馬太福音 10 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

馬太福音 10:1-42

差遣使徒

1耶穌叫了十二位門徒來,將權柄賜給他們,使他們能夠趕出污鬼、醫治各樣的疾病。 2以下是這十二位使徒的名字:

首先是西門,又名彼得,還有彼得的兄弟安得烈西庇太的兒子雅各雅各的兄弟約翰3腓力巴多羅買多馬、稅吏馬太亞勒腓的兒子雅各達太4激進黨人10·4 激進黨人」指當時激進的猶太民族主義者,常以行動反抗統治他們的羅馬政府。西門和出賣耶穌的加略猶大

5耶穌差遣這十二個人出去,囑咐他們:「外族人的地方不要去,撒瑪利亞人的城鎮也不要進, 6要到以色列人當中尋找迷失的羊。

7「你們要邊走邊傳,『天國臨近了!』 8要醫好病人,叫死人復活,使痲瘋病人痊癒,趕走邪靈。你們白白地得來,也應當白白地給人。 9出門時錢袋裡不要帶金、銀、銅幣, 10不要帶行李、備用的衣服、鞋子或手杖,因為做工的理應得到供應。 11你們無論到哪座城、哪個村,要在那裡尋找願意接待你們的人,然後住在他家,一直住到離開。 12你們進他家的時候,要為他們祝福。 13如果那家配得福氣,你們的祝福必臨到他們;如果那家不配蒙福,祝福仍歸給你們。 14如果有人不接待你們,不聽你們傳的信息,你們離開那家或那城時,就把腳上的塵土跺掉作為對他們的警告。 15我實在告訴你們,在審判之日,他們所受的痛苦比所多瑪蛾摩拉所受的還大!

將臨的迫害

16「聽著,我差你們出去,就好像使羊走進狼群一般。所以,你們要像蛇一樣機靈,像鴿子一樣馴良。

17「你們要小心謹慎,因為人們要把你們送上法庭,也要在會堂裡鞭打你們。 18你們要因我的緣故被帶到官長和君王面前,在他們和外族人面前為我做見證。 19當你們被押送公堂時,不用顧慮如何應對,或說什麼話,那時必會賜給你們當說的話。 20因為那時候說話的不是你們自己,乃是你們父的靈藉著你們說話。

21「那時,人必把自己的弟兄置於死地,父親必把兒子置於死地,兒女必反叛父母,置他們於死地。 22你們將為我的名而被眾人憎恨,但堅忍到底的必定得救。 23如果你們在一個地方遭迫害,就避到另一個地方。我實在告訴你們,沒等你們走遍以色列的城鎮,人子就來了。

24「學生不能高過老師,奴僕也不能大過主人。 25學生頂多和老師一樣,奴僕頂多和主人一樣。連一家之主都被罵成是別西卜10·25 別西卜」是鬼王的名字。,更何況祂的家人呢?

26「不要害怕那些迫害你們的人。因為掩蓋的事終會暴露出來,隱藏的秘密終會被人知道。 27你們要把我私下告訴你們的當眾講出來,你們要在屋頂上把聽到的悄悄話宣告出來。 28那些只能殺害身體,不能毀滅靈魂的人,不用怕他們。但要畏懼那位有權將身體和靈魂一同毀滅在地獄裡的上帝。 29兩隻麻雀不是只賣一個銅錢嗎?然而沒有天父的許可,一隻也不會掉在地上。 30就連你們的頭髮都被數過了。 31所以不要害怕,你們比許多麻雀更貴重!

32「凡公開承認我的,我在天父面前也必承認他; 33凡公開不承認我的,我在天父面前也必不承認他。

跟從主的代價

34「不要以為我來了會讓天下太平,我並非帶來和平,乃是帶來刀劍。 35因為我來是要叫兒子與父親作對,女兒與母親作對,媳婦與婆婆作對, 36家人之間反目成仇。

37「愛父母過於愛我的人不配作我的門徒;愛兒女過於愛我的人不配作我的門徒; 38不肯背起他的十字架跟從我的人不配作我的門徒。 39試圖保全自己生命的反而會失去生命,但為我捨棄生命的反而會得到生命。

得賞賜

40「人接待你們就是接待我,接待我就是接待差我來的那位。 41因為某人是先知而接待他的,必得到和先知一樣的賞賜;因為某人是義人而接待他的,必得到和義人一樣的賞賜。 42人若接待我門徒中最卑微的人,並因為他是我的門徒而給他一杯涼水喝,我實在告訴你們,那人必得到賞賜。」

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Mathayo 10:1-42

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Marko 3:13-19; 6:7-13; Luka 6:12-16; 9:1-6)

110:1 Mk 3:13-15; Lk 9:1-5Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.

210:2 Lk 6:13-16Haya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili: wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye; 3Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; 410:4 Mk 14:10; Mdo 1:16Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu.

510:5 1Fal 16:24; Lk 10:33Hawa kumi na wawili, Yesu aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria. 610:6 Yer 50:6; Mt 15:24Lakini afadhali mshike njia kuwaendea kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. 710:7 Mt 3:2; Lk 19:9Wakati mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’ 810:8 Mdo 20:33Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure. 910:9 Lk 22:35Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba kwenye vifuko vyenu. 1010:10 1Tim 5:18; Hes 18:31Msichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtendakazi anastahili posho yake.

