1 Nyakati 9 – NEN & CCB

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 9:1-44

19:1 1Nya 5:25Waisraeli wote waliorodheshwa katika koo zilizoandikwa kwenye kitabu cha wafalme wa Israeli.

Watu Katika Yerusalemu

Watu wa Yuda walichukuliwa mateka kwenda Babeli kwa sababu ya kukosa uaminifu kwa Mungu. 29:2 Yos 9:27; Ezr 2:70; 8:20; Neh 7:5; Law 26:33; 2Nya 33:11; 36:5Basi watu wa kwanza kurudi kukaa kwenye milki zao katika miji yao walikuwa baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi na watumishi wa Hekalu.9:2 Yaani Wanethini.

39:3 Neh 11:1Wale waliotoka Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase ambao waliishi Yerusalemu walikuwa:

Jamaa Za Yuda

49:4 Mwa 38:29; 46:12; Hes 26:20Uthai mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imri, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.

5Wazao wa Washiloni waliorudi ni:

Asaya mzaliwa wa kwanza na wanawe.

6Kwa wana wa Zera:

Yeueli.

Watu wa Yuda jumla yao walikuwa watu 690.

Jamaa Za Benyamini

7Kwa Benyamini walikuwa:

Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;

8Ibneya mwana wa Yerohamu, Ela mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya.

9Watu kutoka Benyamini kama walivyoorodheshwa katika koo zao jumla yao ni 956. Watu hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao.

Jamaa Za Makuhani

109:10 Neh 11:10; 12:19Wa jamaa za makuhani walikuwa:

Yedaya, Yehoyaribu na Yakini;

11Azaria mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu aliyekuwa afisa kiongozi wa nyumba ya Mungu.

129:12 Neh 10:3; Yer 38:1Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yahzera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri.

13Makuhani waliokuwa viongozi wa jamaa zao walikuwa 1,760. Walikuwa watu wenye uwezo, waliowajibika kuhudumu katika nyumba ya Mungu.

Jamaa Za Walawi

149:14 1Nya 6:19; Neh 11:15-19Jamaa za Walawi walikuwa:

Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari. 159:15 2Nya 20:14; Neh 11:22Bakbakari, Hereshi, Galali na Matania mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu. 169:16 Neh 12:28; 1Nya 2:54; Neh 7:26Obadia mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. Berekia mwana wa Asa, mwana wa Elikana, ambao waliishi katika vijiji vya Wanetofathi.

Jamaa Za Mabawabu

179:17 Ezr 2:42; Neh 7:4; 1Nya 23:5; 26:1; Za 84:10Mabawabu katika Hekalu la Bwana waliorudi walikuwa:

Shalumu, Akubu, Talmoni, Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mlinzi wao mkuu. 189:18 Eze 43:1; 46:1; 2Fal 11:19; Eze 44:23Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi. 199:19 Yer 35:4; Hes 26:9-11Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani ya Bwana. 209:20 Hes 25:7-13; Kut 6:25; Hes 3:32; 31:6; Yos 22:30-31; Za 106:30Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, naye Bwana alikuwa pamoja naye:

219:21 1Nya 26:2, 14Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania.

229:22 1Nya 26:1; 2Nya 31:15, 18; 1Sam 9:9Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli. 23Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba ya Bwana, nyumba iliyoitwa Hema. 249:24 1Nya 26:13-19Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini. 259:25 2Fal 11:5; 2Nya 23:8Ndugu zao katika vijiji vyao walikuwa wakija mara kwa mara na kuwasaidia katika kazi zao kwa vipindi mbalimbali vya siku saba. 269:26 1Nya 26:22Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu. 279:27 Hes 3:38; 1Nya 23:30-32; 1Sam 22:22Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi.

28Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu; walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa. 299:29 Hes 3:23; 1Nya 23:29Wengine walipangiwa kutunza mapambo na vifaa vingine vya patakatifu, pamoja na unga, divai, mafuta, uvumba na vikolezo. 309:30 Kut 30:25; 37:29; Yer 6:20; Eze 27:19-22; Mk 14:3Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo. 319:31 Law 24:5-8; 2Nya 13:11; Law 6:21Mlawi aliyeitwa Matithia, mwana mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, wa ukoo wa Kora, alikabidhiwa wajibu kwa ajili ya kuoka mikate ya sadaka. 329:32 Kut 40:23; Ebr 9:2, 24; Yn 6:32, 33Baadhi ya ndugu zao wa ukoo wa Kohathi walikuwa viongozi wa kuandaa mikate ya Wonyesho kwa ajili ya kila Sabato, mikate iliyokuwa inawekwa mezani.

339:33 1Nya 25:1-31; 2Nya 5:12; Za 134:1; 1Nya 6:31; 13:8; 15:16Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yoyote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo usiku na mchana.

34Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa za Walawi, wakuu kama walivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.

Ukoo Wa Sauli

(1 Nyakati 8:29-38)

359:35 1Nya 8:29Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni. Mke wake aliitwa Maaka, 36mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu, 37Gedori, Ahio, Zekaria na Miklothi. 38Miklothi akamzaa Shimeamu. Wao pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.

399:39 1Nya 8:33; 1Sam 9:1; 13:22; 2Sam 2:8Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli. Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.9:39 Anajulikana pia kwa jina la Ish-Boshethi, maana yake Mtu wa Aibu (2Sam 2:8).

