Jeremia 45 – HOF & NEN

Hoffnung für Alle

Jeremia 45:1-5

Eine Botschaft für Baruch

1Im 4. Regierungsjahr des judäischen Königs Jojakim, des Sohnes von Josia, sagte der Prophet Jeremia zu Baruch, dem Sohn von Nerija, der gerade Jeremias Botschaften auf eine Schriftrolle geschrieben hatte: 2»So spricht der Herr, der Gott Israels: 3Baruch, du klagst: ›Ich unglücklicher Mensch! Leide ich nicht schon genug? Und nun lädt mir der Herr noch neuen Kummer auf! Vom vielen Seufzen bin ich völlig erschöpft und finde keine Ruhe!‹ 4Ich, der Herr, sage dir: Was ich in diesem Land aufgebaut habe, zerstöre ich wieder, und was ich eingepflanzt habe, reiße ich wieder aus! 5Und da hoffst du, du könntest in Glück und Frieden leben? Erwarte nicht zu viel! Denn ich, der Herr, lasse Unheil über alle Menschen hereinbrechen. Doch eines verspreche ich dir: Wo immer du hingehst, wirst du mit dem Leben davonkommen!«

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yeremia 45:1-5

Ujumbe Kwa Baruku

145:1 Yer 32:12; 36:18, 32; Isa 50:4; Yer 51:59; Kut 17:14; Za 40:7; 2Nya 36:5Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruku mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruku kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule: 2“Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruku: 345:3 Ay 23:2; Za 69:3; Isa 24:16; 1Kor 9:16; Mk 14:34; Rum 9:2; Ay 6:10; Ebr 4:3; Mt 11:24Ulisema, ‘Ole wangu! Bwana ameongeza huzuni juu ya maumivu yangu, nimechoka kwa kulia kwa uchungu wala sipati pumziko.’ ”

445:4 Isa 5:5; Yer 11:17; Kum 30:9; Yer 42:10; 18:7-10; Kum 28:63Bwana akasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Nitakibomoa kile nilichokijenga, na kungʼoa kile nilichokipanda katika nchi yote. 545:5 Mt 6:25-27, 33; Yer 21:9; 32:8; 11:11; 40:2; 2:35; Za 68:20Je, utajitafutia mambo makubwa kwa ajili yako mwenyewe? Usiyatafute hayo. Kwa kuwa nitaleta maangamizi juu ya watu wote, asema Bwana, lakini popote utakapokwenda, nitayaokoa maisha yako.’ ”