Galatians 5 – KJV & NEN

King James Version

Galatians 5:1-26

1Stand fast therefore in the liberty wherewith Christ hath made us free, and be not entangled again with the yoke of bondage.

2Behold, I Paul say unto you, that if ye be circumcised, Christ shall profit you nothing. 3For I testify again to every man that is circumcised, that he is a debtor to do the whole law. 4Christ is become of no effect unto you, whosoever of you are justified by the law; ye are fallen from grace. 5For we through the Spirit wait for the hope of righteousness by faith. 6For in Jesus Christ neither circumcision availeth any thing, nor uncircumcision; but faith which worketh by love. 7Ye did run well; who did hinder you that ye should not obey the truth? 8This persuasion cometh not of him that calleth you. 9A little leaven leaveneth the whole lump. 10I have confidence in you through the Lord, that ye will be none otherwise minded: but he that troubleth you shall bear his judgment, whosoever he be. 11And I, brethren, if I yet preach circumcision, why do I yet suffer persecution? then is the offence of the cross ceased. 12I would they were even cut off which trouble you. 13For, brethren, ye have been called unto liberty; only use not liberty for an occasion to the flesh, but by love serve one another. 14For all the law is fulfilled in one word, even in this; Thou shalt love thy neighbour as thyself. 15But if ye bite and devour one another, take heed that ye be not consumed one of another. 16This I say then, Walk in the Spirit, and ye shall not fulfil the lust of the flesh. 17For the flesh lusteth against the Spirit, and the Spirit against the flesh: and these are contrary the one to the other: so that ye cannot do the things that ye would. 18But if ye be led of the Spirit, ye are not under the law. 19Now the works of the flesh are manifest, which are these; Adultery, fornication, uncleanness, lasciviousness, 20Idolatry, witchcraft, hatred, variance, emulations, wrath, strife, seditions, heresies, 21Envyings, murders, drunkenness, revellings, and such like: of the which I tell you before, as I have also told you in time past, that they which do such things shall not inherit the kingdom of God. 22But the fruit of the Spirit is love, joy, peace, longsuffering, gentleness, goodness, faith, 23Meekness, temperance: against such there is no law. 24And they that are Christ’s have crucified the flesh with the affections and lusts. 25If we live in the Spirit, let us also walk in the Spirit. 26Let us not be desirous of vain glory, provoking one another, envying one another.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Wagalatia 5:1-26

Uhuru Ndani Ya Kristo

15:1 Gal 5:13; 2:4; Yn 8:32; Rum 7:4; 1Kor 16:13; Mt 23:4Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa.

25:2 Gal 5:3; Mdo 15:1Sikilizeni! Mimi, Paulo, nawaambieni kwamba kama mkikubali kutahiriwa, basi Kristo hatawafaidia chochote. 35:3 Rum 2:25; Gal 3:10; Yak 2:10Namshuhudia tena kila mtu anayekubali kutahiriwa kwamba inampasa kushika sheria yote. 45:4 Rum 3:28; Ebr 12:15; 2Pet 3:17Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu. 55:5 Rum 8:23, 24; 2Tim 4:8; 1Kor 7:19Kwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki. 65:6 Rum 16:3; 1Kor 7:19; 1The 1:3; Yak 2:22Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.

75:7 1Kor 9:24; Gal 3:1Mlikuwa mkipiga mbio vizuri. Ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 85:8 Rum 8:28; Gal 1:6Ushawishi wa namna hiyo haukutokana na yule anayewaita. 95:9 1Kor 5:6; 15:33“Chachu kidogo huchachua donge zima.” 105:10 2Kor 2:3; Flp 3:15; Gal 1:7Nina hakika katika Bwana kwamba hamtakuwa na msimamo mwingine. Mtu anayewachanganya anastahili adhabu, hata awe nani. 115:11 Gal 4:29; 6:12; Lk 2:34Lakini ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa, kwa nini bado ninateswa? Katika hiyo hali basi, kwazo la msalaba limeondolewa. 125:12 Gal 5:10; Yos 7:25; 1Kor 5:13; Gal 1:8, 9; Mdo 15:1, 2, 24Laiti hao wanaowavuruga wangejihasi wao wenyewe!

135:13 Gal 5:1, 24; 1Kor 8:9; 1Pet 2:16; 1Kor 9:19; 2Kor 4:5Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo. 145:14 Law 19:18; Mt 5:43; Gal 6:2Kwa maana sheria yote hukamilika katika amri moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 15Kama mkiumana na kutafunana, angalieni, msije mkaangamizana.

Maisha Ya Kiroho

165:16 Gal 5:18, 25; Rum 8:2, 4-6, 9; 14; 2Kor 5:17; Gal 5:14Kwa hiyo nasema, enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 175:17 Rum 8:5-8; 7:15-23Kwa maana mwili hutamani yale yaliyo kinyume na Roho, naye Roho hutamani yale yaliyo kinyume na mwili. Roho na mwili hupingana na kwa sababu hiyo hamwezi kufanya mnayotaka. 185:18 Rum 2:12; 6:14; Gal 5:16; 1Tim 1:9Lakini kama mkiongozwa na Roho, hamko chini ya sheria.

195:19 1Kor 6:18; 3:3; Efe 5:3; Kol 3:5; Yak 3:14, 15Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, ufisadi, 20kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 215:21 Rum 13:13; Mt 15:19; 25:34; 1Kor 6:9husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.

225:22 Mt 7:16-20Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria. 24Wote walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili na shauku zake pamoja na tamaa zake. 25Kwa kuwa tunaishi kwa Roho, basi, tuenende kwa Roho. 265:26 Flp 2:3; Mt 18:15; Yak 2:19Tusijisifu bure, tukichokozana na kuoneana wivu.