約翰福音 21 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

約翰福音 21:1-25

海邊顯現

1後來,耶穌在提比哩亞海邊又向門徒顯現。當時的情形是這樣的: 2西門·彼得、綽號「雙胞胎」的多馬加利利迦拿拿但業西庇太的兩個兒子以及其他兩個門徒都在一起。

3西門·彼得對他們說:「我要去打魚了!」

眾人說:「我們也跟你去。」於是他們就出去,上了船,但那一夜什麼也沒打到。 4天將破曉的時候,耶穌站在岸上,但門徒都不知道是耶穌。

5耶穌對他們說:「孩子們,打到魚沒有?」

他們回答說:「沒有!」

6耶穌說:「在船的右邊下網就會打到魚。」於是他們照著祂的話把網撒下去,網到的魚多到連網都拉不動。

7耶穌所愛的那個門徒對彼得說:「是主!」那時西門·彼得赤著身子,一聽見是主,立刻束上外衣,跳進海裡。 8其他門徒離岸不遠,約有一百米,他們隨後用船把那一網魚拖到岸邊。 9他們上岸後,看見有一堆炭火,上面有魚和餅。

10耶穌說:「拿幾條剛打的魚來。」 11西門·彼得就上船把網拉上岸。網裡一共有一百五十三條大魚!雖然魚這麼多,網卻沒有破。

12耶穌又說:「你們來吃早餐吧!」沒有一個門徒敢問祂是誰,他們都知道祂是主。 13耶穌就過來把餅和魚分給他們。

14這是耶穌從死裡復活後第三次向門徒顯現。

耶穌和彼得

15吃過早餐,耶穌對西門·彼得說:「約翰的兒子西門,你比這些人更愛我嗎?21·15 你比這些人更愛我嗎」或譯「你愛我比愛這些更深嗎」。

彼得說:「主啊!是的,你知道我愛你。」

耶穌對他說:「你要餵養我的小羊。」

16耶穌第二次問:「約翰的兒子西門,你愛我嗎?」

彼得說:「主啊!是的,你知道我愛你。」

耶穌說:「你要牧養我的羊。」

17耶穌第三次問:「約翰的兒子西門,你愛我嗎?」

彼得因為耶穌一連三次這樣問他,就難過起來,於是對耶穌說:「主啊!你是無所不知的,你知道我愛你。」

耶穌說:「你要餵養我的羊。 18我實實在在地告訴你,你年輕力壯的時候,自己穿上衣服,想去哪裡就去哪裡。但到你年老的時候,你將伸出手來,別人要把你綁起來帶你到你不願意去的地方。」 19這話是暗示彼得將要怎樣死來使上帝得榮耀。之後,耶穌又對他說:「你跟從我吧!」

20彼得轉身看見耶穌所愛的那個門徒跟在後面,就是吃最後的晚餐時靠在耶穌身邊問「主啊!是誰要出賣你?」的那個門徒。 21彼得問耶穌:「主啊!他將來會怎樣呢?」

22耶穌說:「如果我要他活到我再來,與你有什麼關係?你只管跟從我吧!」

23於是在信徒中間就傳說那個門徒不會死。其實耶穌並沒有說他不會死,只是說:「如果我要他活到我再來,與你有什麼關係?」

24為這些事做見證、記錄這些事的就是那個門徒,我們都知道他的見證是真實的。 25耶穌還做了許多其他的事,如果都寫成書,我想整個世界也容納不下。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Yohana 21:1-25

Yesu Awatokea Wanafunzi Saba

121:1 Yn 21:14; 20:19, 26Baada ya haya Yesu akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia.21:1 Yaani Bahari ya Galilaya. Yeye alijionyesha kwao hivi: 221:2 Yn 11:16; 1:4; 2:1; Mt 4:21Simoni Petro, Tomaso aitwaye Didimasi, yaani Pacha, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. 321:3 Lk 5:5Simoni Petro akawaambia wenzake, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Tutakwenda pamoja nawe.” Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata chochote.

