1 Samweli 29 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Samweli 29:1-11

Akishi Amrudisha Daudi Huko Siklagi

129:1 1Sam 28:1; 4:1; Yos 17:16; 1Fal 18:45; 21:1; 2Fal 9:30; Yer 50:5; Hos 1:4; 5:11; 2:22; Yos 12:18Wafilisti wakakusanya majeshi yao yote huko Afeki, nao Waisraeli wakapiga kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli. 229:2 1Sam 28:2Watawala wa Wafilisti walipokuwa wakipita pamoja na vikosi vyao vya mamia na vya maelfu, Daudi na watu wake walikuwa wakitembea huko nyuma pamoja na Akishi. 329:3 1Nya 12:19; 1Sam 27:7; Dan 6:5; Yn 19:6; 1Pet 3:16Majemadari wa Wafilisti wakauliza, “Vipi kuhusu hawa Waebrania?”

Akishi akajibu, “Huyu si Daudi, aliyekuwa afisa wa Sauli mfalme wa Israeli? Ameshakuwa pamoja nami kwa zaidi ya mwaka, naye tangu alipomwacha Sauli hadi sasa, sikuona kosa lolote kwake.”

429:4 1Nya 12:19; 1Sam 14:21Lakini majemadari wa Wafilisti wakamkasirikia na kusema, “Mrudishe mtu huyu, apate kurudi mahali pale ulipompangia. Haimpasi kufuatana pamoja nasi vitani, asije akageuka, akawa kinyume chetu vitani. Ni kwa njia ipi bora zaidi angeweza kujipatia tena kibali kwa bwana wake, isipokuwa kwa vichwa vya watu wetu wenyewe? 529:5 1Sam 18:7; 21:11Je, huyu si ndiye Daudi walioimba kumhusu katika ngoma zao, wakisema:

“ ‘Sauli amewaua elfu zake,

naye Daudi makumi elfu yake’?”

629:6 1Sam 27:8-12; Hes 27:17; 2Sam 3:25; 2Fal 19:27; Za 121:8; Isa 37:28Basi Akishi akamwita Daudi na kumwambia, “Kama vile Bwana aishivyo, wewe umekuwa mtu mwaminifu, nami ningependa utumike pamoja nami katika jeshi. Tangu siku ile uliyofika kwangu hadi sasa, sijaona kosa lolote kwako, lakini hao watawala hawakukubali. 7Rudi na uende kwa amani; usifanye chochote cha kuwakasirisha watawala wa Kifilisti.”

8Daudi akamuuliza Akishi, “Lakini mimi nimefanya nini? Je, umeona nini kibaya juu ya mtumishi wako tangu siku ile niliyokuja kwako hadi leo? Kwa nini nisirudi na kupigana na adui za bwana wangu mfalme?”

929:9 2Sam 14:17, 20; 19:27Akishi akamjibu Daudi, “Mimi ninajua ya kuwa wewe umekuwa wa kupendeza machoni pangu kama vile malaika wa Mungu. Lakini hao majemadari wa Wafilisti wamesema, ‘Huyu haimpasi kwenda vitani pamoja nasi.’ 1029:10 1Nya 12:19Sasa amka mapema, pamoja na watumishi wa bwana wako waliofuatana nawe, nanyi ondokeni asubuhi mara kutakapopambazuka.”

1129:11 Za 37:23; 73:2; Mit 16:9; 20:24; Isa 30:21; Yer 10:23; 1Kor 10:23; 10:13; 2Sam 4:4Hivyo Daudi na watu wake wakaamka asubuhi na mapema, wakaenda zao kurudi katika nchi ya Wafilisti, nao Wafilisti wakapanda kwenda Yezreeli.

New International Version

1 Samuel 29:1-11

Achish Sends David Back to Ziklag

1The Philistines gathered all their forces at Aphek, and Israel camped by the spring in Jezreel. 2As the Philistine rulers marched with their units of hundreds and thousands, David and his men were marching at the rear with Achish. 3The commanders of the Philistines asked, “What about these Hebrews?”

Achish replied, “Is this not David, who was an officer of Saul king of Israel? He has already been with me for over a year, and from the day he left Saul until now, I have found no fault in him.”

4But the Philistine commanders were angry with Achish and said, “Send the man back, that he may return to the place you assigned him. He must not go with us into battle, or he will turn against us during the fighting. How better could he regain his master’s favor than by taking the heads of our own men? 5Isn’t this the David they sang about in their dances:

“ ‘Saul has slain his thousands,

and David his tens of thousands’?”

6So Achish called David and said to him, “As surely as the Lord lives, you have been reliable, and I would be pleased to have you serve with me in the army. From the day you came to me until today, I have found no fault in you, but the rulers don’t approve of you. 7Now turn back and go in peace; do nothing to displease the Philistine rulers.”

8“But what have I done?” asked David. “What have you found against your servant from the day I came to you until now? Why can’t I go and fight against the enemies of my lord the king?”

9Achish answered, “I know that you have been as pleasing in my eyes as an angel of God; nevertheless, the Philistine commanders have said, ‘He must not go up with us into battle.’ 10Now get up early, along with your master’s servants who have come with you, and leave in the morning as soon as it is light.”

11So David and his men got up early in the morning to go back to the land of the Philistines, and the Philistines went up to Jezreel.