הבשורה על-פי יוחנן 13 – HHH & NEN

Habrit Hakhadasha/Haderekh

הבשורה על-פי יוחנן 13:1-38

1לפני חג הפסח, ישוע ידע שהגיעה שעתו לעזוב את העולם ולשוב אל אביו. ישוע תמיד אהב מאוד את בחיריו בעולם הזה, ועתה עמד להוכיח להם כי אין גבול לאהבתו. 2לעט סעודת הערב השטן כבר המריץ את יהודה איש־קריות להסגיר את ישוע. 3ישוע ידע כי אביו נתן בידו את הכול, וכי הוא בא מאלוהים וישוב אל אלוהים. 4לכן הוא קם מהשולחן בארוחת הערב, הסיר את בגדיו וקשר למותניו מגבת. 5אחר כך לקח קערה, מילא אותה מים, החל לרחוץ את רגלי תלמידיו וניגב אותן במגבת הקשורה למתניו. 6כאשר הגיע תורו של שמעון פטרוס הוא קרא: ”אדוני, איך ייתכן שאתה תרחץ את רגלי?“

7”כעת אינך מבין מדוע אני עושה זאת, אולם יבוא יום שתבין זאת“, השיב ישוע.

8”לא,“ מחה פטרוס, ”לעולם לא תרחץ את רגלי!“

”אם לא ארחץ אותך, לא יהיה לך חלק בי“, השיב ישוע.

9”אם כך,“ קרא פטרוס, ”רחץ לא רק את רגלי, אלא גם את ידי וראשי.“

10”מי שרחץ כבר את כל גופו צריך לרחוץ את רגליו בלבד כדי להיות נקי וטהור. עתה אתם נקיים, אבל לא כולכם.“ 11ישוע אמר דברים אלה מפני שידע מי עמד להסגירו.

12כשסיים ישוע לרחוץ את רגליהם לבש את בגדיו, התיישב ושאל: ”האם אתם מבינים מה עשיתי לכם? 13אתם קוראים לי ’מורה‘ ו’אדון‘, ואכן נוהגים אתם בצדק, כי זוהי האמת. 14לכן אם אני, האדון והמורה, רחצתי את רגליכם, גם אתם צריכים לרחוץ איש את רגלי רעהו. 15נתתי לכם דוגמה כדי שתנהגו כמוני. 16האמינו לי, העבד אינו חשוב מאדוניו, והשליח אינו חשוב משולחו. 17כאשר תבינו את משמעות הדברים האלה ותנהגו לפיהם, יהיה לכם טוב ותתברכו.

18”איני מתכוון לכולכם, כי אני יודע במי בחרתי. הכתובים מנבאים שאחד מאוכלי לחמי יבגוד בי. 19אני מספר לכם זאת עכשיו כדי שתאמינו לי כשכל זה יתרחש.

20”אמן אומר אני לכם: כל המקבל את מי שאני שולח מקבל למעשה אותי, וכל המקבל אותי מקבל למעשה את שולחי.“

21בסיימו דברים אלה נאנח ישוע אנחה עמוקה ואמר: ”אכן, זוהי האמת – אחד מכם יבגוד בי.“ 22התלמידים הביטו איש ברעהו בתמיהה ובמבוכה, משום שלא ידעו למי התכוון. 23תלמידו החביב של ישוע היה סמוך לחיקו, 24ולכן רמז לו שמעון פטרוס לשאל אותו למי כוונתו.

25התלמיד הטה את ראשו וקרבו לראשו של ישוע. ”אדוני, למי כוונתך?“ שאל בלחישה.

26”למי שאגיש את פרוסתי הטבולה ברוטב“, השיב ישוע.

הוא טבל את הפרוסה והגישה ליהודה בן שמעון איש־קריות. 27כאשר סיים יהודה לאכול את הלחם נכנס השטן ללבו. ”סיים את העניין במהירות“, אמר לו ישוע.

