Watumwa wako wako Gathi.” 402:40 Hes 3:9; Ezr 3:9Kwa ajili ya hili, Shimei akatandika punda wake, akaenda kwa Akishi huko Gathi kuwatafuta watumwa wake. Basi Shimei akaondoka na kuwarudisha watumwa wake kutoka Gathi.

412:41 1Nya 15:16Solomoni alipoambiwa kuwa Shimei ametoka Yerusalemu na kwenda Gathi na amekwisha kurudi, 422:42 1Sam 3:15; 1Nya 9:17mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa Bwana na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine popote, uwe na hakika utakufa?’ Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’ 432:43 1Nya 9:2Kwa nini basi hukutunza kiapo chako kwa Bwana na kutii amri niliyokupa?”

44Pia mfalme akamwambia Shimei, “Unajua katika moyo wako makosa uliyomtendea baba yangu Daudi. Sasa Bwana atakulipiza kwa ajili ya mabaya yako uliyotenda. 45Lakini Mfalme Solomoni atabarikiwa, na kiti cha ufalme cha Daudi kitakuwa imara mbele za Bwana milele.”

46Kisha mfalme akatoa amri kwa Benaya mwana wa Yehoyada, naye akatoka nje, akampiga Shimei na kumuua.

Sasa ufalme ukawa umeimarika kikamilifu mikononi mwa Solomoni.

Thai New Contemporary Bible

1พงศ์กษัตริย์ 2:1-46

ดาวิดกำชับโซโลมอน

(1พศด.29:26-28)

1เมื่อดาวิดใกล้จะสิ้นพระชนม์ พระองค์ทรงกำชับโซโลมอนโอรสของพระองค์ว่า

2“พ่อกำลังจะจากไปตามธรรมดาโลก ฉะนั้นเจ้าจงเข้มแข็งและเป็นชายชาตรี 3จงรักษาข้อกำหนดที่พระเจ้าพระยาห์เวห์ทรงวางไว้ ดำเนินในทางของพระองค์และปฏิบัติตามกฎหมาย พระบัญชา บทบัญญัติ และข้อกำหนดของพระองค์ ตามที่บันทึกไว้ในบทบัญญัติของโมเสส เพื่อเจ้าจะเจริญก้าวหน้า ไม่ว่าจะไปที่ไหนหรือทำสิ่งใด 4และเพื่อองค์พระผู้เป็นเจ้าจะทรงทำตามพระสัญญาที่พระองค์ทรงให้ไว้กับพ่อว่า ‘หากลูกหลานของเจ้าระมัดระวังวิถีการดำเนินชีวิตของตน ซื่อสัตย์ภักดีต่อเราสุดใจสุดวิญญาณแล้ว เจ้าจะไม่ขาดคนครองบัลลังก์อิสราเอลเลย’

5“นี่แน่ะ! ลูกเองก็รู้สิ่งที่โยอาบบุตรนางเศรุยาห์ทำกับพ่อ ที่เขาได้ฆ่าแม่ทัพอิสราเอลสองนายคือ อับเนอร์บุตรเนอร์และอามาสาบุตรเยเธอร์ ทำให้เขาทั้งสองหลั่งเลือดในยามสงบราวกับยามศึก โลหิตจึงแปดเปื้อนผ้าคาดเอวและรองเท้าของโยอาบ 6ลูกจงใช้สติปัญญาจัดการกับเขา อย่าปล่อยให้เขาแก่ตายอย่างสงบ

7“แต่จงแสดงความกรุณาแก่ลูกๆ ของบารซิลลัยแห่งกิเลอาด และให้เขามาร่วมโต๊ะเสวยด้วย พวกเขาอยู่ฝ่ายพ่อเมื่อพ่อหนีอับซาโลมพี่ชายของเจ้าไป

