Isaiah 30 – KJV & NEN

King James Version

Isaiah 30:1-33

1Woe to the rebellious children, saith the LORD, that take counsel, but not of me; and that cover with a covering, but not of my spirit, that they may add sin to sin: 2That walk to go down into Egypt, and have not asked at my mouth; to strengthen themselves in the strength of Pharaoh, and to trust in the shadow of Egypt! 3Therefore shall the strength of Pharaoh be your shame, and the trust in the shadow of Egypt your confusion. 4For his princes were at Zoan, and his ambassadors came to Hanes. 5They were all ashamed of a people that could not profit them, nor be an help nor profit, but a shame, and also a reproach. 6The burden of the beasts of the south: into the land of trouble and anguish, from whence come the young and old lion, the viper and fiery flying serpent, they will carry their riches upon the shoulders of young asses, and their treasures upon the bunches of camels, to a people that shall not profit them. 7For the Egyptians shall help in vain, and to no purpose: therefore have I cried concerning this, Their strength is to sit still.30.7 concerning…: or, to her

8¶ Now go, write it before them in a table, and note it in a book, that it may be for the time to come for ever and ever:30.8 the…: Heb. the latter day 9That this is a rebellious people, lying children, children that will not hear the law of the LORD: 10Which say to the seers, See not; and to the prophets, Prophesy not unto us right things, speak unto us smooth things, prophesy deceits: 11Get you out of the way, turn aside out of the path, cause the Holy One of Israel to cease from before us. 12Wherefore thus saith the Holy One of Israel, Because ye despise this word, and trust in oppression and perverseness, and stay thereon:30.12 oppression: or, fraud 13Therefore this iniquity shall be to you as a breach ready to fall, swelling out in a high wall, whose breaking cometh suddenly at an instant. 14And he shall break it as the breaking of the potters’ vessel that is broken in pieces; he shall not spare: so that there shall not be found in the bursting of it a sherd to take fire from the hearth, or to take water withal out of the pit.30.14 the potters’…: Heb. the bottle of potters 15For thus saith the Lord GOD, the Holy One of Israel; In returning and rest shall ye be saved; in quietness and in confidence shall be your strength: and ye would not. 16But ye said, No; for we will flee upon horses; therefore shall ye flee: and, We will ride upon the swift; therefore shall they that pursue you be swift. 17One thousand shall flee at the rebuke of one; at the rebuke of five shall ye flee: till ye be left as a beacon upon the top of a mountain, and as an ensign on an hill.30.17 a beacon: or, a tree bereft of branches, or, boughs: or, a mast

18¶ And therefore will the LORD wait, that he may be gracious unto you, and therefore will he be exalted, that he may have mercy upon you: for the LORD is a God of judgment: blessed are all they that wait for him. 19For the people shall dwell in Zion at Jerusalem: thou shalt weep no more: he will be very gracious unto thee at the voice of thy cry; when he shall hear it, he will answer thee. 20And though the Lord give you the bread of adversity, and the water of affliction, yet shall not thy teachers be removed into a corner any more, but thine eyes shall see thy teachers:30.20 affliction: or, oppression 21And thine ears shall hear a word behind thee, saying, This is the way, walk ye in it, when ye turn to the right hand, and when ye turn to the left. 22Ye shall defile also the covering of thy graven images of silver, and the ornament of thy molten images of gold: thou shalt cast them away as a menstruous cloth; thou shalt say unto it, Get thee hence.30.22 thy graven…: Heb. the graven images of thy silver30.22 cast: Heb. scatter 23Then shall he give the rain of thy seed, that thou shalt sow the ground withal; and bread of the increase of the earth, and it shall be fat and plenteous: in that day shall thy cattle feed in large pastures. 24The oxen likewise and the young asses that ear the ground shall eat clean provender, which hath been winnowed with the shovel and with the fan.30.24 clean: or, savoury: Heb. leavened 25And there shall be upon every high mountain, and upon every high hill, rivers and streams of waters in the day of the great slaughter, when the towers fall.30.25 high hill: Heb. lifted up, etc 26Moreover the light of the moon shall be as the light of the sun, and the light of the sun shall be sevenfold, as the light of seven days, in the day that the LORD bindeth up the breach of his people, and healeth the stroke of their wound.

27¶ Behold, the name of the LORD cometh from far, burning with his anger, and the burden thereof is heavy: his lips are full of indignation, and his tongue as a devouring fire:30.27 burden…: or, grievousness of flame30.27 heavy: Heb. heaviness 28And his breath, as an overflowing stream, shall reach to the midst of the neck, to sift the nations with the sieve of vanity: and there shall be a bridle in the jaws of the people, causing them to err. 29Ye shall have a song, as in the night when a holy solemnity is kept; and gladness of heart, as when one goeth with a pipe to come into the mountain of the LORD, to the mighty One of Israel.30.29 mighty…: Heb. Rock 30And the LORD shall cause his glorious voice to be heard, and shall shew the lighting down of his arm, with the indignation of his anger, and with the flame of a devouring fire, with scattering, and tempest, and hailstones.30.30 his glorious…: Heb. the glory of his voice 31For through the voice of the LORD shall the Assyrian be beaten down, which smote with a rod. 32And in every place where the grounded staff shall pass, which the LORD shall lay upon him, it shall be with tabrets and harps: and in battles of shaking will he fight with it.30.32 in every…: Heb. every passing of the rod founded30.32 lay…: Heb. cause to rest upon30.32 with it: or, against them 33For Tophet is ordained of old; yea, for the king it is prepared; he hath made it deep and large: the pile thereof is fire and much wood; the breath of the LORD, like a stream of brimstone, doth kindle it.30.33 of old: Heb. from yesterday