28איש מהנוכחים לא ידע למה ישוע התכוון. 29היו שחשבו כי ישוע ביקש ממנו לקנות את צרכי החג או לתת כסף לעניים, מפני שיהודה היה הגזבר. 30יהודה עזב מיד את המקום ויצא. היה אז לילה.

31לאחר שעזב יהודה את החדר אמר ישוע: ”הגיעה שעתי; עתה יתפאר בן־האדם, ואלוהים יפואר בו. 32אם אלוהים יפואר בי, הוא בעצמו יפאר אותי ואף יעשה זאת במהרה. 33ילדי היקרים, עוד מעט עלי ללכת מאתכם. לאחר שאלך לא תוכלו לבוא אלי גם אם תחפשו אותי, כפי שכבר אמרתי למנהיגי היהודים.

34”אני מפקיד בידיכם מצווה חדשה: אהבו איש את רעהו כשם שאני אוהב אתכם. 35אהבתכם החזקה איש לרעהו תוכיח לעולם שאתם תלמידי.“

36”לאן אתה הולך, אדון?“ שאל שמעון פטרוס.

”אינך יכול לבוא איתי עכשיו, אולם עוד זמן מה תצטרף אלי גם אתה“, השיב ישוע.

37”אבל מדוע איני יכול ללכת איתך כעת?“ פטרוס לא הבין. ”אני מוכן אפילו למות למענך!“

38”למות למעני?“ שאל ישוע. ”אני אומר לך שעד מחר בבוקר לפני קריאת התרנגול, תכחיש שלוש פעמים אפילו את העובדה שאתה מכיר אותי!“

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 13:1-38

Yesu Awanawisha Wanafunzi Wake Miguu

113:1 Yn 11:55; 12:33; 16:28Ilikuwa mara tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua ya kuwa wakati wake wa kuondoka ulimwenguni ili kurudi kwa Baba umewadia. Alikuwa amewapenda watu wake waliokuwa ulimwenguni, naam, aliwapenda hadi kipimo cha mwisho.

213:2 Lk 22:3Wakati alipokuwa akila chakula cha jioni na wanafunzi wake, ibilisi alikuwa amekwisha kutia ndani ya moyo wa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu. 313:3 Mt 28:18; Yn 8:42; 17:8Yesu akijua ya kwamba Baba ameweka vitu vyote chini ya mamlaka yake na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, 413:4 Mt 11:29; 20:29; Lk 12:37hivyo aliondoka chakulani, akavua vazi lake la nje, akajifunga kitambaa kiunoni. 513:5 Lk 7:44Kisha akamimina maji kwenye sinia na kuanza kuwanawisha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa kile kitambaa alichokuwa amejifunga kiunoni.

613:6 1Pet 5:5Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, je, wewe utaninawisha mimi miguu?”

713:7 Yn 13:12Yesu akamjibu, “Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa.”

813:8 Yn 3:5; 1Kor 6:11; Efe 5:26; Tit 3:5; Ebr 10:22Petro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.”

Yesu akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.”

9Ndipo Simoni Petro akajibu, “Usininawishe miguu peke yake, Bwana, bali pamoja na mikono na kichwa pia!”

1013:10 Yn 15:3Yesu akamjibu, “Mtu aliyekwisha kuoga anahitaji kunawa miguu tu, kwani mwili wake wote ni safi. Ninyi ni safi, ingawa si kila mmoja wenu.” 1113:11 Mt 10:4Kwa kuwa yeye alijua ni nani ambaye angemsaliti, ndiyo sababu akasema si kila mmoja aliyekuwa safi.

12Alipomaliza kuwanawisha miguu yao, alivaa tena mavazi yake, akarudi alikokuwa ameketi, akawauliza, “Je, mmeelewa nililowafanyia? 1313:13 Mt 26:18; Yn 11:28; Mdo 10:36Ninyi mnaniita mimi ‘Mwalimu’ na ‘Bwana,’ hii ni sawa, maana ndivyo nilivyo. 1413:14 1Pet 5:5Kwa hiyo, ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi. 1513:15 Mt 11:29; 1Tim 4:12Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi. 1613:16 Mt 10:24; Lk 6:40Amin, amin nawaambia, mtumishi si mkuu kuliko bwana wake, wala aliyetumwa si mkuu kuliko yule aliyemtuma. 1713:17 Lk 11:28; 1:25Sasa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri yenu ninyi kama mkiyatenda.