8“และก็อย่าลืมชิเมอีบุตรเกราคนเบนยามินจากบาฮูริม ผู้ซึ่งแช่งด่าพ่ออย่างเจ็บแสบตอนที่พ่อไปยังมาหะนาอิม เมื่อเขาลงมาต้อนรับพ่อที่จอร์แดน พ่อก็ได้สาบานกับเขาโดยอ้างองค์พระผู้เป็นเจ้าว่า ‘เราจะไม่ฆ่าเจ้าด้วยดาบ’ 9แต่บัดนี้อย่าถือว่าเขาพ้นผิด ลูกเป็นคนฉลาดย่อมรู้ว่าจะจัดการกับเขาอย่างไร จงประหารเขาเสีย”

10จากนั้นดาวิดก็ทรงล่วงลับไปอยู่กับบรรพบุรุษ และถูกฝังไว้ในเมืองดาวิด 11ดาวิดทรงปกครองอิสราเอลเป็นเวลา 40 ปี ปกครองในเมืองเฮโบรน 7 ปี และในกรุงเยรูซาเล็มอีก 33 ปี 12โซโลมอนจึงขึ้นครองบัลลังก์ของดาวิดราชบิดา และรัชกาลของพระองค์มั่นคงเป็นปึกแผ่น

บัลลังก์ของโซโลมอนมั่นคง

13ฝ่ายอาโดนียาห์โอรสของพระนางฮักกีทมาเข้าเฝ้าพระนางบัทเชบาราชมารดาของโซโลมอน พระนางตรัสว่า “เจ้ามาอย่างสันติหรือ?”

อาโดนียาห์ทูลว่า “ข้าพระบาทมาอย่างสันติ” 14เขากล่าวอีกว่า “ข้าพระบาทมีเรื่องมากราบทูล”

พระนางตรัสว่า “พูดไปเถิด”

15อาโดนียาห์ทูลว่า “ตามที่ทรงทราบดีว่าราชอาณาจักรเป็นของข้าพระบาท อิสราเอลทั้งปวงล้วนคาดหมายว่าข้าพระบาทจะได้เป็นกษัตริย์ แต่เหตุการณ์กลับตาลปัตร ราชอาณาจักรตกเป็นของน้องชายแทน เพราะการนี้เป็นมาจากองค์พระผู้เป็นเจ้า 16บัดนี้ข้าพระบาทมีสิ่งหนึ่งจะทูลขอ ขออย่าทรงปฏิเสธเลย”

พระนางตรัสว่า “พูดมาเถิด”

17อาโดนียาห์ทูลว่า “โปรดทูลกษัตริย์โซโลมอน เพราะพระองค์จะไม่ทรงปฏิเสธพระนาง ขอพระราชทานอาบีชากชาวชูเนมให้เป็นภรรยาของข้าพระบาทด้วยเถิด”

18บัทเชบาตรัสว่า “ตกลง เราจะไปขอกษัตริย์ให้”

19เมื่อบัทเชบาเข้าพบกษัตริย์โซโลมอนเพื่อทูลขอให้อาโดนียาห์ กษัตริย์ก็ทรงยืนขึ้นต้อนรับและหมอบคำนับ แล้วประทับบนบัลลังก์ ทรงให้ยกพระแท่นมาถวายราชมารดา พระนางจึงประทับเบื้องขวาพระหัตถ์

20พระนางตรัสว่า “แม่จะขออะไรสักอย่างหนึ่ง อย่าปฏิเสธแม่เลย”

กษัตริย์ตรัสตอบว่า “เสด็จแม่บอกมาเถิด ลูกไม่ปฏิเสธอยู่แล้ว”

21พระนางจึงตรัสว่า “ขอยกอาบีชากชาวชูเนมให้แต่งงานกับอาโดนียาห์พี่ชายของลูก”

22กษัตริย์โซโลมอนตรัสตอบราชมารดาว่า “ทำไมเสด็จแม่ขออาบีชากชาวชูเนมให้อาโดนียาห์? ขอราชบัลลังก์ให้เขาด้วยสิเพราะเขาเป็นพี่ชายของลูก ปุโรหิตอาบียาธาร์และโยอาบบุตรนางเศรุยาห์ก็เป็นฝ่ายเขา!”

