1 Timotheo 3 – NEN & KJV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Timotheo 3:1-16

Sifa Za Waangalizi

13:1 1Tim 1:15; Flp 1:1Hili ni neno la kuaminiwa, kwamba mtu akitamani kazi ya uangalizi, atamani kazi nzuri. 23:2 Tit 1:6-8; Rum 12:13; 2Tim 2:24Basi, imempasa mwangalizi awe mtu asiye na lawama, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi, anayejitawala, anayeheshimika, mkarimu, ajuaye kufundisha, 33:3 2Tim 2:24; Lk 16:14; 1Pet 5:2asiwe mlevi, wala mkali bali awe mpole, asiwe mgomvi wala mpenda fedha. 43:4 Tit 1:6Lazima aweze kuisimamia nyumba yake mwenyewe vizuri na kuhakikisha kwamba watoto wake wanamtii na kuwa na heshima kwa kila njia. 53:5 1Kor 10:32(Kwa maana kama mtu hajui jinsi ya kusimamia nyumba yake mwenyewe, atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu?) 63:6 1Tim 6:4Asiwe mtu aliyeokoka karibuni asije akajivuna na kuangukia kwenye hukumu ile ile ya ibilisi. 73:7 2Tim 2:26Inampasa pia awe na sifa njema kwa watu walio nje, ili asije akalaumiwa na kuanguka kwenye mtego wa ibilisi.

Sifa Za Mashemasi

83:8 Flp 1:1; Tit 2:3Vivyo hivyo, mashemasi nao wawe watu wanaostahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili au wenye kujifurahisha kwa mvinyo, wala wanaotamani faida isiyo halali. 93:9 1Tim 1:9; Mdo 23:1Inawapasa kushikamana sana na ile siri ya imani kwa dhamiri safi. 103:10 1Tim 5:22Ni lazima wapimwe kwanza; kisha kama hakuna neno dhidi yao, basi na waruhusiwe kuhudumu kama mashemasi.

113:11 2Tim 3:3; Tit 2:3Vivyo hivyo, wake zao wawe wanawake wanaostahili heshima, wasio wasingiziaji, bali wawe na kiasi na waaminifu katika kila jambo.

123:12 1Tim 3:2, 4Shemasi awe mume wa mke mmoja na inampasa aweze kusimamia watoto wake na watu wa nyumbani mwake vyema. 133:13 Mt 25:21Wale ambao wamehudumu vyema katika huduma ya ushemasi hujipatia msimamo bora na ujasiri mkubwa katika imani yao ndani ya Kristo Yesu.

14Ingawa ninatarajia kuja kwako hivi karibuni, ninakuandikia maagizo haya sasa ili kwamba, 153:15 1Kor 10:32; Efe 2:21kama nikikawia, utajua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambayo ndiyo kanisa la Mungu aliye hai, lililo nguzo na msingi wa kweli. 163:16 Rum 16:25; Yn 1:14; Kol 1:23; Mk 16:19Bila shaka yoyote, siri ya utauwa ni kubwa:

Alidhihirishwa katika mwili wa kibinadamu,

akathibitishwa kuwa na haki katika Roho,

akaonekana na malaika,

akahubiriwa miongoni mwa mataifa,

akaaminiwa ulimwenguni,

akachukuliwa juu katika utukufu.

King James Version

1 Timothy 3:1-16

1This is a true saying, If a man desire the office of a bishop, he desireth a good work. 2A bishop then must be blameless, the husband of one wife, vigilant, sober, of good behaviour, given to hospitality, apt to teach; 3Not given to wine, no striker, not greedy of filthy lucre; but patient, not a brawler, not covetous; 4One that ruleth well his own house, having his children in subjection with all gravity; 5(For if a man know not how to rule his own house, how shall he take care of the church of God?) 6Not a novice, lest being lifted up with pride he fall into the condemnation of the devil. 7Moreover he must have a good report of them which are without; lest he fall into reproach and the snare of the devil. 8Likewise must the deacons be grave, not doubletongued, not given to much wine, not greedy of filthy lucre; 9Holding the mystery of the faith in a pure conscience. 10And let these also first be proved; then let them use the office of a deacon, being found blameless. 11Even so must their wives be grave, not slanderers, sober, faithful in all things. 12Let the deacons be the husbands of one wife, ruling their children and their own houses well. 13For they that have used the office of a deacon well purchase to themselves a good degree, and great boldness in the faith which is in Christ Jesus. 14These things write I unto thee, hoping to come unto thee shortly: 15But if I tarry long, that thou mayest know how thou oughtest to behave thyself in the house of God, which is the church of the living God, the pillar and ground of the truth. 16And without controversy great is the mystery of godliness: God was manifest in the flesh, justified in the Spirit, seen of angels, preached unto the Gentiles, believed on in the world, received up into glory.