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Isaya 30:1-33

Ole Wa Taifa Kaidi

130:1 Isa 29:15; 8:12; Kum 29:19; 21:18; 2Fal 17:4Bwana asema,

“Ole kwa watoto wakaidi,

kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu,

wakifanya makubaliano, lakini si kwa Roho wangu,

wakilundika dhambi juu ya dhambi,

230:2 Mwa 25:22; Hes 27:21; 2Fal 25:26; Isa 36:6; Yer 2:18, 36; 42:14; Eze 17:15; 29:16wale washukao kwenda Misri

bila kutaka shauri langu,

wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao,

watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio.

330:3 Yer 37:5-7; Isa 20:4-5; Amu 9:8-15; Za 44:13Lakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu,

kivuli cha Misri kitawaletea fedheha.

430:4 Hes 13:22; Isa 19:11Ingawa wana maafisa katika Soani

na wajumbe wamewasili katika Hanesi,

530:5 Isa 20:5; 36:6; 2Fal 18:21; Za 108:12; Yer 37:3-5; Eze 17:15kila mmoja ataaibishwa

kwa sababu ya taifa lisilowafaa kitu,

ambalo haliwaletei msaada wala faida,

bali aibu tu na fedheha.”

630:6 Kut 1:3; Yer 11:4; Kum 8:15; Hos 8:9; Kut 5:10; Isa 13:1; 5:30; 5:29; Mwa 42:26Neno kuhusu wanyama wa Negebu:

Katika nchi ya taabu na shida,

ya simba za dume na jike,

ya nyoka mwenye sumu kali na nyoka warukao,

wajumbe huchukua utajiri wao juu ya migongo ya punda,

hazina zao juu ya nundu za ngamia,

kwa lile taifa lisilokuwa na faida,

730:7 Yer 2:36; Ay 9:13; 2Fal 18:2kuvipeleka Misri,

ambaye msaada wake haufai kabisa.

Kwa hiyo nimemwita “Rahabu Asiyefanya Chochote.”

830:8 Kut 17:14; Hab 2:2; Kum 27:8; Yer 25:13; Yos 24:26-27; Isa 8:1; Yer 30:2Nenda sasa, liandike neno hili juu ya kibao kwa ajili yao,

liandike kwenye kitabu,

ili liweze kuwa shahidi milele

kwa ajili ya siku zijazo.

930:9 Isa 28:15; Kum 32:20; Isa 59:3-4; Za 78:8; Eze 2:6Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu,

watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya Bwana.

1030:10 Amo 7:13; Yer 11:21; 32:3; 1Sam 9:9; 1Fal 22:8; Yer 4:10; Eze 13:7; Rum 16:18; 2Tim 4:4Wanawaambia waonaji,

“Msione maono tena!”

Nako kwa manabii wanasema,

“Msiendelee kutupatia maono

ambayo ni ya kweli!

Tuambieni mambo ya kupendeza,

tabirini mambo ya uongo.

1130:11 Mdo 13:8; Ay 21:14; Isa 35:8-9; Mit 3:6; Isa 29:19; 48:17Acheni njia hii,

ondokeni katika mapito haya,

nanyi acheni kutukabili pamoja

na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!”

1230:12 Isa 5:19; 5:24; Za 10:7; 12:5; Isa 5:7, 24Kwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Kwa sababu mmekataa ujumbe huu,

mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu,

1330:13 Neh 2:17; Za 80:12; 1Fal 20:30; Isa 17:14; Za 62:3dhambi hii itakuwa kwenu

kama ukuta mrefu,

wenye ufa na wenye kubetuka,

ambao unaanguka ghafula,

mara moja.

1430:14 Za 2:9; 2Pet 2:4-5Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo

ukipasuka pasipo huruma

ambapo katika vipande vyake

hakuna kipande kitakachopatikana

kwa kuukulia makaa kutoka jikoni

au kuchotea maji kisimani.”

1530:15 Isa 32:17; 2Nya 20:12; Mt 23:37Hili ndilo Bwana Mwenyezi, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, asemalo:

“Katika kutubu na kupumzika ndio wokovu wenu,

katika kutulia na kutumaini ndizo nguvu zenu,

lakini hamkutaka.

1630:16 Yer 46:6; Kum 17:16; 1Fal 10:28-29Mlisema, ‘Hapana, tutakimbia kwa farasi.’

Kwa hiyo mtakimbia!

Mlisema, ‘Tutakimbia kwa farasi waendao kasi.’

