Matej 8 – CRO & NEN

Knijga O Kristu

Matej 8:1-34

Isus iscjeljuje gubavca

(Mk 1:40-44; Lk 5:12-14)

1Veliko je mnoštvo pohrlilo za Isusom dok je silazio s gore. 2Odjednom mu pristupi neki gubavac, pokloni mu se do zemlje i zamoli ga: “Gospodine, ako hoćeš, možeš me iscijeliti!”

3Isus ispruži ruku i dotakne čovjeka. “Hoću! Budi čist!” reče mu. I guba odmah nestane. 4Isus mu reče: “Nikome o tomu ne govori, već idi ravno svećeniku te sa sobom ponesi žrtveni dar prema Mojsijevu zakonu kao javno svjedočanstvo svojeg ozdravljenja.”

Vjera rimskoga stotnika

(Lk 7:1-10; 13:28-29)

5Kad Isus dođe u Kafarnaum, pristupi mu neki stotnik 6i reče: “Gospodine, sluga mi kod kuće leži uzet i u teškim mukama!”

7“Doći ću ga iscijeliti”, odgovori mu Isus.

8Stotnik odgovori: “Gospodine, nisam dostojan da uđeš u moju kuću. Samo reci da moj sluga ozdravi i on će ozdraviti! 9Jer i ja moram slušati svoje nadređene. A podređenom vojniku kažem: ‘Idi!’ i on ode, te drugome: ‘Dođi!’ i dođe; a sluzi kažem: ‘Učini to!’ i on učini.”

10Kad je to čuo, Isus se zadivi. Okrene se mnoštvu, pa reče: “Zaista vam kažem, takve vjere nisam vidio ni u koga u cijelom Izraelu. 11Kažem vam da će mnogi s istoka i zapada sjesti u nebeskom kraljevstvu s Abrahamom, Izakom i Jakovom, 12a mnogi Izraelci8:12 U grčkome: sinovi kraljevstva. biti izbačeni u mrklu tamu gdje će biti plač i škrgut zuba.”

13Zatim reče rimskome stotniku: “Idi! Neka ti bude kako si vjerovao!” I sluga mu istog trena ozdravi.

Mnoga ozdravljenja

(Mk 1:29-34; Lk 4:38-41)

14Kad je Isus došao u Petrovu kuću, Petrova punica ležala je bolesna, u vrućici. 15Isus joj dotakne ruku i vrućica nestane. Žena ustane i počne ga posluživati.

16Te mu večeri dovedu mnoge opsjednute. Na njegovu riječ svi su zli duhovi izlazili, a svi bolesnici ozdravljali. 17Tako se ispunilo što je napisao prorok Izaija:

“On slabosti naše uze

i ponese naše bolesti.”8:17 Izaija 53:4.

Cijena učeništva

(Lk 9:57-60)

18Kad je Isus vidio koliko se mnoštvo okuplja, zapovjedi da otplove na drugu stranu jezera.

19Tada mu priđe neki pismoznanac i reče: “Učitelju, slijedit ću te kamo god ti pošao.”

20Isus mu odgovori: “Lisice imaju jame i ptice imaju gnijezda, a Sin Čovječji nema gdje ni glavu nasloniti.”

21Drugi mu od učenika reče: “Gospodine, dopusti mi da najprije pokopam svojeg oca.” 22Ali Isus mu odgovori: “Pođi za mnom i pusti da mrtvi pokapaju svoje mrtvace!”

Isus smiruje oluju

(Mk 4:36-41; Lk 8:22-25)

23Isus se ukrca u lađu, a za njim uđu i njegovi učenici. 24Odjednom nastane tako silna oluja da su se valovi prelijevali preko lađice. Isus je spavao. 25Učenici dođu k njemu i probude ga: “Gospodine, spasi nas! Izginut ćemo!” 26Isus im reče: “Malovjerni! Što se toliko strašite?” Ustane zatim i zaprijeti vjetru i valovima, a oluja se stiša i nastane velika tišina.

27Ljudi su se u čudu pitali: “Pa tko je on da mu se i vjetrovi i more pokoravaju?”

Isus iscjeljuje dvojicu opsjednutih

(Mk 5:1-17; Lk 8:26-37)

28Kad su stigli na drugu stranu jezera, u gadarski kraj8:28 U nekim rukopisima geraski ili gergezenski kraj. Vidjeti: Marko 5:1; Luka 8:26., susretnu ga dvojica opsjednutih koji su dolazili iz grobnica i bili tako goropadni da zaradi njih nitko nije mogao proći tim putem. 29Odjednom poviču: “Što hoćeš od nas, Sine Božji? Došao si nas ovdje mučiti prije vremena?”