421:4 Lk 24:16; Yn 20:14Mara baada ya kupambazuka, Yesu akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Yesu.

521:5 Lk 24:41Yesu akawaambia, “Wanangu, je, mna samaki wowote?”

Wakamjibu, “La.”

621:6 Lk 5:4-7Akawaambia, “Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki.” Wakashusha nyavu na tazama wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua.

721:7 Yn 13:23Yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia haya, akajifunga nguo yake kwa kuwa alikuwa uchi, naye akajitosa baharini. 8Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliyojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa 20021:8 Dhiraa 200 ni kama mita 90. 921:9 Yn 18:18; 21:10, 13Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake na mikate.

10Yesu akawaambia, “Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi.”

11Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu pwani. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa 153. Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika. 1221:12 Mdo 10:41Yesu akawaambia, “Njooni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanafunzi aliyethubutu kumuuliza, “Wewe ni nani?” Kwa sababu walijua ya kuwa ni Bwana. 1321:13 Yn 21:9Yesu akaja, akachukua ule mkate, akawapa na vivyo hivyo akawagawia pia wale samaki. 1421:14 Yn 20:19, 26Hii ilikuwa mara ya tatu Yesu kuwatokea wanafunzi wake baada yake kufufuliwa kutoka kwa wafu.

Yesu Amuuliza Petro Kama Anampenda

1521:15 Lk 24:41Walipokwisha kula, Yesu akamuuliza Simoni Petro, “Je, Simoni mwana wa Yohana, unanipenda kweli kuliko hawa?”

Yeye akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.”

Yesu akamwambia, “Lisha wana-kondoo wangu.”

1621:16 2Sam 5:2; Mt 2:6Yesu akamwambia tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?”

Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.”

Yesu akamwambia, “Chunga kondoo zangu.”

1721:17 Yn 2:24, 25; 16:30Kwa mara ya tatu Yesu akamuuliza Petro, “Simoni mwana wa Yohana, unanipenda?”

Petro akahuzunika sana kwa kuwa Yesu alimuuliza mara ya tatu, “Unanipenda?” Akamjibu, “Bwana, wewe unajua yote, unajua ya kuwa ninakupenda.”

Yesu akamwambia, “Lisha kondoo wangu. 18Amin, amin nakuambia, ulipokuwa kijana ulivaa na kwenda unakotaka, lakini utakapokuwa mzee utanyoosha mikono yako na mtu mwingine atakuvika na kukupeleka usipotaka kwenda.” 1921:19 Yn 12:33; 18:32Yesu alisema haya ili kuashiria ni kifo cha aina gani Petro atakachomtukuza nacho Mungu. Kisha Yesu akamwambia Petro, “Nifuate!”

2021:20 Yn 16:22; 21:7; 13:23Petro akageuka, akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akiwafuata. (Huyu ndiye yule mwanafunzi aliyeegama kifuani mwa Yesu walipokula naye chakula cha mwisho na kuuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?”) 21Petro alipomwona huyo mwanafunzi, akamuuliza Yesu, “Bwana na huyu je?”

2221:22 Mt 16:27, 28; 25:31; 1Kor 4; 5; 11:26; Ufu 2:25; 3:11; 22:7, 20Yesu akamjibu, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini? Wewe inakupasa unifuate!” 2321:23 Mdo 1:16Kwa sababu ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea miongoni mwa ndugu kwamba huyu mwanafunzi hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini?”

2421:24 Yn 15:27; 19:35Huyu ndiye yule mwanafunzi anayeshuhudia mambo haya na ndiye ambaye ameandika habari hizi. Nasi tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.

2521:25 Yn 20:30Lakini kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu alifanya. Kama yote yangeliandikwa, nadhani hata ulimwengu wote usingekuwa na nafasi ya kutosha kuweka vitabu vyote ambavyo vingeandikwa. Amen.