1 Nyakati 5 – NEN & NIV

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

1 Nyakati 5:1-26

Wana Wa Reubeni

15:1 Mwa 29:32; 35:22; 49:4; 48:16; 49:26; 48:5; 1Nya 26:10Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yosefu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa. 25:2 Mwa 49:10; 49:12; Za 60:7; Mt 2:6; Mwa 25:31; Hes 2:3; 7:12; Za 108:8; 78:68-71; Yer 23:5-6; Mik 5:2Na ingawa Yuda alikuwa na nguvu zaidi ya ndugu zake wote, na mtawala alitoka kwake, haki za mzaliwa wa kwanza zilikuwa za Yosefu.) 35:3 Kut 6:19; Hes 26:5-11; 26:5; Mwa 46:9Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli walikuwa:

Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.

4Wazao wa Yoeli walikuwa:

Shemaya mwanawe, Gogu mwanawe;

Shimei mwanawe, 5Mika mwanawe,

Reaya mwanawe, Baali mwanawe,

65:6 2Fal 16:10; 2Nya 28:20; 2Fal 15:29na Beera mwanawe, ambaye Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alimchukua kwenda uhamishoni. Beera alikuwa kiongozi wa Wareubeni.

75:7 Mit 17; Yos 13:17Jamaa zao kulingana na koo zao, walioorodheshwa kwa kufuata koo zao kama ifuatavyo:

Yeieli aliyekuwa mkuu wao, Zekaria, 85:8 Hes 32:34; Amu 11:26; Yos 13:17Bela mwana wa Azazi, mwana wa Shema, mwana wa Yoeli. Hao waliishi katika eneo kuanzia Aroeri mpaka Nebo na Baal-Meoni. 95:9 Hes 32:26; Yos 22:9; Wim 4:1; Mik 7:14Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi.

105:10 Mwa 25:12Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi.

Wana Wa Gadi

115:11 Mwa 30:11; Yos 13:24-28; Kum 3:10; Yos 13:11Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka.

12Yoeli ndiye alikuwa mkuu wao, Shafamu wa pili, na wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani.

13Ndugu zao kulingana na koo zao walikuwa saba:

Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Zia na Eberi.

14Hawa walikuwa ndio wana wa Abihaili mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yeshishai, mwana wa Yahdo, mwana wa Buzi.

15Ahi mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa ndiye kiongozi wa jamaa yao.

165:16 Mit 18:21; 1Nya 27:31; Isa 35:2; 65:10Wagadi waliishi Gileadi, huko Bashani pamoja na vijiji vilivyoizunguka, pia katika nchi yote ya malisho ya Sharoni kote walikoenea.

175:17 2Fal 15:32; 14:23Yote haya yaliwekwa katika kumbukumbu za ukoo wao wakati wa utawala wa Yothamu, mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.

185:18 Hes 1:3Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa na watu mashujaa 44,760 waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya vita: watu wenye nguvu, hodari wa kutumia ngao na upanga, mashujaa wa kutumia upinde, waliokuwa tayari kwa ajili ya kazi hiyo. 195:19 Mwa 28:15; 1Nya 1:31; Mwa 25:15Walipigana vita dhidi ya Wahagari, Yeturi, Nafishi na Nodabu. 205:20 Za 46:5; 54:4; 20:7-9; 2Nya 6:34; Isa 26:3; Dan 6:23; Za 9:10; Yer 17:7-8Walisaidiwa katika kupigana nao, Mungu akawatia Wahagari pamoja na wote walioungana nao mikononi mwao, kwa sababu walimlilia Mungu wakati wa vita. Alijibu maombi yao, kwa sababu walimtegemea. 21Walitwaa mifugo ya Wahagari: ngamia 50,000, kondoo 250,000, punda 2,000. Pia wakateka watu 100,000, 225:22 Kum 20:4; 2Nya 32:8; 1Nya 5:10; 2Fal 15:29na wengine wengi waliuawa kwa sababu vita vilikuwa ni vya Mungu. Nao waliendelea kuikalia nchi hiyo mpaka wakati wa uhamisho.

Nusu Ya Kabila La Manase

235:23 Kum 3:8, 9; Wim 4:8Idadi ya nusu ya kabila la Manase walikuwa wengi sana, Wakakaa kuanzia Bashani hadi Baal-Hermoni, yaani mpaka Seniri na mlima Hermoni.