23แล้วกษัตริย์โซโลมอนตรัสปฏิญาณโดยอ้างองค์พระผู้เป็นเจ้าว่า “ขอพระเจ้าทรงจัดการกับเราอย่างรุนแรงที่สุด หากอาโดนียาห์ไม่ชดใช้ด้วยชีวิตที่บังอาจขอเช่นนี้! 24องค์พระผู้เป็นเจ้าทรงสถาปนาเราไว้บนบัลลังก์ของเสด็จพ่อดาวิด และทรงตั้งราชวงศ์ขึ้นเพื่อเราตามที่ทรงสัญญาไว้ ดังนั้นองค์พระผู้เป็นเจ้าทรงพระชนม์อยู่แน่ฉันใด อาโดนียาห์จะต้องตายในวันนี้ฉันนั้น!” 25กษัตริย์โซโลมอนจึงตรัสสั่งเบไนยาห์บุตรเยโฮยาดา เขาก็ไปประหารชีวิตอาโดนียาห์

26กษัตริย์ตรัสกับปุโรหิตอาบียาธาร์ว่า “จงกลับไปยังที่ของท่านในอานาโธท ท่านสมควรตาย แต่เราจะไม่ประหารท่านเวลานี้ เพราะท่านได้หามหีบพันธสัญญาของพระยาห์เวห์องค์เจ้าชีวิตในรัชกาลเสด็จพ่อของเรา และท่านได้ร่วมทุกข์ร่วมสุขกับเสด็จพ่อมาโดยตลอด” 27โซโลมอนจึงทรงถอดอาบียาธาร์จากตำแหน่งปุโรหิตขององค์พระผู้เป็นเจ้า เป็นอันสำเร็จตามพระบัญชาขององค์พระผู้เป็นเจ้าที่ชิโลห์เกี่ยวกับวงศ์วานของเอลี

28ครั้นข่าวมาถึงโยอาบผู้สมคบกับอาโดนียาห์ แม้เมื่อก่อนไม่ได้คบคิดกับอับซาโลม โยอาบก็หนีไปที่พลับพลาขององค์พระผู้เป็นเจ้าและจับเชิงงอนของแท่นบูชาไว้ 29มีผู้ไปทูลโซโลมอนว่าโยอาบหนีไปยังพลับพลาขององค์พระผู้เป็นเจ้าและอยู่ข้างๆ แท่นบูชา โซโลมอนจึงตรัสสั่งเบไนยาห์บุตรเยโฮยาดาว่า “ไปประหารเขา!”

30เบไนยาห์ก็เข้าไปในพลับพลาขององค์พระผู้เป็นเจ้าและกล่าวกับโยอาบว่า “กษัตริย์ตรัสสั่งให้ออกไป!”

แต่โยอาบตอบว่า “ไม่ เราจะตายที่นี่”

เบไนยาห์จึงกลับไปทูลกษัตริย์ตามที่โยอาบบอก

31กษัตริย์ตรัสสั่งเบไนยาห์ว่า “ทำอย่างที่เขาบอก ฆ่าเขาแล้วเอาไปฝัง ตัวเราและวงศ์วานของเสด็จพ่อจะได้พ้นจากมลทินที่เขาได้ฆ่าผู้บริสุทธิ์ 32องค์พระผู้เป็นเจ้าจะให้เขาเองรับผิดชอบที่ใช้ดาบฆ่าชายสองคนซึ่งดีกว่าและชอบธรรมกว่าเขา เพราะเสด็จพ่อของเราไม่ได้มีส่วนร่วมใดๆ กับความตายของอับเนอร์บุตรเนอร์แม่ทัพอิสราเอล และอามาสาบุตรเยเธอร์แม่ทัพยูดาห์ 33ขอให้โทษผิดจากโลหิตนั้นตกอยู่แก่โยอาบกับวงศ์วานตลอดไป ส่วนดาวิดกับวงศ์วาน ราชวงศ์ และราชบัลลังก์ ขอให้มีสันติสุขขององค์พระผู้เป็นเจ้าสืบไปนิรันดร์”

