啟示錄 9 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

啟示錄 9:1-21

1第五位天使吹號的時候,我見有一顆星從天上墜落到地上,有無底坑的鑰匙賜給它。 2它打開無底坑時,濃煙從坑裡冒出來,好像大火爐的煙一樣,太陽和天空都變得昏暗了。 3有蝗蟲從煙裡飛出來,落到地上,有地上蠍子的能力賜給牠們。 4牠們得到命令,不得毀壞地上的青草、樹木和其他植物,只傷害額上沒有上帝印記的人, 5但不可殺死他們,只折磨他們五個月。那種折磨就像被蠍子蟄到一樣。 6那時候,人求死,卻求不到;想死,死卻躲避他們。

7那些蝗蟲好像預備出征的戰馬一樣,頭上好像戴了金冠,面孔好像人臉, 8毛髮好像女人的頭髮,牙齒好像獅子的牙, 9胸前有甲,如同鐵甲,鼓動翅膀時聲音如同千軍萬馬奔赴戰場。 10牠們像蠍子一樣尾巴上有毒鉤,可以折磨人五個月。 11牠們的王是無底坑的天使,希伯來文名叫亞巴頓希臘文名叫亞玻倫,意思是「毀滅者」。

12第一樣災禍過去了,另外兩樣接踵而來。

13第六位天使吹號的時候,我聽見有一個聲音從上帝面前的金祭壇的四個角發出來, 14對剛才吹號的第六位天使說:「將那捆綁在幼發拉底河的四個天使放出來!」 15那四個天使就被釋放了,他們為了此年、此月、此日、此刻已經預備好了,要殺掉人類的三分之一。 16我聽見他們共有二億兵馬。 17我在異象中看見了馬和騎士。騎士胸甲的顏色像火焰、紫瑪瑙和硫磺。馬的頭像獅子的頭,口中噴出火、煙和硫磺。 18馬口中噴出的這三樣災害殺死了世上三分之一的人口。 19這些馬的殺傷力不只在口,也在尾巴。牠們的尾巴像蛇,有頭能咬傷人。

20其餘沒有被這些災害所殺的人仍不肯悔改、停止手中的惡行,還是去拜魔鬼和那些用金、銀、銅、石、木所造,不能看、不能聽、不能行走的偶像。 21他們不肯爲自己所犯的兇殺、邪術、淫亂和偷盜悔改。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Ufunuo 9:1-21

Tarumbeta Ya Tano

19:1 Ufu 8:10; Lk 8:31Malaika wa tano akaipiga tarumbeta yake, nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka toka angani hadi ardhini. Nyota hiyo ilipewa ufunguo wa lile Shimo.9:1 Yaani Abyss kwa Kiyunani; maana yake ni Kuzimu, yaani makao ya pepo wachafu. 29:2 Mwa 19:28; Kut 19:18; Yoe 2:2-10Alipolifungua hilo Shimo, moshi ukapanda kutoka humo kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vikatiwa giza na ule moshi uliotoka katika hilo Shimo. 39:3 Kut 10:12-15Ndipo katika ule moshi wakatoka nzige wakaenda juu ya nchi, nao wakapewa nguvu kama zile za nge wa duniani. 49:4 Ufu 7:2-3; 6:6; 8:7; Eze 9:4; Ufu 7:3Wakaambiwa wasidhuru nyasi ya nchi, wala mmea wala mti wowote, bali wawadhuru tu wale watu ambao hawana muhuri wa Mungu kwenye vipaji vya nyuso zao. 59:5 Ufu 9:3, 10Wakaruhusiwa kuwatesa kwa muda wa miezi mitano, lakini wasiwaue. Uchungu wa kuuma kwao ulikuwa kama ule wa mtu aumwapo na nge. 69:6 Ay 7:15; Ufu 6:16Katika siku hizo watu watatafuta kifo lakini hawatakiona, watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia.

79:7 Yoe 2:4; Dan 7:8Wale nzige walikuwa na umbo kama la farasi waliotayarishwa kwa ajili ya vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji za dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu. 89:8 Yoe 1:6Walikuwa na nywele kama za wanawake, na meno yao yalikuwa kama ya simba. 99:9 Yoe 2:5Walikuwa na dirii kama za chuma, na sauti za mabawa yao zilikuwa kama ngurumo za farasi wengi na magari mengi yakikimbilia vitani. 109:10 Ufu 9:3, 5, 19Walikuwa na mikia yenye miiba ya kuumia kama nge. Nguvu yao ya kutesa watu kwa huo muda wa miezi mitano ilikuwa katika hiyo mikia yao. 119:11 Ufu 9:1, 2; Lk 8:31; 16:16; Ay 26:6; 28:22Walikuwa na mfalme wao, ambaye ni malaika wa lile Shimo, ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani ni Apolioni.9:11 Abadoni au Apolioni maana yake ni Mharabu, yaani Yule aharibuye.

129:12 Ufu 8:13Ole ya kwanza imepita, bado nyingine mbili zinakuja.

Tarumbeta Ya Sita

139:13 Kut 30:1-3; Ufu 8:3Malaika wa sita akaipiga tarumbeta yake, nami nikasikia sauti ikitoka katika zile pembe za madhabahu ya dhahabu iliyoko mbele za Mungu. 149:14 Ufu 16:12Ile sauti ikamwambia yule malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie wale malaika wanne waliofungwa kwenye ule mto mkubwa Frati.” 159:15 Ufu 20:7; 8:7; 9:12Basi wale malaika wanne, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya saa hiyo, na siku hiyo, na mwezi huo, na mwaka huo ili wawaue theluthi ya wanadamu wakafunguliwa. 169:16 Ufu 5:11; 7:4Idadi ya majeshi wapanda farasi ilikuwa 200,000,000. Nilisikia idadi yao.

179:17 Ufu 11:5Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika maono yangu: Wapanda farasi walivaa dirii vifuani zenye rangi nyekundu sana kama ya moto na yakuti samawi na kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vichwa vya simba, na moto, moshi na kiberiti vilitoka vinywani mwao. 189:18 Ufu 8:7; 9:15, 17Theluthi ya wanadamu wakauawa kwa mapigo hayo matatu, yaani, huo moto, moshi na kiberiti, vilivyotoka kwenye vinywa vya hao farasi. 199:19 Isa 9:15Nguvu za hao farasi zilikuwa katika vinywa vyao na kwenye mikia yao, kwa sababu mikia yao ilikuwa kama nyoka, yenye vichwa ambayo waliitumia kudhuru.

209:20 Mik 5:13; Mdo 7:41; 1Kor 10:20; Dan 5:23Wanadamu waliosalia, ambao hawakuuawa katika mapigo hayo, bado walikataa kutubia kazi za mikono yao na hawakuacha kuabudu mashetani na sanamu za dhahabu, za fedha, za shaba, za mawe na za miti, ambazo haziwezi kuona, kusikia wala kutembea. 219:21 Ufu 2:21; 18:23; 17:2-5Wala hawakutubu na kuacha matendo yao ya uuaji, uchawi, uasherati wala wizi wao.