24Hawa ndio waliokuwa viongozi wa jamaa za kabila hilo: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia na Yahdieli. Walikuwa askari shujaa watu maarufu, viongozi wa jamaa zao. 255:25 2Fal 17:7; 2Nya 12:2; Kut 34; 15; Law 18:3; Yer 5:7; Kum 32:15Lakini hawakuwa waaminifu kwa Mungu wa baba zao, nao wakafanya ukahaba kwa miungu ya mataifa, ambayo Mungu alikuwa ameyaangamiza mbele yao. 265:26 Isa 37:7; 2Fal 15:19; 15:29; 17:6; 18:11Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

New International Version

1 Chronicles 5:1-26

Reuben

1The sons of Reuben the firstborn of Israel (he was the firstborn, but when he defiled his father’s marriage bed, his rights as firstborn were given to the sons of Joseph son of Israel; so he could not be listed in the genealogical record in accordance with his birthright, 2and though Judah was the strongest of his brothers and a ruler came from him, the rights of the firstborn belonged to Joseph)— 3the sons of Reuben the firstborn of Israel:

Hanok, Pallu, Hezron and Karmi.

4The descendants of Joel:

Shemaiah his son, Gog his son,

Shimei his son, 5Micah his son,

Reaiah his son, Baal his son,

6and Beerah his son, whom Tiglath-Pileser5:6 Hebrew Tilgath-Pilneser, a variant of Tiglath-Pileser; also in verse 26 king of Assyria took into exile. Beerah was a leader of the Reubenites.

7Their relatives by clans, listed according to their genealogical records:

Jeiel the chief, Zechariah, 8and Bela son of Azaz, the son of Shema, the son of Joel. They settled in the area from Aroer to Nebo and Baal Meon. 9To the east they occupied the land up to the edge of the desert that extends to the Euphrates River, because their livestock had increased in Gilead.

10During Saul’s reign they waged war against the Hagrites, who were defeated at their hands; they occupied the dwellings of the Hagrites throughout the entire region east of Gilead.

Gad

11The Gadites lived next to them in Bashan, as far as Salekah:

12Joel was the chief, Shapham the second, then Janai and Shaphat, in Bashan.

13Their relatives, by families, were:

Michael, Meshullam, Sheba, Jorai, Jakan, Zia and Eber—seven in all.

14These were the sons of Abihail son of Huri, the son of Jaroah, the son of Gilead, the son of Michael, the son of Jeshishai, the son of Jahdo, the son of Buz.

15Ahi son of Abdiel, the son of Guni, was head of their family.

16The Gadites lived in Gilead, in Bashan and its outlying villages, and on all the pasturelands of Sharon as far as they extended.

17All these were entered in the genealogical records during the reigns of Jotham king of Judah and Jeroboam king of Israel.

18The Reubenites, the Gadites and the half-tribe of Manasseh had 44,760 men ready for military service—able-bodied men who could handle shield and sword, who could use a bow, and who were trained for battle. 19They waged war against the Hagrites, Jetur, Naphish and Nodab. 20They were helped in fighting them, and God delivered the Hagrites and all their allies into their hands, because they cried out to him during the battle. He answered their prayers, because they trusted in him. 21They seized the livestock of the Hagrites—fifty thousand camels, two hundred fifty thousand sheep and two thousand donkeys. They also took one hundred thousand people captive, 22and many others fell slain, because the battle was God’s. And they occupied the land until the exile.

The Half-Tribe of Manasseh

23The people of the half-tribe of Manasseh were numerous; they settled in the land from Bashan to Baal Hermon, that is, to Senir (Mount Hermon).

24These were the heads of their families: Epher, Ishi, Eliel, Azriel, Jeremiah, Hodaviah and Jahdiel. They were brave warriors, famous men, and heads of their families. 25But they were unfaithful to the God of their ancestors and prostituted themselves to the gods of the peoples of the land, whom God had destroyed before them. 26So the God of Israel stirred up the spirit of Pul king of Assyria (that is, Tiglath-Pileser king of Assyria), who took the Reubenites, the Gadites and the half-tribe of Manasseh into exile. He took them to Halah, Habor, Hara and the river of Gozan, where they are to this day.