1813:18 Za 41:9; Mt 26:23“Sisemi hivi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni ili Andiko lipate kutimia, kwamba, ‘Yeye aliyekula chakula changu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.’

1913:19 Yn 14:29; 16:4; 4:26; 8:24“Ninawaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa Mimi ndiye. 2013:20 Mt 10:40; Lk 10:16Amin, amin nawaambia, yeyote anayempokea yule niliyemtuma anipokea mimi, naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenituma mimi.”

Yesu Anatabiri Kusalitiwa Kwake

(Mathayo 26:20-25; Marko 14:17-21; Luka 22:21-23)

2113:21 Yn 12:27; Mt 26:21Baada ya kusema haya, Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.”

22Wanafunzi wake wakatazamana bila kujua kuwa alikuwa anamsema nani. 2313:23 Yn 20:2; 21:7, 20Mmoja wa wanafunzi wake ambaye Yesu alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Yesu. 24Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi, akamwambia, “Muulize anamaanisha nani.”

2513:25 Mt 26:22; Yn 21:20Yule mwanafunzi akamwegemea Yesu, akamuuliza, “Bwana, tuambie, ni nani?”

2613:26 Mt 10:4Yesu akajibu, “Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya kwenye bakuli.” Hivyo baada ya kukichovya kile kipande cha mkate, akampa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni. 2713:27 Lk 22:3Mara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, Shetani akamwingia.

Yesu akamwambia Yuda, “Lile unalotaka kulitenda litende haraka.” 28Hakuna hata mmoja wa wale waliokuwa wameketi naye mezani aliyeelewa kwa nini Yesu alimwambia hivyo. 2913:29 Yn 12:6Kwa kuwa Yuda alikuwa mtunza fedha, wengine walifikiri Yesu alikuwa amemwambia akanunue vitu vilivyohitajika kwa ajili ya Sikukuu, au kuwapa maskini chochote. 3013:30 Lk 22:53Mara tu baada ya kupokea ule mkate, Yuda akatoka nje. Wakati huo ulikuwa ni usiku.

Yesu Atabiri Petro Kumkana

(Mathayo 26:31-35; Marko 14:27-31; Luka 22:31-34)

3113:31 Yn 7:39; 12:23; 17:4; 1Pet 4:11Baada ya Yuda kutoka nje, Yesu akasema, “Sasa Mwana wa Adamu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. 3213:32 Yn 17:1Ikiwa Mungu ametukuzwa ndani ya Mwana, Mungu atamtukuza Mwana ndani yake mwenyewe naye atamtukuza mara.

3313:33 Yn 7:33, 34“Watoto wangu, mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama vile nilivyowaambia Wayahudi, vivyo hivyo sasa nawaambia na ninyi. Niendako, ninyi hamwezi kuja.

3413:34 1Yn 2:7-11; 3:11; Law 19:18; 1The 4:9; Efe 5:2; 1Yn 4:10, 11; 2:14“Amri mpya nawapa: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. 3513:35 Yn 3:14; 4:20Kama mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.”

3613:36 Yn 16:5; 14:2; 21:18, 19; 2Pet 1:4Simoni Petro akamuuliza, “Bwana, unakwenda wapi?”

Yesu akamjibu, “Ninakokwenda huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.”

3713:37 Mt 26:33, 34, 35; Mk 14:29, 30, 31; Lk 22:33, 34Petro akamuuliza tena, “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Mimi niko tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako.”

3813:38 Yn 18:27Yesu akamjibu, “Je, ni kweli uko tayari kuutoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin nakuambia, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”