30Nedaleko je paslo veliko krdo svinja. 31Zli duhovi zamole Isusa: “Ako nas istjeraš, pošalji nas u ono krdo svinja.”

32“Idite!” reče im Isus. Oni iziđu iz opsjednutih i uđu u svinje. Nato cijelo krdo jurne niz strminu u more i podavi se u vodi. 33Svinjari pobjegnu u grad te razglase što se dogodilo s opsjednutima. 34Tada sav grad iziđe u susret Isusu. Kad su ga ugledali, zamole da ode iz njihova kraja.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 8:1-34

Yesu Amtakasa Mwenye Ukoma

(Marko 1:40-45; Luka 5:12-16)

1Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata. 28:2 Law 13:45; Lk 17:12; Mt 18:26; 20:22Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.”

3Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Mara yule mtu akatakasika ukoma wake. 48:4 Mk 8:30; Lk 4:41; Law 14:2-32Kisha Yesu akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Mose, ili kuwa ushuhuda kwao.”

Yesu Amponya Mtumishi Wa Jemadari

(Luka 7:1-10)

58:5 Lk 7:1; Yn 4:27Yesu alipoingia Kapernaumu, jemadari mmoja alimjia, kumwomba msaada, 68:6 Mt 4:24akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani na amepooza, tena ana maumivu makali ya kutisha.”

7Yesu akamwambia, “Nitakuja na kumponya.”

88:8 Za 107:20Lakini yule jemadari akamwambia, “Bwana, mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona. 9Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya.”

108:10 Mt 15:28Yesu aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, “Amin, nawaambia, hata katika Israeli sijapata kuona yeyote mwenye imani kubwa namna hii. 118:11 Za 107:3; Mal 1:11; Lk 13:29Ninawaambia kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaki na Yakobo katika Ufalme wa Mbinguni. 128:12 Mt 13:38; 25:30; Lk 13:28Lakini warithi wa Ufalme watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwako kilio na kusaga meno.”

138:13 Mt 9:22-29Kisha Yesu akamwambia yule jemadari, “Nenda na iwe kwako sawasawa na imani yako.” Naye yule mtumishi akapona saa ile ile.

Yesu Aponya Wengi

(Marko 1:29-34; Luka 4:38-41)

148:14 1Kor 9:5Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa. 158:15 Mk 1:29-34Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia.

168:16 Mt 4:23-24Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote. 178:17 Isa 53:4; Mt 1:22Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:

“Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu

na alichukua magonjwa yetu.”

Gharama Ya Kumfuata Yesu

(Luka 9:57-62)

188:18 Mk 4:35; Lk 8:22Yesu alipoona makutano mengi wamemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake wavuke mpaka ngʼambo ya ziwa. 198:19 Lk 9:57, 58Kisha mwalimu mmoja wa sheria akamjia Yesu na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata kokote uendako.”

208:20 Dan 7:13; Mk 2:10Naye Yesu akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”

218:21 1Fal 19:20Mwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

228:22 Mt 4:19; Rum 6:13Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, uwaache wafu wawazike wafu wao.”

Yesu Atuliza Dhoruba

(Marko 4:35-41; Luka 8:22-25)

238:23 Za 4:8Naye alipoingia kwenye mashua, wanafunzi wake wakamfuata. 248:24 Mk 4:37; Lk 8:26Ghafula, kukainuka dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Yesu alikuwa amelala usingizi. 25Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunazama!”

268:26 Mt 6:30; Za 65:7; 89:9Naye Yesu akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?” Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nako kukawa shwari kabisa.

27Wale watu wakashangaa, wakisema, “Ni mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!”

Wawili Wenye Pepo Waponywa

(Marko 5:1-20; Luka 8:26-39)

288:28 Mt 4:24Walipofika ngʼambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu walitoka makaburini nao wakakutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile. 298:29 Lk 4:34; 2Pet 2:4Wakapiga kelele, “Una nini nasi, Mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati ulioamriwa?”

30Mbali kidogo kutoka pale walipokuwa, kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha. 31Wale pepo wachafu wakamsihi Yesu, “Ukitutoa humu, turuhusu twende kwenye lile kundi la nguruwe.”

32Akawaambia, “Nendeni!” Hivyo wakatoka na kuwaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremka gengeni kwa kasi, likaingia katika ziwa na kufa ndani ya maji. 33Wale watu waliokuwa wakiwachunga hao nguruwe wakakimbia wakaingia mjini, wakaeleza yote kuhusu yale yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu. 348:34 Lk 5:8; Mdo 16:39Kisha watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Yesu. Nao walipomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.