34เบไนยาห์บุตรเยโฮยาดาจึงไปประหารโยอาบ ศพของโยอาบถูกฝังไว้ในที่ดินของตน2:34 หรือฝังไว้ในอุโมงค์ฝังศพของเขาในถิ่นกันดาร 35กษัตริย์ทรงแต่งตั้งเบไนยาห์เป็นแม่ทัพแทนโยอาบ และให้ศาโดกเป็นปุโรหิตแทนอาบียาธาร์

36กษัตริย์ทรงให้คนไปตามชิเมอีมา และตรัสกับเขาว่า “จงสร้างบ้านและอาศัยอยู่ในกรุงเยรูซาเล็มนี้ อย่าไปที่อื่นใดเลย 37วันใดที่เจ้าออกไปพ้นหุบเขาขิดโรน เจ้าก็แน่ใจได้ว่าเจ้าจะต้องตาย และถือเป็นความผิดของเจ้าเอง”

38ชิเมอีทูลว่า “ฝ่าพระบาทตรัสชอบแล้ว ผู้รับใช้จะปฏิบัติตาม” ชิเมอีจึงอาศัยอยู่ในกรุงเยรูซาเล็มเป็นเวลานาน

39แต่สามปีต่อมา ทาสของชิเมอีสองคนหลบหนีไปเข้าเฝ้ากษัตริย์อาคีชโอรสของมาอาคาห์แห่งเมืองกัท เมื่อมีผู้มาบอกชิเมอีว่า “ทาสของท่านอยู่ที่เมืองกัท” 40เขาก็ขึ้นลาไปเข้าเฝ้าอาคีชที่เมืองกัทเพื่อตามหาทาสและนำตัวทาสกลับมาจากเมืองนั้น

41เมื่อโซโลมอนทราบว่าชิเมอีออกจากกรุงเยรูซาเล็มไปยังเมืองกัทและกลับมาแล้ว 42กษัตริย์ก็ให้ตามชิเมอีมา และตรัสกับเขาว่า “เราเตือนเจ้า และให้เจ้าสาบานในพระนามของพระยาห์เวห์แล้วไม่ใช่หรือว่า ‘วันใดที่เจ้าออกไปที่อื่นเจ้าจะต้องตาย’? เจ้าก็ตอบว่า ‘ฝ่าพระบาทตรัสชอบแล้ว ข้าพระบาทจะปฏิบัติตาม’ 43แล้วเหตุใดเจ้าจึงไม่ทำตามที่ปฏิญาณไว้ต่อองค์พระผู้เป็นเจ้าและไม่ทำตามคำสั่งของเรา?”

44กษัตริย์ตรัสกับชิเมอีด้วยว่า “เจ้ารู้อยู่แก่ใจถึงความเลวร้ายทั้งสิ้นที่เจ้าทำไว้กับดาวิดราชบิดาของเรา บัดนี้องค์พระผู้เป็นเจ้าจะทรงคืนสนองความผิดที่เจ้าได้ทำ 45แต่กษัตริย์โซโลมอนจะได้รับพร และราชบัลลังก์ของดาวิดจะยั่งยืนมั่นคงต่อหน้าองค์พระผู้เป็นเจ้าตลอดไป”

46จากนั้นกษัตริย์ตรัสสั่งเบไนยาห์บุตรเยโฮยาดา เขาก็ออกไปประหารชิเมอี

ราชอาณาจักรจึงมั่นคงเป็นปึกแผ่นในพระหัตถ์ของโซโลมอน