歷代志下 17 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

歷代志下 17:1-19

猶大王約沙法

1亞撒的兒子約沙法繼位,他發憤圖強對抗以色列2他派兵駐守猶大所有的堅城,又把守備軍安置在猶大和他父親亞撒所征服的以法蓮各城邑。 3耶和華與約沙法同在,因為他效法他祖先大衛起初所行的,沒有尋求巴力4只尋求他父親的上帝,遵行祂的誡命,沒有效法以色列人的行為。 5因此,耶和華鞏固他的王位,所有的猶大人都向他進貢,他極有財富和尊榮。 6他專心遵行耶和華的道,剷除猶大境內的邱壇和亞舍拉神像。

7他在執政第三年委派官員便·亥伊勒俄巴底撒迦利雅拿坦業米該亞猶大各城教導民眾, 8與他們同去的還有利未示瑪雅尼探雅西巴第雅亞撒黑示米拉末約拿單亞多尼雅多比雅駝·巴多尼雅,還有祭司以利沙瑪約蘭9他們帶著耶和華的律法書,走遍猶大各城鎮教導民眾。 10猶大周圍的列國都懼怕耶和華,不敢與約沙法爭戰。 11一些非利士人向他進貢禮物和銀子,阿拉伯人也給他送來公綿羊和公山羊各七千七百隻。

12約沙法日漸強大,在猶大境內修建堡壘和儲貨城, 13猶大各城儲備大量物資。他又在耶路撒冷屯駐精兵, 14其人數按宗族記在下面。

猶大族有千夫長押拿,率領精兵三十萬; 15其次是千夫長約哈難,率領軍兵二十八萬; 16其次是自願事奉耶和華的細基利的兒子亞瑪斯雅,率領精兵二十萬。 17便雅憫族有勇士以利雅大,率領手持弓箭和盾牌的軍兵二十萬; 18其次是約薩拔,率領全副武裝的軍兵十八萬。 19以上都是服侍王的軍兵,不包括王派去駐守猶大各堅城的軍兵。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

2 Nyakati 17:1-19

Yehoshafati Mfalme Wa Yuda

1Yehoshafati mwanawe akawa mfalme baada yake na akajiimarisha dhidi ya Israeli. 217:2 2Nya 15:8; 11:11Akaweka jeshi katika miji yote ya Yuda yenye ngome na kuweka askari walinzi katika Yuda na katika miji ya Efraimu ile ambayo baba yake Asa alikuwa ameiteka.

317:3 Rum 8:31; 1Fal 22:43Bwana Mungu alikuwa na Yehoshafati kwa sababu katika miaka yake ya mwanzoni alienenda katika njia za Daudi baba yake. Hakutafuta Mabaali 417:4 1Fal 12:28; 2Nya 22:9bali alimtafuta Mungu wa baba yake na kuzifuata amri zake badala ya kufuata desturi za watu wa Israeli. 517:5 1Sam 10:27; 2Nya 18:1; 1Fal 10:25-27Kwa hiyo Bwana akauimarisha ufalme chini ya uongozi wake, nao Yuda wote wakamletea Yehoshafati zawadi, hivyo akawa na utajiri mwingi na heshima. 617:6 1Fal 8:61; 2Nya 14:3; 15:17Moyo wake ukawa hodari katika njia za Bwana na zaidi ya yote, akaondoa mahali pa juu pa kuabudia miungu na nguzo za Maashera katika Yuda.

717:7 Neh 8:7; Mal 2:7; 2Nya 15:3Katika mwaka wa tatu wa utawala wa akatuma maafisa wake ambao ni: Ben-Haili, Obadia, Zekaria, Nethaneli na Mikaya ili kufundisha katika miji ya Yuda. 817:8 Hos 4:6Pamoja nao walikuwepo Walawi fulani nao ni: Shemaya, Nethania, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, Tob-Adonia, pamoja nao walikuwepo makuhani Elishama na Yehoramu. 917:9 Kum 6:4-9; 28:61; Law 10:11; 2Nya 35:3; Neh 8:7; Mal 2:7Wakafundisha Yuda yote, wakiwa wamechukua Kitabu cha Sheria ya Bwana wakazunguka miji yote ya Yuda na kufundisha watu.

1017:10 Mwa 35:5; Kum 2:25; Kut 15:15; 2Nya 14:14Hofu ya Bwana ikawa juu ya falme zote za nchi zilizozunguka Yuda, hivyo hawakufanya vita na Yehoshafati. 1117:11 2Nya 9:14; 26:8; 21:16; 2Sam 8:2Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi na fedha kama ushuru, nao Waarabu wakamletea mifugo: kondoo dume 7,700 na mbuzi 7,700.

12Yehoshafati akaendelea kupata nguvu zaidi na zaidi, akajenga ngome na miji ya hazina katika Yuda 13na akawa na wingi mkubwa wa vitu katika miji ya Yuda. Pia aliweka askari wa vita wenye uzoefu huko Yerusalemu. 1417:14 2Sam 24:2Wakaandikishwa katika jamaa zao kama ifuatavyo:

Kutoka Yuda, majemadari wa vikosi vya elfu:

Jemadari Adna akiwa na askari wa vita 300,000;

15aliyefuata ni jemadari Yehohanani, akiwa na askari 280,000 walio tayari kwa vita;

1617:16 Amu 5:9; 1Nya 29:9-17; 2Kor 8:12; Za 110:3aliyefuata ni Amasia mwana wa Zikri, ambaye alijitolea kwa ajili ya kazi ya Bwana, akiwa na askari 200,000.

17Kutoka Benyamini:

Eliada, askari shujaa akiwa na watu 200,000 wenye silaha za nyuta na ngao;

18aliyefuata ni Yehozabadi, akiwa na askari 180,000 wenye silaha za vita.

1917:19 2Nya 25:5; 11:10Hawa ndio waliomtumikia mfalme, mbali na wale mfalme aliweka katika miji yenye ngome huko Yuda yote.