但以理書 8 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible (Traditional)

但以理書 8:1-27

公綿羊和公山羊的異象

1在看見先前的異象之後,我但以理伯沙撒王執政第三年又看見一個異象。 2我在異象中看見自己在以攔省的書珊城,又看見自己站在烏萊河畔。 3我舉目觀看,見一隻長著長角的公綿羊站在河邊,其中一角比另一角長,較長的角是後長出來的。 4我看見這公綿羊向西方、北方和南方頂撞,沒有獸能抵擋牠,或逃脫牠的威力。牠隨心所欲,狂妄自大。

5我正沉思的時候,忽然從西面出現一隻公山羊,穿越大地,腳不沾地。牠雙眼之間有一個大角。 6這公山羊來到我之前看見的那隻站在河邊的雙角公綿羊那裡,憤怒地向牠頂去。 7我看見公山羊憤怒地頂向公綿羊,攻擊牠,折斷了牠的雙角。公綿羊無力抵擋,被撞倒在地,踐踏在腳下,無人能救牠脫離公山羊的威力。 8公山羊極其狂妄自大。但正值鼎盛之時,牠的大角突然折斷,在原處又長出四個奇特的角,朝著天的四方。 9其中一個角又長出一個小角,向南方、東方和佳美之地8·9 佳美之地」指以色列,下同11·1641擴張勢力。 10它逐漸強大,高及天軍,將一些天軍和星宿拋到地上,用腳踐踏。 11它狂妄自大,要與天軍的統帥比高,它廢除日常獻給祂的祭,毀壞祂的聖所。 12因為反叛的緣故,天軍和日常所獻的祭都交給了它。它將真理拋在地上,它所行的無不順利。

13接著,我聽見一位聖者在說話,另一位聖者問他:「異象中出現的有關日常所獻的祭,毀滅性的反叛和踐踏聖所及天軍的事要持續多久呢?」 14他對我說:「兩千三百個晝夜。之後,聖所才會潔淨。」

解釋異象

15但以理看見這異象,正想明白它的意思,忽然有一個外貌像人的站在我面前。 16我聽見有人聲從烏萊河兩岸之間呼喊:「加百列啊,要讓此人明白這異象。」 17於是,他朝我站的地方走來,當他走來的時候,我嚇得俯伏在地。他對我說:「人子啊,你要明白,這異象是關於末後的時期。」 18他和我說話的時候,我伏在地上昏睡過去,他便輕拍我,扶我起來, 19對我說:「我要告訴你將來上帝發烈怒時所發生的事,因為這異象是關於那定好的末後時期。 20你看見的那隻有兩角的公綿羊指瑪代波斯的諸王。 21公山羊指希臘王,在牠雙眼之間的大角指第一個王。 22大角折斷後,從原處長出四個角表示四個國必從這國興起,但都不及這國強大。 23在四國的末期,人們惡貫滿盈的時候,必有一個面貌兇惡、詭計多端的王興起。 24他勢力強大,卻不是靠自己的力量。他必帶來可怕的毀滅,而且凡事亨通,他必毀滅強者和聖民。 25他利用詭計和騙術得逞,心高氣傲,乘人不備突然毀滅許多人,甚至要攻擊萬君之君,然而他終必被擊垮,但並非被人的手擊垮。 26異象中所說的兩千三百個晝夜是真的。但你要保密,不可告訴別人,因為這指的是遙遠的將來。」

27但以理精疲力盡,病了幾天。後來我起來照常辦理王的事務,但我對這異象感到驚奇不已,不明白它的意思。

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Bibilia Takatifu)

Danieli 8:1-27

Maono Ya Danieli Ya Kondoo Dume Na Beberu

18:1 Dan 5:1Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Mfalme Belshaza, mimi Danieli, nilipata maono, baada ya maono ambayo yalikuwa yamenitokea mbeleni. 28:2 Mwa 10:22; Es 2:8; Ezr 4:9Katika maono yangu, nilijiona nikiwa ndani ya ngome ya Shushani katika jimbo la Elamu. Katika maono nilikuwa kando ya Mto Ulai.8:2 Mto Ulai ni mfereji uliokuwa kati ya Shushani na Elymaisi; sasa unaitwa Mto Karuni. 38:3 Dan 10:5; Ufu 13:11Nikatazama juu, na hapo mbele yangu kulikuwa na kondoo dume mwenye pembe mbili, akiwa amesimama kando ya mto, nazo pembe zake zilikuwa ndefu. Pembe moja ilikuwa ndefu kuliko hiyo nyingine, lakini iliendelea kukua baadaye. 48:4 Dan 11:3, 16; Isa 41:3Nikamtazama yule kondoo dume alivyokuwa akishambulia kuelekea magharibi, kaskazini na kusini. Hakuna mnyama yeyote aliyeweza kusimama dhidi yake, wala hakuna aliyeweza kuokoa kutoka nguvu zake. Alifanya kama atakavyo, naye akawa mkuu.

5Nilipokuwa ninatafakari hili, ghafula beberu mwenye pembe moja kubwa sana katikati ya macho yake alikuja kutoka magharibi, akiruka kasi juu ya dunia yote bila kugusa ardhi. 6Alikuja akimwelekea yule kondoo dume mwenye pembe mbili niliyemwona akisimama kando ya mto, akamshambulia kwa hasira nyingi. 78:7 Dan 7:7; 11:11Nikamwona akimshambulia yule kondoo dume kwa hasira nyingi, akimpiga yule kondoo dume na kuvunja pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuwa na nguvu za kumzuia yule beberu, hivyo akamwangusha yule kondoo dume chini na kumkanyaga, wala hakuna aliyeweza kumwokoa yule kondoo dume kutoka nguvu za huyo beberu. 88:8 2Nya 26:16-21; Dan 5:20; 7:2; Ufu 7:1Yule beberu akawa mkubwa sana, lakini katika kilele cha nguvu zake ile pembe yake ndefu ilivunjika, na mahali pake pakaota pembe nne kubwa kuelekea pande nne za dunia.