Kwa hiyo wanaowafukuza watakwenda kasi!

1730:17 Kum 28:25; 2Fal 7:7; Law 26:8; Yos 23:10Watu 1,000 watakimbia

kwa ajili ya kitisho cha mtu mmoja,

kwa vitishio vya watu watano

wote mtakimbia,

hadi mtakapoachwa kama mlingoti wa bendera

juu ya kilele cha mlima,

kama bendera juu ya kilima.”

1830:18 Mwa 43:31; 2Pet 3:9, 15; Za 27:14; Mao 3:25; Isa 5:16; 42:14; 48:9; Yon 3:10Hata hivyo Bwana anatamani kutupatia neema,

anainuka ili kuwaonyesha huruma.

Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa haki.

Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

1930:19 Isa 61:3; Ay 22:27; Mt 7:7-11; Isa 25:8; Ay 24:12; Zek 13:9; Za 86:7; Isa 41:17Enyi watu wa Sayuni, mnaoishi Yerusalemu, hamtalia tena. Tazameni jinsi atakavyokuwa na huruma mtakapolia kwa kumwomba msaada! Mara asikiapo, atawajibu. 2030:20 1Fal 22:27; Za 74:9; Isa 28:9; Amo 8:11Ingawa Bwana huwapa chakula cha shida na maji ya taabu, walimu wenu hawatafichwa tena, kwa macho yenu wenyewe mtawaona. 2130:21 Kum 5:32; Mit 4:27; Isa 29:24; Ay 33:11Mkigeuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.” 2230:22 Kut 32:4; Isa 2:20; Law 15:19-23; Eze 7:19-20Kisha mtanajisi sanamu zenu zilizofunikwa kwa fedha, na vinyago vyenu vilivyofunikwa kwa dhahabu. Mtazitupilia mbali kama vitambaa vya wakati wa hedhi na kuziambia, “Haya, tokeni hapa!”

2330:23 1Tim 4:8; Za 65:13; Kum 28:12; Isa 65:21-22; Yer 31:14; Ay 36:31Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana, tena tele. Katika siku ile, ngʼombe wenu watalisha katika shamba pana la majani. 2430:24 Mt 3:12; Lk 3:17; Isa 32:14; Ay 6:5Maksai na punda walimao watakula majani makavu na vyakula vilivyotengenezwa, vinavyotandazwa kwa uma na sepeto. 2530:25 Isa 13:5; Kut 17:6; Isa 32:2; Yoe 3:18Katika siku ile ya mauaji makuu, wakati minara itakapoanguka, vijito vya maji vitatiririka juu ya kila mlima mrefu na kila kilima kilichoinuka sana. 2630:26 Zek 14:7-8; Ufu 21:23; 2Nya 7:14; Hos 14:4; Isa 60:19-20; Yer 3:22; 17:14Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utangʼaa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakati Bwana atakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuwaponya vidonda alivyowatia.

2730:27 1Fal 18:24; Isa 26:20; 60:14; Eze 22:31; Ay 41:21Tazama, Jina la Bwana linakuja kutoka mbali,

likiwa na hasira kali inayowaka

pamoja na wingu zito la moshi,

midomo yake imejaa ghadhabu

na ulimi wake ni moto ulao.

2830:28 2The 2:8; Amo 9:9; 2Fal 19:28; Isa 37:29; 11:4; 28:15; Za 50:3Pumzi yake ni kama mkondo wa maji yaendayo kasi,

yakipanda hadi shingoni.

Hutikisa mataifa katika chekecheke ya uharibifu,

huweka lijamu katika mataya ya mataifa

ambayo huwaongoza upotevuni.

2930:29 Mt 26:30; Za 42:4; Isa 25:9; 1Sam 10:5; Mwa 49:24Nanyi mtaimba kama usiku ule mnaadhimisha

sikukuu takatifu.

Mioyo yenu itashangilia

kama vile watu wanapokwea na filimbi

kwenye mlima wa Bwana,

kwa Mwamba wa Israeli.

3030:30 Kut 19:18; Za 29:3; Kut 20:18; Isa 47:14; 9:12Bwana atawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu,

naye atawafanya wauone mkono wake ukishuka

pamoja na hasira yake kali na moto ulao,

kukiwa na tufani ya mvua,

ngurumo za radi na mvua ya mawe.

3130:31 Isa 10:5, 12; 11:4Sauti ya Bwana itaivunjavunja Ashuru,

kwa fimbo yake ya utawala atawapiga.

3230:32 Isa 11:15; 10:26; Eze 32:10; Kut 15:20Kila pigo Bwana atakaloliweka juu yao

kwa fimbo yake ya kuadhibu,

litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi,

anapopigana nao katika vita

kwa mapigo ya mkono wake.

3330:33 2Fal 23:10; Yer 7:31; Mwa 19:24; Ufu 9:17; 2Sam 22:16Tofethi imeandaliwa toka zamani,

imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme.

Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu

na kwa upana mkubwa,

likiwa na moto na kuni tele;

pumzi ya Bwana,

kama kijito cha kiberiti,

huuwasha moto.