1110:11 Lk 10:8“Mji wowote au kijiji chochote mtakapoingia, tafuteni humo mtu anayestahili, nanyi kaeni kwake mpaka mtakapoondoka. 1210:12 1Sam 25:6; Lk 10:5-6Mkiingia kwenye nyumba, itakieni amani. 1310:13 Lk 10:5; Za 35:13Kama nyumba hiyo inastahili, amani yenu na iwe juu yake. La sivyo, amani yenu na iwarudie ninyi. 1410:14 Neh 5:13; Mk 6:11Kama mtu yeyote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo. 1510:15 Mwa 18:20; Yud 7; Mdo 17:30; Mt 11:22-24Amin, nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa miji ya Sodoma na Gomora kustahimili katika hukumu kuliko mji huo.

Mateso Yanayokuja

(Marko 13:9-13; Luka 21:12-17)

1610:16 Lk 10:3; Mdo 20:29; Rum 16:19; 1Kor 14:20“Tazama, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo mwe werevu kama nyoka na wapole kama hua.

1710:17 Mt 5:22; Mdo 22:19; 26:11“Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga kwenye masinagogi yao. 1810:18 Mdo 25:24-26Nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na kwa watu wa Mataifa. 1910:19 Kut 4:12; Lk 12:11-12Lakini watakapowapeleka humo, msisumbuke kufikiria mtakalosema, kwa maana mtapewa la kusema wakati huo. 2010:20 Mdo 4:8; Yn 14:26Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akinena kupitia kwenu.

2110:21 Mik 7:6; Mt 10:35-36“Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, naye baba atamsaliti mtoto wake. Watoto nao wataasi dhidi ya wazazi wao na kusababisha wauawe. 2210:22 Lk 21:19; Ufu 2:10Watu wote watawachukia kwa ajili ya Jina langu. Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. 2310:23 Mt 16:28; Lk 17:30Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Amin, amin nawaambia, hamtamaliza miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu kuja.

2410:24 Lk 6:40; Yn 15:20“Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake, wala mtumishi hamzidi bwana wake. 2510:25 Mk 3:22; Mt 12:24Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa mkuu wa nyumba ameitwa Beelzebuli,10:25 Beelzebuli kwa Kiyunani ni Beelzebubu, yaani mkuu wa pepo wachafu. je, si watawaita zaidi wale wa nyumbani mwake!

Anayestahili Kuogopwa

(Luka 12:2-9)

2610:26 Mk 4:22; Lk 8:17“Kwa hiyo msiwaogope hao, kwa maana hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna siri ambayo haitajulikana. 27Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe. Na lile mnalosikia likinongʼonwa masikioni mwenu, lihubirini juu ya nyumba. 2810:28 Isa 8:12-13; Ebr 10:31Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu.10:28 Jehanamu kwa Kiyunani ni Gehena, maana yake ni Kuzimu, yaani motoni. 29Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini pasipo Baba yenu kujua. 3010:30 1Fal 1:52; Lk 21:18Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. 3110:31 Mt 6:26; 12:12Hivyo msiogope; kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

3210:32 Rum 10:9“Kila mtu atakayenikiri mbele ya watu, mimi nami nitamkiri yeye mbele za Baba yangu aliye mbinguni. 3310:33 Mk 8:38; 2Tim 2:12Lakini yeyote atakayenikana mimi mbele ya watu, mimi nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni.”

Sikuleta Amani, Bali Upanga

(Luka 12:51-53; 14:26-27)

3410:34 Lk 12:51-53“Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga. 3510:35 Mik 7:6Kwa maana nimekuja kumfitini

“ ‘mtu na babaye,

binti na mamaye,

mkwe na mama mkwe wake;

3610:36 Mik 6:7nao adui za mtu watakuwa

ni wale watu wa nyumbani kwake.’

3710:37 Lk 14:26“Yeyote ampendaye baba yake au mama yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. Yeyote ampendaye mwanawe au binti yake kuliko anavyonipenda mimi, hastahili kuwa wangu. 3810:38 Mt 16:24-25; Lk 14:27Tena yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu. 3910:39 Lk 17:33; Yn 12:44Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.

Watakaopokea Thawabu

(Marko 9:41)

4010:40 Kut 16:8; Gal 4:14; Lk 10:16; Yn 12:44“Mtu yeyote atakayewapokea ninyi atakuwa amenipokea mimi, na yeyote atakayenipokea mimi atakuwa amempokea yeye aliyenituma. 4110:41 1Fal 17:10; 18:4; 2Fal 4:8Mtu yeyote anayempokea nabii kwa kuwa ni nabii atapokea thawabu ya nabii, naye mtu anayempokea mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki atapokea thawabu ya mwenye haki. 4210:42 Mt 25:40; Mdo 10:4; Mit 14:30; Mk 9:41Kama yeyote akimpa hata kikombe cha maji baridi mmoja wa hawa wadogo kwa kuwa ni mwanafunzi wangu, amin, nawaambia, hataikosa thawabu yake.”