98:9 Eze 20:6; Dan 11:16; Za 48:2; Dan 7:8Kutoka mojawapo ya zile pembe nne palitokea pembe ndogo ukaongezeka nguvu kuelekea kusini, na kuelekea mashariki, na kuelekea Nchi ya Kupendeza. 108:10 Isa 14:13; Ufu 8:10; 12:4; Dan 7:7Pembe hiyo ikaendelea kukua hadi kufikia jeshi la mbinguni, nayo ikalitupa baadhi ya jeshi la vitu vya angani hapa chini duniani, na kulikanyaga. 118:11 Dan 11:36-37; Eze 46:13-14; Dan 12:11; 11:31Pembe hiyo ikajikweza ili iwe kama Mkuu wa hilo jeshi; ikamwondolea dhabihu ya kila siku, napo mahali pake patakatifu pakashushwa chini. 12Kwa sababu ya uasi, jeshi la watakatifu na dhabihu za kila siku vikatiwa mikononi mwake. Ikafanikiwa katika kila kitu ilichofanya, nayo kweli ikatupwa chini.

138:13 Kum 33:2; Dan 4:23; 12:6; Lk 21:24; Isa 28:18; Ufu 11:2Kisha nikamsikia mtakatifu mmoja akizungumza na mtakatifu mwingine, akamwambia, “Je, itachukua muda gani maono haya yatimie: maono kuhusu dhabihu ya kila siku, uasi unaosababisha ukiwa, kutwaliwa kwa mahali patakatifu, na jeshi litakalokanyagwa chini ya nyayo?”

148:14 Dan 12:11-12Akaniambia, “Itachukua siku 2,300. Ndipo mahali patakatifu patawekwa wakfu tena.”

Tafsiri Ya Maono

158:15 Eze 2:1; Dan 10:16-18Mimi Danieli nilipokuwa ninaangalia maono na kujaribu kuelewa, mbele yangu alisimama mmoja aliyefanana na mwanadamu. 168:16 Dan 9:21; Lk 1:19; Dan 7:16Kisha nikasikia sauti ya mwanadamu kutoka Mto Ulai ikiita, “Gabrieli, mwambie mtu huyu maana ya maono haya.”

178:17 Eze 44:4; Ufu 1:17; Hab 2:3; Eze 1:28; Dan 2:46Alipokuwa akikaribia pale nilipokuwa nimesimama, niliogopa, nikaanguka kifudifudi. Akaniambia, “Mwana wa mwanadamu, fahamu kuwa maono haya yanahusu siku za mwisho.”

188:18 Dan 10:9; Eze 2:2; Zek 4:1Alipokuwa akinena nami, nilikuwa katika usingizi mzito, huku nimelala kifudifudi. Ndipo aliponigusa na kunisimamisha wima.

198:19 Isa 10:25; Za 102:13Akaniambia, “Nitakuambia yale yatakayotokea baadaye wakati wa ghadhabu, kwa sababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho ulioamriwa. 208:20 Eze 27:10Kondoo dume mwenye pembe mbili ambaye ulimwona anawakilisha wafalme wa Umedi na Uajemi. 218:21 Dan 10:20; 11:2Yule beberu mwenye nywele nyingi ni mfalme wa Uyunani, nayo ile pembe ndefu katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza. 22Zile pembe nne zilizoota badala ya ile pembe iliyovunjika zinawakilisha falme nne ambazo zitatokea kutoka taifa lake, lakini hakuna hata mmoja utakaokuwa na nguvu kama ule uliovunjika.

23“Katika sehemu ya mwisho ya utawala wao, wakati waasi watakapokuwa waovu kabisa, atainuka mfalme mwenye uso mkali, aliye stadi wa hila. 248:24 Dan 7:25; 2:34; 11:21; Ay 34:7Atakuwa na nguvu nyingi, lakini si kwa uwezo wake mwenyewe. Atasababisha uharibifu wa kutisha, na atafanikiwa kwa chochote anachofanya. Atawaangamiza watu maarufu na watu watakatifu. 258:25 Dan 11:36; 11:21; Ay 34:20Atasababisha udanganyifu ustawi, naye atajihesabu mwenyewe kuwa bora. Wakati wajisikiapo kuwa wako salama, atawaangamiza wengi, na kushindana na Mkuu wa wakuu. Lakini ataangamizwa, isipokuwa si kwa uwezo wa mwanadamu.

268:26 Isa 8:16; Ufu 10:4; Dan 10:14; Eze 12:27; Isa 29:11; Ufu 22:10“Maono kuhusu jioni na asubuhi ambayo umepewa ni kweli, lakini yatie muhuri maono haya, kwa maana yanahusu wakati mrefu ujao.”

278:27 Dan 2:47-48; Isa 21:3; Dan 7:28; 10:8; 4:19Mimi Danieli nilikuwa nimechoka sana, na nikalala nikiwa mgonjwa kwa siku kadhaa. Ndipo nikaamka, nikaenda kwenye shughuli za mfalme. Nilifadhaishwa na maono hayo, nami sikuweza kuyaelewa.