409:40 2Sam 4:4Yonathani akamzaa Merib-Baali,9:40 Pia anajulikana kwa jina la Mefiboshethi.

naye Merib-Baali akamzaa Mika.

419:41 2Sam 9:12; 1Nya 8:35Wana wa Mika walikuwa:

Pithoni, Meleki, Tarea, na Ahazi.

42Ahazi akamzaa Yara, Yara akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa. 43Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.

44Aseli alikuwa na wana sita, na haya ndiyo majina yao:

Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa ndio waliokuwa wana wa Aseli.

Chinese Contemporary Bible (Simplified)

历代志上 9:1-44

1所有以色列人都按照谱系记在以色列的列王史上。

归回的被掳之民

犹大人因为犯罪而被掳到了巴比伦2首先从巴比伦回到自己城邑的地业居住的有祭司、利未人、殿役和其他以色列人。 3一些犹大人、便雅悯人、以法莲人和玛拿西人住在耶路撒冷4其中有犹大的儿子法勒斯的后代乌太乌太亚米忽的儿子,亚米忽暗利的儿子,暗利音利的儿子,音利巴尼的儿子。 5示罗的子孙中包括长子亚帅雅及其众子, 6谢拉的后代耶乌利及其宗族共六百九十人。 7便雅悯人有哈西努的曾孙、何达威雅的孙子、米书兰的儿子撒路8耶罗罕的儿子伊比尼雅米基立的孙子、乌西的儿子以拉伊比尼雅的曾孙、流珥的孙子、示法提雅的儿子米书兰9以及他们的亲族,按家谱的记载共有九百五十六人。以上这些人都是各家的族长。

10回来的祭司有耶大雅耶何雅立雅斤11还有管理上帝殿的亚萨利雅亚萨利雅希勒迦的儿子,希勒迦米书兰的儿子,米书兰撒督的儿子,撒督米拉约的儿子,米拉约亚希突的儿子。 12回来的祭司还有玛基雅的曾孙、巴施户珥的孙子、耶罗罕的儿子亚大雅,以及亚第业的儿子玛赛亚第业雅希细拉的儿子,雅希细拉米书兰的儿子,米书兰米实利密的儿子,米实利密音麦的儿子。 13回来的祭司共一千七百六十人,全是族长,善于办理上帝殿的事务。

14回来的利未人有米拉利的后代哈沙比雅的曾孙、押利甘的孙子、哈述的儿子示玛雅15拔巴甲黑勒施迦拉亚萨的曾孙、细基利的孙子、米迦的儿子玛探雅16耶杜顿的曾孙、迦拉的孙子、示玛雅的儿子俄巴底以利加拿的孙子、亚撒的儿子比利迦。他们都住在尼陀法人的村庄里。

17负责守门的是沙龙亚谷达们亚希幔和他们的亲族,沙龙是他们的首领, 18在朝东的王门任职;他们曾是利未营中的守门人。 19可拉的曾孙、以比雅撒的孙子、可利的儿子沙龙和其他可拉族人负责看守会幕的门,他们的祖先曾负责看守耶和华会幕的入口。 20以利亚撒的儿子非尼哈曾做他们的首领,耶和华也与他同在。 21米施利米雅的儿子撒迦利雅是在会幕守门的。 22被选来守门的共有二百一十二人,都按各自所住的村庄载入家谱。大卫撒母耳先见委派他们担此重任。 23他们及其子孙负责看守耶和华的殿门,也就是会幕的门。 24东西南北四面都有守卫。 25他们村庄的同族弟兄每隔七天就来换班。 26四个殿门守卫长都是利未人,负责看守上帝殿的房间和库房。 27他们住在殿周围负责看殿,每天早晨开门。

28有些利未人负责管理敬拜时用的器皿,每次取出或送回,他们都要统计清楚。 29还有一些人负责管理圣所的其他器具,以及细面粉、酒、油、乳香和香料。 30有些祭司负责配制香料。 31利未玛他提雅可拉沙龙的长子,他负责烤祭饼。 32哥辖宗族中还有些人负责预备每个安息日需用的供饼。 33利未各宗族的族长负责歌乐,他们住在圣殿的房间里,昼夜专职于这项工作,不用做别的事。 34以上都是利未各宗族的族长,他们住在耶路撒冷

扫罗王的族谱

35耶利建立了基遍城,定居在那里,他妻子名叫玛迦36他的长子是亚伯顿,其他儿子还有苏珥基士巴力尼珥拿答37基多亚希约撒迦利雅米基罗38米基罗示米暗的父亲。这些人也住在耶路撒冷,与他们的亲族为邻。 39尼珥基士基士扫罗扫罗约拿单麦基舒亚亚比拿达伊施·巴力40约拿单米力·巴力米力·巴力米迦41米迦毗敦米勒他利亚亚哈斯42亚哈斯雅拉雅拉亚拉篾亚斯玛威心利心利摩撒43摩撒比尼亚比尼亚利法雅利法雅以利亚萨以利亚萨亚悉44亚悉有六个儿子,他们是亚斯利干波基路以实玛利示亚利雅俄巴底雅哈难。这些都是亚悉的儿子。